Wanafunzi wasichapwe, serikali mnafikiria nini

Wanafunzi wasichapwe, serikali mnafikiria nini

Kuna video clip moja niliiona ikimuonesha mtoto aliyekuwa akichekewa darasani kila siku na Mwalimu wake kila siku alikuwa anamchapa kiasi kwamba mtoto huyo akazowea akawa akifika anampa mkono Mwalimu amchape.

Kumbe nyuma ya pazia mtoto huyo alikuwa akimuuguza baba yake aliyekuwa hatembei kabisa mpaka siku moja ambapo yule Mwalimu alipomuona mtoto huyo akimuendesha Baba yake.

Mwalimu huyo alihuzunika sana.
Fimbo ni mbaya sana na hizina faida
 
Mtoto na Mwalimu wanatakiwa kuwa Marafiki na waheshimiane:
Wenzetu walio endelea Ulaya na America hawachapi watoto na wanaongoza kwa kuelimika:

Mtoto hajala nyumbani, katembea kwa mguu kwenda shuleni kilomita Tano au Tatu au moja, pesa ya kula mchana hana:
Anafika shuleni viboko kwa kuchelewa bila kumwuliza kwanini kachelewa:
Akiingia dalasani kila Mwalimu anatamani kumchapa viboko;

Ni wajinga pekee na masikini Wanaotaka kuchapa viboko watoto:
Mtoto ni wa kuongea naye na kumfanya kuwa rafiki ili akuelezee shida zake katika kila eneo:

Jinga kabisa
Kabisa. Madhara ya viboko ni makubwa sana kuliko inayoonekana kuwa ni faida!
 
Tatizo sio fimbo bali unaporuhusu kuchapa fimbo tatu basi wao wanapiga mpaka 20 kisa tu fimbo zinaruhusiwa
Kama shule singe kuwa zinawaita wazazi mara kwa mara na kujua yanayoendelea kwa mtoto basi wengi wangejirekebisha
 
Tatizo sio fimbo bali unaporuhusu kuchapa fimbo tatu basi wao wanapiga mpaka 20 kisa tu fimbo zinaruhusiwa
Kama shule singe kuwa zinawaita wazazi mara kwa mara na kujua yanayoendelea kwa mtoto basi wengi wangejirekebisha
Si jambo kutopiga fimbo lakini tatizo lipo kwa wachapaji walimu wako very stressed ndio maana ni naona ni sawa kwa sheria hii, nakumbuka niliwahi kuchapwa viboko bila idadi kwa kosa dogo ambalo nilistahiki kurekebishwa tu.
 
Si jambo kutopiga fimbo lakini tatizo lipo kwa wachapaji walimu wako very stressed ndio maana ni naona ni sawa kwa sheria hii, nakumbuka niliwahi kuchapwa viboko bila idadi kwa kosa dogo ambalo nilistahiki kurekebishwa tu.
Siku hizi hawachapi watukutu kama zamani bali hata ukipata 80% unakula fimbo za kutosha
Najiuliza hizo fimbo ni kwa ajili ya nini
Kwanza hata private nao wanapiga sana kisa ufaulu.

Kupiga sio kufundisha bali ni kuwaacha na matatizo ukubwani pia
Wazazi wanaopiga sana pia ni tatizo kubwa
Watoto wanahitaji kujifunza na sisi kama watu wazima ni lazima tuelewe hilo
Kuna watu wanapiga watoto kisa anacheza
Kuhusu kupigwa kweli tumechapwa lakini mengine ni kufundisha tu na hata kukaza uso inasaidia pia kuonyesha kuwa hujapenda

Watoto wafundishwe bila kuchapwa hii inampa mtoto confidence ya kuweza hata kuuliza maswali waalimu
Ukimpiga kila siku anaogopa hata kukuuliza swali je ni sawa mtoto asikuulize kitu kwa sababu anaogopa?
 
Mtoto na Mwalimu wanatakiwa kuwa Marafiki na waheshimiane:
Wenzetu walio endelea Ulaya na America hawachapi watoto na wanaongoza kwa kuelimika:

Mtoto hajala nyumbani, katembea kwa mguu kwenda shuleni kilomita Tano au Tatu au moja, pesa ya kula mchana hana:
Anafika shuleni viboko kwa kuchelewa bila kumwuliza kwanini kachelewa:
Akiingia dalasani kila Mwalimu anatamani kumchapa viboko;

Ni wajinga pekee na masikini Wanaotaka kuchapa viboko watoto:
Mtoto ni wa kuongea naye na kumfanya kuwa rafiki ili akuelezee shida zake katika kila eneo:

Jinga kabisa

Sijawahi kuelewa hawa watu wanaolinganisha maisha ya ulaya na huku kwetu.

Yaani mfumo wa elimu wa ulaya ndo tuulinganishe na mfumo wa elimu wa malawi? Una akili timamu?
 
Walio chapwa wenyewe wamebaki kuwa waoga, wanafiki na ndio ndio, huku wakisiginwa haki, uhuru na usawa wao, hawana cha kufanya, hizo Fimbo ndio zimewafanya wawe hivyo.
Lol
 
Mwalimu anakuja shule na stress zake za kunyimwa unyumba au ugomvi na mumewe hasira zinaishia kwa mwanafunz
 
KUZUIWA KWA ADHABU YA VIBOKO KWA WATOTO SIO MWISHO WA NIDHAMU/MWANZO WA KUBOMOKA MAADILI

Uko sahihi kabisa, na mtazamo wako unaakisi mbinu za kisasa na salama za malezi ambazo kitaalamu zinathibitishwa kuwa na matokeo mazuri na ya muda mrefu kuliko vipigo. Malezi bora hayajengwi juu ya woga wa viboko, bali yanajengwi juu ya uelewa, nidhamu ya ndani, na msingi imara wa maadili.
Zifuatazo ni mbinu mbadala ulizozitaja na jinsi zinavyofanya kazi kwa ufanisi mkubwa kumjenga mtoto bila kumuumiza kimwili au kisaikolojia:

1. Matumizi ya "Positive na Negative Reinforcement" (Kuimarisha Tabia)

Kama ulivyofafanua, nadharia ya saikolojia ya tabia inaonyesha kuwa mtoto anajifunza haraka zaidi kupitia matokeo ya vitendo vyake:
• Positive Reinforcement (Kichocheo Chanya): Kumpongeza, kumzawadia, au kumpa kipaumbele mtoto anapofanya vizuri. Hii inamfanya atake kurudia tabia hiyo njema ili apate furaha hiyo tena.
• Negative Reinforcement / Punishment kwa mtindo wa kunyimwa (Withdrawal): Mtoto anapokosea, badala ya kumpiga, unamnyima kitu anachokipenda (kama muda wa kuangalia katuni, kucheza na marafiki, au zawadi fulani). Hii inamfundisha kuwa tabia mbaya ina gharama, na inamfanya afikirie kabla ya kurudia.

2. Kuzungumza na Mtoto (Communication & Dialogue)

Watoto wana uwezo mkubwa wa kuelewa kuliko watu wengi wanavyofikiri.
• Kukaa chini na mtoto na kumueleza kwa nini jambo alilofanya ni baya na jinsi gani linawaumiza wengine au kumdhuru yeye mwenyewe, kunajenga uwezo wake wa kufikiri (reasoning).
• Viboko mara nyingi huzima kelele kwa muda lakini havibadili nia ya mtoto; viondoshwapo, mtoto anaweza kurudia kosa kwa siri. Mazungumzo yanajenga dhamiri (conscience) safi ndani yake.

3. Madhara ya Kipigo cha Kimwili (Corporal Punishment)

Umesema kweli kabla kwamba wazazi wengi huzidisha kiwango kwa sababu wanapiga wakiwa na hasira. Kitaalamu, adhabu za mwilini zinasababisha:
• Kuharibu uhusiano: Mtoto anaanza kumuogopa mzazi badala ya kumheshimu na kumpenda.
• Kujenga ukatili: Mtoto anayezoea kupigwa hujifunza kuwa nguvu na mabavu ndiyo njia ya kutatua matatizo, hivyo anaweza kuwa mkorofi kwa watoto wenzake au shuleni.
• Msongo wa mawazo (Stress): Inaweza kushusha tutajiri yake (self-esteem) na kumfanya ajione hana thamani.

4. Msingi wa Kiroho na Maadili (Mfundishe Mtoto Njia ya Bwana)

Msisitizo wako juu ya Mithali 22:6 ni nguzo kuu. Kumkuza mtoto katika kumjua Mungu kunampa "dira ya ndani" (internal compass).
• Mtoto anapomjua Mungu na kuwa na hofu ya Mungu, atafanya yaliyo sahihi hata wakati wazazi au walimu hawamwoni.
• Kuhusu maandiko yanayotaja "fimbo", wachambuzi wengi wa sasa wa maandiko na wanasaikolojia wa Kikristo wanaeleza kuwa "fimbo" katika muktadha wa kichungaji ilikuwa ni alama ya uongozi, mwongozo, na ulinzi (kama fimbo ya mchungaji mwema), na si chombo cha kumuumiza au kumtesa kondoo.
Hitimisho: Ukatazwaji wa viboko si mwisho wa nidhamu, bali ni mwanzo wa malezi yenye akili, upendo, na utu. Wazazi hawajapokwa uwezo wa kunyoosha tabia za watoto wao, bali wamepewa changamoto ya kutumia mbinu za kiungwana na zenye matokeo endelevu.
 
Back
Top Bottom