Wanaharakati wa Italia waiandikia barua kamusi kubadilisha kisawe cha neno 'mwanamke'

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Zaidi ya watu 100 wamesaini barua kuitaka Kamusi ya Mtandaoni nchini Italia, Treccani kubadilisha kisawe cha neno mwanamke katika kamusi yake.

Kampeni hiyo inalenga kuondoa neno 'puttana' kama kisawe cha neno 'mwanamke' ambalo linatafsiriwa kama 'kahaba' wakidai kuwa linamfanya mwanamke kuonekana kama chombo na kumfanya dhaifu.

Kampeni inayofanana na hii iliwahi kuifanya Kamusi ya Kiingereza ya Oxford kuondoa visawe vya neno 'mwanamke' kutoka kutumia maneno 'bint' au 'bird' kumaanisha 'mwali' au 'mwanamke anayevutia' baada ya kampeni ya mtandaoni kukusanya sahihi zaidi ya elfu kumi kuitaka Kamusi hiyo kutoa visawe hivyo hasi.

Mwanaharakati aliyefanikisha kampeni hiyo kwa Kamusi ya Oxford, Maria Beatrice Giovanardi anasema maneno yanayomtambulishwa mwanamke hutumia maana hasi ukilinganisha na yale yanayomtambulisha mwanaume, mfano 'mfanyabiashara.'

"Lugha inajenga uhalisia na kushawishi jinsi wanawake wanavyoonekana na kuchukuliwa katika jamii," aliandika katika barua yake.

Kamusi hiyo haijatoa majibu kuhusu malalamiko ya kampeni za wanaharakati hao, lakini iliwahi kuandika katika chapisho la blogu mwezi Novemba mwaka jana kuwa haiangalii maadili inapochagua misamiati ya kuweka katika kamusi yake.

"Ikiwa jamii na tamaduni zitaonesha hali hasi kupitia maneno, kamusi haiwezi kuacha kuhifadhi maneno hayo," chapisho hilo lilisomeka.
 
Hapa kwetu tubadili neno TANZIA linatuharibia jina la nchi yetu. Halafu ^Pombe^ (kilevi haramu) itafutiwe jina lingine, ili Rais wetu asibughudhiwe. Au nasema uongo ndugu zangu!?
 
Hapa kwetu tubadili neno TANZIA linatuharibia jina la nchi yetu. Halafu ^Pombe^ (kilevi haramu) itafutiwe jina lingine, ili Rais wetu asibughudhiwe. Au nasema uongo ndugu zangu!?
Ndiyo 🤣🤣🤣 maneno ya badilishe hayo mana baraza la kiswahili wakogo vizuri kutafuta maneno mtamu matamu ebu watupe mana nzuri ya Pombe
 
Back
Top Bottom