Waliotorosha Twiga kwenda Uarabuni watinga mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waliotorosha Twiga kwenda Uarabuni watinga mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by LINCOLINMTZA, Jun 11, 2011.

 1. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Saturday, 11 June 2011 09:17 0diggsdigg

  Daniel Mjema, Moshi
  RAIA wawili wa kigeni na Watanzania wanne, wamepandishwa kizimbani wakituhumiwa kwa makosa nane ya uhujumu uchumi kwa kusafirisha wanyama hai wakiwamo Twiga kwenda Doha, Qatar.
  Wanyama hao wenye thamani ya dola 113,715 za Marekani, sawa na Sh170.5 milioni, wanadaiwa kusafirishwa kwenda Doha Novemba 26, kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia).Washtakiwa hao waliofikishwa kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa Kilimanjaro, Simon Kobelo, ni Kamrani Ahamed (29), raia wa Pakistan na Jane Simon Mbogo (33), raia wa Kenya.

  Ahamed ambaye ni mshtakiwa wa kwanza, ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Osaka Traders Limited na Jane ambaye ni mshtakiwa wa nne, anafanya kazi Kampuni ya Equity Aviation Services uwanja wa Kia.Washtakiwa wengine ni Hawa Mang'unuka (51), Mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Martin Kimati (58), mkaguzi wa Zoo Sanitary na maofisa wawili wanaoshughulikia ulinzi na usalama uwanja wa Kia.

  Maofisa hao ni Veronica Beno (51), ambaye ni ofisa mfawidhi wa ulinzi na usalama katika Kampuni ya Kilimanjaro Airport Development Company (Kadco) inayoendesha Kia na mwenzake Locken Kimaro (50).

  Miongoni mwa mashtaka yanayowakabili, ni kuongoza uhujumu uchumi, kumiliki isivyo halali nyara za serikali, kufanya biashara ya wanyama isivyo halali na kusafirisha nje ya nchi nyara za serikali kinyume cha sheria.
  Mashtaka hayo yalisomwa mahakamani na Wakili wa Serikali Kanda ya Moshi, Veritas Mlay, anayesaidiana na mawakili wenzake, Rajana Zakayo na Mchunguhela Malangwe, wanaotokea Dar es Salaam.

  Washtakiwa Martin Kimath, Veronica Beno, Locken Kimaro na Jane Mbogo wameshtakiwa kwa makosa mbadala, yakiwamo uzembe wa kushindwa kuzuia kosa na kushindwa kutoa taarifa ya watu wenye nyara za serikali.

  Wanyama wanaodaiwa kusafirishwa kwa magendo ni Twiga wanne wenye thamani ya Sh40 milioni, Choroa sita wenye thamani ya Sh25 milioni na aina mbalimbali za Swala wenye thamani ya Sh65.7 milioni.

  Washitakiwa hao wanakabiliwa pia na mashtaka ya kusafirisha aina mbalimbali ya ndege.
  Mshtakiwa wa kwanza ndiye anayekabiliwa na mashtaka mengi zaidi ya kuandaa, kusimamia, kuelekeza na kufadhili mpango mzima wa uhalifu wa kusafirisha kwa magendo nyara hizo.

  Hata hivyo, baada ya kusomewa mashtaka hayo, kuliibuka mabishano makali ya kisheria kuhusu uhalali wa mashtaka dhidi ya washtakiwa na kama chini ya sheria ya uhujumu uchumi walitakiwa kujibu chochote.Wakili anayemtetea mshtakiwa wa kwanza, Median Mwale, anayesaidiana na Andrew Maganga, walitaka mashtaka hayo yafutwe kwa kuwa yamefunguliwa bila kupata kibali cha Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

  Akijibu hoja hiyo, Wakili wa Serikali, Zakayo alidai kuwa sheria hiyo inataka kuwapo kibali cha DPP katika usikilizaji, lakini kilichofanywa na upande wa mashtaka ni kufungua mashtaka ya awali.Hakimu Kobelo alikubaliana na hoja za upande wa mashtaka na kuamuru washtakiwa kwenda rumande hadi Juni 24, suala la dhamana litakapoamliwa.

  Source: Mwananchi Saturday, 11 June 2011 09:17
   
 2. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mshtakiwa wa kwanza ndiye anayekabiliwa na mashtaka mengi zaidi ya kuandaa, kusimamia, kuelekeza na kufadhili mpango mzima wa uhalifu wa kusafirisha kwa magendo nyara hizo.

  Ahamed ambaye ni mshtakiwa wa kwanza ni Kamrani Ahamed (29), raia wa Pakistan . Kweli mgeni anafanya vitu vyote hivyo katika nchi iliyopata uhuru miaka karibia 50 iliyopita? Huku ni kulea uhuru, uzembe au ubinafsi?
   
 3. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hawa wanastahili kunyongwa ili iwe fundisho kwa wengine,, Pambaf zao!
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kazi ya usalama wa taifa ni nini? kama watu wanaweza kusafirisha wanyama vipi madini na madawa ya kulevya....
   
 5. F

  Fenento JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watu kama hawa si wakuwapeleka mahakamani kupoteza muda na rasilimali nyingine za serikali. Hawa ingekuwa moja kwa moja jera au kuwafilisi mali zao kwani hakuna utawala wa sheria kwa watu wa namna hii.
   
 6. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inadaiwa walisafirishwa kwa ndege ya jeshi la Qatar, tujiulize ndege ya jeshi kutoka nchi nyingene ibebe nyara za taifa bila kibali! vyombo vya usalama vilikuwa wapi? Kumbuka kwamba inadaiwa walisafirishwa usiku Wadanganyika wakiwa wamelala fofofo, huku majukumu ya ulinzi wa Taifa yakiwa mikononi mwa Jeshi JWTZ. Sasa tuambieni jeshi na usalama wa Taifa nao walikuwa wamelala???.
   
 7. A

  Antar bin Shaddad JF-Expert Member

  #7
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  na kama si vyombo vya habari kfichua utoroshwaji huo na kuandika (gazeti la Raia Mwema) basi watuhumiwa hao wasingefikishwa mahakamani.Kweli Tz shamba la Bibi aliyezeeka sana mwenye miaka 120!
   
 8. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #8
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Intelijensia ya magamba una expect nini? wanachunguza maandamano ya chadema tu ndiyo kazi yao!!
   
 9. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #9
  Jun 11, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Raia mwema wameiandika sana hii habari!! Hii inaweza kuhatarisha hata usalawa wa taifa kama ndege inaweza kutua na kupakia mzigo mkubwa kiasi hicho huku wazee wa intelijensia wamelala tu!!
   
 10. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #10
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiangalia kiundani zaidi unaweza kukuta hao waliofikishwa mahakamani ni geresha tu! wametolewa kama mbuzi wa kafara. Wenye mali au wahusika wakuu wako sehemu wanakula kuku kwa mrija tu. Kesi ikishajumisha raia wa kigeni - Pakistani kwenye mtandao wa Kigaidi kesi itaisha katika mazingira ya utata. Kinachotakiwa Wanyama hao warejeshwe nchini haraka iwezekanavyo.
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  In fact, utoroshaji ulioripotiwa na Raia Mwema ni mwingine. Huu unaoshotakiwa ulitokea mwaka Jana. Inaelekea kuwa huu ulikuwa mradi wa muda mrefu.
   
 12. h

  hans79 JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2011
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  ni kuwakata viongoz wa nyama mbadala ili kuilinda ccmagambaz
   
 13. Y

  Yetuwote Senior Member

  #13
  Jun 11, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani wazee wa intellijensia walijua kila kitu, hawakulala.
   
 14. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kama watu wanaweza kuja na ndege, wakapakia twiga na wanyama wengine wazima .... (twiga huwezi kumpitisha kwenye brief case), IGP Mwema, Mkuu wa polisi mkoa wa Arusha, wakuu wa polisi wilaya walimopitishwa wanyama hawa, WAZIRI wa mambo ya nchi na Waziri wa ULINZI wajiuzuru kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao!
   
 15. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  ni kwamba mpaka sasa doha qatar wanatangaza zoo yao kuuubwa aljazeera na cnn,utaona twiga na wanyama kila dizaini humo,toka mwanzo nimeona tangazo nilijua tayari wanyama wanaibiwa TZ.
   
 16. G

  GJ Mwanakatwe JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 241
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hawa waliofikishwa mahakamani ni dagaa tu, kambale bado, tunataka kambale nao wafikishwe mahakamani kwa kuwa mtankadao wa wizi huo ni mrefu ambao umewahusisha wafanyakazi wa serikalini ikiwa ni tanapa na wizara ya maliasili, hao wote wafikishwe mahamani.
   
 17. a

  alles JF-Expert Member

  #17
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 14, 2006
  Messages: 356
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu Kichuguu, Utoroshaji ulioripotiwa na Raia Mwema kuanzia toleo number 186,187,188 na 189 ndio huu na sio mwingine. Ukianza na toleo la 186, Raia mwema paragraph ya kwanza wameanza na kuripoti siku utoroshaji ulipofanyika pale Kadco tarehe 26 November 2010.(Ambayo ni mwaka jana). Pili majina ya watuhumiwa Ahmed Kamrani na Jane Mbogo ndio hao hao waliofikishwa mahakamani. Ukifuatilia mwendelezo wa nakala hizo utagundua kwamba kama issue isingetoka gazetini wasingefikishwa mahakani, kwa sababu hata watu wa upepelzi wa makosa ya jinai walikua wananyima access ya kupata vielelezo zaidi na maafisa wa wizara ya maliasili na utalii. Nakubaliana nawe huu ni mradi wa muda mrefu.Story unaweza kuifuatilia zaidi kwenye Raia mwema online kwa hayo matoleo niliyoyataja hapo juu.
   
 18. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #18
  Jun 11, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,817
  Likes Received: 1,164
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]


  [​IMG]

  HAYA WANYAMA NDIO HAO WASHAFIKISHWA ZOO HUKO DOHA QATAR
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Naogopa kutamka neno nisije pewa ban bure. Ngoja ni control hasira iliyo kifuani kwangu
   
 20. Nanyaro Ephata

  Nanyaro Ephata Verified User

  #20
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 979
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 60
  Wakati kesi inaendelea serikali iwasiliane na serikali ya Qatar ili warudishe wanyama wetu,
  Kulikuwa na habari ya mzungu kushikwa na pundamilia maeneo ya Olasiti sijui imefikia wapi?
   
Loading...