utanitukana sana lakini huo ndiyo ukweli, mimi siongei kama CCM wala chama chochote cha siasa, wewe sikushangai kwa vile matusi yenyewe yanakuelezea wewe ni CHADEMA. Najua vita haichagui, lakini siamini kuwa itachagua CCM tu ndo wafe, tunajidanganya sana, madamu mlishalianzisha na REDBRIGADE yenu hamna budi kuikubali hali halisi kwa vile CCM nao wanaonekana kuchoka.
Dar es Salaam.Kauli ya Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka wanachama, wadau na makada wa CCM,kuondokana na unyonge, imepokewa kwa hisia tofauti huku ikielezwa kuwa ni yavitisho. Juzi, wakati akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuuya CCM mjini Dodoma, Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hichotawala alisema: Ni wakati wa kuacha unyonge na uvumilivu una kikomo chake. Alisema CCM inaingia kwenye uchaguzi hukuikishindana na wagomvi: ...Ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wao kufanya siasa,alisema Kikwete bila kutaja jina la chama chochote cha siasa. Alisemaamechoshwa na vitendo vya ugomvi huku akitolea mfano wa tukio la Kahama mkoaniShinyanga ambako kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi na mwinginekumwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa ubunge Igunga, mkoani Tabora. Akizungumza kwa simu jana, Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe alieleza kushangazwa kwake na kauli ya Rais Kikwete akisema:Nimeipokea kwa mshtuko na ninawataka wafuasi wa chama changu kuwa watulivu nakuchukua tahadhari kubwa. Nilichokifanya ni kuwaagiza wafuasi wa Chademakufanya kampeni za kistaarabu kwa kutolipiza kisasi ili kuhakikisha kwambahakuna damu ya Mtanzania itakayomwagika Kalenga, alisema. Hatua ya Rais Kikwete, imekuja baada ya CCMkumtangaza, Godfrey Mgimwa kuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga. Mgimwa nimtoto wa aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, ambaye pia alikuwa Waziri wa Fedha,hayati Dk William Mgimwa aliyefariki mwezi uliopita nchini Afrika Kusini. Mgombea huyo atachuana na mgombea wa Chadema, GraceTengega. Jana, Mbowe alisema ingawa Kikwete ni Mwenyekiti waCCM, alitakiwa kufahamu kwamba ni kiongozi wa nchi na ni Amiri Jeshi Mkuuambaye vikosi vya Ulinzi na Usalama vipo chini yake. Anapotoakauli nzito kama hiyo, inatakiwa afahamu kwamba yeye si Mwenyekiti wa CCM tu,bali ni Rais na Amiri Jeshi Mkuu, hakustahili kutoa kauli kama hiyo inayowezakuamsha hisia, alisema Mbowe. Alisema kauli zake za kiitikadi za kupendelea chamachake wakati akifahamu kuwa yeye ni kiongozi wa Watanzania wote, zinawafanyawananchi wagawanyike kwa misingi ya vyama. RaisKikwete anadai kwamba mtu wao alimwagiwa tindikali na mwingine kutolewa machokwa bisibisi, lakini hazungumzii viongozi na wanachama wa Chadema waliouawa kwakupigwa risasi na wengine kwa mabomu. Anasema hayo huku akifahamu fika kwambakuna vyombo vya dola na Mahakama ambavyo vinashughulikia matukio hayo. Mbowe alidai kuwa Juni 15, 2013 wakati akifungakampeni za udiwani mkoani Arusha, alirushiwa bomu la kivita na kusababisha vifovya watu wanne lakini uongozi wa chama hicho ulipomwomba Rais aunde tume huruya kimahakama hakuna kilichofanyika. Tumemwomba mara kadhaa Rais Kikwete kuunda tumehuru ya kimahakama ili kuchunguza mauaji ya viongozi na wanachama wa Chademaambayo yamekuwa yakitokea, lakini hakuna kilichofanyika, alisema Mbowe ambayeni pia kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni. Alisema: Rais Kikwete anasema wamekubaliana kwenyeHalmashauri Kuu (ya CCM) kuacha unyonge, Halmashauri Kuu ina viongozi wotewakuu wa nchi, wanakubaliana kuwatenga wananchi kwa kufuata itikadi za chamachao, hii ni hatari. Mbowealisema kauli ya Rais Kikwete inafanana na ile ya Waziri Mkuu, Mizengo Pindaaliyoitoa bungeni ya kuwataka askari polisi kuwapiga raia kwa wale wasiotakakutii amri halali. Mbatia ataka ufafanuzi Akizungumzia kauli hiyo, Mwenyekiti wa Kituo chaDemokrasia Tanzania (TCD), James Mbatia alisema ameshtushwa na kauli ya RaisKikwete na kumtaka kuitolea ufafanuzi ili kuondoa mgawanyiko katika jamii. Alisema kauli ya unyonge CCM sasa basi haikupaswakutolewa naye hasa ikizingatiwa kwamba ndiye kiongozi mkuu wa nchi ambayevyombo vya ulinzi na usalama viko chini yake. Ni kama amevielekeza vyombo vya ulinzi na usalamakuchukua hatua kali dhidi ya vyama vingine vya siasa, ninamwomba alitoleeufafanuzi suala hili kabla halijaleta madhara kwenye jamii, alisema Mbatia. CUF yahofia Kalenga Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisemakauli ya Kikwete inaashiria kuwa kutakuwa na matumizi makubwa ya vyombo vyadola katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga. Ninavyofahamu siyo kwamba anawaagiza wafuasi waCCM kuacha unyonge na kuchukua hatua, bali anavielekeza vyombo vya dola kutumianguvu kubwa zaidi, alidai. Mtatiroalisema anashangaa kauli ya namna hiyo kutolewa na Rais wakati ndiyeanayetakiwa kuhubiri amani na kuvumiliana. Akizungumza suala hilo, Mhadhiri wa Chuo Kikuu chaDar es Salaam, Bashiru Ali alisema wananchi wanatakiwa kuwa makini na kauli zawanasiasa zenye kujenga chuki. Vijanatusipigane kwa kugombanishwa na wanasiasa, tofauti zetu za kiitikadizisitufanye tugombane kwani malengo ya wanasiasa ni kutoa kauli zenye utata kwalengo la kupata kura, matatizo yetu yatuunganishe, alisema Bashiru. Chanzo mwananchi
`Natoa mfano tu:-
Mimi ni askofu. Makanisa yetu yamechomwa. Mapadri wangu wengine kule Zenj wameuwawa na wengine kumwagiwa tindikali. Kule Olasiti tumelipuliwa kwa bomu tukiwa kwenye misa, na watu wakafa. Juzi ktk mwaka mpya kule Usa river wakawapiga waumini wetu mabomu hata askofu wangu Lebulu akalia machozi akisema, "Mbona ni kanisa letu tu? Tumekosa nini?" Wakati wote katika mahubiri yetu mimi na maaskofu wangu tumehubiri uvumilivu na kutojichukulia sheria mkononi kwa namna yoyote kwa ajili ya amani na utengemano wa Kitaifa. Kama leo mimi ningesimama na kuwataka waumini wangu waache kuwa wanyonge kwa kuwa uvumilivu una mwisho, hata kama singesema wajibu mapigo, ningeelewekaje? Ningetafsiriwaje na ninyi wana JF? Wale watu wangu ninaowaongoza wangechukuliaje kauli yangu hiyo? Je Vyombo vya usalama vya dola vingenielewaje? Nadhani Mwenyekiti wa chama tawala akisema hivyo, vyombo vya dola vingesimama nyuma yake kuhakikisha kauli yake inatekelezwa, na kwa mimi wangejiandaa kunifhibiti na huenda ningeitwa kuhojiwa na Polisi! Hii ndiyo hatari ya kauli ile ya kusema uvumilivu una mwisho na unyonge basi na hasa kama inatolewa na amirijeshi mkuu. Ni vizuri tuendelee kutoa kauli za kuvumiliana kisiasa na kiitikadi na hata kidini huku tukihamasisha kuwa wote tuko chini ya sheria, na vyombo vya ulinzi vitekeleze majukumu yake bila kupendelea upande wowote! Tusipofanya hivyo tunaumba matatizo yatakayotugharimu damu za watu wetu sasa hivi!!!!
Rais lazima atambue wakati wote kuwa yeye ni KIONGOZI WANCHI na kauli yake inamshiko mkubwa sana katika jamii. Rais hawezi kuongozanchi kwa kauli za mihemko. Tamko la raislazima libebe ndani yake kipimajoto kinachomuashiria mtikisiko unaowezakusababishwa na tamko lake. "Tumekubaliana kuacha unyonge, lazima tujibumapigo" ni kauli mbaya, inastusha na inaogopesha haswa kabisa ni kwa vilesiku moja baada ya kauli hii kule Nigeria BOKO HARAM wamechinja watu zaidi ya100. Nadhani hata Nyerere ndani ya kaburi lake ameshtuka na kupepesa macho.Siku zote imesemwa kuwa tatizo la kwanza kabisa la Afrika ni VIONGOZI WAKE naKikwete hawezi kuwa tofauti. Cha muhimu hapa ni watanzania wote kuikataa kabisakauli hii na tusikubali kutumiwa na mtu yeyote.
[h=1][/h]
Dr Slaa
by Abdallah Khamis
KAULI aliyopata kuitoa Waziri Mkuu Mizengo Pinda bungeni kuwataka polisi wawapige wapinzani, na kauli ya juzi ya Rais Jakaya Kikwete kuwaagiza wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wajibu mapigo pale wanaposhambuliwa na wapinzani, imeelezwa kuliingia taifa vitani.
Akifungua kikao cha Halmashauri Kuu (NEC) ya CCM taifa mjini Dodoma, Rais Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho taifa, alisema bila kumungunya maneno akiwataka Wana-CCM kuacha unyonge na kujibu mashambulizi pale wapinzani wanapoendesha siasa za vurugu.
Waziri Mkuu Pinda katika kipindi cha Maswali na Majibu bungeni aliwahi kutoa kauli ya kuwataka polisi wawapige wafuasi wa CHADEMA kwa vile walikuwa wakiendesha maandamano katika sehemu mbalimbali nchini, ambayo Serikali ya CCM ilitafsiri kama vurugu.
Pinda ambaye hivi sasa amefunguliwa kesi mahakamani ya kuvunja katiba kutokana na kauli hiyo, alisema serikali imechoka na haina njia nyingine zaidi ya kuwataka polisi wawapige wapinzani.
Wakitoa maoni yao kuhusu msimamo wa Rais Kikwete, baadhi ya wanazuoni, viongozi wa siasa wameeleza kushangazwa na kauli ya kiongozi huyo mkuu wa nchi kwani ameliingiza taifa vitani.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kauli ya Rais Kikwete inatisha, inashangaza na haikupaswa kutolewa na kiongozi mkuu wa nchi.
Alisema kauli yoyote inayotolewa na rais pasipo kujali yupo sehemu gani ni amri kwa walio chini yake, na kwamba kinachofuata ni utekelezaji.
Waswahili wanasema ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni. Hivi karibuni tulishangaa kauli ya Pinda kutaka polisi wawapige tu wapinzani, leo rais naye anawataka CCM waache unyonge, wajibu mapigo. Hii ni hatari sana, alisema Dk. Slaa.
Kwa maoni yetu, CHADEMA tunasema Rais Kikwete ameliingiza taifa vitani, amefungua milango ya uvunjifu wa amani, kinachofuata ni umwagaji damu.
Dk. Slaa aliongeza kwa kusema kuwa anatilia shaka uwezo wa Rais Kikwete katika kuchambua taarifa
anazofikishiwa mezani na wasaidizi wake, ambazo safari hii zimemfanya aamini wanaoanzisha vurugu katika uchaguzi ni wapinzani.
Alisema licha ya Tume ya Jaji Amir Manento na ile ya Haki za Binadamu kulitaja Jeshi la Polisi na CCM kuwa chanzo cha vurugu zinazosababisha mauaji ya watu nchini, Rais Kikwete ameziba masikio na kuwarushia tuhuma hizo wapinzani.
Watu wameuawa Nyololo na Arusha, ripoti ya Haki za Binadamu anayo ofisini kwake ameifungia na kisha ametoa zawadi ya kuwapandisha vyeo wale waliosababisha mauaji hayo, leo anathubutu vipi kusema wapinzani ndio chanzo cha vurugu? alisema na kuhoji Dk. Slaa.
Alisisitiza kuwa licha ya Rais Kikwete kuwasingizia wapinzani kuwa chanzo cha fujo, bado ameshindwa kuunda tume huru ya kimahakama ili kuujua ukweli wa matukio hayo.
Alisema kimsingi CHADEMA haitakubali damu ya Mtanzania hata mmoja imwagike kwa sababu ya kupata madaraka, na kwamba agizo la Rais Kikwete linavilazimisha vyama vya upinzani kuwaandaa vijana wao ili kujilinda.
Hivi kama na sisi tutaamua kuwaambia vijana wetu wajilinde, na katika hali hii ya kunyanyaswa na kuonewa na hao CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola, unadhani nchi itabaki salama? alihoji Dk Slaa.
Mwenyekiti wa Chama Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amemsikitikia Rais Kikwete kwa kupoteza uelekeo wa kulinda amani ya nchi.
Alisema ameshtushwa na kauli hiyo aliyoieleza kuwa imekosa uvumilivu wa kisiasa, huku akiainisha kuwa chanzo cha vurugu katika sehemu mbalimbali nchini ni CCM kwa kushirikiana na vyombo vya dola.
Alisema alitegemea Rais Kikwete ahimize Watanzania kutii sheria bila shuruti badala ya kuonyesha dalili za wazi kuwa hakuna haja ya kutii sheria, na hata vyombo vinavyotafsiri sheria hiyo.
CCM ndio waanzilishi wa vurugu zote nchini, na kama mwenyekiti wao ametoa kauli hiyo, unategemea nini kitatokea ikiwa yeye ndiye amiri jeshi mkuu? alihoji Lipumba.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia, kwa upande wake alisema kauli ya Rais Kikwete itamfanya abebe dhamana juu ya jambo lolote la uvunjifu wa amani litakalotokea kuanzia sasa.
Alisema ni hivi karibuni taifa liliingia katika maridhiano ya kuandika katiba mpya kwa ajili ya Watanzania, hivyo Rais Kikwete hakupaswa kutoa kauli hiyo wakati huu.
Hii kauli haina viashiria vizuri kwa taifa, ni vema aje hadharani atuambie alikusudia nini, vinginevyo atabeba dhamana ya jambo lolote litakalojitokeza, alisema.
Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ambaye ni mchambuzi wa masuala ya kisiasa na jamii, Bashiru Ally, alisema Watanzania wategemee visa vingi wakati huu wa kuelekea uchaguzi wa 2015.
Alisema nchi inaweza kuingia kwenye machafuko ambayo hayajawahi kutokea
kutokana na kauli za wanasiasa, zinazolenga kuwanufaisha wao binafsi badala ya maslahi ya taifa.
Aliongeza kuwa kitendo cha Mwenyekiti wa CCM kuwaagiza wafuasi wake wasiwe wanyonge na wajibu mapigo, siyo suluhisho la tatizo bali ni kuongeza tatizo.
Alisema NEC ya CCM badala ya kukaa na kuamua kupambana, wangetafuta jibu juu ya kiini cha mapambano hayo yanayodaiwa kutokea katika jamii.
Mwenyekiti amekuja na majibu mepesi katika maswali magumu, na mimi nasema kuchoka uvumilivu si jawabu la tatizo, wajitokeze hadharani kutibu chanzo, alisema Bashiru.
Alisema rais kuruhusu hali hiyo ni kutangaza vita ya wenyewe kwa
wenyewe kwa kuwa kauli yake ni amri kwa walio chini yake, na kwamba wananchi watakapokataa kunyanyaswa, madhara yake yatakuwa makubwa kwa jamii nzima.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, alipoulizwa kama kauli ya rais inaashiria Jeshi la Polisi limeshindwa kutekeleza wajibu wake wa kuwalinda Watanzania na pia kama si uchochezi wa wazi, alisema hajapata taarifa hizo wala kusikia, na kwamba atafanyia kazi ajue kama alichoelezwa kimetamkwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Mimi ndiyo kwanza ninasikia kutoka kwako, wewe ndiyo unaniambia, ngoja nifuatilie nijue kama kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM, alisema IGP Mangu.
Akifungua mkutano wa NEC ya CCM juzi mjini Dodoma, Rais Kikwete aliwataka wanachama wa chama hicho kuacha unyonge kwani uvumilivu waliokuwa nao umefika kikomo chake.
Alisema chama hicho kinaingia kwenye uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga mkoani Iringa, kinashindana na vyama vingine ambavyo alisema ni wagomvi, maana kwao ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wa kufanya kazi ya siasa.
Tulizungumza nalo hilo kwenye Kamati Kuu, tulikubaliana kuacha unyonge. Ndiyo, kwenye Kamati Kuu tumekubaliana, tumesema jamani watu wote waende wakaseme tumekubaliana kuacha unyonge, alisema huku akicheka na kupigiwa makofi na wajumbe wa NEC.
Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alitolea mfano wa tukio lilitokea Kahama mkoani Shinyanga, ambapo kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi, na tukio la Igunga ambapo kijana mmoja alimwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
Acheni unyonge na hata katika taarifa ya habari leo (jana) mtoe hivyo hivyo. Na muache habari zote mseme hii tu (waandishi wa habari). Uvumilivu una ukomo wake, alisema huku wajumbe wakiendelea kumpigia makofi.
Nalisema kwa sababu yanayotokea yanasikitisha sana. Pale Igunga kijana yule wamemmwagia tindikali, pale Kahama kijana ametolewa macho kwa bisibisi, alisema.
Uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga lililopo mkoani Iringa unatarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu, huku tayari vyama vya CCM na CHADEMA vikiwa vimetaja wagombea wao.
Chanzo Tanzania Daima
Nina kipindi kirefu sana sijaona unatoa maneno yenye uhai kwako na kwa members humu ndani, napata shida kuamini kama una ubinadamu yako. Very spoilt mind..
`Natoa mfano tu:-
Mimi ni askofu. Makanisa yetu yamechomwa. Mapadri wangu wengine kule Zenj wameuwawa na wengine kumwagiwa tindikali. Kule Olasiti tumelipuliwa kwa bomu tukiwa kwenye misa, na watu wakafa. Juzi ktk mwaka mpya kule Usa river wakawapiga waumini wetu mabomu hata askofu wangu Lebulu akalia machozi akisema, "Mbona ni kanisa letu tu? Tumekosa nini?" Wakati wote katika mahubiri yetu mimi na maaskofu wangu tumehubiri uvumilivu na kutojichukulia sheria mkononi kwa namna yoyote kwa ajili ya amani na utengemano wa Kitaifa. Kama leo mimi ningesimama na kuwataka waumini wangu waache kuwa wanyonge kwa kuwa uvumilivu una mwisho, hata kama singesema wajibu mapigo, ningeelewekaje? Ningetafsiriwaje na ninyi wana JF? Wale watu wangu ninaowaongoza wangechukuliaje kauli yangu hiyo? Je Vyombo vya usalama vya dola vingenielewaje? Nadhani Mwenyekiti wa chama tawala akisema hivyo, vyombo vya dola vingesimama nyuma yake kuhakikisha kauli yake inatekelezwa, na kwa mimi wangejiandaa kunifhibiti na huenda ningeitwa kuhojiwa na Polisi! Hii ndiyo hatari ya kauli ile ya kusema uvumilivu una mwisho na unyonge basi na hasa kama inatolewa na amirijeshi mkuu. Ni vizuri tuendelee kutoa kauli za kuvumiliana kisiasa na kiitikadi na hata kidini huku tukihamasisha kuwa wote tuko chini ya sheria, na vyombo vya ulinzi vitekeleze majukumu yake bila kupendelea upande wowote! Tusipofanya hivyo tunaumba matatizo yatakayotugharimu damu za watu wetu sasa hivi!!!!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.