Wanajeshi, polisi watwangana risasi

Wanajeshi, polisi watwangana risasi

wew achaa ufalaaa mwenye jukumu la kulinda nchi ni jeshi na sii police. police vibaraka vya ccm au huoni.?
nawa pugweee tuu kama wakuu wao wanavyosemaaa

mdogo,jeshi limechafuka siku hz,naishia hapa
 
jamaa huwadharau sana polisi na kuwaita raia wakakamavu. nadhani walitaka kuonyeshana nani zaidi.
 
Hakuna mtu ninae mchukia kama polisi. Watu wanavyosema polisi wapigwe ni kwamba wameshataabishwa sana na hawa watesa raia mara nyingi.
 
Haya majeshi mawili nchini huwa hayapatani kabisa. Waliwahi kupigana tena pale igoma Mwanza.

Sidhani kama ni tatizo la haya majeshi mawili. Tatizo kubwa lililopo ni JWTZ. Hawa wanajiona wapo juu ya sheria na wanaweza kufanya chochote watakacho. Mara kadhaa na sehemu mbalimbali hapa Tanzania wamewapiga raia amabo ndiyo waliowapa hizo ajira.

Matendo haya hayakuanza leo. Kuna miaka ya huko nyuma, wakati wa Nyerere waliwahi kufanya vitendo kama hivyo lakini walisemwa sana kwa majuma kadhaa hasa kwenye kipindi cha RTD cha Mazungumzo Baada ya Habari. Baada ya hapo sikusikia tena wanajeshi wakipiga raia hadi siku za hivi karibuni.

Serikali inatakiwa ikaripie vitendo viovu vinavyofanywa na wanajeshi wa JWTZ. Ni aibu sana kwa nchi yetu. Sijui ni nchi gani ambako wanajeshi wana tabia kama za hawa JWTZ.
 
Huyu mwandishi wa habari na Dc wote waongo tu, wananchi walifurahia sana kitendo cha polisi kupigwa na JWTZ watatu na waliopiga risasi ni polisi sio wanajeshi bhana, kama wale madogo wangepata silaha ingekuwa mengine! na huu ni utovu wa nidhamu na uvutaji bhangi holela wa hawa vijana wetu wa vyombo vya usalama, siku hiyo polisi walituharasi sana na mabomu ya machozi hata tusiojua nini kinaendelea!!!
 
huyu mwandishi wa habari na dc wote waongo tu, wananchi walifurahia sana kitendo cha polisi kupigwa na jwtz watatu na waliopiga risasi ni polisi sio wanajeshi bhana, kama wale madogo wangepata silaha ingekuwa mengine! Na huu ni utovu wa nidhamu na uvutaji bhangi holela wa hawa vijana wetu wa vyombo vya usalama, siku hiyo polisi walituharasi sana na mabomu ya machozi hata tusiojua nini kinaendelea!!!

tumekuskia ila sio hivyo.
 
Hakuna aliye pewa mamlaka makubwa ktk nnch kama askari polisi ndio maana utamkuta anatembea na smg doria kila siku anayo na mnao sema polisi wamepigwa ni maneno tu muziki upo polisi ndio maana kila siku laia tuna lalamika polisi wana uwezo kibattle ndio jwtz wanaitana uwezo wa mmoja mmoja hawana mnaofaham mnaelewa hlo nadhan mmesoma vizuri post ya mtoa mada waliopigwa risasi ni jwtz 2 big up polisi tz kwa kazi nzuri kila mkoa wjeda wakipigwa waandishi wa habari et polisi ndio wamepigwa hakuna atakae weza piga pt n mm raia mwema mwenye kulipenda jesh la polisi tanzania
 

Meja%20Erick%20Komba-October3-2014.jpg

Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Erick Komba


Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na askari wa Jeshi la Polisi, wameshambuliana kwa silaha mbele ya raia na kusababisha baadhi ya maofisa waandamizi kujeruhiwa kwa risasi, baadhi yao vibaya.

Tukio hilo lilitokea juzi saa 11:00 jioni katika Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Tarime.

Waliojeruhiwa katika tukio hilo ni askari JWTZ, Aloyce Filbert (24), aliyepigwa risasi mguuni na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya, SSP Salum, aliyejeruhiwa kichwani pamoja askari kadhaa.

Askari wengine saba walijeruhiwa kwa kupigwa risasi mguuni na Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Tarime/Rorya (RCO), SSP Salum, alijeruhiwa kichwani huku askari kadhaa wa majeshi hayo wakijeruhiwa katika vurugu hizo ambazo zilisababisha maduka kufungwa na huduma kukwama.

Kutokana na tukio hilo, wananchi walilazimika kufunga maduka yao kwa muda na huduma muhimu kwa jamii kusitishwa kwa hofu ya kujeruhiwa au kuuawa kwa silaha za moto zilisohusika katika mapambano hayo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, Lazaro Mambosasa, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo kati ya Polisi na JWTZ wa Kikosi cha Nyandoto na kueleza kuwa Jeshi la Polisi linawashikilia askari wawili wa JWTZ kwa mahojiano.

"Tunakwenda kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama kuzungumzia masuala haya, taarifa kamili mtaipata baadaye ," alisema kamanda huyo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo ambao hawakutaka majina yao kutajwa gazetini, walisema chanzo ni askari wa JWTZ aliyejulikana kwa jina moja la Mkama ambaye alikuwa anaendesha pikipiki bila kuvaa kofia ngumu akiwa na wenzake, Alyoce Filbert na Deus Dominick, kukamatwa na askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani.

Walisema baada ya kukamatwa, askari wa JWTZ aliomba msamaha huku akionyesha kitambulisho cha kazi, lakini trafiki hao walikamata pikipiki yake huku Mkama naye akijaribu kuwazuia ndipo walipowaita polisi wengine kwa msaada zaidi.

Walisema Polisi walifika na magari mawili wakiongozwa RCO huku askari wa JWTZ nao wakiitana na kufikia zaidi ya 10, akiwamo mkubwa wao ambao walijaribu kusuluhisha kusitokee vurugu bila mafanikio.

"Wakati RCO na Mkuu wa askari wa JWTZ (ambaye hajafahamika kwa jina), wakizungumza mmoja wa askari wa JWTZ alimpiga kwa kitu RCO shavuni na kichwani na ndipo askari Polisi walipojibu mashambulizi kwa kurusha mabomu na risasi iliyompata Aloyce mguuni," alisema.

"Hali ilikuwa ngumu risasi zilirindima ovyo kila mmoja aliogopa na kujificha alikoweza ikiwamo kufunga biashara," alisema mwananchi huyo.

Aidha, walisema hali hiyo inashangaza kwa kuwa kazi za vyombo hivyo zinafanana na kwamba vyote ni vyombo vya usalama vinavyotegemewa na raia katika ulinzi.

Mwenyekiti wa Chama Cha MAapinduzi (CCM) Wilaya ya Rorya, Samwel Kiboye, alilaani tukio hilo na kusema ni la kushangaza kwani kila chombo kina majukumu yake ya kisheria kimoja kulinda mipaka ya Tanzania na kingine usalama wa raia na mali zake.

Alisema ni vyema wangezungumza na kumaliza badala ya kutumia jazba kwani wanaiharibu taswira ya JWTZ na Jeshi la Polisi kwa kushambuliana na kujeruhiana hadharani kwa kutumia silaha za moto.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya Tarime, Dk. Benard Makonyu, alithibitisha kupokea majeruhi Filbert na Dominic wakiwa na majeraha waliyoyapata katika vurugu hizo.

Alisema Polisi waliodaiwa kujeruhiwa na kupatiwa matibabu na kuondoka ni Ally Guma (26), Makoye Kitula (25), Sylivester Michael (31), Abdallah Khalid, Over Msabita na Deo Tryphone.

NIPASHE ilimtafuta Msemaji wa JWTZ, Luteni Kanali Erick Komba, kueleza kuhusiana na tukio hilo ambapo alisema yuko mkoani Shinyanga na kumwelekeza mwandishi kuwasiliana na msaidizi wake, Meja Masanja, ambaye naye alidai yupo kwenye foleni kuelekea Lugalo, jijini Dar es Saalam.

Meja Masanja alisema asingeweza kuzungumza kwa kuwa alikuwa anaendesha gari na kutaka atafutwe baadaye.

Hata hivyo, hadi tunakwenda mitamboni Meja Masanja hakupatikana.




Source: Nipashe

http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=72793

Hii hatari aisei CC: kadoda11 Geza Ulole Bulldog Askari Kanzu
 
anachosema Mantombazane kina logic ni mara nyingi TPDF imehusika na ukiukwaji wa sheria na hasa haki za binadam kwa kupigapiga raia bila sababu na kuwashambulia polisi(polisi wa usalama barabarani) rejea tukio la ubungo si mara moja,kwani sisi raia hatuna haraka??walishamtwanga traffic pale,ila kuvamia mitaani na kupiga raia si mara moja mdau lutamyo ni mara nyingi sana,wiki 2 zilizopita hapahapa jamvini iliripotiwa kuwa JWTZ wanajesh wake wamewapiga vijana keko ambao walikuwa wakihisiwa kuiba simu ya sh 25,000/= ajabu sasa huyo aloibiwa wala si mwanajeshi,hawakuishia hapo wanajesh wale waliwanywesha maji machafu wale vijana,uhasama kati ya raia na wanajesh upo sana kama ulivyo kati ya askari wa wanyama pori na wakaz wanaokaa pembezon wa hifadh za taifa.
Wanajesh si malaika usiwasifie kiasi hiko wapo micharuko,wapo wengi sana Mwamunyange alivalie njuga hili,
ila mwisho nasapot POLISI KULAMBISHWA KICHAPO maana nadhan wanajesh wanatimiza kauli ya 'WAPIGWE TU' sikumbuk aloitamka hii kaul

ha ha umeeleza vizuri mwanzoni, ulivyomalizia umenichekesha bure
 
Last edited by a moderator:
Naomba msishabikie hii kama ni ukweli. Labda ni joke.
Vyombo hivi ni muhimu kwetu vikawa na heshima busara na uzalendo kwa hio kusikia
- mwanajeshi amevunja sheria hadi amekamatwa na polisi ni jambo la kufanyia kazi.

-au kusikia polisi wamekamata mwanajeshi bila hatia ni jambo baya pia
- kuwa jeshi JWTZ wanachukua hatua za kupiga individual police men Ni jambo la kutisha

Tuwaombee viongozi wote wenye dhamana ya maamuzi kwa level yoyote wapate busara uimara na ujasiri wa kutekeleza majukumu yao kizalendo
Kuna taarifa kuwa ni kweli walifanya kosa lakini polisi walianza kuwanyanyasa na kudhalilisha ndo wakaweka ngumu, baada ya wao kukataa udhalilishaji polisi wakaanza kuwapiga ndipo ugomvi ukaanza rasmi kwa wao kujibu mashambulizi. Je taratibu zinaruhusu polisi kudhalilisha watuhumiwa? Au hata kuwapiga?
 
Kuna taarifa kuwa ni kweli walifanya kosa lakini polisi walianza kuwanyanyasa na kudhalilisha ndo wakaweka ngumu, baada ya wao kukataa udhalilishaji polisi wakaanza kuwapiga ndipo ugomvi ukaanza rasmi kwa wao kujibu mashambulizi. Je taratibu zinaruhusu polisi kudhalilisha watuhumiwa? Au hata kuwapiga?

Hii naweza ielewa Polisi ni wepesi sana kudhalilisha na kupiga hii tabia wanayo haswa!!!
 
Back
Top Bottom