Wana JF, ni halali kweli UDOM kuitwa chuo cha kata?

Wana JF, ni halali kweli UDOM kuitwa chuo cha kata?

Wakuu japo sio rasmi,chuo cha UDOM kinasemekana ni chuo cha kata.Imeelezwa kuwa sababu kubwa ni kuwa na walimu wasio na sifa pamoja na course "bwerere"!Wenye taarifa watujuze

Nashangaa sana unakuja na hoja za kijinga kama hizi, yaani hata kufikiria tu hutaki.

1. Kati ya Elimu ya baadhi ya vyuo na UDOM ni chuo kipi elimu yake ni SPOON FEEDING?
2. Tafuta Tests na University Exams za Udom na vyuo unavyovisifia wewe ulinganishe hapo ndio utajua ukweli kuwa Udom ipo vizuri kuliko baadhi ya vyuo vyako bora.
3. Uliza bodi mbalimbali za mitihani kama ile ya watu wanaosoma PROCUREMENT watakwambia kuwa Udom wako vizuri sana sana.

Nakushauri ukitaka kusema kuhusu UDOM uliza wanafunzi wake watakwambia chuo chao kikoje ukiachilia mbali chamgamoto za uchanga wa chuo. Kuna vyuo hapa tanzania wanafunzi huandikiwa ubaoni kila kitu na mwalimu hutoa kilekile alichofundisha yaani anabadili namba tu na vitu vidogo sana.

Unaposema Udoma wanafundishwa na watu wasio na sifa halafu husemi ni sifa gani hizo unakuwa unaongea kishabiki tu.
Nenda kwenye collage za UDOM ukaulize utakuja kutueleza hapa na usijaji chuo kwa maneno ya chuki.
 
Wanaokiponda UDOM ni wale waliyoomba nafasi za kazi wakakosa kutokana na kutokuwa na vigezo stahiki,ni wale waliofukuzwa chuo kutokana na Migomo,pia kuna kundi la watu waliodisco hasa miaka ya 2010 na 2011
 
Ni kweli UDOM ni chuo cha kata, wanachuo wanafundishwa uoga tu, watu wanafukuzwa kila saa, wafanyakazi nao unafki mtupu...
 
Elimu siyo siasa!!!! Ni chuo cha kata na sababu hizi hapa

1) Wanagraduate bila mafunzo ya vitendo
2) Walimu wao wengi wana bachelor au masters degree (Kawaida hawa ni tutorial assistants)
3) wanaoapply hapo wengi ni wasio na matumaini vyuo vizuri hapa TZ

Labda wewe unafikiri chuo ni majengo! La hasha! Chuo ni elimu bora.

Conclusion

UDOM ni chuo cha kata mpaka hapo kitakapokuwa na walimu wenye sifa na wanafunzi bora

namshukuru Mungu nimemaliza hapo 2 nyuma, na sasa nina impact kubwa sana kwa jamii yangu hapa, nawasaidia vijana kuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ili kusaidiana kujiendeleza kimaisha. kwa hoja no 3 si kweli kabisa mimi nilipata udsm na udom nikachagua kozi mpya ya udom. kuhusu field ni kweli sikufanya na ndio mgomo mkubwa ulitokea, ila sio ishu maana nilijichanganya kwenye Ngo's mbalimbali. kuhusu walimu ni kweli wengi ni mabwana na mabibi, ma dr na prof walikuwa ni wachache.( muda niliomaliza mimi). UDOM hakiwezi kuwa chuo cha kata hata siku moja, na elewa elimu ya chuo kikuu ilivyo. viva THE UDOM du nimekumbuka sana maisha yale.
 
Kuna watu wabishi tu kwa asili hawataki kuambiwa ukweli. Wanaoita Chuo cha kata ni wanafunzi wenyewe wa Udom sasa wengine huku wanapanic na kuanza kutukana wenzao mara umesoma wapi? sijui hujasoma? mara taahira? Lakini ukweli upo palepale hata kama ni mchungu UDOM ni Chuo cha Kata tu hakina jina jingine kwa sasa

Msichukie jina la kuitwa chuo cha kata kinaitwa hivyo kwakuwa kinasaidia wanafunz wengi waliokuwa wakikosa nafas,mimi wakat nahitimu kidato cha sita mwaka 2002 usingeweza kupata nafas ya kwenda chuo kikuu tena masomo ya sayansi km angalau huna CD kwenye masomo mawili lkn kwasasa hata SUA wameogopa kukosa wanafunzi wanachukua mpak EE kwa sayansi! hiyo yote ni compition ya kudahili wanafunzi iliyoletwa na udom,wenzetu Uganda na Kenya walishakuwa na vyuo vikuu vingi kitambo kiasi kwamba hakuna mwenye sifa anaekosa nafas ya chuo kikuu na ndo maana tumeachwa nyuma kielimu! m binafsi naipongeza serikali kwa kuanzisha chuo kikuu cha Udom naamin matatizo yaliyopo ni changamoto tu hata mtoto mtoto huanza kutambaa mwisho hukimbia,Udsm yenyewe ilianzia Lumumba street wakiwa na jengo moja na walimu wa kuungaunga lkn baada ya kusomesha wanafunzi wao na kuwaendeleza mpaka kuwa professors mambo yamekwenda vizur na elimu imeboreka. msitake kuturudisha enz za umeshinda lkn hukuchaguliwa
 
  • Thanks
Reactions: SG8
Hii thread ya mwaka 2010!UDOM ya leo,ina lecturers wa kutosha,ina chukua wanafunz weny pass kubwando maana weng wanakosa
 
Thread imepitwa na wakati,bcoze kwa sasa tunaenda field & kila mtu shahidi,profs& dkts wanatosha,ingawa weng ni wakigen
 
Udom yasasa c ya mwaka 2007,changamoto nying zimetatuliwa,walioomba wakakosa,waliofukuzwanawaliodisko ndo wanaoponda.
 
Kama siyo chuki binafsi mtu timamu hawezi iita UDOM ya sasa chuo cha kata! UDOM HII!?.Ni hawa waliokosa/fukuzwa,wivu tu!
 
Kiufupi vyuo haviwezi fanana hata iweje ila kuita cha kata mna maana wanaoenda hapo ni watu wa kata za dodoma tu ama ni vip, kata gani?
 
Anaesema udom chuo cha kata namkaribisha aje coes ,bsc in geology, geoinformatics, mining ,petroleum and mineral processing engineering ,,,,,,,, we payuka wanaume tunachukua ujuzi tunawahi migodini !!!!!!!!!!
 
Basi tanzania kuna maendeleo sana,kama mpaka kila kata ina chuo kikuu!hata marekani hawajafikia maendeleo hayo aisee..
 
Basi tanzania kuna maendeleo sana,kama mpaka kila kata ina chuo kikuu!hata marekani hawajafikia maendeleo hayo aisee..

Ni baadhi ya kata tu kama za dodoma zimepata hio bahati
 
Hizo ni fikra tu za watu kingekuwa chuo cha kata sidhani kama baadhi ya course zingekuwa zinatolewa hapo vyuo vingine hamna kama engineering in petroleum hata udsm haipo na inatambulika kimataifa ndio maana hao watu wanapata sponsor ya kwenda kusomeshwa nje
 
Back
Top Bottom