Wanadamu na maisha ya kindoa - kwanini wanyama hawana licha ya mifanano mingi?

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722
Wote wanasifa zifuatazo:
Mwanaume/dume kusababisha mimba/mtoto
Wote hutamani kingono
wote wana wivu wa kimapenzi
wote huandaa ujio wa watoto
wote hulea watoto wao ( hutafuta rizki, hulinda kwa kushirikiana)

Licha ya yote haya, kwanini wanyama hawana maisha ya kindoa?
Kwanini binadamu kaumbiwa maisha ya kindoa?

Nifahamisheni
 
Licha ya yote haya, kwanini wanyama hawana maisha ya kindoa?
Kwanini binadamu kaumbiwa maisha ya kindoa?

Nifahamisheni

Unless umewahi kuwa mnyama na kuishi maisha ya kinyama kama mnyama ndo unaweza kusema kwa uhakika kuwa wanyama hawaishi kindoa au la!

Zaidi ya hapo itakuwa ni speculation zinazotokana na labda observation ambazo na zenyewe zinaweza zisiwe sahihi. Au wewe ulitaka uone mbwa nao wanavaa tuxedo na shela (shera?) na wanaenda mbele ya mbwa mwingine kufunga ndoa ndo uamini kuwa na wao wanaishi maisha ya kindoa?

Manake huwezi jua, huenda na wao kivyao kivyao na katika dunia yao wanaishi maisha ya kindoa ya kivyao halafu na wao wakawa wanatushangaa sisi kwa nini hatuishi kama wao na kufanya mambo kama wao.
 
NN,
Nimeuliza swali hili baada ya kusikiliza kipindi cha mawaidha leo Ijumaa nikaguswa japo sijapata majibu kamili.
 
Kupata majibu kamili itakuwa vigumu unless waje watu humu ambao wamewahi kuwa mbwa wafunguke.

Aliyekuwa anahutubia aliishia kuonyesha ni kwa vipi wanyama wao huendelea kutamaniana na kuzaliana bila mipaka, kwamba kwa wanyama,mzazi aweza kuzaa na mtoto wakati kwa binadamu kuna mipaka baina ya kuingiliana wazazi na watoto ( japo hili hufanyika ni kinyume na sheria/dini), pia akaendelea kuonyesha kuwa wanadamu wao wamevuka mipaka kwa kuanza kutamaniana watu wa jinsi moja. Ila sikuona akionyesha ni vipi ndoa za binadamu zinazuia mabaya haya.Nikafikiria pengine angelenga kuonyesha utashi wa binadamu ambao wanyama wamekosa, kama ndilo chimbuko la utaratibu wa kuwepo na ndoa ili kuwa na "mfumo" wenye utaratibu wa claim over rights, responsibilities etc kwa maana mtoto wa binadamu unlike wa mnyama huchukua muda mrefu sana kabla hajaweza kujitegemea.Mnyama kama twiga, swala etc huzaliwa na baada ya dakika chache huanza kukimbia ili kujilinda dhidi ya kuliwa ( survival of the fittest). Wanyama wanaishi katika utaratibu wa survival of the fittest, na inapotokea kasheshe hata kuuana hakuna kesi.Ndio mwisho.Kwa binadamu hapo kuna kazi.Ukiingilia mke wa mtu hata sheria itakubana maana wako tayari kwenye mfumo....
 
Back
Top Bottom