MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
You want a simple answer? POLITICS!
Serikalini ni shamba la bibi, unaweza ukawa successful kwenye private sector kwa sababu kule kuna wenyewe so hauwezi kufanya upuuzi ila vitu vya serikali ni kama havina mwenyewe kwa hy unakula uwezavyo.
Mkuu Eliahkamwela, sijakuelewa hata kidogo, nadhani MM Mwanakiji ametumia hekima zaidi kutokujibu. He is right.
Back to the point.
Kwa maoni yangu tatizo la Tanzania ni katiba mbovu. Huko Serikalini mtu ye yote akianza kuchapa kazi anakatishwa tamaa na bosi wake, ambaye naye ameshakata tamaa siku nyingi kutokana na yeye pia kukatishwa tamaa. kukatishana tamaa huko kunaanzia ngazi ya kitongoji kwenda juu hadi kwa mawaziri na bosi wao Rais. Ndo maana hali mbaya ktk sekta ya umma imeanzia kipindi cha Mwinyi hadi leo. Ifahamike kuwa serikalini hakuna check and balance and there is no accountability ambayo ilipaswa kuwepo kama tungekuwa na Bunge imara na mahakama imara. Kwa hiyo, waziri anafanya atakavyo as long as Rais hajui kumfuatilia au hawezi, at the same time anajua wabunge hawawezi kumfanya kitu cho chote. Na Waziri akiwa mchapa kazi anawafanya waliochini yake wizarani hadi ngazi ya chini yake wawe kama yeye, na akiwa vise versa (mla rushwa) the opposite is true (Bahati mbaya sekta ya umma haina watu wa jinsi hiyo).
Kwa upande Sekta binafsi top management ikiwa safi ina maanisha kuwa kila mtu lazima achape kazi na taasisi hiyo itasonga mbele daima.
Unasikitisha sana!! no research...no data...no right to speak!!!
Mwaikambo aliyekuwa Bima (N.I.C) ni kabila gani?? inajulikana alipoifikisha bima yetu...
Serikalini walikuwepo na bado wapo wengi kutoka Kyela mbona watu bado wanalalamika??
Acha ukabila...Lawama siyo ya mtu mmoja wala kabila au dini bali ni ya mfumo...ambao tulirithi
toka kwa wakoloni na tukashindwa kuukarabati ili utunufaishe. Mfano ni tafsiri ya maneno "MALI YA UMMA"
haikuwekwa katika hali ya kila mtu ahisi kuwa ni yake na anawajibika kuilinda. Utaona watu wanasifiwa mitaani
kutokana na utajiri walioupata kutokana na wizi wa mali ya umma. Wengine wamefanikiwa kuwa watunga sheria
kupitia chama tawala na hata upinzani. wezi na waharibifu wa miundombinu mfano nyaya za umeme na simu, vyuma vya
madaraja, mabomba, alama za barabarani na nyara za serikali tunawajua, tunaishi nao mitaani, ni rafiki zetu, dada zetu, kaka
zetu na wazazi wetu, hatujajitolea kwa dhati kuilinda mali yetu. Badala yake kila jambo tumeligeuza kuwa siasa. Hakuna ukombozi wa maana tutakaoupata hata tukibadili majina ya vyama vitakavyounda serikali endapo FIKRA zetu hazitabadilika.
[/COLOR]
Mpumbavu,mjinga na ms**ng****** mkubwa wewe!
Nani kakwambia watanzania hatuna akili?
Kweli sisi wanyakyusa kwetu ni Malawi?
*********** WEEEEEEEEEE;Acha niishie hapa nisije kula ban;ndio kwanza nimetoka jela!!!
Mkuu Eliahkamwela, sijakuelewa hata kidogo, nadhani MM Mwanakiji ametumia hekima zaidi kutokujibu. He is right.
Back to the point.
Kwa maoni yangu tatizo la Tanzania ni katiba mbovu. Huko Serikalini mtu ye yote akianza kuchapa kazi anakatishwa tamaa na bosi wake, ambaye naye ameshakata tamaa siku nyingi kutokana na yeye pia kukatishwa tamaa. kukatishana tamaa huko kunaanzia ngazi ya kitongoji kwenda juu hadi kwa mawaziri na bosi wao Rais. Ndo maana hali mbaya ktk sekta ya umma imeanzia kipindi cha Mwinyi hadi leo. Ifahamike kuwa serikalini hakuna check and balance and there is no accountability ambayo ilipaswa kuwepo kama tungekuwa na Bunge imara na mahakama imara. Kwa hiyo, waziri anafanya atakavyo as long as Rais hajui kumfuatilia au hawezi, at the same time anajua wabunge hawawezi kumfanya kitu cho chote. Na Waziri akiwa mchapa kazi anawafanya waliochini yake wizarani hadi ngazi ya chini yake wawe kama yeye, na akiwa vise versa (mla rushwa) the opposite is true (Bahati mbaya sekta ya umma haina watu wa jinsi hiyo).
Kwa upande Sekta binafsi top management ikiwa safi ina maanisha kuwa kila mtu lazima achape kazi na taasisi hiyo itasonga mbele daima.
Nilikuwa nimepata nafasi ya kuzungumza na jamaa zangu kadhaa ambao kwa kweli wamefanikiwa katika sekta binafsi hapo nyumbani. Wengi wa hawa jamaa walikuwa serikalini na baadaye wakaenda uraiani wakashiriki kuanzisha makampuni au mashirika na wamekuwa very successful. Namkumbuka mmoja wao ambaye alipopewa kampuni kuiendesha wafanyakazi walianza kulalamika ati "amepewa Mswahili, kampuni itakufa". Miaka kama kumi baadaye ni mojawapo ya mashirika yanayofanya vizuri zaidi Tanzania na yakiwa yamefikia viwango vya kimataifa.
Sasa katika kufuatilia fuatilia nikagundua ni kweli wapo Watanzania wengi tu ambao wameweza kujionesha wanaweza kuwa viongozi, na wasimamizi vizuri na wana principles za utawala nzuri na wamefanikiwa. Yaani, unaweza kabisa kuona kazi zao kiasi kwamba wakati mwingine mtu akiambiwa anayefanya hivi ni "Mtanzania" watu wanaonekana kushangaa kana kwamba Mtanzania hawezikuwa meneja au mtawala mzuri.
Sasa, ni hapo ndio nimejikuta najiuliza hasa tukiangalia mashirika kama Reli, ATC n.k na hata taasisi nyingine ambazo zinaonekana kuwa na matatizo ya kiutawala (kama hospitali zetu). Sasa najiuliza kwanini watu hawa wenzetu waliofanikiwa katika sekta binafsi na wana rekodi za kugeuza mashirika au makampuni na kuwa bora hawapewi nafasi au kuitwa hata kwa mkataba mnono wa kugeuza mashirika yaliyoshindwa? Hivi ni kweli kabisa tunahitaji menejimenti toka nje?
Fikiria kwa mfano Chizi wa ATCL amepewa kuligeuza hilo shirika hivi ni kwa kiasi gani amejitofautisha kuwa ni mtawala na meneja mzuri? Hivi, kumpa mtu Reli wakati hajawahi kuendesha kampuni yoyote ya maana au kuonesha kuwa anaweza kugeuza a non-profitable company into a profitable one inaingia akilini kweli?
Au ni kweli hawa Watanzania waliofanikiwa kwenye sekta binafsi ni tishio kwa wanasiasa hasa kama wataletwa kuendesha mashirika ya umma? Na kama wapo ni kama watu gani ambao unafikiria wanaweza wakawa wazuri sana kwenye serikali kwa sababu wana rekodi nzuri uraiani?