Wana Momba wakataa uzushi wa Mbunge wao

DodomaTZ

Member
May 20, 2022
71
107
Waswahili walisema msafiri alikiri "mwenda pole hajikwai" alaa akijikwaa haanguki na kama akianguka kuumia kwake ni kidogo tu.

Usemi huu ni matokeo ya uzoefu wa safari ndefu ya maisha ya babu zetu walioishi miongo na Karne zilizopita nasi twauishi na kuakisi uzoefu wa maisha hayo kwakuwa hakuna jipya Chini ya Jua... YALIYOPO ndiyo YALIYOKUWAKO na ndiyo yatayokuwa.

Ni majira ya saa kumi jioni wana momba tuliposhangazwa kuona kauli ya Kiongozi wa CCM bungeni, aliepewa dhamana na Serikali ya CCM kubeza kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya CCM ndani ya Jimbo la Momba.

Hakika ni mshangao uliotulazimisha wana momba kuvunja ukimya na kuamua kuwaeleza watanzania kwa USHAHIDI jitihada kubwa zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na Serikali ya CCM ili KUMTUA msichana, binti na Mama ndoo kichwani.

Ni meeeeengi yamefanywa lakini leo ngoja tueleze haya machache ikiwa ni sehemu tu ya miradi iliyotekelezwa, inayotekelezwa na itakayotekelezwa ili kumsaidia mtanzania wa Momba kupata huduma bora ya Maji safi na salama

Mpaka sasa Jumla ya Miradi 20 yenye thamani ya Bilioni 7,105,120,491.47 imetekelezwa na kukamilishwa na Serikali ya CCM chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na kuwanufaisha zaidi ya wananchi 150,000 wa jimbo la Momba. Miradi hiyo ni kama ifuatavyo 👇

1. Mradi wa Maji Kamsamba
Kamsamba wenye Thamani ya Tshs 256,000,000.00

2. Mradi wa Maji Mkonko wa Tshs 46,890,000.00

3. Mradi wa Maji Mpapa, Masanyinta na Kasanu wa Tshs 1,235,000,000.00

4. Mradi wa Maji Itumbula wa Tshs 456,000,000.00

5. Mradi wa Maji Mkomba wa Tshs 450,559,000.00

6. Mradi wa Maji Mbao wa Tshs 211,000,000.00

7. Mradi wa Maji Tindingoma, wa Tshs 593,170,973.00

8. Mradi wa Maji Chitete na Nkala wa Tshs 508,247,154.00

9. Mradi wa Maji Mnyuzi wa Tshs 345,000,000.00

10. Mradi wa Maji Chilulumo wa Tshs 546,700,000.00

11. Mradi wa Maji Mkulwe wa Tshs 126,865,340.00

12. Mradi wa Maji Itelefya wa Tshs 348,757,051.47

13. Mradi wa MajiNamtambalala wa Tshs 387,987,000.00

14. Mradi wa Maji Namsinde II wa Tshs 110,565,733.00

15. Mradi wa Maji Ikana wa Tshs 65,000,000.00

16. Mradi wa Maji Ndalambo Tshs 345,833,830.00

17. Mradi wa Maji Chiwanda Tshs 240,000,000.00

18. Mradi wa Maji Iyendwe wa Tshs 376,000,000.00

19. Mradi wa Maji Kasinde wa Tshs 55,091,000.00

20. Mradi wa Maji Nkangamo wa Tshs 400,453,410.00

Aidha, ipo miradi iliyotekelezwa baada ya Ziara ya Aweso Jimbo la Momba Mwezi August, 2023 ambayo ni:

1. Uchimbaji wa visima 11 (kumi na Moja) vijiji vya Usoche Kamsamba, Senga Samang'ombe, Lwatwe, Ivuna, Sante, Siliwiti, Tontela, Chuo, Naming'ongo, Msangano, Chole n.k.

2. Ujenzi wa tenki la Maji lenye ujazo wa lita 150,000 na mnara wa mita 9 kijiji cha Kamsamba

3. Ujenzi wa tenki la maji lenye ujazo wa lita 150,000 na mnara wa mita 9 kijiji cha Isanga

4. Utafiti wa maji chini ya ardhi kwenye vijiji 39 ambao unaendelea,

5. Ujenzi wa mradi wa maji Mlomba Tindingoma n.k

_Kazi zote hizi zimetekelezwa kwa muda mfupi ikiwa ni maelekezo ya Mhe. Waziri wa Maji Jumaa Aweso Jimboni Momba kwa niaba ya Rais wa JMT yenye dhima ya KUMTUA MWANAMAMA NDOO KICHWANI.

Miradi inayoendelea kutekelezwa hivi sasa ni yenye thamani ya zaidi ya Bilioni 8,221,689,635.00 👇 _ikiwa ni jitihada za Serikali ya CCM Chini ya Rais Samia Suluhu Hassani kupitia Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso.

1. Mradi wa Maji Msangano utakaonufaisha wananchi 34,162 wa Vijiji vya Naming‘ongo, Msangano, Ipata, Ntinga, Chindi, Nkala, Makamba, Yala sawa na 13.2% ya Wakazi wa Jimbo la Momba wenye tahamani ya Tshs 6,132,891,450.00 Ujenzi unaendelea.

2. Mradi wa Maji Isanga Kakozi utakaonufaisha wananchi zaidi ya 7,853 sawa na 3% ya Wakazi ya Jimbo la Momba wenye thamani ya Tshs1,756,119,878.00 Ujenzi unaendelea.

3. Ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 150,000 na mnara wa mita 9 umekamilika. Ujenzi wa pampu house na vituo vya kuchotea maji unaendelea.

4. Mradi wa Maji Tindingoma Mlomba utakaowanufaisha zaidi ya Wananchi 3,751 wakazi wa Momba wenye thamani ya 332,678,307.00 miradi hii imekamilika na wananchi wanatumia maji safi na salama.

Watanzaniaeeee Kazi inafanyika Momba, Visima vinachimbwa, matank ya maji ya Maji yanajengwa, mabomba ya maji yanalazwa ardhini kila uchao tena kwa jitihada kubwa ili maji kumfikia kila mtanzania, Hakika Aweso kazi anaifanya.

Na kwa mwendo huu tunaamini ifikapo Disemba 2024 zaidi ya 90% ya Wana Momba watazidi kuifurahia nchi yao kwa kupata maji safi na salama.

Walimwengu, Walimwengu....
"UKWELI USIFICHWE KWAKUWA UONGO HUENEA KWA KASI"
 
Mbuge anatoa kero za maji Momba. Chawa anadanganya umma. Unahesabu miradi bubu ya kamsamba, Mpapa, na Mkonko?
Hiv wew ni mwanamomba kweli?
 
Back
Top Bottom