Wamasai wameshindikana Zanzibar, lipelekwe Jeshi kuwapora marungu, fimbo na sime

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Zanzibar ina sheria zake na sehemu ndogo kuna sheria za Muungano.

Wamasai hawataki kufuata sheria, ni vizuri jeshi liende huko kuwakabili.

Wa Zanzibar wakija Bara wanaweza kuendelezatamaduni zao sababu wanakuwepo Tanzania kimuungano

 
Jamani eh.
Hebu niambieni mtajisikiaje Wazanzibari kesho kuwa mwiko kupika au kula rojo....haijalishi

Wazaramo watajisikiaje kusikia kuwa kesho ni mwiko kucheza ngoma ya mdundiko na lazima waka surrender ngoma zao na zana zingine za jadi yao?

Narudi Zanzibar, mtajisikiaje kesho mkiambiwa muache kuvaa kanzu, makobazi na kula supu la pweza, ati, vinahatarisha usalama wa wengine?

Utajisikia vipi ukiambiwa uache utambulisho wako, urithi wako, mtindo wako wa maisha? Waweza kuacha kula rojo? Waweza kuacha mdundiko, waweza kuacha kuvaa makobazi na kanzu.

Sasa, hayo ndiyo yanayowakumba Wamaasai leo.

Wanalazimishwa kuacha Utamaduni wao wa muda mrefu, desturi ya kubeba rungu na sime, vitu ambavyo vimekuwa ndio utambulisho wao. Utambulisho unaoonyesha ujasiri wao na ujuzi wa vita..

Zana hizi zimekuwa muhimu maishani mwao, kama wafugaji na Warriors kwa karne na karne.

Wamelinda ardhi yao, bahati mbaya wameshindwa safari hii, lakini wamekuwa wakijilinda na kulinda mifugo yao na heshima(dignity) yao for S.A.W sake! for centuries.

Wamerithishana kwa vizazi na vizazi kama tambiko na heshima kwa vijana baada ya kubalehe, sasa wanaambiwa wakavisalimishe! wawe kama Wazungu, wapoteze utambulisho(uniqueness) wao/yao.

Suala hili haliko sawa kabisaaa, na Sikubaliani nalo, huu sio Ubinadamu sio Uislamu, sio Ukristo, sio Ushetani, sio uwekezaji- its GENOCIDE

Namalizia

NB:Sasa unaweza kufikiri haya yanasikitisha, la hasha.

Yanayosikitisha zaidi, mbali na CCM ambaye ndie muuaji, ni CHADEMA, chama ambacho kinajinadi, kinadai haki. Wako kimya sana? Unayoyasikia ni haki yao ya kuja kuendesha ma V8 na kurusha helikopta.

Sera zenu zinasema nini kuhusu hawa ndugu zetu Wamaasai?

Mtawarudisha Loliondo au na nyie ndio mje muwamalize muwavue na nguo zao za jadi?


STOP THE GENOCIDE
 
Utajisikia vipi ukiambiwa uache utambulisho wako, urithi wako, mtindo wako wa maisha? Waweza kuacha kula rojo? Waweza kuacha mdundiko, waweza kuacha kuvaa makobazi na kanzu.
Hata sisi wamakonde tukiambiwa tuache kuaruka na kula ming'oko kwa kweli tutalianzisha 😄😄
 
Zanzibar ina sheria zake na sehemu ndogo kuna sheria za Muungano.

Wamasai hawataki kufuata sheria, ni vizuri jeshi liende huko kuwakabili.

Wa Zanzibar wakija Bara wanaweza kuendelezatamaduni zao sababu wanakuwepo Tanzania kimuungano

View attachment 2890387
Muwe mnafikiria vizuri nyie watu!!

Tumezoea mapigano ya wakulima na wafugaji morogoro huko,sio Zanzibar,kwanini Leo!!?

Hivi hapo kisiwani Kuna malisho ya mifugo ya kitosha wamasai!!?

Warudishieni eneo lao la ngoro ngoro,naona wamechoka kukaa msomera wanataka kisiwa sio msomera!!

Ni wamasai kweli!!?au wamasai was mchongo kama ilivyo wavuvi was mchongo was miaka ya mapinduzi ileeee ya kina karume!!!!!


Msije ingilia operation za watu bila kujua!!
 
Hata sisi wamakonde tukiambiwa tuache kuaruka na kula ming'oko kwa kweli tutalianzisha 😄😄
Mkuu, we acha tu. If my memory serves me right, Mzee Ben Mkapa R.I.P nilimchukia kwa kisa chake cha kuwalazimisha wamakonde wasipige Tatoo zao za jadi....Hicho kitu kiliniuma. Akaja na Jakaya Kikwete, huyu naye aliwakataza Wamaasai kufanya uwindaji wakati wa Jando-rite of passage ya vijana wakimaasai iliniumai, sijui kwanini, lakini I felt something amiss na mie sio Mmakonde au Mmaasai.

Vitu kama hivi, vya kujidhalilisha wenyewe Waafrika vinanikera sana.

Mie naona walianzishe tu. This is beyond Utumwa. Ni GENOCIDE mkuu.
 
Huu ni unyanyasaji wa hali ya juu sana!

Rungu na sime pamoja na rubega ni jadi na ni utambulisho wa mmasai.
Kuwanyang'anya huo utambulisho ni kuingilia uhuru wao na haki yao ya msingi.

Btw, kwanini iwe kwa masai pekee yao...kama ni suala la kuheshimu utamaduni wa Zanzibar, mbona wazungu wanatembea uchi mitaani na ni kinyume na taratibu za huko na hawabugudhiwi!?
 
Back
Top Bottom