Wana MMU tumchangie mwenzetu ajenge CHOO

Wana MMU tumchangie mwenzetu ajenge CHOO

Nazjaz

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2011
Posts
7,802
Reaction score
9,283
DADA+10.jpg

Tumemsikia Mwazani Said leo katika leo tena akituelezea namna alivyonusurika katika ajali ya gari iliyopelekea wasanii 13 ya band ya taarab ya 5stars kupoteza maisha.Ajali hiyo ilitokea tarehe 22 mwezi wa 3 mwaka 2011.Mwazani alisafiri na band kama mcheza show lakini yeye ilikuwa ni mara ya kwanza.Rafiki yake ambae alikufa kwenye band ndio alimwambia kuna kazi ya kucheza mikoani ambayo atatoka na pesa kidogo kuliko kukaa bure.


DADA+13.jpg


Wakasafiri na kuzuru mikoa mitano na yeye akafanya kazi yake ambayo alilipwa Tsh 100,000.Siku mbili kabla ya kurejea Dar wasanii waliopoteza maisha walikuwa wakiona vitu vya mauza uza.Msanii Issa Kijoti na mwimbaji mwingine wa kike walitokewa na mtu aliyevaa nguo nyeupe.Wakawaambia wenzao juu ya hilo wakawafanyia kisomo na dua ili waweze kukaa sawa.

Pia kulizuka ugomvi mkubwa ambao wasanii walikuwa wakigombana wao kwa wao mpaka Sheba Juma ambae ni marehemu alitaka kuondoka mwenyewe kurudi Dar.Lakini Ali J ambae yu hai alinusurika alisuluhisha ugomvi huo wakawa sawa.

DADA+3.jpg


Katika ajali hiyo wakiwa kwenye basi mwazani alikuwa amelala.Alikaa siti moja na marehemu Sheba Juma akamuomba wabadilishane siti ili yeye Mwazani alale maana alikuwa na usingizi.Alipolala alikuja kuzinduka baada ya siku 5 na kujikuta yupo hospital mkono umepooza na mguu umefanyiwa upasuaji na kuwekewa vyuma.Akamuuliza mama yake kumetokea nini mbona yupo hospital mama hakumjibu.Baba ndio akamletea gazeti akasoma na kuona kilichotokea na yule shosti wake aliyemuita wakacheze alipoteza maisha.




DADA+11.jpg


Baada ya ajali ile mpaka sasa mkono wake wa kushoto umepooza na mguu wa kushoto pia unavyuma bado.Walilipwa pesa ambazo yeye alizinunulia eneokanyumba kadogo kakuishi.

DADA+9.jpg


Wakati ananunua hapa sio yeye alikuja kununua.Kuna ndugu yake alikuja kupanunua lakini hakukuwa na choo.Ni mwaka sasa amekuwa akitumia choo cha jirani na kwa sasa amepigwa marufuku kutumia choo cha wenyewe.Baada ya kupigwa marufuku akarudi kwa baba yake ambae amepanga chumba na sebule.Baba na mama wanalala chumbani yeye analala sebuleni.

DADA+4.jpg



Sebule katika nyumba yake hiyo ambayo ipo Yombo dovya.

DADA+12.jpg


DADA+6.jpg


Huyu ndio jirani mwenye choo chake lakini amepigwa marufuku

DADA+1.jpg


Hapa ni chumbani kwake.
Kama ambavyo amesikika kwenye leo tena Mwazani anaomba kusaidiwa pesa ili aweze kujenga choo.Iwapo uliguswa na matatizo yake mchangie kwa namba 0759 789863 na 0657 795654.


Read more: KUTANA NA BINTI ALIYENUSURIKA KUFA KATIKA AJALI YA BASI ILIYOUWA WANAMUZIKI WA BEND YA 5 STAR AKIWEMO "ISSA KIJOTI" MWAKA 2011..SOMA SIMULIZI YA MAUZAUZA YAKIYOTOKEA KABLA YA AJALI HIYO | VITUKO VYA MTAA
 
Hujafa hujaumbika...kuna watu wanateseka duniani hapa!!
 
Aaaaaanh siku ishakuw nusu tena!!!!!!!!

Haya organizer aweke mambo sawa tuanze
 
Oh myGod! Dah! Basi mjipange dada asaidiwe na hata mtaji wa biashara pia nyumba na vitu ndani!
Hadi uchungu! Imagine mtoto huyo maskini!
 
hapo maskini unakuta kula kwa nadra! Dah jamani maisha haya!
Me saingine badala ya kutoa sadaka kanisani,to be honest bora umsaidie mtu kama huyu na Mungu atakubariki maramia maana kuliko kutoa kanisani uonekane bora umpe huyu akisema asante basi yatosha!
 
Namba hizo zilizobandikwa ni za Clouds FM, lakini pia twaweza kujipanga sisi kama sisi tukakabidhi michango yetu kama wana www.jamiiforums.com

Naunga mkono hoja ila napendekeza tukuteue wewe au yeyote atakaependekezwa na JF aratibu hilo zoezi ili lengo la watakaoguswa kuchangia ujenzi wa choo litimie. Ni maoni yangu tu.
 
Naunga mkono hoja ila napendekeza tukuteue wewe au yeyote atakaependekezwa na JF aratibu hilo zoezi ili lengo la watakaoguswa kuchangia ujenzi wa choo litimie. Ni maoni yangu tu.

Kwa hisani yenu naomba watu8 na ladyfurahia wawe viongozi wa shughuli hii

Hewaaaaaa..... naona ndio nilichokua namaanisha hapo juu. Binafsi sina kinyongo na uteuzi wako watoe tu namba za kutuma michango, na kutujulisha utaratibu unaendaje!
 
Naunga mkono hoja ila napendekeza tukuteue wewe au yeyote atakaependekezwa na JF aratibu hilo zoezi ili lengo la watakaoguswa kuchangia ujenzi wa choo litimie. Ni maoni yangu tu.
Ningelisimamia vizuri kabisa zoezi hili, ila ni kwamba leo usiku nasafiri, narudi kazini kwangu Southern Sudan, na nitakuwepo kwa siku 35 ndipo nirudi tena home
 
hee jamani ndo kwanza nafungua uzi huu nakutakana
na haya matatizo jamani pole bestito mwazani

acha nianze kazi ya kuwaconvisi wanajf kama wako
ambao watajitokeza ili twende tukapaone hapo anapoishi
ila dada naz naomba mwongozo wa kupajua anapoishi pls
Kwa hisani yenu naomba watu8 na ladyfurahia wawe viongozi wa shughuli hii
 
ingekuwa ni vyema kupajua anapoishi huyo mdada ingekuwa vizuri
hivyo naomba mnitajie anapoishi kwa Tanzania
Hewaaaaaa..... naona ndio nilichokua namaanisha hapo juu. Binafsi sina kinyongo na uteuzi wako watoe tu namba za kutuma michango, na kutujulisha utaratibu unaendaje!
 
sasa baba wewe ukijitoa itakuwaje? wakati mwanao nakutegemea wewe
Kipenzi nashukuru kwa pendekezo lako la uratibu wa shughuli hii, naomba tu niombe uzuru kuwa sitaweza kuratibu jambo hili.

Natanguliza samahani!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom