palalisote
JF-Expert Member
- Aug 4, 2010
- 8,335
- 1,463
Pole sana Mkuu ni rahisi kwa wale ambao hawajakutwa na hali kama hii kusema msamehe mkeo muendelee na maisha yenu lakini baada ya kumuona mkeo katika hali aliyokuwa nayo hata ile hamu ya kumgusa tu haipo tena achilia mbali idea ya kuishi nyumba moja. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba ulishamuonya lakini hakukusikia na kudharau onyo lako. Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na Ulimwengu sasa madili yake ya kutwa kucha tena bila kukushirikisha mumewe yamemtokea puani. Asilimia kubwa ya wanaume baada ya kumuona mke katika hali aliyokuwa nayo baada ya kubakwa wengi wangechukua maamuzi kama yako. Pole sana.
Mkuu umeongea point sana. Mkeo akikudharau wewe chuna tu muda utafika unamkumbushia tu: ni kiburi, unafiki na dharau zimemfikisha hapo wala asitafute mchawi wala sympathy.