Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,055
- 79,399
WANAJESHI/ POLISI NA USALAMA WAFUNDISHWE UJASIRI WA KUPINGA DHULMA NA KUTETEA HAKI NDANI YA NCHI. HUO NDIO UJASIRI WA KWELI NA SIO VINGINEVYO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Moja ya sifa kuu za mwanajeshi na askari ni kuwa JASIRI na ili Mwanajeshi aitwe Jasiri lazima awe jasiri wa kupigania HAKI za Watu wa taifa lake.
Kuzuia na kupambana na maadui wa ndani na nje ya taifa lake wanaotaka kuharibu Haki za watu wake.
Kupigana na kupinga uonevu, dhulma ndani ya nchi.
Uanajeshi ni kulinda usalama. Kuwa mlinzi wa watu wako na nchi yako.
Na ulinzi na usalama ni kuhakikisha Haki ipo ndani ya jamii yako na kuitetea ili wananchi wako(wakiwemo viongozi na wewe mwenyewe muweze kuishi kwa Amani).
Huwezi kujiita Mwanajeshi au Askari alafu mtaani unapoishi kuna watu wanaonewa na kudhulumiwa alafu wewe huna ujasiri wa kupigania haki zao. Wewe sio mwanajeshi wala huna vigezo vya kuwa Mwanajeshi wala Askari
Mwanajeshi ni kuwa na nidhamu kwa oda au amri za HAKI. Sio uendeshwe kama Roboti. Kwamba kila kitu ukiambiwa useme ndio Mkuu hata kama amri ya kishenzi au ya dhulma. Huo ni woga.
Hakunaga mtu jasiri wa ndio Mkuu kwa kila kitu. Huyo mtu hayupo. Ujasiri ni pamoja na kupinga oda na amri za kijinga na kipuuzi bila kujali anayesema ni nani.
Mwanajeshi huheshimu watu kwa vyeo lakini hufuata amri za haki.
Ukiona huna uwezo wa kumkatalia kiongozi wako akikuagiza jambo baya ujue hukufuzu mafunzo. Wewe sio mwanajeshi na haupo kundi la watu jasiri.
Mwanajeshi sio kibaraka
Mwanajeshi sio Mbwa kwamba akiambiwa shii kamata anakamata hata kama amri hiyo ni haramu.
Mwanajeshi sio roboti kwamba umesetiwa kama yale maroboti ya Elon Musk.
Sasa kama unafuata chochote unakosa vigezo vya kuitwa mwanajeshi.
Wewe ni Coward, Mwoga.
Watawala waovu wengi wameweka mfumo kuwa mwanajeshi ni mbwa wa kufuata kila kitu jambo ambalo kiuhalisia sio kweli.
Mwanajeshi asiyefuata Haki na anayefuata hata amri haramu ni mwoga na mara nyingi hudharauliwa na kutumika kama risasi tuu. Ikishatofyatuka hakuna mwenye habari nayo.
Kijana, unapofikiri kuwa mwanajeshi lazima kitu cha kwanza ufikirie HAKI.
Kwa sababu upo kwaajili ya kupambana na maadui wa watu wako ambao hawatendi HAKI bila kujali nafasi zao.
Jeshi likiwa na haki automatically hakuna mwanasiasa atakayeleta michezo ya kijingajinga, dhulma itapungua kwa kiasi kikubwa.
Na wananchi watakuwa Safe.
Ukiona wanasiasa wanamatatizo, mafisadi au wanafanya matendo ya kihalifu lazima ujue kuna tatizo kubwa katika mfumo wa jeshi, askari, usalama, polisi.
Kwa sababu hao ndio kimbilio na egemeo la wanasiasa.
Hakuna mwanasiasa au mtu atakayeweza kutawala bila kuwa na jeshi/dola.
Hivyo mtu anavyotawala iwe kwa ubaya au kwa wema lazima kuna baraka za jeshi.
Kufikia hapa sina la ziada.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam