Mangi Mkuu Thomas Marealle Mangi Mswahili

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,261
MANGI MKUU THOMAS MAREALLE MANGI MSWAHILI

Mara yangu ya kwanza kusoma historia ya Mangi Mkuu Thomas Marealle ilikuwa ndani ya Nyaraka za Sykes wakati natafiti kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Kwa bahati mbaya sikuweza kutumia yale niliyosoma katika kitabu nilichokuja kuandika kwa kuwa mengi katika yale niliyosoma yaikuwa mambo binafsi zaidi kuliko historia ya TANU na harakati za kudai uhuru ingawa jina la Nyerere lilikuwa likijitokeza.

Nimekuja kukutana na Mangi Mkuu Thomas Marealle katika Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama wakati natafiti maisha yake.

Napenda nieleze machache katika yale ambayo nimejifunza katika kusoma barua walizokuwa wakiandikiana watu hawa wawili kutoka Kilimanjaro kila mmoja akiwa na nafasi muhimu katika jamii ya kabila la Wachagga.

Thomas Marealle akiwa kwanza Mangi wa Marangu kisha Mangi Mkuu wa Wachagga wote na Rajabu Kirama yeye akiwa kiongozi wa Waislam Uchaggani.

Chief Thomas Marealle alikuwa kila akija Moshi Mjini lazima atakwenda numbani kwa Mama bint Maalim kumwamkua atakaa pale kuzungumza na kunywa kahawa.

Mama bint Maalim alikuwa katika wanawake mstari wa mbele katika TANU pamoja na akina mama wengine kama Bi. Halima Selengia na Bi. Amina Kinabo.

Chief Thomas Marealle yeye mwenyewe akijinasibu kuwa anaujua Uislam.

Hii inatokana na kuwa alifanyakazi Zanzibar na huko ndiko alipoingiliana na Waislam na kujenga mapenzi na Wazanzibar kupelekea yeye aje kuwa na uhusiano mzuri na Waswahili wa Moshi Mjini.

Chief Thomas Marealle alikuwa na ulimi mzuri wa kuzungumza Kiingereza na ukimfananisha na Mangi wenzake yeye elimu yake ilikuwa juu zaidi kwani alisoma London School of Economics and Political Science.

Baada ya kufanya kazi Zanzibar alifanya kazi pia Dar es katika miaka ya mwanzoni ya 1950 na alipata kuchaguliwa kuwa President wa Tanganyika African Government Servants Assocation Secretary akiwa Ally Sykes.

Yawezekana sana huku kuingiliana kwake na wanamji wa Dar es Salaam katika miaka ile kulimsaidia sana katika kuendesha utawala wake pale mwaka wa 1952 alipotawazwa na kuwa Mangi Mkuu.

Ingawa nguvu za Mangi zilikuwa zaidi Mlimani Uchaggani lakini Uislam ulijenga nguvu ya pekee nje ya utawala wa Mangi ambao ingawa nguvu hii haikuonyesha uadui wa wazi dhidi ya Ukristo Kilimanjaro, nguvu hii ilihitaji kulelewa kwa tahadhari na kujenga uhusiano mzuri na watawala waliokuwa Uchaggani.

Hivi ndivyo ikawa Chief Thomas Marealle akawa karibu na Waislam akihudhuria sherehe na misiba mingi ya Waislam akishuka Moshi Mjini kutoka Marangu akiwa ndani ya gari lake la fahari na bendera ikipepea.

Haijulikani kama Chief Marealle alipanga hili au ilitokea tu, madereva wake wote waliokuwa wakimwendesha walikuwa Waislam.

Mangi Thomas Marealle ana historia muhimu katika machifu na viongozi wa Tanganyika.

Inashangaza sana kuwa wanahistoria hawajatafiti maisha yake na kuyaandika kwa kina watu wakamjua.

1704835596076.jpeg

Mangi Mkuu Thomas Marealle na mkewe Bi. Elifuraha Ndesamburo Urio wakiwa Accra katika sherehe za uhuru wa Ghana 1957.​
 
View attachment 2866902

Lengo la huu uzi wako ni lipi?
 
Lengo la huu uzi wako ni lipi?
Yoda,
Kumueleza Mangi Mkuu Thomas Marealle kama nilivyomsoma katika kwanza Nyaraka za Sykes kisha katika Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama.

Pili kueleza yale ambayo wengi hawajapata kusoma popote kuhusu Chief Marealle.

Vipi kwani?
 
Ilikuwa ni lazima kuuzungumzia uchifu wa Marealle ukiunganisha na uislam? Tunataka utoe historia yake kama kiongozi wa wachaga na sio mwenye uhusiano na uislam
 
MANGI MKUU THOMAS MAREALLE MANGI MSWAHILI

Mara yangu ya kwanza kusoma historia ya Mangi Mkuu Thomas Marealle ilikuwa ndani ya Nyaraka za Sykes wakati natafiti kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.

Kwa bahati mbaya sikuweza kutumia yale niliyosoma katika kitabu nilichokuja kuandika kwa kuwa mengi katika yale niliyosoma yaikuwa mambo binafsi zaidi kuliko historia ya TANU na harakati za kudai uhuru ingawa jina la Nyerere lilikuwa likijitokeza.

Nimekuja kukutana na Mangi Mkuu Thomas Marealle katika Nyaraka za Rajabu Ibrahim Kirama wakati natafiti maisha yake.

Napenda nieleze machache katika yale ambayo nimejifunza katika kusoma barua walizokuwa wakiandikiana watu hawa wawili kutoka Kilimanjaro kila mmoja akiwa na nafasi muhimu katika jamii ya kabila la Wachagga.

Thomas Marealle akiwa kwanza Mangi wa Marangu kisha Mangi Mkuu wa Wachagga wote na Rajabu Kirama yeye akiwa kiongozi wa Waislam Uchaggani.

Chief Thomas Marealle alikuwa kila akija Moshi Mjini lazima atakwenda numbani kwa Mama bint Maalim kumwamkua atakaa pale kuzungumza na kunywa kahawa.

Mama bint Maalim alikuwa katika wanawake mstari wa mbele katika TANU pamoja na akina mama wengine kama Bi. Halima Selengia na Bi. Amina Kinabo.

Chief Thomas Marealle yeye mwenyewe akijinasibu kuwa anaujua Uislam.

Hii inatokana na kuwa alifanyakazi Zanzibar na huko ndiko alipoingiliana na Waislam na kujenga mapenzi na Wazanzibar kupelekea yeye aje kuwa na uhusiano mzuri na Waswahili wa Moshi Mjini.

Chief Thomas Marealle alikuwa na ulimi mzuri wa kuzungumza Kiingereza na ukimfananisha na Mangi wenzake yeye elimu yake ilikuwa juu zaidi kwani alisoma London School of Economics and Political Science.

Baada ya kufanya kazi Zanzibar alifanya kazi pia Dar es katika miaka ya mwanzoni ya 1950 na alipata kuchaguliwa kuwa President wa Tanganyika African Government Servants Assocation Secretary akiwa Ally Sykes.

Yawezekana sana huku kuingiliana kwake na wanamji wa Dar es Salaam katika miaka ile kulimsaidia sana katika kuendesha utawala wake pale mwaka wa 1952 alipotawazwa na kuwa Mangi Mkuu.

Ingawa nguvu za Mangi zilikuwa zaidi Mlimani Uchaggani lakini Uislam ulijenga nguvu ya pekee nje ya utawala wa Mangi ambao ingawa nguvu hii haikuonyesha uadui wa wazi dhidi ya Ukristo Kilimanjaro, nguvu hii ilihitaji kulelewa kwa tahadhari na kujenga uhusiano mzuri na watawala waliokuwa Uchaggani.

Hivi ndivyo ikawa Chief Thomas Marealle akawa karibu na Waislam akihudhuria sherehe na misiba mingi ya Waislam akishuka Moshi Mjini kutoka Marangu akiwa ndani ya gari lake la fahari na bendera ikipepea.

Haijulikani kama Chief Marealle alipanga hili au ilitokea tu, madereva wake wote waliokuwa wakimwendesha walikuwa Waislam.

Mangi Thomas Marealle ana historia muhimu katika machifu na viongozi wa Tanganyika.

Inashangaza sana kuwa wanahistoria hawajatafiti maisha yake na kuyaandika kwa kina watu wakamjua.

View attachment 2866902

Mangi Mkuu Thomas Marealle na mkewe Bi. Elifuraha Ndesamburo Urio wakiwa Accra katika sherehe za uhuru wa Ghana 1957.​
Kabisa ndio maana mpaka leo...kwa kichaga kanisani...wanaita..msikitini
 
Back
Top Bottom