Wanafunzi kulipa Tsh. Milioni 4.8 kwenda China na Air Tanzania

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), imepunguza gharama za safari zao za ndege kwa wanafunzi wanaosafiri kutoka Tanzania kwenda China kutoka Dola za Marekani 3800 hadi Dola za Marekani 2100.

Akizungumza leo, Balozi wa Tanzania nchini China, Mbelwa Kairuki, amesema mpaka sasa gharama za safari za ndege kweda nchini humo ni kati ya dola za kimarekani 3800 mpaka 6500.

Balozi Kairuki amesema uamuzi wa ATCL umekuja kufuatia malalamiko mengi yaliyotolewa na wanafunzi, waliosema kuwa hawawezi kumudu gharama za usafiri.

“Wanafunzi wengi wameuelezea ubalozi kwamba hawataweza kumudu gharama za sasa za usafiri, na kweli hizi gharama zipo juu na kwakweli nyingine zinazidi hata gharama za kulipa ada ya shule.

“Kilio hiki tumekifikisha kwa mamlaka mbalimbali za hapa China na nyumbani,” Balozi Kairuki alisema.

Pia alisema bei hizo mpya zitajumuisha gharama zingine muhimu, kama vile gharama za kukaa kwenye karantini nchini Tanzania kabla ya safari na gharama za vipimo vya Uviko-19.

Akitoa ufafanuzi, Balozi huyo alisema, wanafunzi ambao tayari wameanza masomo watatakiwa kuonyesha ushahidi kwamba wanayo visa ya china na wanacho kitambulisho cha chuo.

Amesema kwa wanafunzi wapya watatakiwa kuonesha viza ya China na barua ya usaili au cheti cha kuwaruhusu kuingia nchini humo.
 
Ni kwaajili ya kuwafurahisha wanafunzi, kutoa tu huduma, kutafuta kura za wanyonge au ina faida kibiashara?
 
Back
Top Bottom