Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Unahitaji saikolojia ya juu kugundua tatizo la ugonjwa wa akili alionao mtu mzima. Kuna mambo yanaendelea naona kabisa huyu mtu hayuko sawa!
Chengachenga network haikamati vizuri. Nchi nyingine bunge lingemuhoji utendaji wake au hata kumuondoa.
 
Huyo mtoto alireseat akaendelea acheni ushambenga matokeo ya kureseat hamna mnaongea kishiranga kishambenga kikunanku kishombondokoloko kitawaponza
Kufeli, ku-reseat, kubadili fani, elimu za kuungaunga, na kozi fupifupi ni changamoto za maendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa nchini.
 
Inaonekana kuna informer wa mkuu anayemlisha matango pori mbaya.
Inawezekana Mwanzoni kuna umbea alipatiapatia akaaminiwa jumla jumla.
Sasa anampeleka mkuu chaka kwa kutumia usafiri wa mwendokasi.
 
Hahahahaha pochilangu umenichekesha balaaa hii nchi inaongozwa na siasa za kipuuzi......hatuwezi kupiga hatua kamwe
 
udom+students.jpg

Mwakilishi wa wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), waliofukuzwa Gibson Johnson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Beatrice Moses
By Waandishi wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.

“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.

“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.

“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”

Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.

Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.

“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.

Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.

“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.

Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.

“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.

My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?

Beatrice, naomba kukuuliza swali, kwanza Asante kwa kutuweka wazi kuhusu ufaulu wa Hawa Vijana. Swali: Hawa wanafunzi walifukuzwa chuo na Serikali au au uongozi Chuo? Walimu wanapogoma kufundisha haimfanyi mwanafunzi kupoteza haki ya masomo, which means hawafukuzwi, ila chuo kinaweza kuhahirisha masomo wakati bado wakitatua migomo ya walimu. Je walimu wakikubali kuendelea kuwafundisha Hawa Watoto mtawarudisha chuoni au mtawafanyaje?

Natanguliza shukrani!
 
udom+students.jpg

Mwakilishi wa wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), waliofukuzwa Gibson Johnson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Beatrice Moses
By Waandishi wetu, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co.tz
IN SUMMARY
Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.

“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.

“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.

“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”

Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.

Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.

“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.

Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.

“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.

Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.

“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.

My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?

Nendeni mahakamani acheni longo longo, majaji sio mashemaji zake JPM, kule kuna majaji kibao wanatamani wanangiwe kesi za serikali.
 
Sukari imeshindikana sasa Hili la wanafunzi nalo ni wazi kachemsha is he a manager or a leader? i wonder
 
Kwa huu utofauti wa kauli,mh Ndalichako,msemaji wa chuo na mwakilishi wa wanafunzi wanaongea kauli sawa.Mh JPM anasema walikuwa ni vilaza.Sasa tuanzie hapa kujua ukweli uko wapi.Kisha tutafute suluhu.Pia napata mashaka kuwa Mh Raisi anaweza kuwa anadanganywa
 
Sasa kama msemaji wa UDOM anasema hao walioitwa vilaza walikuwa na ufaulu wa division one,two,na wachache three,mh rais atawaambia nini watanzania anapodai walikuwa na division four? Hii si ushahidi kwamba rais hapati taarifa sahihi na mwisho wa siku anafanya maamuzi ya kuumiza watu? Ni nani alimpelekea rais taarifa hizo? Mbona UDOM kupitia msemaji wao na bi ndalichako kauli zao zinafanana? Za rais zinatoka wapi na ni naani mpasha habari wake? Wangapi wameshaumia kwa staili hii tangu aingie madarakani? Hawa watoto wakienda mahakamani watashinda kwa hakika,serikali itachukua kodi za nani kuwalipa fidia? Hiyo fidia na kuwaacha waendelee kusoma kipi cha busara?
Iparamasa, iko hivi: Washauri wa Rais kwa wakati huu wanamshauri au kumweleza kile anachokihitaji yeye mwenyewe. Kwamba, Rais anakuwa tayari ameshajishauri mwenyewe, kwa hiyo washauri wanapomfuata wanampa kile ambacho amejishauri mwenyewe!
 
Ndalichako naye kumbe ni mkurupukaji kama bosi wake?
 
Huyo msemaji wa udom nae anatuchanganya.anawezaje kusema kuwa wanafunzi walofukuzwa wana ufaulu mzuri wa grade 1,2and 3.!!! inamaana hajui kama jesca John yupo UDOM?
km jesca amedahiliwa UDOM,uwezekano wa kwepo kwa wanafunzi wa aina yake upo.cha msingi UDOM waweke file zima la wanafunzi hao tuone matokeo yao.
Ndio ninyi mnaoongozwa na methali/misemo ya samaki moja akioza, Wote wameoza. Badala ya kukaa chini ukafanya uchunguzi wa yupi kaoza na yupi hajaoza. Mwisho wa siku unaona ni bora uingie hasara isiyo na tija kwa ufinyu wa fikra. Haya mawazo ungempa mapema waziri husika/ Rais wake kabla ya maamuzi yao, na si kumpa msemaji wa chuo muda huu tayari "samaki wameisha mwangwa" wote
 
Tatizo mnaongea sanaaaaa ila maamuzi ya Magufuli hayarudi nyuma
Haiwezekani serikali ibebe mzigo wakati wangeweza enda soka A level
Huyu naye......
Kwani hiyo program ilianzishwa na nani?
Nani aliwadhawishi wasiende A level badala yake wakapunguze tatizo la uhaba wa walimu wa sayansi mashuleni???
-Inawezkana umekurupukia mada usiyoijua! Pole sana
Kaulize afu uje upya
 
Sasa kama msemaji wa UDOM anasema hao walioitwa vilaza walikuwa na ufaulu wa division one,two,na wachache three,mh rais atawaambia nini watanzania anapodai walikuwa na division four? Hii si ushahidi kwamba rais hapati taarifa sahihi na mwisho wa siku anafanya maamuzi ya kuumiza watu? Ni nani alimpelekea rais taarifa hizo? Mbona UDOM kupitia msemaji wao na bi ndalichako kauli zao zinafanana? Za rais zinatoka wapi na ni naani mpasha habari wake? Wangapi wameshaumia kwa staili hii tangu aingie madarakani? Hawa watoto wakienda mahakamani watashinda kwa hakika,serikali itachukua kodi za nani kuwalipa fidia? Hiyo fidia na kuwaacha waendelee kusoma kipi cha busara?

Gazeti la jamhuri ndo source za taarifa...au vijigazeti vingine vya udaku
 
Back
Top Bottom