Elections 2010 Wanachama 16 wa CCM waliomnyima JK kura

PayGod

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
1,259
57
Nawapongeza wanachama 16, wa CCM waliopiga kura ya HAPANA,kwa JK wameonyesha ukomavu wa kisiasa, hiyo ndio demokrasia.
 
Ningekuwa mwana CCM nikawa katika kundi hilo lililokuwa Dodoma idadi ingekuwa 17. Jamaa tunawahitaji maana hawakukubali kuimbishwa mapambio wakaangalia performance ya candidate. Safi sana japo ni wachache sana. Unaweza kukuta yumo Shein, Bilal na Nahodha pia humu
 
Demokrasia ya style hii imebana kidogo, ingekuwa kama ya Z'bar, yaani wagombea zaidi ya mmoja hao ndani ya 99.16% wangempa mtu mwingine! Kwani kwa Z'bar Sheni amepita kwa karibu 54%!!! Hii ya kuwa mgombea peke yake yawezekana ni mbinu ya kuwaadaa watanzania wafuata upepo ili wafikiri kuwa JK ni muhimu sana na anakubalika sana hivyo wamchague!
 
Nawapongeza wanachama 16, wa CCM waliopiga kura ya HAPANA,kwa JK wameonyesha ukomavu wa kisiasa, hiyo ndio demokrasia.
Vipi na wale waliopiga kura ya NDIO uwapongezi kwa kutumia haki yao vema!?
 
Demokrasia ya style hii imebana kidogo, ingekuwa kama ya Z'bar, yaani wagombea zaidi ya mmoja hao ndani ya 99.16% wangempa mtu mwingine! Kwani kwa Z'bar Sheni amepita kwa karibu 54%!!! Hii ya kuwa mgombea peke yake yawezekana ni mbinu ya kuwaadaa watanzania wafuata upepo ili wafikiri kuwa JK ni muhimu sana na anakubalika sana hivyo wamchague!

Ni muhimu kutambua kuwa hiyo 99% aliyopata Kikwete ni toka "biased" sample ya wanaccm 2000!! Population ya Bongo ni zaidi ya watu milloni 40; na zaidi ya millioni 20 ni wenye umri wa kupiga kura ingawa wengi hawakujiandikisha.
 
Ningekuwa mwana CCM nikawa katika kundi hilo lililokuwa Dodoma idadi ingekuwa 17. Jamaa tunawahitaji maana hawakukubali kuimbishwa mapambio wakaangalia performance ya candidate. Safi sana japo ni wachache sana. Unaweza kukuta yumo Shein, Bilal na Nahodha pia humu
Bila shaka na mtoto wa mkulima na EL wamo ndani
 
Listi ya hao wanachama 16 hii hapa....

1. Edward Ngoyai Lowassa
2.
3.
4.
5.
 
Yeye mwenyewe vipi anajikubali lakini...................? Sometimes unasifiwa lakini we mwenyewe unaona wanazidisha chumvi
 
CCM hakuna democracy kwa wakati huu wa vyama vingi. Kwanza mambo ya kupitisha jina moja yamepitwa na wakati, pili mambo ya kusubiri ati kamati kuu kutangaza na kubariki ushindi kutoka mikoani kwa watakaogombea ubunge vile vile sio democracy. CCM haiwezi kubadilika kwa sababu walioanzisha hili chama hawapo ni sawa na gari ambalo dreva wake amekufa kwenye usukani na abiria bado wanafikiria watafika kwenye safari yao - Nop! JK na genge lake la wahuni hawawezi kuliongoza hili gari wanajifanya tu wanaweza.
 
Hii habari haitusaidii. Mimi kwa kweli sioni maana yoyote kujadili habari hii. Hapa twahitaji kuzungumza mikakati ya maana ya kumuondoa huyu bwana anayeanza kututawala kwa vitisho. tuache kujadili habari za watu waliokuwa hawamtaki. Wao ni kama sisi tu na walikuwa na sababu ya kufanya hivyo. Hatuna haja ya kuwafahamu kwa majina. Walifanya vyema.
Tuwahamasishe watu kutopigia si kikwete tu kura bali hata kumpigia kura mwana sisi m ionekane ni uhaini.
 
Hiyo asilimia 99 ni wepesi katika kufikiri kwani JK yeye mwenyewe anajijua kuwa hawezi, atakuwa anawashangaa wanamwaminije kiasi hicho huku wakizingatia rekodi yake ya uongozi ya miaka mitano. Rekodi inaonyesha alikwama katika mambo mengi lakini wengi ndani ya chama wengi wanamwona anaweza, ni ajabu kutegemea aliyeshindwa kuleta mabadiliko yanayohitajika.

Waliompigia kura ya hapana naungana nao kuwa wameona ukweli kuhusu JK naomba wawaambukize na wengine wenye akili nyepesi.
 
Back
Top Bottom