Wanafunzi hawa waliopata zero wanaenda wap?

Wanafunzi hawa waliopata zero wanaenda wap?

Division 4 ni 0 pia

Hao ndo madada poa

Ndo wadangaji

Ndo machinga

Ndo boda boda

Ndo wapiga debe

Ndo wafanya biashara
akili yako ndo inavyokuaminisha kuwa failure wote wanafanya hizi kazi?? Vipi akawepo mwenye degree zake anayefanya ubodaboda??
 
Kabisaa. Kuna mtu unakutana naye kwenye harakati, akakusimulia kiwango chake cha elimu hadi unamuuliza 'Na hapa unafanyaje sasa?' kwa nini uko hapa? 😢
Hao ni kati ya wale waliokuwa na matazamio (ambitious) kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wao na hawakukubaliana na Ukweli kwamba maisha sio lelemama (sio mtelezo)au sio matamu kama pipi. Ndo hao wanapata msongo wa mawazo (stress) akingali ni kijana mdogo (kiumri) hajaoa na hana maono(Vision). Ukimwuliza unataka uwe nani katika Jamii, utamsikia anabwatuka "nataka niwe kama Lissu" Hahahaaa. halafu nijenge bonge la nyumba huko Bunju.....
 
Maisha ni fomula sio Division na Kupata ziro sio kuwa na ziro maishani.
Unaweza ukawa na 1 mtaani ukaliftiwa na 0.

Akili mkichwa, division 0 ana alternative!

Wote wakifaulu mjini tutakosa mboga.
Ukitaka mambo yaende fanya kazi na ambaye hajasoma, kwani
wasomi wengi akili yao imelala, ni wavivu wa kujitoa.
Mkuu umeongea point, Ujue watanzania wengi bado tunaamini Div 1 ni tikite ya mtu kufanikiwa kwenye maisha, yaani ameisha toboa maisha,
 
Kupata zero maana yake yeye ameshindwa kukariri vitu ya darasani na sio kuelewa, kwa sababu bata hao wa Div 1 ukimuweka leo mtaani hawezi ishi kabisa
Ataendesha Bodaboda au Bolt na Uber na maisha yatasogea ila tu tunaongeza idadi ya Mavijana majinga na ya hovyo mtaani
 
safari hii NECTA wamefanya vizuri sana tena sana kuacha mchezo wa kutangaza shule bora na mwanafunzi bora.
hakika huu ulikuwa ni ujinga, wenye shule ambao waalikuwa wanategemea promotion ya kutangazwa wamepigwa butwaaa.
Sema wamechelewa sana aisee ila bonge la Idea, Mitihani isha geuka kuwa Biashara,
 
Kuna Boda Wana diploma..
Kuna wadangaji Wana masters na PhD...
Tembea uone
Diploma au Degree mkuu? Mimu kuba nibao wajua wamemaliza Chuo kikuu na ni Boda boda, ujue watu hatutaku kuamini kwba nyakati zimechange sana hilo watu hawataki kuamini
 
Kwa hio wa Div 1 watakuja kuajiriwa na nani? Serikali? Huwa hatutakua kuukubali ukweli kwamba kwa sasa nyakati zimechange sana, mtaani kuna Graduate wasio kuwa na idadi, hizi mentality za kukariri kwamba ufaulu mzuri ni tiketi ya maisha mazuri ni za kizamani sana, Time will tell
Kweli kabisa mkuu. Ufaulu mzuri ulitakiwa uchukuliwe kama ni kielelezo tu cha uwezo wa kiakili au Maarifa na ni mtu anayeweza kujiongeza fasta endapo atapatiwa Fursa. I stand to be corrected.
 
Diploma au Degree mkuu? Mimu kuba nibao wajua wamemaliza Chuo kikuu na ni Boda boda, ujue watu hatutaku kuamini kwba nyakati zimechange sana hilo watu hawataki kuamini
Lazima degrees wapo wengi..nawajua watu wenye masters hawana ajira
 
Anazungumzia Scholarship...! Kwahiyo una Verification badge ila mambo kama haya huyajui na huyaelewi pia?!
Hahaaa wangapi wanapata hizi Scholar ship? Unaweza kuta ni 1% tu, hata hio 1 inaweza isitimie, Kufeli Sio kwamba ndio kufeli life hilo eleweni hivyo, kafeli mitihani ya Formal education, ila hajafeli informal education
 
akili yako ndo inavyokuaminisha kuwa failure wote wanafanya hizi kazi?? Vipi akawepo mwenye degree zake anayefanya ubodaboda??
Bodaboda wenye degree wapo wengi tu mkuu. Sio wa kutafuta.
 
Kumbe wenye zero ndio wanaajirigi wenye one, basi sawa.
Hujamuelewa enzi za kuajiriwa zisha isha mkuu kwa sasa ni retrechment za kufa mtu huko Duniani, ajira zinaenda zinaisha kama sio kupungua.

na hao wa Div 0 kwani ndio wamefeli life sasa wanangoja kuzikwa?
 
Sema wamechelewa sana aisee ila bonge la Idea, Mitihani isha geuka kuwa Biashara,
awamu ya 6 inatumia akili kubwa sana, hawakurupiki, naamini kila kitu kitawekwa sawa. japo tulichelewa lakini sio mbaya.

Kongole kwa Waziri wa Elimu Prof. Mkenda hakika anaitendea haki hii wizara, angalau sasa tuna matumaini kuhusu elimu yetu kuwa itaboreka zaidi.
 
awamu ya 6 inatumia akili kubwa sana, hawakurupiki, naamini kila kitu kitawekwa sawa. japo tulichelewa lakini sio mbaya.

Kongole kwa Eaziri wa Elimu Prof. Mkenda hakika anaitendea haki hii wizara, angalau sasa tuna matumaini kuhusu elimu yetu.
Ujue shule nyingi zilikuwa zinatumia haya matokeo kama Biashara za kuvuta wanafunzu na kuwahzia fomu wazazi kwa sh 50, 000/ hapo fomu zinatolewa 4000 huku wao wakihitahi wanafunzi 150 pekee
 
Back
Top Bottom