Uko tayari kulala saa kumi na moja jioni?
Ameyasema hayo wakati wa kikao cha NEC alipokuwa anazungumzia machafuko yanayotokea kwenye chaguzi ndogo especially ile ya kahama.
Amewataka wana CCM kuacha unyonge. Amejihami kwa kusema kwamba hata kama alichokisema kitakuwa ndio habari nzito kwenye vyombo ya habari sawa tu.
Source: News, TBC1
Sijaielewa hii kauli ya kikwete alikuwa anamaanisha nini.
Hapa nimeshindwa kumuelewa; anataka wana CCM wareact vipi? Kwa kuua au?
Hii ni hali ya kutojielea kua yuko position gani katika nchi hii. Kwa hakika kiongozi wetu huyu kachoka akapumzike kwa sasa maana hii ni kama kuidhinisha watu wauane.
Mkuu Tuko nadhani wewe ndio uko out of your mind ... hizi propaganda za kumchafua Rais wa Tanzania tumeshazibaini, na hatutaziacha ziendelee!
Hivi ndivyo nilivyomuelewa mimi, kama tunavyojua unyonge ni kukosa nguvu, na nguvu anayoiongelea ni nguvu ya hoja sio ya msuli, kushindwa kujieleza mbele ya wananchi bila kukiponda chama kingine au mtu fulani, ni unyonge (udhaifu), kushindwa kujenga hoja ni unyonge, kutegemea dola ni unyonge, kutumia wingi wenu kupitisha jambo badala ya hoja au manufaa ya taifa ni unyonge.
Huo ni wito katoa kwa wanaccm, mwenye sikio na asikie. Jifunzeni uzalendo, na kujiamini pia
Tunashindana na wenzetu wagomvi, maana wao ugomvi ndiyo sehemu ya mwongozo wa kufanya kazi ya siasa,alisema Kikwete bila kutaja chama chochote cha siasa kwa jina.
Tulizungumza nalo hilo kwenye Kamati Kuu, tulikubaliana kuacha unyonge. Ndiyo, kwenye Kamati Kuu tumekubaliana, tumesema jamani watu wote waende wakaseme tumekubaliana kuacha unyonge, alisema huku akicheka na kupigiwa makofi na wajumbe wa Nec.
Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, alitolea mfano wa tukio lilitokea Kahama mkoani Shinyanga, ambapo kijana mmoja alitolewa macho kwa bisibisi, na tukio la Igunga ambapo kijana mmoja alimwagiwa tindikali katika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
Acheni unyonge na hata katika taarifa ya habari leo (jana) mtoe hivyo hivyo. Na mwache habari zote mseme hii tu (waandishi wa habari). Uvumilivu una ukomo wake, alisema huku wajumbe wakiendelea kumpigia makofi.
Nalisema kwa sababu yanayotokea yanasikitisha sana. Pale Igunga kijana yule wamemwagia tindikali, pale Kahama kijana ametolewa macho kwa bisibisi.
Tanzania nchi pekee duniani iliyobahatika kuongozwa na boya
tumechoshwa na fujo zenu
unyonge basi
kweli kua ccm ni janga na umbumbumbu wa mwisho,hiyo namba moja mpaka tano ukienda tu hapo libya inchi yenye janwga,ina huduma zote hizo bure sembuse inchi kama hii yenye mabonde maziwa na asali.peleka ujinga wako ccm wa ahedi.muwe mnawauliza mapdre wenu wawatafsirie wamesoma sana biblia ambayo kwa kiwango kikubwa imeandikwa kwa mafumbo la sivyo hamutaweza kujua viongozi wasomi wa ccm wanakuwa wanamaanisha nini kwenye kauli zao. Usitegemee vichwa matope kama cha mbowe, lema, msigwa , lissu, vicent nyerere na ninyi wote mjue wanakuwa wana maanisha nini?
1. Chadema ikiingia madarakani , mfuko wa cement 5000/= . Gharama ya kuzalisha mfuko mmmoja shilingi ngapi?
2. Chadema ikiingia madarakani elimu, afya bure. Tupe mfano wa nchi mojawapo afrika na hata ulaya inayotoa elimu bure?
3.itaichukua chadema mwaka mmoja kuibadilisha tanzania kuwa nchi ya viwanda. Unajua mapinduzi ya viwanda ulaya yalichukua muda gani?
4. Bomba la gesi kutoka mtwara linjaengwa kwenda ulaya na siyo dar es salaam, slaa huyo.
5. Itaichukua chadema siku 100 kuipatia tanzania katiba mpya. Tangu mchakato wa katiba mpya uanze siku 100 bado? Au hiyo ya chadema wangelkaa mtaa wa ufipa na kuiandika ili ndani siku 100 iwe imekamilika?
Kama ni matamshi ya kijinga chadema wanaongoza.
....
...duh!! hii kitu zaidi ya janga !!!!!
Kwa amri ya Rais wa Tanzania sio? Kuna kesi ya kujibu hapa....
ameongea kama mwenyekiti wa CCM...
ametuambia wana CCM
sasa sioni unababaika na nini
Wapi nimebabaika? Nyie ndio mnababaika mnaogopa nguvu ya mabadiliko mnachagua intimidation. Bado unababaika unaposema kuwa alikuwa anaongea kama Mwenyekiti wa CCM.....poor you
fuatilia njia za kukuwezesha kukutoa kwenye boksi acha ushabiki wa kijinga
President of the United Republic Act No.15 of 1984 Art.9: 33.-(1) There shall be a President of the United Republic.
(2) The President shall be the Head of State, the Head of Government and the Commander-in-Chief of the Armed Forces. 37.-(1) Apart from complying with the provisions contained in this Constitution, and the laws of the United Republic in the performance of his duties and functions, the President shall be free and shall not be obliged to take advice
given to him by any person, save where he is required by this Constitution or any other law to act in accordance with the advice given to him by any person or authority.
ameongea kama mwenyekiti wa CCM...
ametuambia wana CCM
sasa sioni unababaika na nini
Kwa nguvu zote hizi za kikatiba ameshindwa nini kulihamuru jeshi la polisi kuwakamata waliovunja sheria huko Kahama?
Ndugu zangu, ni kwa nehema tunavuka salama hawamu ya nne ya J. K. Haya yatukumbushe na kuunganisha matukio ya nyuma kwa jk ni mhusika.
Haiwezekani Mwangosi auawe jk akae kimya na badala yake muaji apandishwe cheo. Mwigulu atuhumiwe mauaji Arusha leo naibu wazir. Mwigulu huyo huyo atembee na mmwagiwa tindikari kuamsha hasira za adhira serikali kimya, naleo tusikie kutoka kwake 'live' akiahamasisha wafuasi wake washike bisi bisi kuua kama 'wapinzani' walivyofanya Kahama.
Inanisikitisha sana! Naomba wenye hekima, jeshi, mahakama haraka walikemee ili. Hali iko wazi CDM haitakuwa tayari kuibiwa kura...razma vyombo vinavyohusika viweke uwazi wa pande zote ktk mchakato wa campaign na kupiga kura.
Huu ni 'unterahamwe'!
....ha ha ha ha nasikia mitambo ya TBC imechakachuwa !!!!!!
Hebu msome kauli zake hapo chini kabla hujajitoa ufahamu.!