Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Hatimaye JK Ameanza Kujibu Mapigo Maana Magu Alizidi Kumdhalilisha Kana Kwamba Kila Jambo Alilofanya Hakuwa Anatumia Akili.
Hii Awamo Ya Maonyesho Itatupeleka Shimoni, Harafu Mpango Wa Kutugawia Sukari Uliishia Wapi Mpaka Sasa Hivi Nimemaliza Mitaa 6 Nimekosa Sukari.
 
Wakurupukaji tuuu.....na mzigo umeshawaelemea mpaka mnaomba maji,hii ni nchi bhana ina taratibu zake,huwezi kuzibadili kama unabadili ratiba ya chakula cha familia yako....hawa walifata taratibu zooote za nchi kuwa UDOM...nyie ndio mnakesha kujifanya mnshauri mpaka macho yanawavimba kumbe mnamchonganisha na wananchi tu
ina maana unapendekeza tuendelee na dola la wala rushwa na wapiga maela - Zakarias, Azizis and the like? mziki unakuja si muda mrefu.
 
Wasiwasi wangu ni kwamba inawezekana hili jambo halikujadiliwa hata kwenye Baraza la mawaziri...kama lingepita basi wasingepishana kauli,ndalichako na msemaji wa UDOM wana kauli moja,rais ana kauli nyingine, lingepita kwenye Baraza la mawaziri lazima wangeitisha ufaulu/matokea ya hao vijana,hii ingeuwa hoja kwamba hao vijana ni vilaza,hukohuko kwenye vikao vyao vya ndani, Pili lingefuata suala la milioni 800 wanazodai walimu,hili nalo si kubwa kwa serikali inayojigamba kuwa na makusanyo makubwa,wangebana huku na kule walipe waalim vijana wamalize shule,hizo hela walizobana kwenye semina na safari za nje wanapeleka wapi? Mbona Huduma za afya ziko vilevile?tunachoona ni ukosefu wa uongozi wa pamoja kati ya mawaziri na mwenyekiti wao rais..
Kuna mmoja anawavuruga
Kikwete oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee. Hapa mazee tumechemka. 2020 kura yangu kaikimbiza
 
Rais anapokosea,hawezi kuomba msamaha. Katika muktadha wa kisheria,husemwa 'Kings do no wrong'. Profesa mkenya P. L. O. Lumumba,aliwahi kutuambia watanzania pale Blue Pearl,Ubungo Plaza kuwa Rais hawezi kuomba msamaha.

Hajanituma. Sijatumwa na yeyote. Mimi namwombea msamaha kivyangu tu. Ni wazi Rais ameteleza kuwaita wapata daraja la nne vilaza na wengine wa madaraja mengine vipanga. Rais aliteleza kuchanganya mambo ya wanafunzi wa St. Joseph na wale wa UDOM. Wale wa UDOM hawakurudishwa nyumbani kwakuwa ni vilaza.

Rais aliyatumia maneno vilaza na vipanga kiutaniutani tu. Hakuwa na nia ya kuudhi,kukejeli wala kuumiza. Kwa vyuoni,hata UDSM,vilaza wapo na vipanga wapo. Kiutaniutani tu. Rais asamehewe na mada ifungwe. Rais anapaswa kufanya mambo mengine!

Mzee Tupatupa-Kilaza wa Lumumba,Dar es Salaam

.....kazi unayo mzee wangu!, huu mwaka mpaka uishe sijui utakuwa na majina mangapi;
....wa "ulevini" lumumba,
...."kilaza" wa lumumba,

loading...!!
 
Tuseme ukweli wanafunzi elfu saba utawafundishaje? Tangu lini form four akamfundisha form four mwenzie? Hawa wanafaa kuwa walimu wa primary, wapelekwe kigulunyembe na korogwe ttc.
 
Unahitaji saikolojia ya juu kugundua tatizo la ugonjwa wa akili alionao mtu mzima. Kuna mambo yanaendelea naona kabisa huyu mtu hayuko sawa!
Uko sahii sana Pochilangu. Kuna haja ya wataalamu wa Psychology, brain na magonjwa yasiyoambukiza kuingia mzigoni. Hapa kuna bonge la tatizo. .........mabarabara hewa kibaooooo...... alisema, the QNS is nani alikuwa msimamizi wa Wizara aliyosema ina mabarabara hewa kibao?. Is it possible mtu anyejitambua akajivua nguo mwenyewe ? Obvious, NOT. sasa kwa nini iwe? KUNA TATIZO
 
Kuna watu watakua wanafurahia sana haya matukio kwangu mimi naona kuna kukurupuka kufanya maamuzi ukijumlisha na kauli zisizo na busara za magu anazidi kujiweka pabaya
 
Kwa huu utofauti wa kauli,mh Ndalichako,msemaji wa chuo na mwakilishi wa wanafunzi wanaongea kauli sawa.Mh JPM anasema walikuwa ni vilaza.Sasa tuanzie hapa kujua ukweli uko wapi.Kisha tutafute suluhu.Pia napata mashaka kuwa Mh Raisi anaweza kuwa anadanganywa
basi watanzania ndio tutakuwa na matatizo, kila mala tunachagua maraisi wanaoshauriwa vibaya na wanaingia mkenge! jk ilikuwa hivyo na huyu hivyohivyo?
 
uwafukuza wale wanafunzi
Magufuli amelisababishia taifa
hasara maana wanafunzi wale
walikuwa wanatumia pesa za umma
kulipiwa gharama zote za masomo
sasa pesa hizo atazilipa nani? Hivi
kuna tatizo gani mwanafunzi wa
form 4 kusoma diploma kwa miaka
3, hata kama wasingelipelekwa
sekondari wangepelekwa hata shule
za msingi ili warejeshe deni letu na
kusaidia kuwajengea msingi mzuri
wa masomo ya sayansi watoto wetu.kwa
 
Wasijidanganye kwenda mahakamani bora wawe wapole tuu...hawana uwezo wa kupambana na Magufuli au serikali halafu wakashinda hakuna na kama wana danganywa na UKAWA watajuta!
 
JPM wangu weeee kalishwa kasa! Kama kweli hakuna Kilaza.....ni hatari kwa nchi kumdanganya President! Isije kutokea kumbe Kilaza ni Jesca pekee alieko UDOM! Naendelea kula pop corn movie ikiendelea!! Aje aombe radhi kwa lugha ya kuudhi!
Rais alieleza waziri wa elimu anafanyia kazi waliofukuzwa na kuona wale wenye ufaulu watataftiwa maeneo ya kuendelea na masomo sasa hizi kelele za nini hii inadhhrisha kuwa baadhi yao kuna vilaza
 
Wasomi wetu hawafanyi tafiti za kutosha wanakopi tuu ndio maana wakipata uongozi unashangaa mtu msomi anakua na maamuzi ambayo sio sahihi kwa jamii...
 
Taarifa alipewa na Jesca John kuwa kati ya wale buku 7 kuna wenye matokeo kama yake.
 
ina maana unapendekeza tuendelee na dola la wala rushwa na wapiga maela - Zakarias, Azizis and the like? mziki unakuja si muda mrefu.
Angekuwa yeye sio mla rushwa angekuwa ameshatolea ufafanuzi kuhusu Jexka
 
Back
Top Bottom