Wana Kagera ( Watani zangu Wahaya ) taratibu Kadinali Rugambwa siyo wa Kwenu Bukoba, bali ni wa Tanzania kote

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,596
108,965
Tena kwakuwa GENTAMYCINE ni Mtani wenu mkubwa kutoka Uzanakini Wilayani Butiama Mkoani Mara ( Musoma ) leo nawachana na mtulie kama mmemwagiwa Maji Baridi sawa?

Kanisa Katoliki halikumteua Kadinali Rugambwa atokae Kwenu Kagera ili awe ni wa Kwenu na muanze Kumtambia na Kutukoga Sisi wengine bali Yeye ni Kadinali wa Wakatoliki wote wa Tanzania ( GENTAMYCINE nikiwemo ) sawa?

Watani zangu wana Kagera bado mna Ushamba Ushamba ( Ugaigai Mwingi ) na sijui lini mtabadilika na kuwa Wastaarabu na Makini kama wana Mkoa wa Mara ( Musoma ) ambao ndiyo umewaleteeni huu Uhuru mnaotamba nao.

Nasikia Watani zangu Wahaya ( wana Mkoa Kagera ) kwa Ushamba wenu na Kupenda Kwenu Sifa hata Matukio makubwa ya Janga la Gonjwa lile, Kuzama kwa MV Bukoba, Tetemeko la Ardhi na Kudumbukia kwa Ndege ya Precision Air mnatamba na kujisifia nayo kuwa yametokea Kwenu tu na kwamba ndiyo Mnapendwa sana na Maulana.

ONYO

Kama unajijua huna Utani wa Kiasili ( wa Makabila ) na Wahaya ( wana Mkoa wa Kagera ) kama nilivyo Mimi GENTAMYCINE nakuonya Usiwatanie kwani Mimi nawamudu kwakuwa ni Mjomba na Shangazi yao.

Watani zangu mpo? Hongereni kwa kutuzalia Kadinali Rugambwa kwani kiukweli haiheshimishi tu Kagera yenu bali ameiheshimisha Tanzania nzima ukiwemo Mkoa uliobarikiwa na wenye Watu wenye Akili Kubwa ( kuwazidi nyie ) wa Mara ( Musoma )
 
Bro siku nyingine kama huna la maana la kuandika unaweza kuwa msomaji tu wa comment. Mimi ni Muhaya, nakutania kaka yangu.
 
Siyo hao watani zako wanatamba, kumbuka kimsingi Kardinali Protase Rugambwa ni matunda ya Jimbo kuu la Tabora. Akitokea huko Kigoma.

Hao watani zako walimzaa tu na kumheshimisha Jina la Rugambwa.

Hapa tu napambana na wimbo wangu wa Mheshimiwa Kadinali Protase Rugambwa,
 
Hongera cardinal Rugambwa
Mkoa wa Kagera unatoa majembe
Makadinal Wawili
Cheo cha sir kimetoka Kagera pale karagwe, Sir George Kahama hakuna mwafrika yeyote mwenye cheo hicho
Popoma leo umepata akili
Njoo Ngara nikupatie ng'ombe wa maziwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tena kwakuwa GENTAMYCINE ni Mtani wenu mkubwa kutoka Uzanakini Wilayani Butiama Mkoani Mara ( Musoma ) leo nawachana na mtulie kama mmemwagiwa Maji Baridi sawa...
Nina wasiwasi Nyerere ana vinasaba vya kihaya

Ndugu zangu akina mura wanaweza kukata mapanga tu
 
Back
Top Bottom