Wamembaka mke wangu, nimeona niachane nae tu

Wamembaka mke wangu, nimeona niachane nae tu

Yote uliyoyaandika ni sahihi, nilikua nakanusha sentensi yako kuwa nilichoka kuonya
Sikuchoka, hadi siku ya tukio anaondoka asubuhi ya jumapili huku natoa risala kwa mke wangu na kumuonya
Nime spend the last 4 yrs nikionya na kukemea na kushauri hadi siku ya tukio

Point yangu ni kuwa msitafute mchawi, mchawi ni yeye mwenyewe ambae hakusikia maonyo

Its ok wakuu, mungu anajua yote
 
Najua kabisa kuwa huu unaweza ukawa sio muda muafaka kwako kufikia uamuzi sahihi (whether wa kuacha au kuendelea naye), kwa sababu utakuwa katika lindi kubwa la ghadhabu. Tulia, jipe muda na utaweza kunyambua situation nzima kwa kuitazama kwa macho mawili.

Tunaenda kwenye nyumba za ibada, kila iitwapo leo, na tunayoambiwa almost ni yale yale...acheni dhambi, mrudieni Mungu wenu, msiseme uongo...and the like. Lakini je, tumewahi kusema kuwa siendi tena ibadani kwa kuwa nayakumbuka yote wanayosema? Jibu ni hapana, na tutaendelea kukumbushwa kila siku mpaka tunaingia kaburini.

Kuamua kuishi wawili si mtihani mdogo, kila mtu amekuja na makuzi na malezi yake (ambayo yamezaa tabia tofauti tofauti), tunafanyaje ili mwisho wa siku tuongee lugha moja? Ni pamoja na kila mmoja kuyachukulia mapungufu ya mwenzio, kukumbushana hapa na pale inapobidi na kadhalika. Labda nikuulize kitu kimoja, lisingetokea la kubakwa ulipanga umuache lini?

Kwenye couples, sijui Mwenyezi Mungu ana makusudi gani, mara nyingi utakuta mmoja ana tabia 'pole' kulinganisha na mwingine. Na tabia zote mbili zikiwa ni zile 'petroli', hiyo ndoa hata haina muda. Sasa kama wewe ulikuwa kwenye hii tabia 'pole', basi usichoke kuitumia kuiweka sawa (manageable level) hiyo ya mkeo. And stop counting kuwa ninaonya kila siku Monday to Friday...Hata kama anajifanya haambiliki, kuna mawili anayosikia. Haya leo limemkuta hili, ndio kufunzwa na ulimwengu sasa, unafikiri atakuwa yule wa jana?

Anyway bro, maamuzi unayo wewe mwenyewe, na bado tutaheshimu maamuzi yako, vyovyote yatakavyo kuwa. Kwa kuwa kiatu umevaa wewe, sisi wengine hata hatujui kinakubana na kukutoa sugu na malengelenge upande upi....

Anyway naomba tuombeane tu
Its ok
 
Hii thread ni ngumu mno....

Mimi nakuombea mema tu nevile pablo, Mungu mwenyewe akafanye njia pasipo na njia
 
Last edited by a moderator:
Wewe ndio wasema hakukuwa na ndoa miaka 4...Uliza mashehe, wachungaji na wanasheria ndoa ni nini...Mna firigisana daily tena kwa hiari (hambakani) afu useme ndoa ilikuwa mfu????Hii ndoa hiko alive and kicking...Tatizo huu ubakaji uloingilia kati... na hasira za pesa ambazo zimekuwa zikimzonga jamaa..Kuna jirani yetu mkewe alibakwa...walivamiwa na majambazi home...lakini baadae iligundulika ni ugomvi wa mumewe kibiashara maana hawakuiba chochote...Mtaa mzima unajua na mke hakudai talaka kwa mume alomponza...Ila sishangai...comments zinawakilisha wanaume wengi katika ubora wao...UMIMITypes ya The Boss ni wachache na kwa mwanamke mwenye bahati ya kuwapata aisee ashikilie vizuri maana ni every woman's dream
Nashangaa kuona wanaume wengi hawampatii ushauri mzuri mwanaume mwenzao,wanaume wengi wakikosana na wanaume wenzao kibiashara au kuchukuliana wanawake visasi huwa wanarudisha kwa mkewe kwa kumbaka tu,hakuna jingine
 
"Only cowards run away from their partners in time of troubles"

Shikamoo The Boss
Kaunga naomba nimkiss mumeo,ah no nimbusu tu!
 
Last edited by a moderator:
maelezo yako yanaonesha wazi upendo ulishatoweka siku nyingi sana ila tu basi huku na jinsi kama inavyojulikana mwanamke mjinga huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe hali kadhalika alie mwerevu huijenga kwa mikono yake mwenyewe. nimejaribu kuvaa viatu vyako nimeona hata ukimrudia haitabadilisha moyo wako kwa kua tu umeshaamua basi ni basi hakuna kitu kizuri kama kuupa moyo kile unachotaka go on na maamuzi yako hata kama ni kifo kiwatenganishe ila hapa kubaki skushauri

nikiaribu kuvaviatu vya huyu dada kwanza namuona ni mwanamke asie na heshima kwa mmewe hata uwe na mal kias gani mme atabakikua mme tu na haibadiiki hafai huyu.
Who is seeking revenge? And against who?
You have missed the point my friend, go back to my writings and read line after line

As for divorce
Yes am doing it, right now, am just waiting for things to cool down a little bit

Ina maana walioachana wote duniani wakaanza upya hawana furaha?
Kwa nn watu waendelee na ndoa zinazowaletea machungu!?

Search urself my friend
 
"Only cowards run away from their partners in time of troubles"

Shikamoo The Boss
Kaunga naomba nimkiss mumeo,ah no nimbusu tuuu
 
Last edited by a moderator:
Na hata ukimuacha, utakayemuoa, naye atabakwa, au atakuwa na mambo yake tu. Bora shetani uliyenaye, kuliko aliye mbali nawe.


Ni rahisi sana kushauri hasa kama ww sio victim. ILa hili la huyu jamaa ni Complicated. I remember kuna Mzee aliwahi niambia, Kama Mke hafai Ww ndio unajua, wala hakuna mwingine wa kukwambia.

Acha afanye sawa sawa na halmashauri yake ya kichwa inavyomwongoza.
 
kwasababu ni mungu mwenyewe ndio amewaunganisha tumwombe yeye akatende jambo, kulegeza moyo wako na kusamehe,
nyote wawili mpo katika kipindi kigumu na wewe hutaki ushauri. pole sana ni jambo zito ila naimani kama ni mpango wa mungu mambo yatenda sawa.
 
Muda unavyozidi kwenda kusamehe ni jambo jepesi. Jambo zito ni kusahau scene aloiona guest na pride yake iliyogaragazwa kwenye mchanga. Haya mambo mawili ndio yanaweza kuinusuru ndoa ktk hali hii. Lakini nani anaweza kusahau tukio hili. nani anaweza kuirudisha heshima yake?
 
Ninaomba tu rafiki yangu msamehe bure na amejifunza na sasa atkuheshimu sana. Mke wa kwanza ukimwacha utapata mwingine kama huyo. Msamehe msamehe na maisha yataendelea.
 
Pole sana
Hupaswi kuwa na jazba

Mke ni dhamana yako kama ilivyo mwanao

Waliombaka mkeo pia 'wamekutukana na wewe na kukuonyesha dharau kubwa'

Hata kama utasema umuache mkeo...kama adhabu yake vipi hao walio mbaka?

Why usijue ukweli wote?

Yaani watu waje wambake mkeo na kumlawiti na wwe unaona tu bora kumuacha mkeo ndo umemaliza?

Na hao jamaa wakihonga mahakama watatoka nje free kabisa?

Nimi ningekuwa wewe ningeanza na hao watu..nijue ukweli na nihakikishe wanazikwa ndo narudi kumuadhibu wife

umeona ee ..mim nimemshangaa sn uyu mkaka ni mme wa aina gn cjui ..mim naanza kuhis anahusika na yeye..aliona amkomoe kidzain hzo mkewe..yn ht chembe ya huruma hana wala woga..lol ..ndo mana uyu mdada alikua anafanya mambo yake koz anamatatzo uyu mwanaume...yani kaniudhii
 
Nna mashaka uyu mme km anahuska na hcho ktendo ..walah jmn ..hv mke anavyouma alf abakwe uchukulie poa eti atapata mme mwngne...mkuu jichunguze deep side una matatIzo ndo mana mkeo aliona bora nae afanye maendeleo yk kmy kmy..you hv prbl thou hujatuambia side yk ..
 
Huwa nashangaa sana inapofika kwenye kumhukumu mwanamke kila mtu anataka kutupa jiwe wa kwanza. Najiuliza mara ngapi mwanaume mkewe anamsihi na kumuonya na hamsikilizi katu katu. Ila yakimpata majanga jamii yote inategemea mwanamke kusimama hapo.

Mara ngapi mwanaume mzinzi na mlevi ana anapata ajali na mke anauguza kwa kuogesha na kubadili hata bed pans? Mara ngapi mwanaume mleviii anamtesa mkewe na anapokaanga ini mkewe analaumiwa kwa kushindwa kummudu na 'kuua' mume.

Mimi nakulaumu kwa kushindwa kumlinda mkeo. Mkeo anatoka nyumbani anaenda huko huna habari hadi giza linafika. Hebu mpe support mkewe acha mambo ya aibu. Unajikomoa na wewe hapo

Hata mm namshangaa sana huyu jamaa kama mume ni kichwa cha familia umeshindwa kusimamia familia yako ndo mana matatizo yametokea ungemuacha kupindi anarudi usiku au kipindi ameenda kiaina bila kukuambia uko kimya inamana ulikuwa unamuogopa kwanza mpaka Mwanamke anatoka Jumapili anaenda kwenye dili zake huko ww umelala ndani unashindwa hata kumuliza uko wapi au ni dili gani hizo . Na kama ww na yy ni kitu kimoja na mwili mmoja iweje ukubali afanye mambo bila makubaliano yenu wawili mbaya zaidi kwenye kesi umejitoa tukisema ww ndo umewatuma wambake tumekosea.samaki mkunje angali mbichi ulishindwa kumkunja. Kwa ushaur wangu tulia kaza moyo mrudie mkeo. Pole sana kwa matatizo
 
Mbona hii story inaonekana huyu mume ndie mtuhumiwa no moja?

Ameandaa Hao watu na mpango Mzima wa kubakwa huyu dada wa watu.
 
pole sana kaka yangu,ushauri wangu mkubwa ni kwamba msamehe tu,nina hakika 95% Atabadilika kupitia hayo yaliyomkuta.ishini pamoja mlee watoto mlionao.
 
Kaka Pablo Uko Sahihi Ndoa Sio Vita Wala Kuumizana Hisia!Take Your's And She Will Take Her's.
 
Nna mashaka uyu mme km anahuska na hcho ktendo ..walah jmn ..hv mke anavyouma alf abakwe uchukulie poa eti atapata mme mwngne...mkuu jichunguze deep side una matatIzo ndo mana mkeo aliona bora nae afanye maendeleo yk kmy kmy..you hv prbl thou hujatuambia side yk ..

kwa muda niliamua kuwa nasoma mawazo ya watu tu jukwaa hili, lakini kwa ulichokiandika imenibidi nitie neno hapa: ni kweli kabisa mke ni wathamani sana tena sana na anatakiwa kuthaminiwa sana tena sana kwani ni mke na mume pekee ndio wanao-shape ulimwengu. hata hivyo inaonekana wewe kichwa chako ni kizito sana tena sababu ya uzito huo ni matokeo ama ya kutowahi kukumbana na tatizo kubwa la kimahusiano au ndo kwanza unaanza mahusiano na hivyo unahisi kuwa kila mwanamke anapomdharau mmewe basi ni lazima na huyo mwanaume awe na tatizo; si lazima iwe hivyo swtbeib! kuna wanawake wengine ( na hawa wako wengi) wanapokuwa na uhakika wa kipato hasa cha kumzidi mumewe na familia yao ikawa njema, dharau haziishi kwa mwanaume huyo na hata kwa familia ya mumewe. siku hizi mnamsemo wenu maarufu eti "HUYO SIO NDUGU YAKO" ni wakati sasa wanawake mpate somo, Mungu alikuumba kuwa chini ya mwanaume na hivyo ndivyo ilivyo na itabaki kuwa hivyo milele na milele amina!!! hizo haki sawa zitawapumbaza na mtaishia kupata matatizo yanayofanana na yaliyompata huyo mwenzenu kisa tu kujifanya na nyie mna haki sawa na wanaume hadi kuleta dharau na kutoambilika. Huwezi kwenda kinyume na mpango wa MUNGU ukabaki salama!
 
Back
Top Bottom