Je Kindamba ni mtu sahihi UDART? Ana exposure yoyote kuhusu sekta ya usafirishaji?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,125
Mradi wa DART umepewa mkurugenzi mpya ambaye ni Kindammba. Kwa utendaji wa Kindammba kama mkuu wa mkoa sidhani kama huyu ni kiongozi wa nafasi za kitaalamu kama makampuni.

Najiuliza baraza la mawaziri lililokaa wiki hii na kumpitisha lilijishauri vyema au lilitumia influence ya kiongozi mkuu kumpitisha?

Kwanini Tanzania tunaogopa kuzishindanisha hizi nafasi watu waombe? Nakumbuka Nehemia Mchechu aliwahi kushauri nafasi za wakuu wa mashirika ziwe zinaombwa badala ya kuwa na nafasi za uteuzi ila mfumo ulimpinga vikali.

Huyu Kindammba siyo mtu wakupewa shirika lililokufa kwasababu yeye mwenyewe ni tegemezi wa fikra na hajawahi kuwa mtu wakuchukua hatua pale anapoona ubadhirifu.
 
Hivi kusimamia hayo mabasi kunahitaji akili gani?

Kuna watanzania wana mabasi karibu 200 na yanasimamiwa na meneja ambaye hata shule hana, na yanaenda vizuri.

Wakati mradi unaanza lazima kulikuwa na maandiko ya jinsi ya kuuendesha, yafuatwe, magari yafanyiwe service, hapo ndio pa muhimu, na ndipo panaua miradi mingi.

Apewe fedha, apewe fedha, apewe fedha anunue mabasi ya kutosha, afanye service na idara ya service aiwekee unoko wa kutosha. Pia, mabasi yanayofuata kuagizwa yatumie gesi ili kupunguza gharama za uendeshaji na uchafuzi wa mazingira.

Baadae, tuweke treni fupi za mjini
 
Kwanini Tanzania tunaogopa kuzishindanisha hizi nafasi watu waombe? Nakumbuka Nehemia Mchechu aliwahi kushauri nafasi za wakuu wa mashirika ziwe zinaombwa badala ya kuwa na nafasi za uteuzi ila mfumo ulimpinga vikali.
Hata mawaziri inatakiwa wawe wanatuma maombi kwa nafasi wazitakazo na wapewe mikataba ya kazi walizoomba na ikitokea wakaenda kinyume na mkataba wa kazi wawajibishe kisheria.

Tumechoka na teuzi zisizo na tija
 
Kuna Dart na Udart,Kindamba ni mkurugenzi wa Udart mkurugenzi wa Dart ni Athuman Kihamia.
Kindamba amechukua nafasi ya Gilliard Ngewe na Athuman Kihamia aliteuliwa Januari 11,2024 kuchukua nafasi ya Dk. Edwin Mhede.
UDART ni Kampuni ya mabasi yaendayo haraka na DART ni Wakala wa mabasi yaendayo haraka.
Nb: Sijajua kiundani tofauti na mipaka ya shughuli zao au nani anawajibika kwa mwenzake.
 
Mradi wa DART umepewa mkurugenzi mpya ambaye ni Kindammba. Kwa utendaji wa Kindammba kama mkuu wa mkoa sidhani kama huyu ni kiongozi wa nafasi za kitaalamu kama makampuni.

Najiuliza baraza la mawaziri lililokaa wiki hii na kumpitisha lilijishauri vyema au lilitumia influence ya kiongozi mkuu kumpitisha?

Kwanini Tanzania tunaogopa kuzishindanisha hizi nafasi watu waombe? Nakumbuka Nehemia Mchechu aliwahi kushauri nafasi za wakuu wa mashirika ziwe zinaombwa badala ya kuwa na nafasi za uteuzi ila mfumo ulimpinga vikali.

Huyu Kindammba siyo mtu wakupewa shirika lililokufa kwasababu yeye mwenyewe ni tegemezi wa fikra na hajawahi kuwa mtu wakuchukua hatua pale anapoona ubadhirifu.
DART ni mfupa ulioshindikana.....kama alishindwa TTCL, acha ajaribiwe huko!
 
Mkuu Kindamba kabla ya kuwa mkuu wamkoa nadhani aliwahi kuwa director kwenye private sector sikumbuki ni wapi Ila naamini ni MTU sahihi ingawa dart ni janga it's a sinking ship
Alikuwa branch manager Diamond Trust Bank kitu kama hicho, kuna mtu kaandika huku juu kusimamia mradi wa magari ni issue ndogo sana cha msingi awe mtendaji na awasimamie wa chini wapige kazi, kindamba si kiongozi mkali, si mwepesi wa kuchukua maamuz magumu hapendi kugombana na watu ndivyo alivyo toka akiwa head prifect Tambaza, Azania.
 
Alikua Shirika la Mawasiliano Tanzania aka TTCL... Usafirishaji nadhan ni Mawasiliano pia...TTCL alikua anasafirisha information..UDART Atasafirisha watu...ninaamini akitumia Experience yake atamudu...SIASA ISIMGUSE KABISA.
 
Hivi hizi haziwezi kuunganishwa zikawa 1? Na umuhimu wa kuzitofautisha ulikuwa ni nini?
Kuna Dart na Udart,Kindamba ni mkurugenzi wa Udart mkurugenzi wa Dart ni Athuman Kihamia.
Kindamba amechukua nafasi ya Gilliard Ngewe na Athuman Kihamia aliteuliwa Januari 11,2024 kuchukua nafasi ya Dk. Edwin Mhede.
UDART ni Kampuni ya mabasi yaendayo haraka na DART ni Wakala wa mabasi yaendayo haraka.
Nb: Sijajua kiundani tofauti na mipaka ya shughuli zao au nani anawajibika kwa mwenza
 
Mradi wa DART umepewa mkurugenzi mpya ambaye ni Kindammba. Kwa utendaji wa Kindammba kama mkuu wa mkoa sidhani kama huyu ni kiongozi wa nafasi za kitaalamu kama makampuni.

Najiuliza baraza la mawaziri lililokaa wiki hii na kumpitisha lilijishauri vyema au lilitumia influence ya kiongozi mkuu kumpitisha?

Kwanini Tanzania tunaogopa kuzishindanisha hizi nafasi watu waombe? Nakumbuka Nehemia Mchechu aliwahi kushauri nafasi za wakuu wa mashirika ziwe zinaombwa badala ya kuwa na nafasi za uteuzi ila mfumo ulimpinga vikali.

Huyu Kindammba siyo mtu wakupewa shirika lililokufa kwasababu yeye mwenyewe ni tegemezi wa fikra na hajawahi kuwa mtu wakuchukua hatua pale anapoona ubadhirifu.
unajua historia ya kindamba? unajua alitoka wapi kabla ya kuwa mkuu wa mkoa?
 
Alikuwa branch manager Diamond Trust Bank kitu kama hicho, kuna mtu kaandika huku juu kusimamia mradi wa magari ni issue ndogo sana cha msingi awe mtendaji na awasimamie wa chini wapige kazi, kindamba si kiongozi mkali, si mwepesi wa kuchukua maamuz magumu hapendi kugombana na watu ndivyo alivyo toka akiwa head prifect Tambaza, Azania.
Tbia za kizmkaz,hatatoboa,ni muda wake wa kula per diem za kutosha na trip za India ,kingereza,USA,ujeruman,south Africa na Dubai kujifunza mwendokasi wa huko wamewezaje🤣🤣🤣
 
Kabla ya ukuu wa Mkoa alikuwa mkurugenzi mkuu wa TTCL
Ni miongoni mwa wakurugenzi vilaza aliyewahi kuiongoza TTCL, Sera yake ilikua ni kupachika wanawake warembo (aliopenda kuwaita visu) kwenye ngazi mbali mbali za management, matokeo yake ilikua ni kuliongezea shirika hasara. Inshort Kindamba ni mwanasiasa mzuri tu ila kwenye suala la Uongozi hususani upande wa usimamizi ni kilaza.

Katika kipindi cha uongozi wake ndio kipindi kilichoongoza kwa wataalamu mbali mbali kuondoka TTCL baada ya kuona shirika limegeuka kuwa brothel (danguro) ambapo binti ukiwa mrembo unateuliwa kuwa manager, huku wataalamu wakiwekwa pembeni bila ya kusikilizwa na utaalamu wao
 
Kuna comment hapo juu, inasema alikuwa branch manager then Mkurugenzi TTCL then RC then Mkurugenzi Udart.

Day amepewa uteuzi TTCL nilishahukumu ni total failure, ikawa hivyo, kwanini exposure na experience ilikuwa haitoshi kupewa shirika kama TTCL na inawezekana ni ukada ndio ulisababisha akawekwa pale.

Narudia tena, sidhani kama pia anaweza kufanikisha kitu pale UDART, nafasi za kiutendaji zinahitaji watu wenye exposure kwenye business husika jumlisha experience ya kufanya kazi underpressure,deadlines na targets.
 
Kuna Dart na Udart,Kindamba ni mkurugenzi wa Udart mkurugenzi wa Dart ni Athuman Kihamia.
Kindamba amechukua nafasi ya Gilliard Ngewe na Athuman Kihamia aliteuliwa Januari 11,2024 kuchukua nafasi ya Dk. Edwin Mhede.
UDART ni Kampuni ya mabasi yaendayo haraka na DART ni Wakala wa mabasi yaendayo haraka.
Nb: Sijajua kiundani tofauti na mipaka ya shughuli zao au nani anawajibika kwa mwenzake.
DKT. ATHUMAN KIHAMIA
Athuman Kihamia photo

Dkt. Athuman Kihamia​

Mtendaji Mkuu DART (UDART)
Wasifu : Usiyoyajua kuhusu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC), Dkt. Athumani Kihamia alivyovuruga Halmashauri

Dr. Athumani Kihamia akiwa kazini wiki iliyopita March 2024

1710096250766.png
 
kufikia level ya kuwa Mkurugenzi la shirika linalohitaji matokeo lazima mhusika awe na series ya promotion au awe ameshika position tofauti tofauti za maamuzi na hata kuwa na evidence ya kuleta mafanikio au ubunifu fulani mahala ulioleta matokeo chanya.
 
Back
Top Bottom