BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,098
...Ama kweli ukistaajabu ya hayawani utaona ya taahira! sijui anataka kumdanganya nani huyu? bora apelekwe Mirembe
Posted Date::1/30/2008
CCM yadai hoja ya ufisadi Benki Kuu Tanzania ni yao
Tausi Mbowe na Habel Chidawali, Dodoma
Mwananchi
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimedai suala la uchunguzi kuhusu matatizo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) halikuibuliwa na wapinzani bali ni ya chama hicho.
Akitoka taarifa ya Kamati Kuu ya CCM iliyokutana mjini Dodoma juzi kwa waandishi wa Habari, Katibu Mwenezi wa CCM, John Chiligati alisema jana kuwa suala la uchunguzi kuhusu mgogoro wa Benki Kuu ya Tanzania haukuibuliwa na wapinzani bali ilikuwa hoja ya CCM tangu mwanzoni mwa mwaka jana.
Chiligati alisema Kamati Kuu ya CCM inasikitishwa na taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa sakata la BOT liliibuliwa na wapinzani na kwamba si la kweli kwani rais alitoa tamko tangu mwanzoni mwa jana kabla ya wapinzani hawajaibua hoja hiyo.
Wapinzani wanatumia hoja hiyo kujipatia umaarufu, wamekuwa wakisema kuwa upinzani ndio watu wanaoweza kuibua hoja zenye maslahi kwa Watanzania wakati si kweli, kwani CCM imekuwa ikishughulikia hayo tangu mwanzoni mwa jana na sasa suala hilo lilikuwa katika hatua za mchakato, alisema Chiligati.
Alisema wapinzani walikuwa wakipitia wazo ambalo tayari lilikuwa linafanyiwa kazi kwa kutafuta mkaguzi baada ya kutangaza tenda kupata mkaguzi, hivyo hawana sababu ya kusema kuwa ni wao walioibua hoja hiyo.
Chiligati alisema kamati hiyo imeiagiza serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafilisi mali zao watu wote watu watakaobainika na Tume hiyo kuwa walijipatia fedha kwa njia zisizokuwa halali.
Wakati huo huo kamati hiyo imefanya uteuzi wa viongozi wake katika kamati ya maadili baada ya ile ya kwanza kumaliza muda wake.
Walioteuliwa katika kamati mpya ni Andrew Chenge , Pindi Chama na Yusuf Omar Yusuf ambao alisema kuwa wataanza kazi yao kuanzia sasa na watakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia sasa.