Wamefanikiwa kwenye sekta Binafsi kwanini hawaitwi kuiokoa serikali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wamefanikiwa kwenye sekta Binafsi kwanini hawaitwi kuiokoa serikali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jan 25, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nimepata nafasi ya kuzungumza na jamaa zangu kadhaa ambao kwa kweli wamefanikiwa katika sekta binafsi hapo nyumbani. Wengi wa hawa jamaa walikuwa serikalini na baadaye wakaenda uraiani wakashiriki kuanzisha makampuni au mashirika na wamekuwa very successful. Namkumbuka mmoja wao ambaye alipopewa kampuni kuiendesha wafanyakazi walianza kulalamika ati "amepewa Mswahili, kampuni itakufa". Miaka kama kumi baadaye ni mojawapo ya mashirika yanayofanya vizuri zaidi Tanzania na yakiwa yamefikia viwango vya kimataifa.
  Sasa katika kufuatilia fuatilia nikagundua ni kweli wapo Watanzania wengi tu ambao wameweza kujionesha wanaweza kuwa viongozi, na wasimamizi vizuri na wana principles za utawala nzuri na wamefanikiwa. Yaani, unaweza kabisa kuona kazi zao kiasi kwamba wakati mwingine mtu akiambiwa anayefanya hivi ni "Mtanzania" watu wanaonekana kushangaa kana kwamba Mtanzania hawezikuwa meneja au mtawala mzuri.
  Sasa, ni hapo ndio nimejikuta najiuliza hasa tukiangalia mashirika kama Reli, ATC n.k na hata taasisi nyingine ambazo zinaonekana kuwa na matatizo ya kiutawala (kama hospitali zetu). Sasa najiuliza kwanini watu hawa wenzetu waliofanikiwa katika sekta binafsi na wana rekodi za kugeuza mashirika au makampuni na kuwa bora hawapewi nafasi au kuitwa hata kwa mkataba mnono wa kugeuza mashirika yaliyoshindwa? Hivi ni kweli kabisa tunahitaji menejimenti toka nje?
  Fikiria kwa mfano Chizi wa ATCL amepewa kuligeuza hilo shirika hivi ni kwa kiasi gani amejitofautisha kuwa ni mtawala na meneja mzuri? Hivi, kumpa mtu Reli wakati hajawahi kuendesha kampuni yoyote ya maana au kuonesha kuwa anaweza kugeuza a non-profitable company into a profitable one inaingia akilini kweli?
  Au ni kweli hawa Watanzania waliofanikiwa kwenye sekta binafsi ni tishio kwa wanasiasa hasa kama wataletwa kuendesha mashirika ya umma? Na kama wapo ni kama watu gani ambao unafikiria wanaweza wakawa wazuri sana kwenye serikali kwa sababu wana rekodi nzuri uraiani?
   
 2. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #2
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watanzania wanaoweza kuongoza wapo na ni wengi tu! Ni bahati mbaya haijatokea kasumba ya kuwatumia watu kutoka sekta binafsi katika shughuli za umma. Bado ule userikali serikali, umejigubika na siasa basi tunaona watendaji bora ni hatari sana. Lakini naamini vitu vichache vinahitaji kutokea ili kuonyesha umuhimu wa watendaji safi wa sekta binafsi kusaidia serikali.

  1. kwanza kutambua uchumi ndio unaoendesha siasa, sio wanasiasa ndio wanaondesha serikali.

  2. Kutengeneza mfumo wa kutambua sekta binafsi na kuipa nguvu katika maswala ya viongozi. Nikimaanisha kwamba, viongozi wa mashirika mbalimbali waangaliwe kwa undani, na maprofile yao yawekwe tu kwenye jamii!
   
 3. F

  FJM JF-Expert Member

  #3
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni lile lile la siku zote - uwajibikaji. Kama napata mshahara, posho, shangingi na dereva, safari za nje na mapochopocho mengine bila kujali ufanisi wa shirika ninaloongoza kwa nini nijisumbue? Kwenye sekta binafsi unajua mapema kabisa kuwa cheque au mlo wako utatokana na utendaji wa kazi. Ukizembea kampuni inakufa na chakula nyumbani kinapotea. Sasa kwenye mashirika ya umma hela ikipungua (hata ya safari) unapiga simu hazina.

  Serikali ya Tanzania kama inataka kurudisha nidhamu na ufanisi kwenye idara/mashirika yake ni LAZIMA (nasisitiza) waanze mfumo wa kazi kwa mkataba. Kuanzia mawaziri, wakurugenzi na wakuu wa idara mbalimbali wapewe kazi kwa mikataba. Kama hufikii kiwango kilochowekwa kwenye mkataba kazi hakuna. Simple. Tunaona kwenye private sector kama kampuni inafanya vibaya general manager au ceo anaachia ngazi. Serikalini tunalisha watu wanaozika mashirika kwa sababu gani?
   
 4. howard

  howard Senior Member

  #4
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  tatizo kubwa tulilonalo watanzania ni ubinafsi tu. mradi kila kitu napata na naishi vizuri na familia yangu basi mimi kufanikiwa ama kutofanikiwa kwa mashirika ya umma hainihusu kabisa. nikija kwenye hoja ya kuchukuliwa watu kutoka private sectors wanaofanya vizuri huwa inategemea sana raisi ana washauri wa aina gani? ni wale wanaohitaji mabadiliko nchini ama mradi wao wanakula posho kwisha habari yake? tunahitaji mabadiliko kuanzia kwa mheshimiwa raisi mpk washauri wake maana kwani unafikiri viongozi mazuri ya hao watu hawayaoni? mfano mzuri angalia national housing Corporation (NHC) yule mchechu anafanya mazuri mangapi? NHC imekuwa kama imefufuka upya lilikuwa linakufa shirika lile. Hii ndio Tanzania tunahitaji mabadiliko makubwa sana kuanzia kifikra kwa mtu mmoja mmoja mpk mabadiliko ya kiongozi kwa sasa
   
 5. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #5
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  Dear mwanakijiji;

  thread yako ni fupi lakini ina mambo mengi ambayo yanaweza kusimama kama yalivyo

  1.walikuwa serekalini .... wakatoka ... wakaanzisha wakawa successfull

  the answer is simply kuwa hawa ni watendaji wazuri ambao

  a. hawakuwa teyari kuwa waste
  b. walikuwa wananyanyaswa kwani walistick to principles za efficiency katika uzalishaji wakawa tatizo kwa wanasiasa na mabosi wao ambao wengi si wazalendo......
  c. pengine hawaamini imani ya chama tawala.......
  d. roho zao ni tajiri na wanafanya rational decision ambazo hufanywa mchana kweupe.........mfano mbowe aliwauliza wanapigania mashangingi, wakiachia ngazi wanapigania visuzuki.......

  2. System is not working properly

  a. kwamba watu hawataki kumueleza ukweli mkubwa ili aone mambo ni poa

  b.wanataka mambo yaendelee kuwa kama yalivyo ili wapate mkate wa kila siku (wao huhangaikia matumbo tu)

  c. mtu akiwa ni mzuri ataundiwa zengwe then hafiki popote


  d. SYSTEM MBAYA YA RECOMMENDATION...E.G. kuulizwa wakuu wa current organisation kuhusu mtu fulani aliyeapply executive post sehemu nyengine...hawa waliopo waliishakula majungu, na walitofasutiana kiutendaji huua reference and that is the end.....at this juncxture. the system collude kuendelea kulifyonza shamba la bibi....

  nakubali its time all executive post kudahiliwa na independent bodies zisizo na attachment na siasa.......

  pia nakubali kuwa kazi ziwe za mkataba....

  by the way, i am thinking quiting government...seems to be enough
   
 6. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #6
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Mkuu,thread hii haifanani na upeo wako...imekaa kiudaku udaku hivi!
  Hujaweka bayana hayo makampuni waliyo shiriki kuyaanzisha;mfano wa hao jamaa zako nk!
  Kiufupi thread hii imesimama hapa sababu tu ni MMM aliye ianzisha;la sivyo ingekuwa moved kwenye jukwaa la UDAKU!
   
 7. +255

  +255 JF-Expert Member

  #7
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,908
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Serikalini ni shamba la bibi, unaweza ukawa successful kwenye private sector kwa sababu kule kuna wenyewe so hauwezi kufanya upuuzi ila vitu vya serikali ni kama havina mwenyewe kwa hy unakula uwezavyo.
   
 8. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  nadhani swala la msingi katika sekta binafsi ili watendaji wake waweze kusaidia mashirika ya umma, wanahitaji kujijengea uwanja wa kujitapa wao wenyewe ili tuunge na maswala ya umma. Tunahitaji kujua viongozi hao wazuri wamefanya nini, wanatambulika kwa lipi?

  Pili, tunahitaji viongozi ambao wanatamani tu maendeleo - nawanajaribu kuyaona yanakuja! Ikuyapenda maendeleo, ukayafanyie kazi yatakuja tu.
   
 9. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  ungetoa mifano ya hayo makampuni binafsi
   
 10. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Tido effect, Tanzania ina watu wengi sana wachapakazi hata humo kwenye sekta ya umma wapo lakini wanakatishwa tamaa na serikali yenyewe. Mfanyakazi wa chini atajitahidi kwa moyo wake kulitumikia taifa lakini ataonekana ni kikwazo anawakwaza (wanasiasa) wanaotaka njia za mkato na matokeo yake ni yeye kutolewa kwenye hiyo nafasi.Sote tunajua utendajikazi wa Tido na tunajua alikuwa anataka kulifanyia nini shirika la TBC ili lijitegemee lakini kwa vile alikuwa hawafurahishi wakubwa hasa wanasiasa basi yaliyotokea yalimtokea. Ni nani mwingine wa sekta binafsi atathubutu kwenda huko na kufanya kazi kwa moyo?.

  Kuna mchangiaji amegusia serikali iajiri kwa mikataba mimi naungana naye, chukulia mfano wa shule binafsi kwanini nyigi zinafanya vizuri huku za serikali zikiboronga wakati zina facilities nzuri kuzidi za binafsi, ni kuwa manager wa shule na mwalimu wamepewa malengo kama hawakutimiza wanawajibika. Mkuu wa shule ya serikali hajali kama shule yake itafaulisha ama la kwa vile anajua mshahara ingawa ni mdogo utakukuja tu. Kwa hiyo hata hawa waliofanikiwa kwenye private sector wakiitwa serikalini kama serikali yenyewe haijajirekebisha itakuwa ni kazi bure, matokeo yake tutatoa cream kwenye sekta binafsi na kuziua mwisho ni kuzorotesha sekta zote za umma na za binafsi.
   
 11. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Precision Air VS Air Tanzania.
   
 12. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  IPP vs
   
 13. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mishirika ya umma yanaendeshwa kwa kufuata sera za serikali iliyoko madarakani. Kama sera ni kupunguza kiwango cha watu wasiokuwa na ajira, mashirika ya umma yanatakiwa kutekeleza sera hii hata kama yataishia kupata hasara. Hivi umewahi kufikiri kwanini vyuo binafsi vinaendeshwa kwa kutegemea ada tuu (school fees) wakati vyuo vya umma pamoja na kulipisha ada bado bajeti zao kwa asilimia kubwa zinategemea ruzuku ya serikali?. Jibu ni idadi kubwa ya wafanyakazi inayozidi mahitaji halisi (Full employment government policy).

  Uamuzi ule wa serikali kujitoa kwenye shughuli za biashara ndio njia pekee ya kuokoa hayo mashirika ya umma kwa kuyaweka kwenye wafanya biashara wa kweli. Hata huku kwenye huduma kama mashule na mahospiali Serikali kuu inatakiwa ijitoe ibaki tuu kufanya kazi za uangalizi (Regulator) na kuachia taasisi za kiraia na watu binafsi kufanya hizo shughuli kitaaluma.
   
 14. Mwamikili

  Mwamikili JF-Expert Member

  #14
  Jan 25, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 416
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  hawa ndio watanzania mungu aliotupa mwe!! na FF ka like this comment! kwa nini nyerere aligombana na banda kuwa kyela ni nchi yake! bora kyela ingekuwa chini ya malawi kuliko tanzania. ee mungu tuludishe kwetu wanyakyusa! wazungu wametugawa kwa watanzania , bora wangetugawa kwa wamalawi
   
 15. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #15
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Lakini hata sisi watumishi wa umma tuna matatizo. Wanasiasa wana matatizo lakini sisi matatizo yetu ni makubwa sana. Tukishapata kazi hatufikirii ufanisi wa vitengo vyetu so long as mshahara unatoka serikalini on monthly basis. Hao hao watumishi wa umma tukiacha kazi serikalini tukaenda let say mgodini kwa mkaburu au IPP kwa Mengi tutafanya kazi kama punda. System yoyote yenye ufanisi ni lazima ifanye assessment kati ya mshahara inaomlipa mfanyakazi wake na faida anayozalisha huyo mfanyakazi. Lakini sekta ya umma Tz mzembe analipwa sawasawa na mwenye bidii kwenye kazi hiyo hiyo, we unategemea nini?

  Mfano chukulia vyuo vikuu vya umma hapa bongo. So long as watu wote mna PhD na mmeajiriwa, let say UDSM salary scale zenu zipo sawa regardless huyu anafundisha fine and performing arts au yule anafundisha electronics. Wengine hata lecture haudhurii vizuri, wengine research hawafanyi, wengine wanapublish kwenye very low quality journals, n.k. System ya design hii haiwezi kuwa sustainable kwa muda mrefu na ndio maana elimu bongo kila siku inashuka. Vyuo vikuu vya umma Marekani kwanza kupata tenure kwa professa ni mbinde lazima awe nondo kweli kweli, pili salary inatofautiana sana, pale Pennsylvania State University kuna professa wa afya ya binadamu anapata 1 million US$ kwa mwaka salary wakati an equivalent professa kwenye arts anapata about 200, 000 US$, cheki hilo gap. Lakini wana maana yao, wanaencourage bidii, maarifa, ubunifu, sayansi na teknologia katika kazi na ndio wako juu.
   
 16. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #16
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Du , mkuu umeelzea the bone of contention!
  Utumishi wa umma na kujituma katika sekta binafsi vina outlook mbili tofauti kabisa.
  Mtu anayesimamia principles na objectivity huwa anawakati mgumu sana serikalini.

  Mimi mwenyewe nikuwa kiongozi katika sekta fulani ambayo nilipoichukua ilianza kufanya kazi kwa malengo,uwajibikaji na matokeo yake hata uongozi wa kitaifa ulianza kuona mabadiliko makubwa.

  Kumbe najichongea.
  Miradi yangu minne ilikuwa katika mlolongo wa kufunguliwa rasmi na mkuu wa nchi.

  Baada ya miradi miwili kufunguliwa , nilianza kurushiwa scud za chini chini halafu za waziwazi, mpaka nilposalimu amri na kujikuta barabarani nikisaga lami.
  Kisa ni kuwa fedha za miradi "wazee" hawakupata migawo.

  Tuseme ukweli , kila mwajiriwa katika umma lengo la kwanza ni kusurvive another day kwa kujilinda au kulindwa na aliyepo juu.
  Mwananchi ni mtu mdogo sana na hana direct influence kwa mtu huyu.
  Na ndio maana watu wanajikomba utafikiri hawajasoma.
  Mfanyakazi huyu huyo anayefanya kazi kwa bidii mwanzishie mradi na utaendelea vizuri sana.

  Leo namshukuru Mungu nina kampuni yangu mwenyewe inayofanya vizuri sana hata kuliko pale nilipofurumushwa.
  Hata nikikaburuza kashangingi kangu na kukutana na yule jamaa aliyekuwa bosi na kuniondoa kazini kwa kweli anaona aibu sana.

  Watanzania tusione aibu kuanzisha miradi yetu wenyewe, kuna faida zaidi kuliko kuajiriwa.
  Asante Mwanakijiji kwa kukumbushia hili.
   
 17. zimmerman

  zimmerman JF-Expert Member

  #17
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 579
  Likes Received: 280
  Trophy Points: 80
  Lakini hata sisi watumishi wa umma tuna matatizo. Wanasiasa wana matatizo lakini sisi matatizo yetu ni makubwa sana. Tukishapata kazi hatufikirii ufanisi wa vitengo vyetu so long as mshahara unatoka serikalini on monthly basis. Hao hao watumishi wa umma tukiacha kazi serikalini tukaenda let say mgodini kwa mkaburu au IPP kwa Mengi tutafanya kazi kama punda. System yoyote yenye ufanisi ni lazima ifanye assessment kati ya mshahara inaomlipa mfanyakazi wake na faida anayozalisha huyo mfanyakazi. Lakini sekta ya umma Tz mzembe analipwa sawasawa na mwenye bidii kwenye kazi hiyo hiyo, we unategemea nini?

  Mfano chukulia vyuo vikuu vya umma hapa bongo. So long as watu wote mna PhD na mmeajiriwa, let say UDSM salary scale zenu zipo sawa regardless huyu anafundisha fine and performing arts au yule anafundisha electronics. Wengine hata lecture haudhurii vizuri, wengine research hawafanyi, wengine wanapublish kwenye very low quality journals, n.k. System ya design hii haiwezi kuwa sustainable kwa muda mrefu na ndio maana elimu bongo kila siku inashuka. Vyuo vikuu vya umma Marekani kwanza kupata tenure kwa professa ni mbinde lazima awe nondo kweli kweli, pili salary inatofautiana sana, pale Pennsylvania State University kuna professa wa afya ya binadamu anapata 1 million US$ kwa mwaka salary wakati an equivalent professa kwenye arts anapata about 200, 000 US$, cheki hilo gap. Lakini wana maana yao, wanaencourage bidii, maarifa, ubunifu, sayansi na teknologia katika kazi na ndio wako juu.
   
 18. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #18
  Jan 25, 2012
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Binafsi bado sijaona deliverables or tangible output aliyofanya Mchechu kwa NHC, Ninachowitness toka NHC ya sasa ni matangazo mengi kwenye vyombo vya habari. Sijaona project mpya zaidi ya zilizokuwepo awali, still no new cormmercial projects, nyumba za walala hoi hakuna labda bado anatumikia waliompa madaraka na marafiki zake wapate nyumba kwanza ndio aanze kufanya kazi othersiwise bado hakuna cha kusifia kwa Mchechu. Asipoangalia naye atatoka hapo akijisifu ameweka logo mpya kama Mataka alivyofanya ATCL.
   
 19. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #19
  Jan 25, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Ya kujiuliza ni mengi.
  Je a nayewateua serikali na chama chake wanazimudu nafasi walizoaminiwa?
  Je haijafika wakati wateule wa mashirika yetu wathibitishwe na bunge?
   
 20. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #20
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Tatizo kubwa ni SYSTEM yetu ambayo maamuzi mengi yanatawaliwa na siasa ni sio professional. I will bet my neck hata wewe MM ukipewa leo hii kuiendesha TANESCO uta fail. Imagine politicians ndiyo wanaingia mikataba ya kifasidi, mathalani wanaingia mkataba wa kununua umeme kwa bei kubwa halafu wanailazimisha TANESCO kuuza umeme kwa wananchi kwa bei ya chini. Hapo TANESCO itajiendesha vipi kifaida.

  Kuna sheria kwamba taasisi/kampuni isipolipa umeme kwa miezi 3 mfululizo ikatiwe umeme. Imewahi kutokea TANESCO wanakwenda kukata umeme Twiga Cement au Zanzibar tena baada ya kupewa notice, amri inakuja kutoka IKULU warudishieni hao umeme. Kwa system hiyo unawezaje kuliendesha shirika kwa faida.

  Ninakumbuka mzungu NMB aliachia ngazi pale Mkapa aliposhinikiza kuuza NMB eti inatengeneza hasara, mzungu akasema huo ni uongo na hayuko tayari huo uongo kutendwa mbele yake akaachia ngazi!

  Akina Marehemu Balali, Eng. Mrema (TANROAD) etc wote walifanya vizuri walipokuwa nje, lakini walipoombwa kurudi kufanya kazi nyumbani they miserably failed
   
Loading...