Wamachinga tunalia mtetezi wetu ameondoka, hatujui kesho yetu

Wamachinga tunalia mtetezi wetu ameondoka, hatujui kesho yetu

Wamachinga wamesema kifo cha rais Magufuli ni pigo kwao kwani ni mtu aliyewaheshimisha na kubadili maisha yao tangu aingie madarakani .

======

Mwanza. Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (Shiuma), Ernest Matondo amesema kifo cha Rais John Magufuli kimewaondolea wamachinga shujaa na mtetezi wao.
Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi kwa njia ya simu leo Alhamisi, Machi 18, Matondo ametaja uhuru na fursa ya kufanya shughuli zao bila bughudha kutoka mamlaka za halmashauri na vitambulisho vya wamachinga kuwa miongoni mwa mambo ambayo kundi hilo litamkumbuka nalo Rais Magufuli aliyefariki dunia jana.

“Kabla ya Rais Magufuli hajaingia madarakani wamachinga hawakuwa na uhakika wa kesho yao; kulikuwa na operesheni za mara kwa mara za kuwaondoa mitaani iliyoambatana na kunyang’anywa au kuharibiwa mali zao. Yote hayo yalikoma chini ya uongozi wa Rais Magufuli,” amesema Matondo.

Ameongeza, “Zamani wamachinga tulikuwa tunatozwa ushuru wa kati ya Sh200 hadi Sh500 kwa siku. Lakini kwa miaka miwili sasa chini ya Jemedari John Pombe Magufuli tunalipa Sh20, 000 pekee kwa mwaka kwa ajili ya vitambulisho vya wamachinga na kufanya biashara popote.”

Kauli ya kumbukumbu njema ya Rais Magufuli kwa wamachinga pia imetolewa na Anna Sylvanus, mfanyabiashara mdogo katika mtaa wa Makoroboi jijini Mwanza anayesema kiongozi huyo alijenga msingi uliowalazimisha viongozi na watendaji wa Serikali kuwasikiliza na kutatua kero za wanyonge.

“Yeye binafsi alitoa nafasi kwa wananchi kueleza kero zao wakati wa ziara zake na mara nyingi alionyesha kukerwa alipobaini baadhi ya kero zingeweza kutatuliwa na viongozi wa chini. Nakumbuka kuna wakati aliwakemea papo hapo wasaidizi wake akiwataka waende kwa wananchi kutatua kero zao,” amesema Anna

Katibu wa wafanyabiashara vijana katika soko la Makoroboi, Joseph Charles amewaomba viongozi wa Serikali kuendeleza yote mema yaliyoasisiwa na kusimamiwa na Rais John Magufuli kama njia ya kumuenzi.


E0NhMwdXIAAW0HL.jpeg
 
Yaani nyinyi wamachinga kujenga vibanda vyenu kwenye ukingo wa barabara ya lami mnaona sawa? Kujenga vibanda kwenye road reserve mnaona sawa? Kupanga biadhaa kwenye njia za wapita kwa miguu mnaona sawa? Serikali kwa kushirikiana na wadau wamewajengea masoko yaliyogharimu mabilioni lakini hamtaki kwenda kisa JIWE alikuwa anawatumia kjinufaisha kisiasa....Fuateni sheria nendeni sehemu mliyopangiwa kufanya biashara zenu.
 
Yaani nyinyi wamachinga kujenga vibanda vyenu kwenye ukingo wa barabara ya lami mnaona sawa? Kujenga vibanda kwenye road reserve mnaona sawa? Kupanga biadhaa kwenye njia za wapita kwa miguu mnaona sawa? Serikali kwa kushirikiana na wadau wamewajengea masoko yaliyogharimu mabilioni lakini hamtaki kwenda kisa JIWE alikuwa anawatumia kjinufaisha kisiasa....Fuateni sheria nendeni sehemu mliyopangiwa kufanya biashara zenu.
Kwani hivyo vibanda vinamwibia nani?
 
Hatutaki kujazana pembezoni mwa barabara eti ni ujasiriamali. Miundombinu ya jiji inaharibika na mpangilio unakosa, mifumo ya majitaka inafeli, hatari kwa wapita kwa miguu. Nenda pale Kariakoo mtaa wa Msimbazi kata kama unaenda kanisa la KKKT, kuna wajasiriamali wameziba barabara hata pikipiki hazipishani.

Wajasiriamali wasiendekezwe kujazana popote, wawe na mipaka. Kama vipi na wafanyabiashara wafurahi kodi za maajabu zitafutwa, eti mtu unafungua biashara unaambiwa kadiria mapato ulipe kodi wakati hujaanza hata kuuza.
Ukweli mchungu
 
Sehemu za kupita Watembea kwa miguu nyie nmezifanya maduka yenu...kila sehemu ya wazi nyie nmezifanya masoko ..tumewachoka kwa kweli
 
Sehemu za kupita Watembea kwa miguu nyie nmezifanya maduka yenu...kila sehemu ya wazi nyie nmezifanya masoko ..tumewachoka kwa kweli
Kwa hiyo huwa mnapita wapi?
 
Mbona yanajengwa masoko ya kisasa maeneo mengi tu sasa wasiwasi wenu nini wakati mnajua kuweka mabanda kufanya biashara kando ya barabara hairuhusiwi na ni hatari kwenu pia
Hawa jamaa wanakera sana, miji yote imegeuka kuwa km vijiji waondoke waende sehemu maalum za kufanya biashara.Tokaaaa!
 
Back
Top Bottom