Wamachinga barabara ya Soko la Kariakoo wapewa wiki mbili kuondoka

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa wiki mbili kwa wafanyabiashara ndogondogo walio katika barabara za kuingia soko kuu la Kariakoo kuondoka.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni kuelekea ufunguzi wa soko hilo, lililokuwa katika ukarabati tangu Julai 10, 2021 baada ya kuungua.

Kutokana na tukio hilo, Serikali ilitoa zaidi ya Sh28 bilioni kwa ajili ya kulikarabati, ukarabati ulioenda sambamba na ujenzi mpya wa soko dogo.

Katika kipindi chote hicho wafanyabaishara waliokuwa wakifanya shughuli zao sokoni hapo, walihamishiwa katika masoko ya Kisutu, Karume na Machinga Complex.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano Mei 28, 2025 kuhusu maendeleo ya soko hilo, Chalamila amesema tayari limeshakamilika kwa asilimia 98 na kinachofuata ni maandalizi ya kulifungua japo hakuweka wazi tarehe rasmi.

Kati ya maandalizi hayo amesema ni pamoja na kuwaondoa Wamachinga waliopo barabara za kuingia sokoni hapo, na tayari wameshawapa maagizo viongozi wao.

“Mpaka sasa ninapozungumza soko limeshakamilika kwa asilimia 98 na kubakia matengenezo madogo madogo ikiwemo uzio.

“Baada ya hapo kinachosubiriwa ni Waziri mwenye dhamana wa Tamisemi, kufanya ziara ya mwisho kukagua na kujiridhisha ukamilifu wake kabla halijaja kuzinduliwa, uzinduzi unaotarajiwa kufanywa rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Chalamila.

Hata hivyo ameleleza kuwa pindi soko hilo litakapofunguliwa kuna utaratibu umewekwa wa kuwapa baadhi ya maeneo wamachinga, ambapo kuna maduka madogo watawekwa ili kupunguza adha hiyo ya wao kukaa barabarani.

Wakati Chalamila akisema hayo, Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Tanzania na Mwenyekiti Soko la Kariakoo, Stephen Lusinde,amesema kazi ya kuwaondoa si kubwa kwao kwa kuwa hata wamachinga wenyewe wanajua maeneo hayo wameyavamia.

Lusinde amefafanua kuwa tangu awali wakati wanawapanga maeneo hayo ya Kariakoo, kuna barabara za mitaa walikubaliana waziache wazi na nyingi ndio hizo zinazoingia katika soko hilo.

Ametaja barabara hizo kuwa ni pamoja na ile ya Mtaa wa Nyamwezi -Mkunguni, Nyamwezi-Tandamti, Tandamti-, Sikukuu -Mkunguni na Mkunguni – Congo (Bigborn).

“Katika maeneo hayo wafanyabiashara wanaelewa kuwa tulishakubaliana pawe wazi ila kwa wale wakaidi waliamua tu kuvamia na wengine maeneo wanayo walishapangiwa, hivyo ikifika muda tutafanya kazi yetu na hakutakuwa na wa kumlaumu,” amesema Lusinde.

Kuhusu na wao kupata maeneo ya kufanya biashara ndani ya soko hilo la kimataifa, Mwenyekiti huyo amesema ni taarifa njema kwao ukizingatia ni kilio chao cha muda mrefu, huku akieleza vipaumbele vitakuwa kwa wale ambao hawakuwa na maeneo na tayari wapo katika kanzidata yao.

Mmoja wa machanga ambaye hakutaka jina lake liandikwe, ameshauri wangeachwa mpaka hapo uhakika wa soko litakapofunguliwa, kwa kuwa ni sehemu ambayo wanategemea kupata rizki kwa sasa.
Screenshot 2025-05-29 142853.png

Chanzo Mwananchi
 
View attachment 3349660

Chanzo Mwananchi
nani kawapa amri? siyo rahisi
 
nani kawapa amri? siyo rahisi
Ngoja tuone.....hao wapiga kura wenu

Ova

Just ku clarify hakuna machinga kuingia soko la kariakoo unless alimaanisha shimoni.

Mtaa wa mkunguni kutoka Lumumba hadi sokoni hakuna Machinga, Mtaa wa Mkunguni toka Big bon hadi soko kariakoo hakuna machinga,

Hata tandamti machinga wachache mno kutokea lumumba hakuna machinga kabisa na kutokea msimbazi kuna majengo yanajengwa wapo machinga wachache ambao ni temporary sio wale wa kukaa.

Shimoni ndio hakupitikii Narung'ombe imefunga.
 
Kwa sahv huko kko hakuna nyomi la wamachinga kuziba barabara
Maana kitambo sijapit huko

Ova
 
Barabara ya kutoka msimbaz b kwenda narung'ombe street idadi imepungua nowdays ila mtaa wa sikukuu ni shida
 
Kwa sahv huko kko hakuna nyomi la wamachinga kuziba barabara
Maana kitambo sijapit huko

Ova
Lipo ila sio sokoni, mtaa mmoja tu baada ya Soko na kuendelea mpaka mtaa wa uhuru kuna mitaa mingi imefungwa magari hayapiti Wamachinga wameteka lami.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa wiki mbili kwa wafanyabiashara ndogondogo walio katika barabara za kuingia soko kuu la Kariakoo kuondoka.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni kuelekea ufunguzi wa soko hilo, lililokuwa katika ukarabati tangu Julai 10, 2021 baada ya kuungua.

Kutokana na tukio hilo, Serikali ilitoa zaidi ya Sh28 bilioni kwa ajili ya kulikarabati, ukarabati ulioenda sambamba na ujenzi mpya wa soko dogo.

Katika kipindi chote hicho wafanyabaishara waliokuwa wakifanya shughuli zao sokoni hapo, walihamishiwa katika masoko ya Kisutu, Karume na Machinga Complex.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano Mei 28, 2025 kuhusu maendeleo ya soko hilo, Chalamila amesema tayari limeshakamilika kwa asilimia 98 na kinachofuata ni maandalizi ya kulifungua japo hakuweka wazi tarehe rasmi.

Kati ya maandalizi hayo amesema ni pamoja na kuwaondoa Wamachinga waliopo barabara za kuingia sokoni hapo, na tayari wameshawapa maagizo viongozi wao.

“Mpaka sasa ninapozungumza soko limeshakamilika kwa asilimia 98 na kubakia matengenezo madogo madogo ikiwemo uzio.

“Baada ya hapo kinachosubiriwa ni Waziri mwenye dhamana wa Tamisemi, kufanya ziara ya mwisho kukagua na kujiridhisha ukamilifu wake kabla halijaja kuzinduliwa, uzinduzi unaotarajiwa kufanywa rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Chalamila.

Hata hivyo ameleleza kuwa pindi soko hilo litakapofunguliwa kuna utaratibu umewekwa wa kuwapa baadhi ya maeneo wamachinga, ambapo kuna maduka madogo watawekwa ili kupunguza adha hiyo ya wao kukaa barabarani.

Wakati Chalamila akisema hayo, Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Tanzania na Mwenyekiti Soko la Kariakoo, Stephen Lusinde,amesema kazi ya kuwaondoa si kubwa kwao kwa kuwa hata wamachinga wenyewe wanajua maeneo hayo wameyavamia.

Lusinde amefafanua kuwa tangu awali wakati wanawapanga maeneo hayo ya Kariakoo, kuna barabara za mitaa walikubaliana waziache wazi na nyingi ndio hizo zinazoingia katika soko hilo.

Ametaja barabara hizo kuwa ni pamoja na ile ya Mtaa wa Nyamwezi -Mkunguni, Nyamwezi-Tandamti, Tandamti-, Sikukuu -Mkunguni na Mkunguni – Congo (Bigborn).

“Katika maeneo hayo wafanyabiashara wanaelewa kuwa tulishakubaliana pawe wazi ila kwa wale wakaidi waliamua tu kuvamia na wengine maeneo wanayo walishapangiwa, hivyo ikifika muda tutafanya kazi yetu na hakutakuwa na wa kumlaumu,” amesema Lusinde.

Kuhusu na wao kupata maeneo ya kufanya biashara ndani ya soko hilo la kimataifa, Mwenyekiti huyo amesema ni taarifa njema kwao ukizingatia ni kilio chao cha muda mrefu, huku akieleza vipaumbele vitakuwa kwa wale ambao hawakuwa na maeneo na tayari wapo katika kanzidata yao.

Mmoja wa machanga ambaye hakutaka jina lake liandikwe, ameshauri wangeachwa mpaka hapo uhakika wa soko litakapofunguliwa, kwa kuwa ni sehemu ambayo wanategemea kupata rizki kwa sasa.
View attachment 3349660

Chanzo Mwananchi
" sisi wamachinga hatupo tayar kwa maandamano wala mikutano ya No reform no election " alisema kiongozi wao
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila ametoa muda wa wiki mbili kwa uongozi wa wafanyabiashara wadogo maarufu kama machinga eneo la kariakoo kuanza kufungua njia ili kuruhushu shughuli za kibiashara kufanyika kwa ufanisi wakati serikali ikielekea kufanya uzinduzi wa soko jipya la Kariakoo

Akizungumza Dar es Salaam Mei 28,2025 na waandishi wa habari RC Chalamila amesema wakati maandalizi ya uzinduzi wa soko jipya yakiendelea ni muhimu Machinga Kariakoo kufungua njia za kuingia ili kupeleka bidhaa kwenye soko jipya la Kariakoo.

"Soko limeshakamilika kwa asilimia 98 hivyo natoa muda wa wiki mbili kuanzia leo Mei 28,2025 Machinga waliopo barabarani Kariakoo wakaondoka kwenda maeneo waliyopangiwa" alisisitiza Chalamila.

Kuhusu wafanyabiashara waliokuwepo kwenye Soko la Kariakoo awali kabla halijaungua Chalamila alisema wote waliokuwepo kuhakikiwa na watarejeshwa kama ambavyo Rais Dkt Samia alivyoelekeza na watapaswa kujaza mikataba,kulipa kodi na kwamba Mkoa huo umefanikiwa kuondoa udalali wa upangishaji maeneo kwa kutuia mfumo wa kidijitali wa TAUSI.

Kwa upande wake Meneja Mkuu Shirika la Masoko Kariakoo Ashraph Abdulkarim alisema Shirika hilo linaendelea kuratibu wafanyabiashara waliokuwepo kurejea kwenye Soko hilo kulingana na mpangilio wa biashara.

Abdulkarim aliongeza kusema idadi ya wafanyabiashara 1150 kati ya 1520 waliohakikiwa tayari wamesajiliwa kwenye mfumo wa TAUSI ili kurejea sokoni na kuwa maeneo mengine ya wazi yaliyobaki yatatangazwa kupitia mfumo huo ili yapate wapangaji wapya.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa wiki mbili kwa wafanyabiashara ndogondogo walio katika barabara za kuingia soko kuu la Kariakoo kuondoka.

Hatua hiyo inakuja ikiwa ni kuelekea ufunguzi wa soko hilo, lililokuwa katika ukarabati tangu Julai 10, 2021 baada ya kuungua.

Kutokana na tukio hilo, Serikali ilitoa zaidi ya Sh28 bilioni kwa ajili ya kulikarabati, ukarabati ulioenda sambamba na ujenzi mpya wa soko dogo.

Katika kipindi chote hicho wafanyabaishara waliokuwa wakifanya shughuli zao sokoni hapo, walihamishiwa katika masoko ya Kisutu, Karume na Machinga Complex.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Jumatano Mei 28, 2025 kuhusu maendeleo ya soko hilo, Chalamila amesema tayari limeshakamilika kwa asilimia 98 na kinachofuata ni maandalizi ya kulifungua japo hakuweka wazi tarehe rasmi.

Kati ya maandalizi hayo amesema ni pamoja na kuwaondoa Wamachinga waliopo barabara za kuingia sokoni hapo, na tayari wameshawapa maagizo viongozi wao.

“Mpaka sasa ninapozungumza soko limeshakamilika kwa asilimia 98 na kubakia matengenezo madogo madogo ikiwemo uzio.

“Baada ya hapo kinachosubiriwa ni Waziri mwenye dhamana wa Tamisemi, kufanya ziara ya mwisho kukagua na kujiridhisha ukamilifu wake kabla halijaja kuzinduliwa, uzinduzi unaotarajiwa kufanywa rasmi na Rais Samia Suluhu Hassan,” amesema Chalamila.

Hata hivyo ameleleza kuwa pindi soko hilo litakapofunguliwa kuna utaratibu umewekwa wa kuwapa baadhi ya maeneo wamachinga, ambapo kuna maduka madogo watawekwa ili kupunguza adha hiyo ya wao kukaa barabarani.

Wakati Chalamila akisema hayo, Makamu Mwenyekiti wa Wamachinga Tanzania na Mwenyekiti Soko la Kariakoo, Stephen Lusinde,amesema kazi ya kuwaondoa si kubwa kwao kwa kuwa hata wamachinga wenyewe wanajua maeneo hayo wameyavamia.

Lusinde amefafanua kuwa tangu awali wakati wanawapanga maeneo hayo ya Kariakoo, kuna barabara za mitaa walikubaliana waziache wazi na nyingi ndio hizo zinazoingia katika soko hilo.

Ametaja barabara hizo kuwa ni pamoja na ile ya Mtaa wa Nyamwezi -Mkunguni, Nyamwezi-Tandamti, Tandamti-, Sikukuu -Mkunguni na Mkunguni – Congo (Bigborn).

“Katika maeneo hayo wafanyabiashara wanaelewa kuwa tulishakubaliana pawe wazi ila kwa wale wakaidi waliamua tu kuvamia na wengine maeneo wanayo walishapangiwa, hivyo ikifika muda tutafanya kazi yetu na hakutakuwa na wa kumlaumu,” amesema Lusinde.

Kuhusu na wao kupata maeneo ya kufanya biashara ndani ya soko hilo la kimataifa, Mwenyekiti huyo amesema ni taarifa njema kwao ukizingatia ni kilio chao cha muda mrefu, huku akieleza vipaumbele vitakuwa kwa wale ambao hawakuwa na maeneo na tayari wapo katika kanzidata yao.

Mmoja wa machanga ambaye hakutaka jina lake liandikwe, ameshauri wangeachwa mpaka hapo uhakika wa soko litakapofunguliwa, kwa kuwa ni sehemu ambayo wanategemea kupata rizki kwa sasa.
View attachment 3349660

Chanzo Mwananchi
kwani gazeti lao linasemaje
 
Makampuni yote Makubwa yaliyokuwa na maofisi Kariakoo yameondoka kwa sababu njia zote za kuingilia kwenye ofisi zao zimezibwa na Wamachinga, huku mamlaka zikikenua meno.

Mojawapo ya Makampuni hayo ni SALAMA PHARMACEUTICALS LTD, waliokuwa mtaa wa Agrey
 
Back
Top Bottom