Elitwege
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 5,294
- 10,977
Wamachinga wamesema kifo cha rais Magufuli ni pigo kwao kwani ni mtu aliyewaheshimisha na kubadili maisha yao tangu aingie madarakani .
======
Mwanza. Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (Shiuma), Ernest Matondo amesema kifo cha Rais John Magufuli kimewaondolea wamachinga shujaa na mtetezi wao.
Akizungumza kwa njia ya simu na Mwananchi kwa njia ya simu leo Alhamisi, Machi 18, Matondo ametaja uhuru na fursa ya kufanya shughuli zao bila bughudha kutoka mamlaka za halmashauri na vitambulisho vya wamachinga kuwa miongoni mwa mambo ambayo kundi hilo litamkumbuka nalo Rais Magufuli aliyefariki dunia jana.
“Kabla ya Rais Magufuli hajaingia madarakani wamachinga hawakuwa na uhakika wa kesho yao; kulikuwa na operesheni za mara kwa mara za kuwaondoa mitaani iliyoambatana na kunyang’anywa au kuharibiwa mali zao. Yote hayo yalikoma chini ya uongozi wa Rais Magufuli,” amesema Matondo.
Ameongeza, “Zamani wamachinga tulikuwa tunatozwa ushuru wa kati ya Sh200 hadi Sh500 kwa siku. Lakini kwa miaka miwili sasa chini ya Jemedari John Pombe Magufuli tunalipa Sh20, 000 pekee kwa mwaka kwa ajili ya vitambulisho vya wamachinga na kufanya biashara popote.”
Kauli ya kumbukumbu njema ya Rais Magufuli kwa wamachinga pia imetolewa na Anna Sylvanus, mfanyabiashara mdogo katika mtaa wa Makoroboi jijini Mwanza anayesema kiongozi huyo alijenga msingi uliowalazimisha viongozi na watendaji wa Serikali kuwasikiliza na kutatua kero za wanyonge.
“Yeye binafsi alitoa nafasi kwa wananchi kueleza kero zao wakati wa ziara zake na mara nyingi alionyesha kukerwa alipobaini baadhi ya kero zingeweza kutatuliwa na viongozi wa chini. Nakumbuka kuna wakati aliwakemea papo hapo wasaidizi wake akiwataka waende kwa wananchi kutatua kero zao,” amesema Anna
Katibu wa wafanyabiashara vijana katika soko la Makoroboi, Joseph Charles amewaomba viongozi wa Serikali kuendeleza yote mema yaliyoasisiwa na kusimamiwa na Rais John Magufuli kama njia ya kumuenzi.