SoC02 Wamachinga wanavyorudishwa nyuma na taasisi ndogo ndogo za mikopo ya fedha (Microfinance)

Stories of Change - 2022 Competition

Robin18

New Member
Aug 7, 2022
1
0
Tanzania ni Moja Kati ya nchi zenye taasisi ndogo ndogo za mikopo ya fedha nyingi zinazokadiriwa kufika zaidi ya makampuni 500. Malengo makubwa ya kampuni hizi za mikopo ni kuisaidia jamii ( wajasiriamali) kuweza kupata huduma za mikopo midogo midogo ambayo hawawezi kupata katika Benki. Hizi taasisi kimsingi husaidia ujuaji wa uchumi wa mtu mmoja mmoja kupitia kukuza mitaji ya biashara zao.

Mfumo wa taasisi hizi (Microfinance) mpaka Sasa hakuna muongozo wa Moja Kwa Moja unaolenga elimu Kwa wajasiriamali, ukomo wa namba za taasisi za kukopa Kwa wakati mmoja na swala la kisheria Kwa mikopo chechefu na ufilisi.

Imekuwa ni kawaida Kwa taasisi na makampuni haya kuwakopesha wajasiriamali Ili Hali wanamikopo mingine katika makampuni na taasisi zingine za fedha. Katika kufanya tathmini ya biashara za hawa wajasiriamali pasipo shaka mtaji na mzunguko wa mjasiriamali hauendani na mikopo aliyonayo, na jambo la kushangaza Bado Kuna taasisi ya mikopo itatoa mkopo Kwa mjasiriamali huyu pasipo kujua au Kwa kujua kama anamkopo mingine Kwa taasisi zingine.

Wajasiriamali wanakosa elimu ya uendeshaji biashara na mikopo kiasi kwamba anakuwa na mikopo mingi kiasi inamshinda kulipa Kwa wakati na kuangukia katika adha ya kufilisiwa na kuzalilishwa. Nani anatakiwa kumpa elimu? Kimsingi taasisi mikopo zinatakiwa kuwapa elimu hawa wajasiriamali juu ya namna Bora ya uendeshaji wa biashara na utunzaji wa fedha Ili kukuza mitaji Yao. Lakin inafanyika kinyume, badala yake taasisi hizi wanachojali ni kuongeza idadi ya wateja Ili kuongeza faida bila kujali kushindwa kutoa elimu itafikia hatua mikopo chechefu itakuwa mingi kushindwa mitaji ambayo wanamiliki.

Riba kubwa inayowekwa katika mikopo hii ni sawasawa na kumnyonya mjasiriamali. Mfano; Ili kupata mkopo unatakiwa ununue form ya kuomba mkopo, ulipie gharama za kutembelewa, gharama za kitabu Cha mteja Cha marejesho, lakin pia gharama za mchakato wa mkopo. Ulipiga hesabu Kwa mkopo mdogo wa laki tatu gharama hizi za awali hufikia mpaka elfu thelathini na mbili. Mjasiriamali anaepokea mkopo wa laki tatu na atatakiwa arudishe ndani ya wiki kumi na mbili Kwa riba ya asilimia thelathini. Uhalisia mjasiriamali atalipa 40.7%.

Ufilisi ndicho hufata baada ya mjasiriamali kushindwa kulipa deni Kwa wakati. Taratibu za ufilisi zinazotumiwa Si za kisheria Hali inayowaacha wajasiriamali hawa kuzidi kuwa masikini na baada ya ufilisi mjasiriamali hulazimika kuanza Upya.
 
Back
Top Bottom