TANZIA Padri Baptist Mapunda afariki dunia kwa ajali ya gari

THE LOST

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,479
2,000
Capture.PNG
Wapendwa katika imani tumsifu Yesu kristo.

Father Baptist Mapunda wa Kanisa Katoliki Parokia ya bikra Maria Usagara Jimbo Kuu la Mwanza amefariki dunia katika ajali ya gari iliyotokea huko Usagara nje kidogo ya jiji la Mwanza. Fr Mapunda alifikwa na umauti huo tarehe 3 ya mwezi huu na mazishi yake yamefanyika leo katika parokia ya BUKUMBI jimbo kuu katoliki la Mwanza.

-----
Father Baptist Mapunda alizaliwa mwaka 1959 huko Mbinga na kujiunga na shirika la wamisionari wa Afrika mwaka 1986 alikula nadhiri ya kanisa mwaka 1990 huko London Uingereza na kuwa shemasi mwaka huohuo huko parokia ya Woodland Uingereza. Mwaka 1991 alipewa upadrisho na Askofu Emmanuel Mapunda huko Songea. Mwaka huo huo alianza huduma katika parokia ya Mansa nchini Zambia. Amelitumikia kanisa katika nchi za Zambia, Ghana, Kenya, Tanzania, Izrael na Uingereza.

Pia soma
 

Tomaa Mireni

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
1,873
2,000
Aliwahi kuhudumu Moshi? Kigango cha singachini kwa sasa parokia miaka ya 2000? Nahisi namjua
.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom