Wamiliki wa mabasi jipangeni ujio wa treni Dar to Moshi

Treni za Bongo hakuna namna zinaweza kuwa bora kiusafiri zaidi ya Mabus Mbeya kuna treni ya tazara lakini Mabus ni Mengi kuliko kawaidaa
Kwa umri wako nadhani hujawahi kupanda train.tuulize sisi tuliwahi kupanda train dar moshi.tukusimulie.pili train ya Tazara inapita porini kwa porini,ingepitia morogoro mjini, iringa mjini na makombako isingefikisha abiria.mwisho ukumbuke train ya Moshi inapita pugu,mombo,korogwe na same kote ni mjini na abiria na mizigilo ni mingi.
 
Mi naona Ile njia ya moshi ina abiria Wengi sana so syo rahis mabasi kukosa abiria
 
Nauli ni affordable kabisa Unaweza safari hata na ukoo mzima
FB_IMG_1574486213310.jpeg
 
Nilisikiliza BBC siku fulani wamiliki wa Malori Kenya walikuwa wakilia baada ya ujio wa SGR huko, hii inatokana na wafanyabishara wengi kutuma njia ya reli kusafirisha mizigo yao kwa sababu ya bei na usalama zaidi.

TRC imetangaza ujio wa treni kutoka Dar kwenda Moshi tena kwa kipindi ambacho Ubungo inakuwa na walanguzi wengi sana na nauli hupanda kutoka 20,000 hadi 50,000 (tena bei unatajiwa kwa jeuri).

Wamiliki wa mabasi jipangeni baadaye msije kulilia serikali kuwa hakuna wateja sababu ya ujio wa treni. Bora muweke bei za kueleweka na kila msafiri.

Unaweza kupanda basi ndani ya basi kuna aliyelipa 40, 50 na hata 30. Pia kibaya zaidi unaweza kukosa basi ikakubidi upande Coster au Eicher.

Nauli hizi hapa kwa treni madaraja yote

Hapa sijajua safari inaanza saa ngapi na kufika Moshi itachukua siku ngapi.
Huko pandishe mizigo na mifugo,akitaka kujua jeuri wa watu wa kaskazini aende ubungo terminal na akae segera pale njia panda aone watu wanavyowahi kuhiji,treni apeleke burigi
 
Nilisikiliza BBC siku fulani wamiliki wa Malori Kenya walikuwa wakilia baada ya ujio wa SGR huko, hii inatokana na wafanyabishara wengi kutuma njia ya reli kusafirisha mizigo yao kwa sababu ya bei na usalama zaidi.

TRC imetangaza ujio wa treni kutoka Dar kwenda Moshi tena kwa kipindi ambacho Ubungo inakuwa na walanguzi wengi sana na nauli hupanda kutoka 20,000 hadi 50,000 (tena bei unatajiwa kwa jeuri).

Wamiliki wa mabasi jipangeni baadaye msije kulilia serikali kuwa hakuna wateja sababu ya ujio wa treni. Bora muweke bei za kueleweka na kila msafiri.

Unaweza kupanda basi ndani ya basi kuna aliyelipa 40, 50 na hata 30. Pia kibaya zaidi unaweza kukosa basi ikakubidi upande Coster au Eicher.

Nauli hizi hapa kwa treni madaraja yote

Hapa sijajua safari inaanza saa ngapi na kufika Moshi itachukua siku ngapi.

Wakisafiri chini ya saa 15 nitashangaa sana.
 
Mi naomba TRL muwe makini nahujuma zinazoweza kupangwa maana watu wa huko wanathamini pesakuliko utu
 
Wafanyabiasha wa Kanda ya kaskazini huwa wanajifanya Wana vichwavigumu kwenye kufanya biashara.ila kwa hili la train ya dar Moshi yafuatayo yatatokea.
1. Ubungo wapigabede wataanza kuwa wazururaji na vibaka kuongezeka dar.
2. Hotel zilizopangwa barabarani korogwe na mombo kufungwa na watu kukosa ajira, na huwa wanauza vyakula bei ya juu nahawana customer care hata kidogo.
3. Mabank kutakuweko na kilio kwa marejesho yatapungua 75% kwa waliokuwa wamekopea kununua mabasi Tena kwa gharama kubwa.
4.Moshi vibaku kuongezeka kwa Kasi kubwakutokana na wapigadebe kukosa kipato.
5.watu au wafanyabiasha wenye mabasi mabovu kuhama mjini.
6. Mabasi mengi kuanza route za vijijini ambako walisahauka.
7. Ajali za mabasi kupungua.
Ongezea chako
Kwasababu ya behewa 20 ??
 
Treni ilikuwepo miaka iliyopita, na haiwezi kufanya mabasi yakose abiria, na kuhusu hizi safari za hija ya desemba bado hiyo treni haitamudu, labda iwe ina safiri kila siku, na ikiwa itasafiri usiku itakua bora na italeta ushindani.
 
kama ufipa wanaanza kwa mbwembwe ohh tunaenda na fulani baadae wanasusa au vipi
Huu mfano ni irrelevant,ungetoa ule mfano wa jiwe kujifanya anakubalika...or mara tunatoa elimu bure,tunanunua ndege zetu wenyewe kwa cash😂😂😂😂,uchaguzi ukifika anawaita watendaji na kuwaambia wakati wa kurudisha fomu wakimbie office ili wagombea wa chama chake wapite bila kupingwa na kuwakata wapinzani wote wanaogombea😂😂😂😂😂😂😂😂....mbwembwe nyingi za kujifanya anakubalika but anaogopa uchaguzi huru na haki...yaani akisikia uchaguzi anaogopa na anaweweseka kabisa😂😂😂😂
 
Hii koment nimeipenda sana,huu ni ukweli mtupu,asee hao uliotaja wajipange mapema kabla ya viliyo
Wafanyabiasha wa Kanda ya kaskazini huwa wanajifanya Wana vichwavigumu kwenye kufanya biashara.ila kwa hili la train ya dar Moshi yafuatayo yatatokea.
1. Ubungo wapigabede wataanza kuwa wazururaji na vibaka kuongezeka dar.
2. Hotel zilizopangwa barabarani korogwe na mombo kufungwa na watu kukosa ajira, na huwa wanauza vyakula bei ya juu nahawana customer care hata kidogo.
3. Mabank kutakuweko na kilio kwa marejesho yatapungua 75% kwa waliokuwa wamekopea kununua mabasi Tena kwa gharama kubwa.
4.Moshi vibaku kuongezeka kwa Kasi kubwakutokana na wapigadebe kukosa kipato.
5.watu au wafanyabiasha wenye mabasi mabovu kuhama mjini.
6. Mabasi mengi kuanza route za vijijini ambako walisahauka.
7. Ajali za mabasi kupungua.
Ongezea chako
 
Kuna mdau hapo juu kasema dar -kigoma ni siku3 wakati kwa basi si zaidi ya masaa 18 kama ni kweli basi shirika la reli ndio lijipange na sio wamiliki wa mabasi...ata kama hyo tren itakua na kumbi za starehe ndani bado siwezi kupoteza mda wangu njiani.
Ukitoka Dar saa nne usiku kwa gari na ukafika Moshi saa kumi na moja asubuhi ni mwendo wa siku mbili, hizo siku tatu ni siku moja tu unayoshinda safarini, hivyo ukiondoka Dar leo Jumatatu saa kumi kesho Jumanne alfajiri utakuwa Dodoma, jioni utakuwa Tabora na Jumatano asubuhi utakuwa Kigoma. Ukiondoka Dar leo saa kumi kesho asubuhi utakuwa Moshi.
 
mabasi tutaanzisha safari za usiku. unatoka Dar saa2 usiku Moshi unaingia saa12 asubuhi. Arusha saa 1 Wakati treni itaanza saa10 jioni. saa2 asububi inafika Moshi.
so ukikosa treni hiyo saa10 unaenda Ubungo tayari kwa kuondoka usiku saa2 na mwendo mdogo na bado unafika kabla ya treni. Watu wa mabasi tunajipanga kutoa ushindani kwa treni ikianza
 
Hakuna athari yeyote kwa wenye mabasi kumbuka inaishia mosho mjin watakaonufaika ni wa pale mjin anaekaa rombo haitaji tren . Gharama ya kupanda tren kwa anaishi rombo ni kubwa sana mfan dar to Moshimjin kwa tren 23500 kutoka moshi had rombo 10000 ,na naulo ya dar to rombo 30000 huon treni ghali sana.
 
Kama itatembea usiku muda ambao nilitakiwa nilale nyumbani nikalala kwenye tren daraja la pili nitakuwa nimeokoa siku nzima, pia wamiliki wa mahoteli wanatupiga sana, bila shaka treni zitasimama vituo ambavyo vyakula ni bei ya kawaida.
 
Mtoa mada kwani hii ndio treni ya kwanza nchini? Hadi sasa watu wanapanda mabasi ya kwenda Moro, Dom, Tabora, Kigoma na Mwanza.
 
kwa uwiano wa nauli na muda wa kufika kuna tofauti kubwa kati ya treni na bus

bado biashara ya mabasi itashamiri kwa hiyo kanda,malori ya Mizigo ndio wajipange zaidi
 
Back
Top Bottom