Wamembaka mke wangu, nimeona niachane nae tu

Wamembaka mke wangu, nimeona niachane nae tu

nevile pablo

Member
Joined
Jun 15, 2015
Posts
18
Reaction score
124
Wakuu salaam,

Mimi ni mwenyeji humu ndani ila tu kutokana uzito wa habari hii niliona nije under cover kwa miaka 4 niliyokaa Jf kuna ambao tunajuana personally na ni wengi tu.

Ndoa yangu sasa ina miaka 8, tuna watoto 3 na tumejenga nyumba mbili, wiki mbili zilizopita mke wangu alibakwa na watu wawili waliokua wamejenga nae ukaribu kwa lengo la kumhadaa. Siku ya tukio alipigiwa simu na hao jamaa kwamba kuna shamba limepatikana Bagamoyo hivyo wakaliangalie sikuwahi kujua kama anahitaji shamba.Ilikuwa ni Jumapili asubuhi akaniacha home nimepumzika akaenda ili alione hilo shamba.

Hatukuwasiliana tena hadi saa nne usiku nilipotaka kujua mwenzangu yuko wapi simu iliita tu bila kupokelewa, nilishtuka kwa kweli maana hana tabia ya kutonipokelea simu, baada ya muda ikawa haipatikani, nikaanza kumpigia kwa namba yake ya Tigo ambayo iliita tu bila kupokelewa, ilipofika saa sita usiku nikampigia mama yake mzazi nae anasema kwa siku hiyo hajafika pale nyumbani.

Tukapeana jukumu la kuendelea kumtafuta hewani ingawa sio mara ya kwanza kurudi home mida hiyo, wakati mwingine anakuja mida hiyo anadai anatoka Kitchen Party na kadi anakuwa nayo kweli, nikimuuliza kwanini hakuomba ruhusa anajibu ""ningekuomba ungenikatalia"."

Hivyo nikajipa moyo kuwa huenda ameenda kwenye Kitchen Party kama siku zingine nikaendelea kusubiri, hadi saa nane usiku wapi hajaonekana, na bahati mbaya hakwenda na Gari lake siku hiyo lilikuwa na matatizo kwenye injini lilikuwa likisumbua wiki yote hiyo, nikaamua kwenda kwao usiku huo huo, nikamwambia housegirl kuwa mama akija sipo mnipigie ila mkae macho yenu yakiwa getini maana Leo hana Gari.

Tukiwa kwao tayari ilikuwa saa Tisa usiku tukashauriana kwenda Muhimbili baada ya kushauriwa na binamu wa wife aliepigiwa simu na mama mkwe usiku huo. Kwa upande wa majeruhi hakuwepo, nikapelekwa walipozipanga maiti zilizoingia usiku huo na ambazo hazijaenda mochwari sikufanikiwa, mama mkwe aliogopa kuzitazama.

Saa kumi na mbili asubuhi nikamrudisha mama mkwe kwake nami nikaa hapo hadi saa tatu nilipoona simu ya wife ya Tigo ikiita nikapokea, ni sauti ya kike ya mtu mwingine mwanamke. Kumbe wale jamaa wawili walimwekea dawa za kulevya wife kwenye soda hivyo akazimika na kuchukua chumba Gesti na kumwingiza humo, asubuhi tukaenda na ndugu kwa wife na mama mkwe baada ya kupokea hiyo simu ya binti wa mapokezi ambae alitumia simu ya wife ya kitochi waliyomwachia kitandani na kunipigia baada ya kukuta jina la hubby.

Tulipofika tulienda kwenye Chumba hicho tulikuta wife anakoroma na kutoa udenda wenye damu kwa mbali, pembeni yake kulikuwa na kondomu zilizotumika na kinyesi kiasi, mama yake alianza kulia kwa sauti.Kaka yake akampa kibano kikali receptionist aseme ukweli lakini binti wa watu akasema hajui chochote kuna watu wawili waliingia wamembeba na kulipia, na wakatoka asubuhi na mapema.

Anyway, kwa kifupi ni kwamba alitibiwa, alikaa hospital siku tano akipewa dripu na dawa za kuondoa sumu mwilini, hadi hali yake ikawa sawa, kwa ushirikiano alioutoa kwa polisi, na kwa kutumia TCRA ambao wana wapelelezi wao wanaoshirikiana na CID madalali wale walikamatwa wote wawili, mhudumu Wa gesti akaunganishwa kwenye kesi hiyo ya ubakaji ingawa yeye mashtaka yake yanasomeka tofauti na wenzie.

Wamepandishwa kizimbani mara moja na kesi yao kutajwa na imeahirishwa, wapo Segerea, sijajua walishindwa masharti ya dhamana au nini kilitokea maana mimi nilijitoa kwenye kesi hiyo nimewaacha ndugu waendelee nayo, nina sababu.

Tulikotoka na mwanamke huyu:-

Kiukweli Haya yaliyompata ni matokeo ya kunidharau na kutoniheshimu kama mumewe, amekuwa mtu wa ratiba masaa 24/7 per week, anachoamua anakifanya bila consultation na Mimi, mfano:-Aliamua kujiunga na masomo ya jioni baada ya kazi kama ifuatavyo. Alijiunga na diploma ya IT ucc inayoanza saa 11 jioni hadi saa moja jioni, hapo hapo akajiunga na masters ya MBA inayoanza saa moja na kuisha saa nane usiku usiku hadi kufika home ni saa tano na kitu nikamuuliza familia yako nani atai attend? Majukumu yako nani atayafanya? Akanijibu ndio hivyo nimeshajiunga, hakuwa na sababu ya kujiunga na IT angeanza na masters (prioritizing)

Wakuu, mambo yake yote ni siri hasemi mipango yake, anajifanya mtu wa madili anadili na wanaume kuhusu biashara mbali mbali bila kunishirikisha ingawa ni muajiriwa. Mama yake ndio msiri wake mkubwa.

Akienda kokote atoi taarifa hadi akifika huko ndio anasema "" hny nipo kwenye send off"".Nikajaribu kutafuta huenda ana mwanaume nje lakini kiukweli upepelezi na intelligence iliyotukuka ilithibitisha pasipo na shaka kuwa hajawahi Ku cheat.

Simu zake zote niliwahi kuziweka under 24 hrs surveillance kupitia watu wangu wanaofanya kwenye mitando ya simu lakini mawasiliaño yote na wanaume ni ya kikazi na madili mbalimbali. Pia niliwahi ku hack namba za simu na account za kijamii zote pia nilitoka bila bila. Lakini hata bedroom life ni nzuri tu, maana ukishindwa kumshika mke kwingineko basi utamshika kwenye haki ya ndoa, mwanamke hawezi kutumikia wanaume wawili kusionekane kasoro,lakini hata upande huo kwa kweli hakuna tatizo.

Sababu niliyoigundua ni mali alizoachiwa na marehemu baba yake ambazo wamepewa mirathi kama miaka minne iliyopita, wapo watatu, baba yao aliacha plot na nyumba nyingi kwenye prime areas hivyo mke wangu amepewa sehemu nyingi anazochukua kodi kubwa sana achilia mbali sehemu alizouza. Hivyo ni mkakati wake na mama yake anifiche vitu vingi ili nisije kumdhulumu anaona ni bora ashirikiane na mama yake kwenye mambo yake.

Hati zangu anajua zilipo in case nimeanguka ghafla ila za kwake zote alizopewa plot zaidi ya 6 ambazo tayari amebadilisha tayari majina kuja ya kwake kazificha nisipopajua nimeshachoka, nashukuru Mungu hili tatizo la kubakwa na kulawitiwa limetokea nimepata pa kumwachia, nasubiri awe vizuri psychologically nianze mchakato wa talaka. Naomba muelewe sikuja hapa kuomba ushauri bali kuwapa funzo wa akina dada na wengine.

Maana nilimwambia hivi. """ hizi mbio zote unazokwenda resi ipo siku watanipigia simu nikufuate Mochwari au Muhimbili"". Na kweli imetokea. Sina haja na pesa zake nina zangu nazopata kazini nilizofanyia maendeleo makubwa tu na miradi kadhaa.Wanashangaa kwanini sijihusishi na hiyo kesi, ni kwa sababu nilimuonya mtoto kwao hakusikia na akanidharau, tried to be a man and more than a man lakini ndo tunazidi kuvurugana. Maana kuna watakaokimbilia kudai "" act like a man"" humu Jf as walikuwa wanaona I am not acting like one.

Mungu akikupa mke wa ovyo hata uki act like Tyson haitasaidia kitu. Sasahivi wamerundikana hapo nyumbani mara leo wamletee pastor, kesho wamletee counselor, mimi jioni naenda zangu kwenye bia narudi nipo vizuri nalala.Juzi alikuja mshauri nasaha kuniambia ameniletea habari njema vipimo vimeonesha wife hana HIV so natakiwa nifurahi.

Nikamjibu mwambie afurahi mwenye matokeo mwenyewe mimi sitaendelea nae, sasa sijui amewaambia, maana mama mkwe ananiangalia jicho kama vile anamwangalia shetani.

Anyway nadhani nimepona rohoni kwa kuwaambia habari hii , sihitaji ushauri, nina maamuzi tayari. Huenda victim mwenyewe akipata mme mwingine atabadilika.
 
Pole sana
Hupaswi kuwa na jazba

Mke ni dhamana yako kama ilivyo mwanao

Waliombaka mkeo pia 'wamekutukana na wewe na kukuonyesha dharau kubwa'

Hata kama utasema umuache mkeo...kama adhabu yake vipi hao walio mbaka?

Why usijue ukweli wote?

Yaani watu waje wambake mkeo na kumlawiti na wwe unaona tu bora kumuacha mkeo ndo umemaliza?

Na hao jamaa wakihonga mahakama watatoka nje free kabisa?

Nimi ningekuwa wewe ningeanza na hao watu..nijue ukweli na nihakikishe wanazikwa ndo narudi kumuadhibu wife
 
Pole mkuu hupaswi kumuacha huyo mwanamke unachotakiwa kufanya ni kumsamehe na kuanza ukurasa mpya wa mapenzi yenu pili fikria kuhusu watoto wenu, nina hakika atakuwa kapata somo.
 
Kutokana na tabia ya usiri ya mkeo bila shaka kuna sababu ya hao jamaa kumbaka mbali na tamaa za kimwili, jitahidi uijue kabla hijakuathiri na wewe
ila endapo utamrudia sasa hivi atakusikiliza na kukutii kupita kiasi kwani somo alolipata ni kubwa
 
Pole sana
hupaswi kuwa na jazba

mke ni dhamana yako kama ilivyo mwanao

waliombaka mkeo pia 'wamekutukana na wewe na kukuonyesha dharau kubwa'

hata kama utasema umuache mkeo...kama adhabu yake vipi hao walio mbaka?

why usijue ukweli wote?

yaani watu waje wambake mkeo na kumlawiti na wwe unaona tu bora kumuacha mkeo ndo umemaliza?

na hao jamaa wakihonga mahakama watatoka nje free kabisa?

mimi ningekuwa wewe ningeanza na hao watu..nijue ukweli na nihakikishe wanazikwa ndo narudi kumuadhibu wife
Kubakwa ni moja tu ya matukio mengi yaliyomuudhi mleta Uzi, mie nampa pole ila mtihani mkubwa
 
Kweli kaka maamuzu uliyochukua ni sahihi kabisa wanawake wasomi wanatabia ya disparage waume zao bora upate hata house wife hakueshimu kuliko et mnachuma wote na hakueshimu km,mwanaume! Japo sijahoa lkn maamuzi uliyoyachukua ni ya kishujaa kakangu.
 
Ingawa stori nyingi za humu ndani ni chai....


Umeongra meeeeeengi lakini ukiangalia ulichokiandika ni hasira ya pesa/ madili /mafanikio ya mkeo ndio yanayokutesa

Na umetumia kubakwa kwake kama sababu


Nikirudi kwa wanawake...mnachochagua waume chagueni wanaume sio tu wanaowapenda kwa dhati kiasi cha kuwa tayari kusupport ndoto zenu. ..watakawaelewa..... na kujitoa kwenu kwa hali na mali.....mwisho mhakikishe Nyumba yenu iwe na mawasiliano
 
Msamehee na endelea nae,wewe sio wa kwanza inawatokea wengi,hapo samehe jikaze kiume na baada ya hili mkeo atakuheshimu na kukuthamini kama mwanzo
 
Pole sana kiongozi...
Ni kweli, kama nyumba haina mawasiliano, maisha ya ndoa yanakuwa machungu sana. Ubabe baina ya wanandoa wala hausaidii bali hubomoa tu. Japo umesema hutaki ushauri, ingekuwa mimi ningetaka kujua sababu za hao madalali kumla mande mke wangu, ningewafanyia mbaya hilo halina ubishi...
 
aiseeeeeeeeeeeee ndoa ndoa ndoaaaaaaaaaaaaaaa ndoa ndoaaaaaaaaaaaa
 
Asiyefunzwa na ***** hufunzwa na ulimwengu! Ameshapata funzo. Pili fahamu kuwa watoto bado wanahitaji malezi yenu. Pamoja na yote aliyokutendea msamehe, kuwa sehemu ya maumivu na mateso yake na atapona kimwili,kiroho na kisaikolojia.

Hili pigo litambadilisha na mtaanza maisha mapya. What if kama ingekuwa ni wewe ulilewa usiku wakakubaka na yeye akachukua maamuzi ya kukuacha? Ungekisikiaje? Fahamu kwamba Hali hii ndo inafanya watu wanajiua!Hakuna aliyemkamilifu! Msamehe! Mwisho nakusihi uende kwa kiongozi wako wa Dini na utapata Masada zaidi! Asante!
 
Pole mkuu, umeshasema hutaki ushauri ila ni km ulikuwa unarafuta mahali pa kuutua mzigo wako wa hasira, napo ni JF!

Wanawake mara nyingi hudanganywa na wanawake wenzao, mfano mzuri ni huyo mama mkwe wako, mkeo mwisho wa siku atamlaumu sana mama yake kwa kuirarua ndoa yake kupitia ushauri wake mbaya.....


Hapo kuna mambo mawili, ukimuacha huyo mwanamke watoto wataathirika sana kumkosa mzazi mmoja! Ila pia ukimuacha ndio atakudharau mara mia zaidi!
 
Ingawa stori nyingi za humu ndani ni chai....


Umeongra meeeeeengi lakini ukiangalia ulichokiandika ni hasira ya pesa/ madili /mafanikio ya mkeo ndio yanayokutesa

Na umetumia kubakwa kwake kama sababu


Nikirudi kwa wanawake...mnachochagua waume chagueni wanaume sio tu wanaowapenda kwa dhati kiasi cha kuwa tayari kusupport ndoto zenu. ..watakawaelewa..... na kujitoa kwenu kwa hali na mali.....mwisho mhakikishe Nyumba yenu iwe na mawasiliano

mkuu BADILI TABIA usimwelewe huyu jamaa kama ana hasira hebu jivike viatu vyake kama ndo limekukuta yani uone ikoje hapo. Kwa kweli sipendi kuna baadhi ya wanawake chake ni chake chako ni cha wote yani chakwake hata utafute na microscope huwezi kuona kila kitu kwake ni siri ukimkanya hakanyiki kisa mko level moja ya elimu.

Na baadhi ya wanaume huona mbali na kukupa kiashiria cha isije ikatokea hivi au inaweza kuwa hivi lakin yeye atakaid mwishowe baya ulomwambia litampata mbelen. Ni tatizo la kutomweshimu mume unakuwa kila kitu kwenu mguu kwenu kama hujaolewa yani kamfanya mama yake msiri wake zaid ya mume? Anyaway simlaum kwa maamuzi yake bora kuponya moyo.
 
Back
Top Bottom