ichumu lya
JF-Expert Member
- Aug 11, 2016
- 2,605
- 2,729
Leo naandika kwa masikitiko makubwa sana baada ya Wakulima wa Vanilla Mkoani Kagera kulia kilio cha samaki na machozi yao kuondoshwa na maji.
Nimepitia maeneo tofauti tofauti mkoani Kagera nimekutana na wakulima wengi waliong'oa mikahawa baada ya anguko la bei na kupanda Vanilla leo vanilla iliyokuwa inanunuliwa kilo moja mbichi Tsh. 100, m000/ kipindi hicho kushuka kufikia Tsh.3, 000/ kwa kilo ni masikitiko na majonzi makubwa kuona bado kuna watu wanajiita viongozi sijui wanaongoza vitu gani wakati wakulima wanalia na kujikataa wenyewe.
Iko hivi Kagera ikiwa mwishoni mwa mikoa ambayo wananchi wana umasikini wa kutupwa nchini kwa mujibu wa tafiti mbalimbali lakini ni mkoa wenye wasomi wengi nchini wasio na faida nyumbani kwao.
Niliwahi kuhoji umuhimu wa kuwa na wasomi wenye kiwango cha mwisho uku ukuongiza kwa umasikini na watu wake kuwa kwenye top ya utapiamlo leo sitaji sifa za mkoa huu unaoongoza kwa vivutio vya uwekezaji Tanzania kwa kuwa katikati ya nchi nne ambazo ingetosha kuwa mkoa unaochangamka kiuchumi kuliko mikoa yote Tanzania.
Niliwahi kuhoji pia kwamba kwanini Kagera isijitenge kutoka Tanzania ili kuruhusu nchi yoyote kuja kuwekeza Kagera kuliko kukaa kwenye nchi isiyotambua/kuona umuhimu wa Kagera iliyozungukwa na Ziwa Victoria mito na mbuga ambazo kama zingetumika vizuri zingetosha kubadili uchumi wa Kagera na kuwa center ya kuichumi kwa nchi hizi nne ikiwamo na Tanzania?
Leo sitaki kabisa kuandika uduni wa miundombinu kama stendi na soko kuu vilivyochoka kama ajuza nasema sitaki kuandika namna Kagera ilivyotengwa kiuwekezaji kwamba ukifika Kyerwa utakutana na madini ya Kutengeneza bao (TIN) wananchi wamekalia utajiri kama wale watani zangu walivyokuwa wanachezea almasi bao.
Ukija mwambao wa Kemondo utakutana na mchanga wa vioo nyumba) bado mchanga huu hutumika kujengea nyumba lakini ukiona mashine za kutengeneza bati ni mashine ndogo isiyohitaji ata mita 100 na ardhi kujenga kiwanda alkadhalka na mashine za vioo.
Njoo kwa upande wa elimu Kagera ni mkoa usiokuwa na chuo kikuu hata kimoja, mkoa wa wasomi hapo simahanishi wasomi wajenge vyuo ila kwa nafasi zao uko walipo wana ushawishi mkubwa ata serikalini nako tumeangukia pua.
Tulikua tumebaki na kilimo lakini miaka zaidi ya 20 tulivamiwa na ugonjwa wa mnyauko ndizi (jeuri ya wanaKagera) zikanyauka lakini serikali haikuona sababu ya kuokoa zao hili badala yake walituacha tupambane na hali zetu apo napo Maprofessor wetu walitwambi mnyauko unatikana na uvivu unaopelekea mashamba kukanda utafiti niliupinga kwa hoja mpaka leo wako kimya.
Niliwauliza kama utafiti wenu umekomea hapo kwanini hamkujishighlisha kwenda Uganda ugonjwa ulikoanzia na leo walishausahau?
Majibu walioyafungia kwenye tafiti zao mliokuwa pale Bukoba coop hotel (Yaasira), nakumbuka nilivyowabana wasomi wetu leo tunalia na umaskini Kagera wakati umetengenezwa na serikali hii tangia vita ya Uganda.
Hapo nitapita kidogo serikali njoo mtuambie baada ya vita ya Uganda mlichukua hatua gani kuinua uchumi wa Kagera ulioathiliwa pakubwa na vita ile ya kitaifa? Nani alipewa fidia ya vita ile?
Nasema leo nina hasira na serikali hii yenye chuki na Kagera na mimi natangaza chuki na serikali hii maana ilinichukia mimi na wanaKagera tangia mwanzo ndiyo maana kila fursa ya uwekezaji ilielekezwa Mwanza sio Kagera.
Rejea miaka ya 1940 Kagera ilivyokuwa linganisha na Mwanza miaka ile Mwanza haikuona ndani kutokana na mchanganyo wa kibiashara kulikua na mwingiliano mkubwa kati ya Uganda na Kagera, Rwanda na Burundi leo tunachekwa na kutukanwa kwa makosa ya serikali.
Kwangu mimi naona mkwamo wa Kagera unatokana na muundo wa Katiba ya nchi yetu kama tungekuwa na serikali za majimbo tukaachana na wakuu wa Wilaya wa kuteuliwa na mtu asiye na historia na maeneo yetu mkuu wa jimbo tungemwajibisha lakini pia asingekuwa anasikiliza majungu kwakuwa angekuwa anatokana na sisi na akivurunda hawezi kuishi kwenye maeneo yetu haya ni maoni yangu nisipigwe pingu.
Sitaki kuzungumzia sheria ya ULANGUZI. ilivyovuruga juhudi za kiuchumi Kagera kuliko mkoa wowote nchini, nikiuliza NHC waliwahi kujenga nyumba ipi katikati ya mji nje ya walizonyang'anya wazee wetu? Msiniulize mengi lengo nikutaka vijana wanaojinasbu kulinda seriki hii wajue wanamkingia kifua adui.
Mimi Katikabakama nalazimika kukaa na kuililia Kagera na kizazi chetu sisi ni yatima kweli kweli mkoa unaoongoza kwa wasomi huku unaongoza kwa umaskini na utapia mlo ardhi ya Kagera imesubiri kupokea miili ya wasomi Madoktor, Maproffesor na wasomi wa viwango tofauti tofauti walioshindwa kutumia elimu kama fursa ya kiuchumi Kagera.
Mtu mmoja miaka ya Karibuni aliwahi kuimba namimi nakubaliana naye kwamba "omukyemba ky'omugaiga embaga yoona eryoomw' omwomworo nalila n'aboruganda bonka" Acha tulie na wanaukoo Kagera ibaki sehemu ya kuzika wasomi wetu wanaoletwa kwenye majeneza ya mamilioni yanayoliwa na wadudu pindi wakioza.
Leo sitoi ushauri kwa serikali maana miaka yote nashauri lakini sikio la kufa haliwezi kusikia dawa. Kwa upande wa Wakulima wote kuanzia Kahawa, Vanilla, na mazao yote ya kibiashara kila mtu ajitafakali siraha ya kuiadhibu serikali hii kila mmoja anayo kichwa
.@Katikabakama-2023