Wameinama, wameinuka wanaona haya haoo!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
...Ama kweli ukistaajabu ya hayawani utaona ya taahira! sijui anataka kumdanganya nani huyu? bora apelekwe Mirembe

Posted Date::1/30/2008
CCM yadai hoja ya ufisadi Benki Kuu Tanzania ni yao
Tausi Mbowe na Habel Chidawali, Dodoma
Mwananchi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimedai suala la uchunguzi kuhusu matatizo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) halikuibuliwa na wapinzani bali ni ya chama hicho.

Akitoka taarifa ya Kamati Kuu ya CCM iliyokutana mjini Dodoma juzi kwa waandishi wa Habari, Katibu Mwenezi wa CCM, John Chiligati alisema jana kuwa suala la uchunguzi kuhusu mgogoro wa Benki Kuu ya Tanzania haukuibuliwa na wapinzani bali ilikuwa hoja ya CCM tangu mwanzoni mwa mwaka jana.

Chiligati alisema Kamati Kuu ya CCM inasikitishwa na taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa sakata la BOT liliibuliwa na wapinzani na kwamba si la kweli kwani rais alitoa tamko tangu mwanzoni mwa jana kabla ya wapinzani hawajaibua hoja hiyo.

Wapinzani wanatumia hoja hiyo kujipatia umaarufu, wamekuwa wakisema kuwa upinzani ndio watu wanaoweza kuibua hoja zenye maslahi kwa Watanzania wakati si kweli, kwani CCM imekuwa ikishughulikia hayo tangu mwanzoni mwa jana na sasa suala hilo lilikuwa katika hatua za mchakato, alisema Chiligati.

Alisema wapinzani walikuwa wakipitia wazo ambalo tayari lilikuwa linafanyiwa kazi kwa kutafuta mkaguzi baada ya kutangaza tenda kupata mkaguzi, hivyo hawana sababu ya kusema kuwa ni wao walioibua hoja hiyo.

Chiligati alisema kamati hiyo imeiagiza serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafilisi mali zao watu wote watu watakaobainika na Tume hiyo kuwa walijipatia fedha kwa njia zisizokuwa halali.

Wakati huo huo kamati hiyo imefanya uteuzi wa viongozi wake katika kamati ya maadili baada ya ile ya kwanza kumaliza muda wake.

Walioteuliwa katika kamati mpya ni Andrew Chenge , Pindi Chama na Yusuf Omar Yusuf ambao alisema kuwa wataanza kazi yao kuanzia sasa na watakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia sasa.

walikua wapi muda wote huo? Hii inaonyesha kweli hii skendo imegusa kwenye nyeti za chama sasa inatafutwa njia ya kuhakikisha hoja inakuwa ya kwao kisha kujisafisha na atakuja mchekeshaji mmoja wa sisiem atasema "kama tulichukua hela kwa ajili ya uchaguzi iweje tena sisi weneyewe tujiumbue"?
 
kama hili skendo waliliibua wao mbona speaker (Mh Sita) na baadhi ya wabunge wa CCM walikuwa wanapinga kwamba hakuna kitu kama hicho wakati Dr Slaa alipokuwa anafichua uchafu huu?. Uchunguzi ulifuatia baada ya nchi wafadhili kama USA, UK nk kulivalia njuga suala hili. Lakini kabla ya hapo CCM walisema hizo ni kelele za mpita njia haziwasumbui kuwanyima usingizi.
 
Hizi story za BOT zimekuwa nyingi na kila moja wapo inakuja na spin yake, sijui lengo la hii habari ni nini asa, wakati report yenyewe haijawekwa hadharani.
 
Yaani wabongo tushasahau Richmond, Buzwagi, Mahalu, Ditto,.....gademu!!!

Nyani, believe me, we are fanatics and sick upstairs! Sisi kujikomboa hasa inatakiwa kukomboa IQ zetu kwanza, lakini hii wanasema ni born-with!! Sasa ndiyo unakuja ule msemo tutakuwa hivi hivi!!
 
inasikitisha sana lakini ndio ukweli wenyewe,labda alikuwa amelewa nafikiri maana mtu mwenye akili sijui kama anaweza kuongea hivyo.
 
this is insanely insane........ukisoma sana hizi story unaweza kuchukua gobore kwenda kufanya massacre huko sijui wapi wanapokutania!!!! Oooooovyo.
 
Na Joyce Kassiki, Dodoma

KAMATI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi imeitaka
Serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni
pamoja na kufilisiwa mali wote watakaobainika
kuhusika na ufisadi katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Akizungumza na waandishi wa habari jana ,Katibu Mwenezi wa
CCM, Kepteni John Chiligati alisema uamuzi huo
ulifikiwa na wajumbe wa Kamati Kuu (CC) walikutana juzi
mjini hapa chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete.

Alisema lengo la kufilisi mafisadi hao ni kurejesha
fedha za umma walizochukua katika benki hiyo kwa njia
isiyo halali.

Aidha alisema kuwa Kamati Kuu imeishauri Serikali
kuiagiza tume iliyoundwa kuchunguza suala hilo
inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kutoa
taarifa kwa umma mara kwa mara ili wananchi
wajue maendeleo ya uchunguzi huo badala ya
kusubiri kipindi cha miezi sita muda ambao umetolewa kwa
tume hiyo kukamilisha uchunguzi huo.

Bw. Chiligati alisema mtu wa kwanza
kuibua hoja hiyo ni Rais Kikwete ambaye alinzisha
ukaguzi ndani ya BoT mapema mwaka jana kabla ya
wapinzani kutoa hoja wakati wa Mkutano wa Bunge la
bajeti .

Akizungumzia hali ya machafuko ya kisiasa nchini Kenya
ambayo yamesababisha mapigano na mauaji baada ya
kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi mwishoni mwa mwaka
jana ,Bw. Chiligati alisema ,CCM imesikitishwa na hali
inayoendelea nchini humo.

“Mauji hayo na uharibifu wa mali unawaathiri wananchi
wasio na hatia hivyo ni muhimu yakomeshwe
haraka,”alisema Bw. Chiligati na kuongeza;

“Kenya ni majirani zetu na ni mwanachama mwenzetu katika Jumuiya
ya Afrika Mashariki hivyo uvunjaji wa amani uliopo
huko unaathiri pia majirani zake kiuchumi, kiusalama
na kuleta wasiwasi katika mustakabali mzima wa
uanzishwaji wa Shirikisho la Afrika Mashariki”

Alisema Kamati Kuu imetoa mwito kwa viongozi wa vyama
vya siasa wa pande zinazovutana kutuliza jazba za
wafuasi wao na kuwata kuacha mapigano badala yake
watumie kikamilifu fursa ya mazungumzo
ya kutafuta suluhu yanayoongozwa na Katibu Mkuu
mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Bw.Kofi Annan.

Akizungumzia kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali madukani
alisema Kamati Kuu imeilekeza Serikali kuchukua hatua zilizo ndani
ya uwezo wake kudhibiti tatizo hilo kwani jambo hilo linachangia ugumu wa maisha kwa wananchi.

“Japokuwa upandaji wa bei katika uchumi mkubwa wa
Taifa umepungua kutoka asilimia 7.3 hadi
asilimia 6.4 Oktoba mwaka jana , hali ya uchumi katika
ngazi ya kaya inaonesha kwamba vitu madukani
vimepanda bei,”alisema.

Alisema Serikali ilielekezwa itafute mbinu za
kudhibiti bei za vyakula ,vifaa vya ujenzi hususan
saruji na bei za vitu vya matumizi mengine ya nyumbani.

Kwa upande wa mikopo ya wajasiriamali, alisema kuwa
katika kipindi cha pili ya utoaji mikopo hiyo,Serikali
imeongeza wakopeshaji kutoka benki mbili hadi kufikia
wakopeshaji 13 ambapo asasi mbalimbali za fedha
zitahusika kutoa mikopo.

Alisema awamu ya kwanza benki mbili ndizo zilizohusika
na shughuli hiyo ambapo imesababisha wananchi wengi wa
vijijini kushindwa kunufaika na mkopo huo wa Serikali
wenye masharti nafuu.

Alisema katika awamu ya pili, kila wilaya itaguswa na
na shughuli hiyo itaanza kwa zile wilaya ambazo hazikuguswa
katika awamu ya kwanza na kusema kuwa utaratibu wa
awamu hii, utawashirikisha viongozi wa kata na vijiji
kwa lengo la kuwaelewa wananchi wanaopewa mikopo ili
waweze kufuatiliwa kwa ajili ya urejeshaji wa mikopo
hiyo.

Akizungumzia suala la maadili ya viongozi, alisema Kamati Kuu
imeishauri Serikali kutazama upya maadili ya wale
wanaotumia nyadhifa zao kwa manufaa binafsi.

Iliamua kanuni na maadili ya CCM irekebishwe na
viongozi wa chama hicho wametakiwa kuwa mfano bora
katika kuonesha maadili hayo.

Aidha alisema Katika kikao hicho kamati hiyo iliteua
wajumbe wapya wa Kamati ya Maadili ambapo
walioteuliwa ni Bw. Andrew Chenge, Bibi Pindi Chana
Bw.Yusuf Omary na Bibi Fatuma Said Ally.

Alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM, kamati hiyo inakuwa chini ya uenyekiti wa Mwenyekiti wa chama hicho Rais Kikwete ambapo Katibu Mkuu wa chama hicho ndiye Katibu wa kamati hiyo.
 
...Ama kweli ukistaajabu ya hayawani utaona ya taahira! sijui anataka kumdanganya nani huyu? bora apelekwe Mirembe

Posted Date::1/30/2008
CCM yadai hoja ya ufisadi Benki Kuu Tanzania ni yao
Tausi Mbowe na Habel Chidawali, Dodoma
Mwananchi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimedai suala la uchunguzi kuhusu matatizo ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) halikuibuliwa na wapinzani bali ni ya chama hicho.

Akitoka taarifa ya Kamati Kuu ya CCM iliyokutana mjini Dodoma juzi kwa waandishi wa Habari, Katibu Mwenezi wa CCM, John Chiligati alisema jana kuwa suala la uchunguzi kuhusu mgogoro wa Benki Kuu ya Tanzania haukuibuliwa na wapinzani bali ilikuwa hoja ya CCM tangu mwanzoni mwa mwaka jana.

Chiligati alisema Kamati Kuu ya CCM inasikitishwa na taarifa zinazotolewa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa sakata la BOT liliibuliwa na wapinzani na kwamba si la kweli kwani rais alitoa tamko tangu mwanzoni mwa jana kabla ya wapinzani hawajaibua hoja hiyo.

Wapinzani wanatumia hoja hiyo kujipatia umaarufu, wamekuwa wakisema kuwa upinzani ndio watu wanaoweza kuibua hoja zenye maslahi kwa Watanzania wakati si kweli, kwani CCM imekuwa ikishughulikia hayo tangu mwanzoni mwa jana na sasa suala hilo lilikuwa katika hatua za mchakato, alisema Chiligati.

Alisema wapinzani walikuwa wakipitia wazo ambalo tayari lilikuwa linafanyiwa kazi kwa kutafuta mkaguzi baada ya kutangaza tenda kupata mkaguzi, hivyo hawana sababu ya kusema kuwa ni wao walioibua hoja hiyo.

Chiligati alisema kamati hiyo imeiagiza serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwafilisi mali zao watu wote watu watakaobainika na Tume hiyo kuwa walijipatia fedha kwa njia zisizokuwa halali.

Wakati huo huo kamati hiyo imefanya uteuzi wa viongozi wake katika kamati ya maadili baada ya ile ya kwanza kumaliza muda wake.

Walioteuliwa katika kamati mpya ni Andrew Chenge , Pindi Chama na Yusuf Omar Yusuf ambao alisema kuwa wataanza kazi yao kuanzia sasa na watakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia sasa.

Kwa kweli kwanza hana aibu kabisa kama mtu mzima umechafua hewa mbele ya watoto ni wakati muafaka kukiri kwani watoto nao wanajua kwamba mzee kaachia ambacho huwa hawafanyi ni kuto kucheka kitu ambacho mtendaji utajua kwamba hawajasikia. Hoja ya BoT ni yao katika maana ya wao ndiyo wezi lakini aliyeibua ni Dr Slaa wa Chadema. Mtu akikwambia unayo hoja ya kujibu ile hoja ni yako unapaswa kuijibu. CCM wezi WAKUBWA
 
Excuse me.....kweli hii kali, namsubiria Makamba na Tinga Tinga wataongea upupu gani jamani hawa vipi akina Chilingati et al wako wazima kweli upstairs...natamani kutukana
 
Excuse me.....kweli hii kali, namsubiria Makamba na Tinga Tinga wataongea upupu gani jamani hawa vipi akina Chilingati et al wako wazima kweli upstairs...natamani kutukana

Mwenzio imenibidi kutumia aina ya tusi kiutu uzima maana nimekereka sana. Hawa wanatufanya hatuna akili.... Hakika siasa ni mchezo mchafu sana
 
tuwe wa kweli hii ilikuwa na ajenda ilioibuliwa na CCM ila walitaka iwe ktk muundo mwengine basi.

tuwasifu wapinzani hasa Dr Slaa kwa kuhakikisha kuwa CCM hawafuniki funiki kama walivyotaka basi.

na suala la madini liko wazi ni la CCM ambapo mheshimiwa kikwete aliahidi kulifanyia kazi ila CCM walitaka kulifanya kivyao vyao na hapa asifiwe Kabwe kwa kulikomalia halipindishwi na kufanya wanavyotaka wao

mwisho ss kwetu si muhimu nani kaibua ila muhimu ni kuhakikisha mali ya nchi yetu haliwi kijinga bila ya kuinufaisha nchi yetu hilo ndio muhimu kwetu

tuache sifa sote na tuangalie ni vipi tutaweza kusaidia nchi yetu

nnaomba kutoa mchango wangu
 
Ukisikia vichekesho ndiyo hivi sasa. Hivi Chiligati na akili zake zote pamoja na watoto wake wote alionao anaweza akasimama na kuongea upumbavu huu mbele za vyombo vya habari? sitaki kuamini kwamba ana matatizo ya akili,hii inaonyesha jinsi gani maji yalivyowakamba shingoni,pale bungen siku zile walipinga kwa nguvu zote kuwepo kwa suala hili,hata waziri Meghji naye alipinga kwa nguvu zote na Balali akakataa kujiuzuru akidai yeye ni msafi na BOT ni safi. Kulikoni leo Chiligati? Ovyoooooooooooooooooooooo
 
Yaani wabongo tushasahau Richmond, Buzwagi, Mahalu, Ditto,.....gademu!!!

Hakisauliki kitu! Richmond na Buzwagi tunasubiri ripoti ya hizo kamati ili tuone watakuja na usanii wa aina gani. Dito huyu yeye kishawalipa wazazi bulungutu nadhani kesi ndiyo imeshafutwa. Mahalu bado tunafuatilia kesi iliyoko mahakamani. NN, ili awamu ya Watanzania kusahau kashfa mbali mbali ilikuwa mwaka 47! 2008 hatusahau kitu!
 
Mwenzio imenibidi kutumia aina ya tusi kiutu uzima maana nimekereka sana. Hawa wanatufanya hatuna akili.... Hakika siasa ni mchezo mchafu sana

Hizi wanaleta kwa sababu wanajivunia amani
Hapa kipigo kikitembea hakuna wakuja na majibu ya kipuuzi namna hii kufikiri wezako ni wapumbafu,wajinga .
 
Unajua problem ya chama tawala kwa ujumla wao huwaza kuwa there is nothing good that can come out of the opposition parties.
Sasa haya imewashika kwa kuona kumbe upinzani pia ni usefull.
 
Kama hawa uwezo wao wa kufanya spining unaishia hapo basi jua hata maisha bora kuna siku watasema hiyo ilikuwa ajenda ya Kikwete na sio ya chama ....

Kama mafisadi wanakaa na kuona njia ya kujisafisha ni kuandika ama kusema uongo na wanamtuma mtu ambaye awali nilikuwa namheshimu yaani chiligati kumbe naye hana tofauti na ze comedy -makamba basi huko hakuna tena .

Haya halimashauri kuu NEC watakaa na kusema buzwagi wao ndio walimtuma Zittoo......
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom