Thread ya kuisusa VodaCom ilishaanzishwa humu siku za nyuma. Tukaijadili mpaka basi. Tusipande pia ndege za PrecisionAir, kuna akina Mramba humo. Mafisadi wamejenga hadi misikiti na makanisa, tusisali humo. Kuna mashule yamejengwa na mafisadi, tuwatoe watoto wetu huko. Rais tulienae kachangiwa sana na mafisadi kwenye kampeni zake 2005, tumkatae, tumwondoe, tumng'oe?
sawa kabisa,hatuwezi kupinga mafisadi wakati tunakula nao.Tukae pembeni tufichue njama zao.Ili tufike huko lazima tuanzie harakati zetu mahali fulani hasa pale palipo dhahiri kama...
Du! sasa tufanye nini? Tuache kupiga simu?Makampuni ya simu Tanzania na ufisadi wake:
(a). VodaCom- Kuna RA (share holder 35 %), Somaiya (Shivacom -super dealer ), Lowasa - Alphatel (dealer)
(b). Zain (wameifisadi TTCL hadi ikabinafsishwa kwa bei chee na wameingia TZ kwa wizi na utapeli mkubwa)
(c). Tigo (wamekuwa wakibadili majina kila baada ya miaka 5 kukwepa kodi: 2001 from Mobitel to Buzz, 2006 from Buzz to Tigo) na ukifuatilia tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993 ikishirikiana na shirika la posta na simu wakati huo mpaka sasa ime-undergo several dubious contracts na serikali. Mpaka sasa kampuni inamilikiwa na Millicom ya Luxemburg kwa asilimia 100 % kinyume na sheria za nchi
(d). TTCL - hii nayo imebinafsishwa kwa Wa-Kanada kifisadi kupita kawaida na bila shaka mafisadi wana share huko. Kwahiyo tunatupa simu zote na kufunga landline zetu zote tuwasiliane kwa internet na barua.
Nilikuwa Tunduma pale nilishangaa watu wanajiproud kwa kutumia Voda huku wakinishangaa mm nae tumia tiGo dah kwakweli watu akili zao hazifanyi kazi kabisaa wametekwa kama si kuzama kabisa.
Mtu anajiona ufahari kutumia pesa nyingi kwenye line ya voda na anasema huu ndo mtandao wa sisi wenye pesa maskini mtaendelea kutumia tigo.
Miafrika jamani bado sana.
voda ni ya wenye uwezo kama mimi,
kama huwezi gharama nenda tigo,
Mkuu Edson tutashukuru sana kama utatuchangia huo uwezo wako na hapa JF......we seriously need your unconditional contributions here to make JF online indefinately!
usiniharibie hamu ya kiti moto hapa kona bar!!!
mweeee
Heee....na huko Norway kuna KONA BAR? au mkuu umeshamaliza ile kozi yako kule?
Mwanakijiji amwambie bosi wake Mengi apige marufuku vyombo vyake vya habari kutoa matangazo ya Vodacom kwanza. Ukimalize hilo weka tundiko la kususia Precision air kwa kuwa Mramba ana hisa na ni fisadi.
Bila kusahau wasafiri wote wa ndege watumie Jomo Kenyata airport halafu waje kwa bus kwa kuwa uwanja wetu wa ndege unatumia rada ya mafisadi. Tususie noti za benki kuu kwani huko ndio asili ya ufisadi mkubwa
Pia usisahau kuhamasisha wananchi wasitumie umeme wa IPTL, Dowans, Songas, Kiwira (kama upo ) nk
it is too late now but not too late enough.. Kama uko kwenye mapambano dhidi ya ufisadi na hauko tayari kusalimu amri, nakushauri kuachilia namba za simu za vodacom asap. As a matter of fact, hamia "kwingine" within the next 72 hours (beginning monday). Do it or be ready to live with the consequences.
Nilikuwepo.
M.m.
hii ni habari?vitisho?mkwara? Wewe kama mwandishi wa siku nyingi wa kijarida na majarida kwa nini usieleze kitu kikaeleweka hata kwa sentence 1 kuliko kutoa vitisho na kuacha habari ina ning'inia itatufanya tuamini hata habari nyingine ni kwa 'bora siku iende'/kusukuma siku mbele au kuchangamsha genge na habari kama hizi ni sensitive sana.
Mwanakijiji kawatahadharisha wanaharakati wa KWELI, wanaofahamika kwa kauli na matendo yao kuhusu ufisadi. Sio sisi tunaopinga ufisadi kwa majina bandia!
SMU,Wildcard,
Kwa nini unadhani JF hakuna wanaharakati wa kweli?
Kuna mbinu nyingi za kupigana vita, si lazima wote tushike bunduki na kwenda mstari wa mbele! Wengine kazi yao inaweza kuwa ni kupeleleza uwezo wa adui na mambo anayokusudia kufanya na si kushambulia!
Masatu nafikiri hapa umekosena kidogo kwa kauli zako zidi ya mwana kijiji, inadhihirisha kuwa wewe ni mtu mmoja wapo moga sana,huyu jamaa ametumia haki yake ya kutowa maoni yake haina mana kwamba kila mtu atakubaliana nae au atapingana nae, mwache ale hoja zake na watu wazipime.Umenifanya niwaze mambo fulani likiwemo hili la hii Blog isije ikawa wazamini wake ni miongoni mwa hao wanaoogopewa ? (I hope I m wrong)hapa kwetu wazee wetu hutwambia (Mficha Uchi Hazai )sasa kama watu wafumbie macho maovu kweli tutafika ?