Wanamuziki wengi hawana Vibali vya kuishi Nchini

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,898
Baada ya utafiki wangu mkubwa kabisa na wenye ushahidi kede kede nimegundua kwamba wanamuziki wengi wa bendi za wakubwa ikiwemo ile ya Kapuya na wengineo ambao ni akina Asha Baraka wafadhili wa CCM hawana vibali vya kuishi nchi hii .Sambamba na maneno ya Mzee Nakandamiza Kibara siku zile juu ya waziri Batilda kuwa na watumishi wa ndani toka Malawi nk , sasa vijilunyungu vimethibitisha kwamba tatizo hili ni sugu na hawa wagusiki kwa kuwa wako na wakubwa .

kalunyungu kamemuuliza Mkuu wa uchunguzi wa Uhamiaji ndugu N juu habari hizi , mkubwa huyo aliishia kujiuma na kusema wakubwa hawakusiki.Vivyo hivyo na hata huko mtaani mipaka yetu iko lose kinoma na bado watu wanasema Nchi inalindwa imara .Tatizo haliko kuwakamata mafisadi pekee kummbe hata mambo yanayo wahusu wale wanao jidai ni wasafi na nguvu yao kubwa ni Chama tawala ,
Ee bwana hii ndiyo habari ya leo .
 
Mkuu Lunyungu,

“Ukitaka biashara yako na mambo yakunyokee jiunge na Chama Cha Mapinduzi” - Mh Fredrick Tluway Sumaye

Hatuna budi kumlaumu kiongozi huyu mpaka pale mauti yatakapomkuta! Nchi hii hakuna cha utawala bora, sheria wala miiko ya kazi! Kila kitu kinaendeshwa kwa kufuata itikadi za vyama!

Huyo jamaa wa Uhamiaji (ndugu N) ulimuonea tu, ulipaswa kumhoji Fredrick Sumaye kuhusu utafiti wako na kauri yake!
 
Maneno yako mkuu think Big ni mazito na sasa kama mwendo ni huu kuna haja gani ya kuwa tuna danganyana kila siku hapa Dodoma na maneno ya utawala bora na Nchi kufuata utawala wa sheria ?
 
Nchi hii haina mipaka hata kidogo. ni pango lenye mali lisilokuwa na mwenyewe. Ni ajabu sana kuwa hakuna tatizo kwa mgeni awaye yote yule kuingia hapa Bongo na kuondoka ili mradi hatumii usafiri wa ndege.
Hili ni tatizo kubwa sana kwa nchi hii, ambayo imejikuta hata wageni wanaukwaa uongozi wa kuongoza wadanganyika bila vibali halali vya kuishi. Kuna waziri mmoja kule burundi aliwahi kuitumikia serikali ya Tanzania katika Halmashauri ya mkoa wa Kigoma kama Mtanzania. hii ni ajabu lakini ni kweli!!!!
 
Sioni shida kwa wanaburudani hao kuwa nchi, ...........mtazameni Abood,RA,Amani,wahindi+waarabu viongozi Tz wote ni multipassports,then wanawaongoza wa-Tz kusaka maisha bora kwa kila mTz....Haikai akilini.
 
Tanzania ulinzi wa mipaka kwa waziri husika ni uwanja wa ndege tu .Nimekuwa sasa katika mipaka ya Namanga, Sirare,Tunduma,Tanga kuingia Mombasa,Bukomba kuingia Uganda basi ni kichekesho kitupu.Kule jamaa wa uhamiaji wanavimba matumbo na kukimbilia kununua magari .

TRA mipakani nao ni miungu watu wanaweka mitego kokote na kushirikiana na FFU , na trafiki ni fedheha wazee .Niliyo yaona naogopa kusema lakini blah blah za wabunge na Uhamiaji na IGP utashangaa sana .
 
Unajua ukitaka kujua kiini cha tatizo ni lazima uende kwenye mzizi,

1. Kwa mara ya kwanza wa-Congo wapiga muziki, waliaza kuletwa Tanzania na Batengas, mfanya biashara maarufu sana zamani aliyekuwa rafiki mkubwa sana wa Mwalimu.

2. Batengas alikuwa akimilki club moja kubwa sana ya muziki pale mahali ambapo sasa kipo kituo cha Tazara, alianza na Nova success ambayo ilikuwa na kina Baba Gaston, Emmy, na Kabila Kabanze hii ilikuwa ni in the 60s, kipindi hiki hakuna aliyejali kama hawa wa-Congo, ana vibali vya kuishi nchini kwetu kwa sababu hakukuwa na competition na Batengas alikuwa ni mtu mwenye big political influence, hakuna aliyeweza kumgusa na hili swali.

3. Siasa zetu za taifa zilipoanza kubadilika, hawa wa-Congo, wakaanza kuhamia Nairobi, na wengine wapya wakazidi kuingia kuanzia in the 70s, wakaja Marquis, Banangenge, na Boma Liwanza, yaani kina Chinyama Chiyanzi, Fataki Masumbuko ya dunia, Nsilu wa Bansilu, Mbuya Makonga, Wabangoi.

- Hapa ndio kwa mara ya kwanza Batengas, akaaanza kushindana na wengine kama kina Hugo Kisima, kwenye hii field ya wanamuziki wa ki-Congo, ndipo kwa mara ya kwanza katika hii competition mpya, maswali ya vibali vya hawa wanamuziki kuwepo nchini hapa yaaanza, yaani kutoka kwa competitors wa Batengas, hatimaye Batengas alioonahawezi tena ku-deal na competition, akaamu kujitoa kwenye hii biashara na ugomvi ukaanza kwa waliobaki kwenye field na neno kubwa likawa vibali vya hawa wanamuziki.

4. Mpaka hapa local wetu, kina Mbaraka Mwinshehe ( Moro Jazz/Super Volcano), Balisidya (Dar Jazz/Afro 70), Wema Abdallah (Tabora Jazz/Western Jazz), Kassim Mapiri (Tabora Jazz), Wilson Peter (Simba Wa Nyika), Ahmed Kipande (Atomic Jazz), Juma Mrisho (Kilwa Jazz), Butiama Jazz, Marijani Rajabu (Saffari Trippers/ Dar International), Juma Ubao (Biashara Jazz), Shaban Dede (Bima Jazz), Salum Abdallah (Cuban Marimba), Gurumo (Msondo Ngoma), Juma Kilaza (Subi Subi), na wengineo walikuwa na fair share kibiashara ya market ya muziki nchini na hawa wa-Congo.

5. Lakini in the 80s, mambo yakabadilika kabisaa, kilikua ni kiipindi cha kuanza kwa matatizo makubwa ya kiuchumi, bendi zetu zikaanza kukosa vyombo vizuri vya muziki, huku wa-Congo wakisaidiwa na their former colonial masters, yaani wa-Faransa na Wa-Belgiji, walianza kurudi kwao na wakaingia kwenye kuu-promote muziki wa wa-Congo, Nairobi nayo kawa mwiba mkubwa sana kwetu kwa sababu kwa mara ya kwanza ikawa very clear kuwa wa-Congo, wana vipaji superior vya muziki kuliko sisi santuri zao zikaanza kutawala sehemu zote za starehe nchini, na nyingi zilikuwa zinatoka Nairobi,

-Mbaraka Mwinshehe ambaye kwa kawaida, alikuwa in the same league na Lwambo Makiadi, maana huko Congo Kinshasa kwenye radio zao na club za starehe miziki ya Mbaraka ilikuwa ikipigwa kwa usawa na ya Lwambo, lakini sasa ikaanza kushuka thamani kwa sababu bendi zetu bongo hazikuwa na vyombo vya kisasa, in fact hata Mbaraka alifariki akiwa anahangaika kutafuta vyombo vya kisasa, kwa sababu ukiangalia muziki wa Albamu ya mwisho ya Mbaraka, yaani "Shida", utaona tofauti kubwa kabisa na muziki wake wa zamani maana huu wa mwisho ulikuwa ni mzuri na uliotengenezwa kifundi kwa kutumia vyombo vya kisasa.

- Mfano mwingine ni Simba Wa Nyika, wao pia walihamia Nairobi na kufanikiwa sana kimziki, kwa kuwa na vyombo vizuri pmaoja na kuhsirikiana sana na wanamuziki wa Kio-Congo.

5. Haya mabadiliko makubwa kimziki kuanzia Nairobi, Congo Kinshasa, mpaka Brusells na Paris, yakaishia kuwapa the edge wanamuziki wa Ki-Congo, yaani sasa iikiiitwa Zaire, hapa bongo bendi za ki-Zaire zikaanza kutawala soko lote la muziki Tanzania, ni bendi mbili tu local yaani Msondo Ngoma, na Urafiki Jazz, ukiacha Tabora Jazz kwa mikoani ndio walioweza kusimama imara na kujaribu kushindana na hawa wa-Zaire, lakini ukweli bado ulikuwa wazi kuwa wa-Zaire wanawazidi sana kwa kupata watu,

-Ndio sasa vibali vya wanamuziki wa Zaire, ukaanza kuwa ishu kubwa sasa, kwa sababu sasa ndio hasa rushwa ilikaza mizizi nchini kwa kushirikiana na wafanya biashara wanamiliki hizo bendi za muziki, ndipo maofisa wachache wa uhamiaji wakagundua hazina kubwa ya hela za rushwa za kirahisi sana huku kwenye hii field ya wanamuziki wa ki-Zaire nchini, ndio maana wale wote waliofanikiwa kimuziki yaani wa-Zaire kama Kiki, Nguza, Chinyama (RIP), Mbuya Makonga (RIP), Assosa, Wabangoi, Massiya Radi (RIP), Kassongo Mpinda, Ndala Kasheba (RIP), Remmy, Makassy, Ilunga Lubaba, Bobo Sukari, Kasaloo Kyanga na wnegineo usingewza kusikia hata siku moja wana matatizo ya vibali vya muziki, ni kwa sababu walikuwa na uwezo mkubwa kipesa kutoa rushwa nzito, ni wale tu waliokuwa na uwezo mdogo kipesa ndio waliokuwa na matatizo ya vibali.

6. Sasa hili tatizo limekuwa too complicated kwa sababu soko la muziki wa dansi nchini, linatawaliwa na marafiki wawili yaani Msilwa (Twanga Pepeta), na Martin (FM Academia), ambao wamesoma pamoja Mlimani na walikuwa wakiishi chumba kimoja pale Mlimani, na ambao originally ndio walioanzisha ile bendi iliyokuwa maarufu sana zamani iliyokuwa pale New African Hotel ya Kassongo Mpinda, lakini baadaye waliachana na kwenda njia tofauti.

7. Martin alianzisha FM Academia, Msilwa akaanzisha Twanga Pepeta, John Komba akaanzisha Achigo Sound akishirikiana na Mundhiri na Nguza.

(a.) Twanga wakaamua kuwa hawataki wa-Zaire kwenye bendi zao ambazo sasa zilikuwa ni Twanga ya Ali Choki na Revolution ya Muumini Muniri na Badi Bakule zikiwa ni bendi zenye wanamuziki wazawa tu.

(b). FM Academia, ikawa ni bendi yenye wa-Zaire tu kina Nyoshi El-Sadat, Jose Mara, na Kitokololo, hawa wakapata mafanikio makubwa sana na ndio wanaotawala soko zima la muziki Dar na hatimaye wameanzisha bendi mpya ya Akudo.

(C). Kuona hivi Twanga Pepeta, ambao hawakuwa na soko zuri sana la biashara wakaanza nao kutafuta wa-Zaire kina Soko la Mandondo Diof, sasa ndio competiton tena imeanza kati ya Martin na Msilwa, kuona hivi dada wa Msilwa akaamia kujitosa kwenye NEC, kutafuta kinga na ubavu wa kupata vibali vya wanamuziki wa ki-Zaire kwenye bendi za kaka yake, huku upande wa pili Martin mzee wa Academia, yeye ni mzee wa system kwa hiyo hana tatizo sana na access ya vibali, lakini ni katika hivi vita vya hawa wapinzani wawili ambao sasa umehamia kwenye wanamuziki wenyewe, yaani hawa wa-Zaire, ndio unapata tatizo hili la vibali vyao vya kuishi hapa na kupiga muziki,

kwa sababu sasa wamefika mahali wanachongeana wenyewe kwa wenyewe, kutokana na kuoneana wivu, kabla ya hapo hakukuwa na tatizo kwa sababu hakukuwa na tatizo la mashindano ni mpaka majuzi tu Twanga, walioamua kuajiri wa-Zaire, sasa m-Zaire akitoka Twanga akaingia Academia tu, basi Twanga ni kwenda kumchongea kuwa hana papers na vice versa,

Kwa maoni yangu ni kwamba:-

Ukweli ni kwamba wengi wao ni watu wa Kigoma, kwa sababu kama umewahi kuishi huko utajua ninachokisema, lakini kwa sababu soko la muziki Dar linataka Wa-Zaire hijfanya wa-Zaire, sasa mpaka ofisa wa uhamiaji aje athibitishe hilo huwa jamaa ameshkaa ndani kwa mwezi mzima na magazeti yamesharipoti yetu uchwara yamesha ripoti bila na uhakika wa habari,

Wanamuziki wa kweli wa-Zaire, wengi wao huwa hawawezi ku-take hiyo risk ya kuja bongo kupiga bila kibali kwa sababu kwa kawaida wao huwa wako transit tu, siku zote wanatafuta kwenda kwenye masoko makubwa ya muziki wao, kama Paris na Brussells, au Nairobi ambako wanajua kuwa hawawezi kwenda huko bila makaratasi, na pia hawa huwa wana masoko hata kwao Zaire, kwa hiyo ni wajibu wa mfanya biashara anayewataka kuwatafutia makaratasi yanayotakiwa, maana hawawezi kukubali kuja bila papers kamili.

Now ni kweli kuwa wapo wachache sana wasiokuwa na makaratasi kabisa, kama na sisi wabongo huko nje, tunachofanya sasa ni kuwaa-abuse pale tu wanapohama bendi moja ya mwenye nguvu kwenda ya asiyekuwa na nguvu, sheria za taifa haziwezi kutumiwa kama kinga kwa baadhi ya wafanya biashara, kama nia na madhumuni ni wote wawe na vibali, basi ifanyike operation kubwa nchini wa-aire wote wapiga muziki wahakikishwe kuwa wana the right papers!

Samahani kwa kuwachosha, lakini nilitaka tu kuiweka hii sawa kidogo!

Ahsante Wakuu!
 
FMES,
Somo zuri sana. Lakini mbona umewasahau Mzee Makassy na Dr Remmy? Huyu katoka Zaire mashariki.
 
FMes,
Niliingia msituni na nikasema sitaandika kwa miezi kadhaa. Kuna mengine huwa tunapishana. Ila kwa hili naona tuko pamoja. Umelichambua vizuri sana. Hii ya wanamuziki wa Kigoma kujifanya ni Wazairwaa, nilishalisikia siku moja. Yupo mzee mmoja Halfcas aitwaye Mntangi, alinieleza juu ya Dr. Remmy na shida ya kupata makaratasi yake pale alipoimba wimbo wa Mrema na Machozi ya samaki. CCM walianza kumpa joto ya jiwe na hapo akaanza kuhaha. Sasa tatizo nasikia akahusisha watu wengi kusolve. Wengine wanadai kuwa Remmy hasa ni mtu wa Kigoma ila alitaka kupandisha chart kwa kutumia Uzairwaa. Sasa sijui ni kweli au vipi. Ila naona huu mchezo kweli upo siku nyingi.
By the way natafuta miziki ya hao mapacha akina Kasolo Kyanga na Kyanga Songo wakati wako Tancut Almasi na ile bendi waliyopiga miaka ya 80 mwishoni nimeisahau liyodumu muda mfupi na kwenda fia Dodoma. Kama unayo looo, itakuwa furaha. Nijulishe kwa PM.

NB:- Hayo majina ya Bendi umenirudisha mbali. Baba Gaston (Ilunga wa Ilunga) na wimbo wake wa X-mas ulipotoka na kupata upinzani na wimbo wa Wna Jobiso (tuombe Mungu akina baba na akina mama - wote tuwe salama). Hivi Nyboma pia alipitia Tz??
 
Sikonge,
Ukizipata nyimbo za TANCUT Almasi usinisahau kwenye ufalme wako. Nyboma hakuwahi kupitia Tanzania. Yeye hata Kiswahili hajui. Kwa sasa anashuttle kati ya Paris na London.
Kuna CD mpya wametoa akishirikiana na Syran Mbeza, Wuta Mayi na Massengo Djeskain wa Sosoliso katika bendi yao inaitwa Kekele. Ukiipata hiyo bomba sana.
 
Somo zuri sana. Lakini mbona umewasahau Mzee Makassy na Dr Remmy? Huyu katoka Zaire mashariki.

1. Mzee Makassy, aliwahi kupigia bendi ya Lwambo ni m-Zaire, haswa na alikuwa na chati kubwa hata alipokuwa Kampala kabla hajaja Dar. na ni m-Zaire wa kwanza kuja bongo akiwa na vyombo vya kisasa sana aina Rangers, ambavyo by then Tanzania hakukuwa na bendi yoyote iliyowahi kuwa navyo zaidi tu ya Lwambo, ambaye alikuja navyo pale uwanja wa taifa.

2. Remmy siamini kama ni m-Zaire, ninaamini ni m-Kigoma aliyejifanya m-Zaire ili tu kupanda chati ya mziki bongo, ndio maana alipopanda tu chati akiwa na Makassy ailyemleta, pale Bahari Beach, hakuchelewa kutoka na kuingia Matimila.

Ingawa amekuwa akidai mara nyingi sana kuwa ametokea jimbo la Kalemie, Zaire East, binafsi siamini hilo.
 
By the way natafuta miziki ya hao mapacha akina Kasolo Kyanga na Kyanga Songo wakati wako Tancut Almasi na ile bendi waliyopiga miaka ya 80 mwishoni nimeisahau liyodumu muda mfupi na kwenda fia Dodoma. Kama unayo looo, itakuwa furaha. Nijulishe kwa PM.

Hawa vijana wawili ninazo kanda zao, walianza na bendi ya baharia Timmy Tomas, iliyokuwa ikiitwa Orch. Toma Toma, (Wana-Tamba Tamba), baharia alipofilisika wakaingia Matimila na Remmy, walishiriki na kur-record naye nyimbo kama mbili yaani [I]"Alimasi"[/I] na "Tembea Ujioneee" kabla ya kwenda Iringa, Tancut

NB:- Hayo majina ya Bendi umenirudisha mbali. Baba Gaston (Ilunga wa Ilunga) na wimbo wake wa X-mas ulipotoka na kupata upinzani na wimbo wa Wna Jobiso (tuombe Mungu akina baba na akina mama - wote tuwe salama). Hivi Nyboma pia alipitia Tz??

1. Baba Ilunga wa Ilunga, au Baba National ndiye m-Zaire wa kwanza mpiga muziki kuja kuishi kwa muda mrefu sana Dar, lakini baadaye alihamia Nairobi, ambako baada tu ya muda mfupi akaondokewa na wapigaji wake wengi wakioongozwa kina Kai Kai, Kabila Kabanze, na Bwami Walumona, walioanzisha Les Mangelepa, na kutoa Albamu cha [I]"Embakasi" [/I], walipopanda chati na wao pia wakagombana na kuanzisha kundi jipya tena la Special Mangelepa, huyu alikuwa ni Kai Kai, ambaye siku zote alikuwa star wa bendi.

2. Nyiboma Muandido, alianzia bendi ya Orch. Bella Bella akiwa na Soki Vangu, akiwa na hii bendi ndipo Verkiys alikuwa ametoka kwenye bendi ya Lwambo, wakiwa kwenye Tour ya Paris,

-Verkicys, akaamua kuanzisha matawi mengine ya bendi, alianza na [I]Orch. Lipwa Lipwa, Orch. Kamale, na Orch. Kiam,[/I] ambako alimrubuni Nyiboma na kutoka kule na kumfanya kuwa kiongozi wa Orch. Lipwa Lipwa ,

-Baaada ya muda Mwanamuziki m-Zaire mwingine kwa jina la Mopero de Kavasha , alianzisha bendi iliyoitwa Orch. Nshama Nshama na alianzisha mtindo wa muziki wa Cavasha, ambao ulikubalika sana na vijana, na bendi zote kule zikaanza kuiga ile style, ndipo hata kwenye Orch. Lipwa Lipwa nao wakaamua kubadili style yao na kujiunga na Cavasha,

-ndipo ikabidi Nyiboma, atoke na kuanzisha bendi mpya ya Orch. Kamale, under Verckyis, ambako alikutana na kina Ricos Kizunga, Asossa, na Mulembu, na Orch. Lipwa Lipwa ikachukuliwa na Vata Mombasa, Mbumbi Malanda, Mongoley, Nsayi, na kina Nzaya na Malanda.

-Baadaye, Assosa, Mulemba, na Kizunga, walitoka na kwa sababu Verkyis alikuwa na political influence kubwa sana, wasingeweza kubaki kule Kinshaha kwa sababu angewatesa sana, hivyo wakaamua kuanzisaha bendi yao mpya waliyoiita Orch. Fuka Fuka na kuhamia Dar, walikuwa Mlimani Park walipo Sikinde sasa.

-Nyiboma hakuja, alibaki na Orch. Kamale, lakini hakuchukua muda mrefu akatoka na kwenda Paris, ambako alianza kupiga muziki kwa kusihirikana na Kabasele ya Mpanya yaani Pepe Kalle', na wakati mwingine alikuwa akishirikiana sana na Diblo Dibala na Lokassa ya Mbongo, na ni hivi karibuni amefikia hapo aliposema mkuu Jasusi,

Nyiboma hajawahi kuja bongo na huwa hajui kabisa kiswahili.

Mkuu Sikonge,

Kuhusu kutokubaliana kwetu humu JF, ninalijua sana hilo na halinipi shida kwa sababu toka nijiunge hapa JF nimekutana na miamba mingi sana, ambayo imejaribu kila njia kunishusha hadhi ambayo nimeifanyia kazi sana hapa JF kuwa nayo, sasa mimi ni politician in my own way ni lazima nijibu mashambulizi tena kiroho mbaya maana haya kwangu ni mazoezi tu ya safari ndefu kisiasa niliyonayo mbele yangu,

Ninajua kuwa una akili nyingi sana na elimu nzito sana ya darasani, lakini I am sorry kwamba siasa nina wasi wasi kuwa sio field yako, mimi ninakuona ukiwa a bureaucratic katika serikali au kampuni za binafsi, siasa ni talent na ni mchezo mgumu sana kuucheza, sivyo kama watu wengi wanavyouona kuwa ni rahisi sana, kutoa maoni kwa wanasiasa ni rahisi sana, lakini kuwa mwanasiasa na ukafanikiwa katika mazingara yetu ya bongo, ni ngumu zaidi mkuu na huu uwanja wa JF unapaswa kuwa mfano mkubwa sana kwetu, kuwa siasa ni mchezo mgumu sana

Otherwise, mimi sijakufukuza wala sina nia mbaya na wewe hapa JF, karibu urudi mkuu tukate ishus taifa liko njia panda yaliyopita sio ndwele mkuu tunaganga yanayokuja!

Ahsante Mkuu.
 
Heshima mbele mkuu, siku zote nimekuwa very active na muziki, ambao pia ninaweza kuupiga kwa kumudu kupiga baadhi ya vyombo vya muziki,

Na pia nimewahi kuwa DJ, kwa kupiga na watu kama DJ Super Deo pale YMCA, na Mkulu wangu Joe Holera pale, Space 1900, Seydou na Gerlad kwenye maparty mbali mbali, hasa IFM.

Unajua ukipenda kitu unafuatilia kwa karibu, hii niliyoitoa hapa sio elimu ya darasani, lakini heshima mbele mkuu tunaelimishana tu kidogo mkuu!
 
FMes,
Juu ya kusema nilkuwa nimeingia mitini, halikuwa na uhusiano na wewe au mtu mwingine yeyote. Nafahamu kuwa SIASA ni kitu kichafu sana na ndiyo maana nilikuandikia ule ujumbe wa mwisho kama unaukumbuka. Kusema huwa tunatofautiana nilikuwa nataka tu kuonyesha kuwa hicho ulichokiandika, umenifanya nikubaliane na wewe kwa asilimia 100, jambo ambalo kwenye siasa huwa ni kwa nadra kuwa upande mmoja kwa asilimia kubwa namna hiyo.
Kisa cha KUINGIA mitini kuandika comment humu ndani ilikuwa ni hii. Nilianza kukaa na kuandika au kusoma hii forum usiku na mchana. Ninasahau hata kula. Nikaogopa na kusema, Mungu wangu, nitakuwa JAMIIFORUM ADICTED sasa hivi. Dawa ngoja nibaki msomaji tu. Hivyo nimekuwa nakuja na kusoma na najitahidi nisiandike chochote. Ila hiyo makala yako ya MZIKI (siwezi kuishi bila musics) imenifanya nivunje mwiko wangu. Hata hivyo nasema tena, NARUDI KUWA SAVIMBI.

NB:- Ahhhh, kumbe na wewe na DJ kama mimi? Hapa naona hobby yetu kweli iko moja. Sawa, ila mie hadi leo bado nina-Practise na Vi-Pioneer CDJ200 + DJM 400 while i'm home......... Mengine ntawasiliana na wewe kwenye PM.
 
FMes,
Vipi kuhusu huyu bwana aitwaye NGUASHI NTIMBO? Kuna wimbo aliimba uitwao Elongi ya Cherie. Mwanzo nilijua kuwa ameimba TPOK jazz, kumbe ni jamaa na wimbo ni wake na kwa hiyo hauko kwenye Album za TPOK jazz ao Luambo. Pia nasoma kuja kukuta pia aliimba na Super Mazembe wimbo wa Shauri yako. Nakumbuka wimbo wake ulitamba sana miaka ya 80 mwanzoni.
Wimbo wa Almasi na Tembea ujionee, sasa kweli umenikumbusha na kujua kwa nini nilikuwa nazipenda. Nikikumbuka naona ni kweli kabisa kuwa ni Mapacha ndiyo walikuwa waimbaji. Maadamu sina, ngoja walau nisikilize wimbo wa USIWE ndumila kuwili wa Dr. Remmy.
Huo wimbo hapo juu nimeutafuta/nautafuta sana (Elongi ya Cherie). Mcongo mmoja alikuwa nao kwenye CD akataka sijui nimbusu miguu ndiyo anipe, nikamuacha na wimbo wake. Hakuna Title wala jina la cd. Anyway siku moja i hope ntaupata nikiwa nchi za watu maana hapa Sikonge kupata ni ndoto. Ukija upata au kama utakuwa nao basi pia ntaomba tuwasiliane.
Samahani kwa wengine kwamba hii habari iko kwenye SIASA na sisi tumeingiza hadi U-DJ na wanamuziki ambao vijana wa sasa nafikiri wanashangaa kuwa hawa ndiyo watu gani tena Yarabi. Ila kama kweli mwapenda muziki na mwataka kuwa wanamuziki wazuri basi tafuteni miziki yao na huko mtakuwa mmpepata MIZIZI ya miziki yetu ya Africa.
 
FMes,
Masahihisho kidogo. Wimbo wa Nguashi unaitwa MANGUTA:-

One of the songs became my favourite, "Manguta" by someone called Nguashi N'timbo: Many years later, when I read the credits on one of Mbilia Bel's LPs I found his name again: As composer of "Shauri Yako". A big hit for her – and as I realised even later, when I listended to Orchestra Super Mazembe's compilation album on Earthworks I heard that song again. Nguashi N'Timbo made his debut in Lubumbashi in the Baba Gaston Band and was with them for many years. Songs associated with him from that time are "Manguta-Elongi ya Cherie," "Nzanzi," and "Bolingo ya sens unique." Arriving in Kinshasa he started Orchestre Sentima and sang alongside Sam Mangwana, notably on "Tangua."
 
Unajua ukitaka kujua kiini cha tatizo ni lazima uende kwenye mzizi,

1. Kwa mara ya kwanza wa-Congo wapiga muziki, waliaza kuletwa Tanzania na Batengas, mfanya biashara maarufu sana zamani aliyekuwa rafiki mkubwa sana wa Mwalimu.

2. Batengas alikuwa akimilki club moja kubwa sana ya muziki pale mahali ambapo sasa kipo kituo cha Tazara, alianza na Nova success ambayo ilikuwa na kina Baba Gaston, Emmy, na Kabila Kabanze hii ilikuwa ni in the 60s, kipindi hiki hakuna aliyejali kama hawa wa-Congo, ana vibali vya kuishi nchini kwetu kwa sababu hakukuwa na competition na Batengas alikuwa ni mtu mwenye big political influence, hakuna aliyeweza kumgusa na hili swali.

3. Siasa zetu za taifa zilipoanza kubadilika, hawa wa-Congo, wakaanza kuhamia Nairobi, na wengine wapya wakazidi kuingia kuanzia in the 70s, wakaja Marquis, Banangenge, na Boma Liwanza, yaani kina Chinyama Chiyanzi, Fataki Masumbuko ya dunia, Nsilu wa Bansilu, Mbuya Makonga, Wabangoi.

- Hapa ndio kwa mara ya kwanza Batengas, akaaanza kushindana na wengine kama kina Hugo Kisima, kwenye hii field ya wanamuziki wa ki-Congo, ndipo kwa mara ya kwanza katika hii competition mpya, maswali ya vibali vya hawa wanamuziki kuwepo nchini hapa yaaanza, yaani kutoka kwa competitors wa Batengas, hatimaye Batengas alioonahawezi tena ku-deal na competition, akaamu kujitoa kwenye hii biashara na ugomvi ukaanza kwa waliobaki kwenye field na neno kubwa likawa vibali vya hawa wanamuziki.

4. Mpaka hapa local wetu, kina Mbaraka Mwinshehe ( Moro Jazz/Super Volcano), Balisidya (Dar Jazz/Afro 70), Wema Abdallah (Tabora Jazz/Western Jazz), Kassim Mapiri (Tabora Jazz), Wilson Peter (Simba Wa Nyika), Ahmed Kipande (Atomic Jazz), Juma Mrisho (Kilwa Jazz), Butiama Jazz, Marijani Rajabu (Saffari Trippers/ Dar International), Juma Ubao (Biashara Jazz), Shaban Dede (Bima Jazz), Salum Abdallah (Cuban Marimba), Gurumo (Msondo Ngoma), Juma Kilaza (Subi Subi), na wengineo walikuwa na fair share kibiashara ya market ya muziki nchini na hawa wa-Congo.

5. Lakini in the 80s, mambo yakabadilika kabisaa, kilikua ni kiipindi cha kuanza kwa matatizo makubwa ya kiuchumi, bendi zetu zikaanza kukosa vyombo vizuri vya muziki, huku wa-Congo wakisaidiwa na their former colonial masters, yaani wa-Faransa na Wa-Belgiji, walianza kurudi kwao na wakaingia kwenye kuu-promote muziki wa wa-Congo, Nairobi nayo kawa mwiba mkubwa sana kwetu kwa sababu kwa mara ya kwanza ikawa very clear kuwa wa-Congo, wana vipaji superior vya muziki kuliko sisi santuri zao zikaanza kutawala sehemu zote za starehe nchini, na nyingi zilikuwa zinatoka Nairobi,

-Mbaraka Mwinshehe ambaye kwa kawaida, alikuwa in the same league na Lwambo Makiadi, maana huko Congo Kinshasa kwenye radio zao na club za starehe miziki ya Mbaraka ilikuwa ikipigwa kwa usawa na ya Lwambo, lakini sasa ikaanza kushuka thamani kwa sababu bendi zetu bongo hazikuwa na vyombo vya kisasa, in fact hata Mbaraka alifariki akiwa anahangaika kutafuta vyombo vya kisasa, kwa sababu ukiangalia muziki wa Albamu ya mwisho ya Mbaraka, yaani "Shida", utaona tofauti kubwa kabisa na muziki wake wa zamani maana huu wa mwisho ulikuwa ni mzuri na uliotengenezwa kifundi kwa kutumia vyombo vya kisasa.

- Mfano mwingine ni Simba Wa Nyika, wao pia walihamia Nairobi na kufanikiwa sana kimziki, kwa kuwa na vyombo vizuri pmaoja na kuhsirikiana sana na wanamuziki wa Kio-Congo.

5. Haya mabadiliko makubwa kimziki kuanzia Nairobi, Congo Kinshasa, mpaka Brusells na Paris, yakaishia kuwapa the edge wanamuziki wa Ki-Congo, yaani sasa iikiiitwa Zaire, hapa bongo bendi za ki-Zaire zikaanza kutawala soko lote la muziki Tanzania, ni bendi mbili tu local yaani Msondo Ngoma, na Urafiki Jazz, ukiacha Tabora Jazz kwa mikoani ndio walioweza kusimama imara na kujaribu kushindana na hawa wa-Zaire, lakini ukweli bado ulikuwa wazi kuwa wa-Zaire wanawazidi sana kwa kupata watu,

-Ndio sasa vibali vya wanamuziki wa Zaire, ukaanza kuwa ishu kubwa sasa, kwa sababu sasa ndio hasa rushwa ilikaza mizizi nchini kwa kushirikiana na wafanya biashara wanamiliki hizo bendi za muziki, ndipo maofisa wachache wa uhamiaji wakagundua hazina kubwa ya hela za rushwa za kirahisi sana huku kwenye hii field ya wanamuziki wa ki-Zaire nchini, ndio maana wale wote waliofanikiwa kimuziki yaani wa-Zaire kama Kiki, Nguza, Chinyama (RIP), Mbuya Makonga (RIP), Assosa, Wabangoi, Massiya Radi (RIP), Kassongo Mpinda, Ndala Kasheba (RIP), Remmy, Makassy, Ilunga Lubaba, Bobo Sukari, Kasaloo Kyanga na wnegineo usingewza kusikia hata siku moja wana matatizo ya vibali vya muziki, ni kwa sababu walikuwa na uwezo mkubwa kipesa kutoa rushwa nzito, ni wale tu waliokuwa na uwezo mdogo kipesa ndio waliokuwa na matatizo ya vibali.

6. Sasa hili tatizo limekuwa too complicated kwa sababu soko la muziki wa dansi nchini, linatawaliwa na marafiki wawili yaani Msilwa (Twanga Pepeta), na Martin (FM Academia), ambao wamesoma pamoja Mlimani na walikuwa wakiishi chumba kimoja pale Mlimani, na ambao originally ndio walioanzisha ile bendi iliyokuwa maarufu sana zamani iliyokuwa pale New African Hotel ya Kassongo Mpinda, lakini baadaye waliachana na kwenda njia tofauti.

7. Martin alianzisha FM Academia, Msilwa akaanzisha Twanga Pepeta, John Komba akaanzisha Achigo Sound akishirikiana na Mundhiri na Nguza.

(a.) Twanga wakaamua kuwa hawataki wa-Zaire kwenye bendi zao ambazo sasa zilikuwa ni Twanga ya Ali Choki na Revolution ya Muumini Muniri na Badi Bakule zikiwa ni bendi zenye wanamuziki wazawa tu.

(b). FM Academia, ikawa ni bendi yenye wa-Zaire tu kina Nyoshi El-Sadat, Jose Mara, na Kitokololo, hawa wakapata mafanikio makubwa sana na ndio wanaotawala soko zima la muziki Dar na hatimaye wameanzisha bendi mpya ya Akudo.

(C). Kuona hivi Twanga Pepeta, ambao hawakuwa na soko zuri sana la biashara wakaanza nao kutafuta wa-Zaire kina Soko la Mandondo Diof, sasa ndio competiton tena imeanza kati ya Martin na Msilwa, kuona hivi dada wa Msilwa akaamia kujitosa kwenye NEC, kutafuta kinga na ubavu wa kupata vibali vya wanamuziki wa ki-Zaire kwenye bendi za kaka yake, huku upande wa pili Martin mzee wa Academia, yeye ni mzee wa system kwa hiyo hana tatizo sana na access ya vibali, lakini ni katika hivi vita vya hawa wapinzani wawili ambao sasa umehamia kwenye wanamuziki wenyewe, yaani hawa wa-Zaire, ndio unapata tatizo hili la vibali vyao vya kuishi hapa na kupiga muziki,

kwa sababu sasa wamefika mahali wanachongeana wenyewe kwa wenyewe, kutokana na kuoneana wivu, kabla ya hapo hakukuwa na tatizo kwa sababu hakukuwa na tatizo la mashindano ni mpaka majuzi tu Twanga, walioamua kuajiri wa-Zaire, sasa m-Zaire akitoka Twanga akaingia Academia tu, basi Twanga ni kwenda kumchongea kuwa hana papers na vice versa,

Kwa maoni yangu ni kwamba:-

Ukweli ni kwamba wengi wao ni watu wa Kigoma, kwa sababu kama umewahi kuishi huko utajua ninachokisema, lakini kwa sababu soko la muziki Dar linataka Wa-Zaire hijfanya wa-Zaire, sasa mpaka ofisa wa uhamiaji aje athibitishe hilo huwa jamaa ameshkaa ndani kwa mwezi mzima na magazeti yamesharipoti yetu uchwara yamesha ripoti bila na uhakika wa habari,

Wanamuziki wa kweli wa-Zaire, wengi wao huwa hawawezi ku-take hiyo risk ya kuja bongo kupiga bila kibali kwa sababu kwa kawaida wao huwa wako transit tu, siku zote wanatafuta kwenda kwenye masoko makubwa ya muziki wao, kama Paris na Brussells, au Nairobi ambako wanajua kuwa hawawezi kwenda huko bila makaratasi, na pia hawa huwa wana masoko hata kwao Zaire, kwa hiyo ni wajibu wa mfanya biashara anayewataka kuwatafutia makaratasi yanayotakiwa, maana hawawezi kukubali kuja bila papers kamili.

Now ni kweli kuwa wapo wachache sana wasiokuwa na makaratasi kabisa, kama na sisi wabongo huko nje, tunachofanya sasa ni kuwaa-abuse pale tu wanapohama bendi moja ya mwenye nguvu kwenda ya asiyekuwa na nguvu, sheria za taifa haziwezi kutumiwa kama kinga kwa baadhi ya wafanya biashara, kama nia na madhumuni ni wote wawe na vibali, basi ifanyike operation kubwa nchini wa-aire wote wapiga muziki wahakikishwe kuwa wana the right papers!

Samahani kwa kuwachosha, lakini nilitaka tu kuiweka hii sawa kidogo!

Ahsante Wakuu!

Nimefurahia sana hii background analysis uliyofanya. Imenikumbusha ujanani kwangu ile miaka ya sabini kabla ya maisha magumu yaliyofuata kuanzia mwaka 1979.

Mwishoni mwa miaka ya sabini zile bend kebekebe za Verkys zilipormoka ghafla huko Zaire ambapo kati ya wananmuziki wakuu walioondoka Zaire wakati huo ni pampja na Sam Mangwana aliyekwenda Kameron na Assosa aliyekuja Tanzania kujiunga na Mzee Makassy baada ya Lemmy kuhamana Makassy na kuwenda Songea kuongoza bendi ya Mzee Matimila. Hawa wanamuziki wawili pamoja na Nyboma ndio waliokuwa mwagiji wa nyimbo maarufu kama "Moni Afinda" na "Masua" ndiyo maana kwenye ule wimbo wa Moni Afinda Asosa anatajwa wazi wazi wakisema "Asosa mama." Asosa aliletwa Tanzania na Mzee Makassy alipoanzisha mtindo wake wa Agwaya. Leo hii ni zaidi ya miaka 30 tangu Assosa alipokuja Tanzania, je kuna aliyewahi kufuatilia kama jamaa huyu alikuja kihalali na anaishi nchini kihalali pia?
 
FMES

Hebu ngoja kidogo:

Hivi ni kweli Nyboma ndiye aliyeongoza Lipwa lipwa? Ninachofahamu ni kuwa Nyboma alikuwa anaongoza Orchestre Kamale, ambapo baada ya kuvurugana na Verckys kutokana na mapato ya wimbo wa Masua, ndipo akaanzisha bendi yake ya Les Kamale na wakati huo ndipo Assosa na Sam Mangwana walipoondoka Zaire. Wimbo mkali ninaoukumbuka kutokea Lipwa Lipwa ulikuwa ukiitwa Novelle Generation ambamo Verkcys alikuwa akidai kuwa ulikuwa ni mziki wa generation mpya kuachana na ule wa akina Lwambo. Nouvelle Generation ilitolewa mwaka 1974 na ailikuwa ngoma kali kwelikweli enzi hizo za Bumping; ilikuwa karibu Franko azirahi kwa kukosa oksijeni baada ya kunyang'awanya soko la muziki kabisa. Wakati Nouvelle Generation inatoka, Kamale nayo ilikuwa inatoa ngoma zake ingawa ule wa Masua na Moni Afinda zilitoka baadaye kwenye miaka ya 76 na 77 hivi.

Hebu FMES weka historia sahihi hapa kwa vile kumbukumbu yangu mie kwenye upande huo siyo nzuri tena.

NYONGEZA: Asosa alililetwa Tanzania na mzee Makassy kama nilivyoeleza hapo juu. Ninaamini kuwa Fuka Fuka ilikuwa ni bendi iliyoanziswa baada ya ile ya Kyauri Voice kuvunjika. Kyauri Voice nadhani ilikuwa inapiga mtindo wa kavasha pale Mpakani maeneo ya Silent Inn. Baada ya kuvunjika baadhi ya wanamziki wake walikwenda Kenya, Zambia na wengine kubaki Dar, wale waliobaki Dar ndio waliounda Fuka Fuka.
 
Vipi kuhusu huyu bwana aitwaye NGUASHI NTIMBO? Kuna wimbo aliimba uitwao Elongi ya Cherie. Mwanzo nilijua kuwa ameimba TPOK jazz, kumbe ni jamaa na wimbo ni wake na kwa hiyo hauko kwenye Album za TPOK jazz ao Luambo. Pia nasoma kuja kukuta pia aliimba na Super Mazembe wimbo wa Shauri yako. Nakumbuka wimbo wake ulitamba sana miaka ya 80 mwanzoni.

Manguta, ulikuwa ni wimbo alioupiga Ntimbo, kwa kweli sinao na nimejaribu sana kuutafuta lakini nimeshindwa kwa sababu aliyeupiga hakuwa big name hiyo hata kwenye store za kuhifadhi nyimbo hizo huko Paris na Brussells haupo, lakini ninaufahamu na kuukumbuka.
 
Back
Top Bottom