Wamiliki wa mabasi jipangeni ujio wa treni Dar to Moshi

Hii koment nimeipenda sana,huu ni ukweli mtupu,asee hao uliotaja wajipange mapema kabla ya viliyo
Mbona reli ya kati na Tazara zipo lakini bado mabasi yanatamba route hizo mkuu, mi nadhani tusubiri kwanza tuone, maana reli yenyewe sio ya kisasa hata
 
Hakuna athari yeyote kwa wenye mabasi kumbuka inaishia mosho mjin watakaonufaika ni wa pale mjin anaekaa rombo haitaji tren . Gharama ya kupanda tren kwa anaishi rombo ni kubwa sana mfan dar to Moshimjin kwa tren 23500 kutoka moshi had rombo 10000 ,na naulo ya dar to rombo 30000 huon treni ghali sana.
Nauli ya Moshi kwenda rombo ni 2500 hadi 4500 kama utashukia Tarakea
 
Ngoja tuone,waweke tu haki pande zote zote mbili,treni wawe huru na mabasi pia wawe huru
 
Kweli nimeona treni za mizigo toka Dar hadi Moshi. Ila naomba yafuatayo:
Tusifanye haraka sana bila kuthibitisha usalama wa hiyo reli. Imekaa muda mrefu bila matunzo.
Tukianza, naomba iwe hata kila siku au wiki mara 4 ili hao mabeberu walioiua wakose pa kupumulia
Usafiri ukifika salama hata mara 4 tu tiyari Ubungo watauzia nyanya mle ndani
Hongera awamu ya tano. Wamethubutu nao wataweza tu
 
Wafanyabiasha wa Kanda ya kaskazini huwa wanajifanya Wana vichwavigumu kwenye kufanya biashara.ila kwa hili la train ya dar Moshi yafuatayo yatatokea.
1. Ubungo wapigabede wataanza kuwa wazururaji na vibaka kuongezeka dar.
2. Hotel zilizopangwa barabarani korogwe na mombo kufungwa na watu kukosa ajira, na huwa wanauza vyakula bei ya juu nahawana customer care hata kidogo.
3. Mabank kutakuweko na kilio kwa marejesho yatapungua 75% kwa waliokuwa wamekopea kununua mabasi Tena kwa gharama kubwa.
4.Moshi vibaku kuongezeka kwa Kasi kubwakutokana na wapigadebe kukosa kipato.
5.watu au wafanyabiasha wenye mabasi mabovu kuhama mjini.
6. Mabasi mengi kuanza route za vijijini ambako walisahauka.
7. Ajali za mabasi kupungua.
Ongezea chako
Haya yote yatategemea huduma zitakazotolewa na TRC. Wakitoa huduma bora watavutia watu na wakitoa huduma mbovu wengi watadharau na kupanda mabasi. BTW Hata zamani treni ilipokuwepo bado kuna watu walikuwa wanapanda mabasi. Ila ikuanza sasa hivi ni huduma ikiwa nzuri basi abiria wa mabasi watapungua. Inachotakiwa kufanya TRC ni: 1. Kuhakikisha muda wa safari kati ya Dar na Moshi unakuwa mfupi kadiri iwezekanavyo. Kwa mfano wakiweza kuondoka Dar around saa 2 usiku na saa 2 asubuhi wafike Moshi. 2. Mabehewa yanakuwa na kiwango kizuri eg: Viti, vitanda, Vyoo. 3. Huduma nzuri. Ukikataji tiketi na bei ziwe nzuri. Ndani ya mabehewa kuwa na huduma nzuri za vyakula na vinywaji.
 
Mjipange,mlisema hivyo hivyo kwa mwendo kasi mkianza mnashindwa ku maintain .Ona ndege zimenunuliwa akina wengine wakaambiwa wajipange matokeo yake ATC ndio inajitahidi kujipanga.Serikali na kutoa huduma ni vitu viwili tofauti kabisa wangebaki kusimamia sheria za nchi waachie watu wananchi watoe huduma au wawe kwenye PPP
 
Huko pandishe mizigo na mifugo,akitaka kujua jeuri wa watu wa kaskazini aende ubungo terminal na akae segera pale njia panda aone watu wanavyowahi kuhiji,treni apeleke burigi
Nani kakudanganya, sio kwa uchumi huu, kama watu wanapandaga hadi gari za magazeti ndio waache kupanda treni ?
 
Kama itatembea usiku muda ambao nilitakiwa nilale nyumbani nikalala kwenye tren daraja la pili nitakuwa nimeokoa siku nzima, pia wamiliki wa mahoteli wanatupiga sana, bila shaka treni zitasimama vituo ambavyo vyakula ni bei ya kawaida.
Treni hazisimami kwenye hoteli wewe! Chakula kinapikwa ndani ya treni na baa imo ndani ya treni, vyoo vimo vingi sana kila behewa.
 
Mkuu maendeleo ya nchi ni kila kitu kipo na watu wote wanapata abiria kutokana na ongezeko la watu. Jiulize inakuwaje nchi zilizoendelea huduma zote zipo na hakuna anaelalamika hata huku itafikia hivyo bus zipo, treni, taxi, coaster, malori na wote wanapata pesa. Mbona Mbeya treni tumeikuta na watu bado wanaagiza bus na biashara wanafanya, ishu ya mwendokasi mlisema hivyo hivyo wengine walikimbia kumbe kinachoongelewa hakipo.
Pia mkumbushe kuwa treni ipo mikoani dar mwanza,dar mbeya kanda ya kati nk na bado mabasi yapo
 
Hiyo treni itahujumiwa mpaka ife maana ni tishio kwao wabongo hawanaga plan B itakachoanza hapo baada ya hiyo treni kuanza kazi ni hujma tu baasi.
 
Back
Top Bottom