Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Waliotimuliwa UDOM waibuka, watoa ya moyoni

Hii serikali sio ya kuomba na ikasikiliza, labda nendeni mkamuombe tulia akson

ah ah tulia akson kawakatalia wabunge sembuse hawa aka vilaza lazima waisome namba ya ccm nadhan wa kulaumiwa ni wazazi wao pia wale waloichagua ccm kwan haina huruma kwa watoto wa masikini
 
JPM wangu weeee kalishwa kasa! Kama kweli hakuna Kilaza.....ni hatari kwa nchi kumdanganya President! Isije kutokea kumbe Kilaza ni Jesca pekee alieko UDOM! Naendelea kula pop corn movie ikiendelea!! Aje aombe radhi kwa lugha ya kuudhi!
Mbona hawajaongelea lile la JPM kusema kwamba Prof. Kikula alilazimishwa?
 
Mimi ninaona serekali ingepaswa kuwapa nafasi hata wale walioingia pale kwa marks mbovu lakini wakaperform na wakawa na GPA nzuri pengine kuliko hata wale wenye one na two.
 
udom+students.jpg

Mwakilishi wa wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), waliofukuzwa Gibson Johnson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Picha na Beatrice Moses

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.

“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.

“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.

“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”

Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.

Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.

“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.

Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.

“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.

Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.

“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.

My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?
Kama hii taarifa ni sahihi najiuliza nachoka nani anapotosha Kati ya Waziri, rais au afisa uhusiano?
 
Ndio ni Vilaza hivi huwa nashangaa kweli MTU unapataje daraja LA tatu katika matokeo ya kidato cha NNE.....si ukilaza huu
Acha mbwembwe,, we ulipata ngapi?? Chunga kauli yako?
 
Mimi ninaona serekali ingepaswa kuwapa nafasi hata wale walioingia pale kwa marks mbovu lakini wakaperform na wakawa na GPA nzuri pengine kuliko hata wale wenye one na two.
Kwa maana hiyo hakutakuwa na maana ya mitihani ya kidato cha nne wala cha sita. Wot3 waingie vyuo vikuu na huko ndio watachujwa kwa GPA.
 
Anko soma hotuba ulioandikiwa ya moyoni yatakuponza mengi
 
Huyo mtoto alireseat akaendelea acheni ushambenga matokeo ya kureseat hamna mnaongea kishiranga kishambenga kikunanku kishombondokoloko kitawaponza
Yani ndio umekaa ukafikiri then ukaona uje na mashudu haya.Kwanza sijui hata kama unajua unaongea nini?Ningekuona wa maana kama ungekuja na hayo matokeo ya kurisiti hapo ningekutofautisha wewe na jesca.
 
Kama hii taarifa ni sahihi najiuliza nachoka nani anapotosha Kati ya Waziri, rais au afisa uhusiano?
Afsa uhusiano anasema kwa niaba ya Prof. Kikula! Mimi hata nashindwa kuelewa nini kinaendelea: Rais anasema, waziri anasema, chuo kinasema, wanafunzi wanasema! Nabaki kuwa kama Mr. Brown; Brown ashika tama.
 
Hivi huyu mzee mwaka 2020 atapata Kura ngapi mbn kila siku majanga afadhali ya jana duh...!
 
udom+students.jpg

Mwakilishi wa wanafunzi, Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), waliofukuzwa Gibson Johnson akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
View attachment 353745
Wawa ni wanafunzi Miongoni mwao wapo walioweza kuathirika na timua hiyo, wamelazimika kukutana na vyombo vya habari katia kujadili suala hilo ambalo mpaka sasa hakuna mwenye tamko la mwisho zaidi ya mheshimiwa Rais wa jamhuri wa Tanzania

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Dar/Dodoma. Sakata Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) limezidi kupanuka baada ya wanafunzi waliorudishwa nyumbani kupinga kuitwa vilaza.

Jana wawakilishi wa wanafunzi hao ambao waliambatana na viongozi wa

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), walisema wanapinga pia hatua ya kutimuliwa chuoni.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Gibson Johnson alisema wanasikitika kuona wanavyozushiwa tuhuma mbalimbali kuhusiana na wao kujiunga na chuo hicho.

Alisema wamekuwa wakijiuliza sababu za Serikali zinazotaka kuhalalisha kutimuliwa kwao chuoni kuwa hawakuwa na sifa, jambo ambalo si la kweli.

“Siyo kweli kwamba sisi ni vilaza (wanafunzi wasiofanya vizuri darasani) na waliofeli na kupata daraja sifuri.

“Sisi ni wanafunzi tuliofaulu kwa viwango vilivyohitajika kwa daraja la kwanza hadi la tatu na tulipangiwa shule za kuendelea na masomo ya kidato cha tano na sita, lakini tulibadili na kuamua kujiunga Udom, hivyo tunaomba Serikali itumie busara zake.

“Hatuwezi kwenda kusoma kidato cha tano na sita kwa kuwa tumepoteza muda wetu.”

Alisema wanamshauri Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako na Rais John Magufuli kutumia busara kuwarudisha chuoni kumalizia masomo yao.

Katibu Mkuu wa TSNP, Alphonce Lusako aliitaka Serikali ichukukue hatua kwa waliohusika kudahili wanafunzi wasio na vigezo na kuwawajibisha.

“Lakini pia wanafunzi wafidiwe fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni, kama hawatapewa haki zao, sisi tutashirikiana na wadau wa elimu zikiwamo asasi za utetezi wa kisheria kutafuta haki mahakama,” alisema Lusako.

Udom yazungumza

Ofisa uhusiano wa Udom, Beatrice Baltazali alisema wanafunzi hao wote walifaulu vizuri wakiwa na daraja la kwanza, pili na wachache daraja la tatu.

“Wanafunzi wote walikuwa na nafasi ya kwenda kidato cha tano, lakini kwa kuwa waliahidiwa ajira, waliona wapitie huku kwa kuwa watapata ajira ya moja kwa moja,” alisema.

Beatrice alisema walimu wa Udom walikuwa wanalipwa fedha za ziada kuwafundisha wanafunzi wa programu hiyo kwa kuwa walikuwa wanatumia muda mwingi zaidi ya kiwango walichokuwa wamepangiwa.

“Kutokana na madai ya malipo hayo, mkaguzi wa ndani aligundua kuna tatizo, ndiyo walimu nao wakaamua kugoma, wanafunzi wakawa hawafundishwi Serikali ikaamua warudishwe nyumbani,” alisema Beatrice.

My take; mh raisi tuelewe lipi na aliangalia wapi mpaka ukajilizisha hawa wanafunzi kufukuzwa ndani ya masaa 24?

=========================

Tamko la Wanafunzi waliofukuzwa

=========================

Ndugu Waandishi wa habari,

Awali yayote tunapenda kupongeza jitihada kadha wa kadha ambazo zimekuwa zikifanywa na serikali kupitia Wizara ya Elimu kuhakikisha inaboresha mfumo wa Elimu nchini.

Pamoja na ukweli kwamba, kumekuwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Elimu haswa katika awamu hii ya Uongozi wa Mh. Raisi, John Pombe Makufuli. Mtandao wa Wanafunzi Tanzania unasikitishwa na kulaani baadhi ya maamuzi yaliyokwishafanyika na kukiuka utu, haki za Wanafunzi na vile vile taratibu, kanuni na sheria za nchi hii.

Kuhusu Sakata la Kufukuzwa Wanafunzi UDOM

Mumesikia hoja za viongozi mbalimbali juu ya sakata la Wanafunzi Waliosimamishwa UDOM, mmesikia hotuba ya Mh. Joyce Ndelichako, Waziri mwenye dhamana katika wizara ya Elimu, lakini vile vile mmesikia hotuba ya Mh. Raisi, John Pombe Makufuli aliyoitoa akiwa chuo kikuu cha taifa (UDSM) tar. 02.06.2016

Tangu tar. 28 mei 2016, mara baada ya agizo la Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi (MoEST) la kuwarejesha nyumbani Wanafunzi takribani 7802 Mtandao huu umekua ukifanya tafiti za kina kupitia idara yake (Reseach& Training Department) na kupata taarifa za pande zote mbili kutoka vyanzo mbalimbali vya taarifa “Wahanga(Wanafunzi waliofukuzwa) na Watawala(Wizara ya Elimu) ”.

Tumejiridhisha kwamba kitendo kilichofanywa dhidi ya Wanafunzi wa UDOM ni ukiukwaji mkubwa wa haki za Wanafunzi ambacho kilikuwa kwanza cha kimabavu na hakikuzingatia kabisa utu wa Wanafunzi husika.

Taarifa zilizotufikia ni kwamba Wanafunzi walifukuzwa kama Wakimbizi ndani ya nchi yao, Polisi walizagaa kila kona na bunduki zao kama wanafukuza majambazi, hofu ilitanda na wanafunzi wengine kuogopa kurudi chuoni kwa hali ilivyokuwa. Mtandao huu unasikitishwa kwa matumizi makubwa ya vyombo vya dola lakini vile vile madhara yaliyowakumba Wanafunzi husika wakati wa zoezi la kuwaondoa chuoni.

Chimbuko la Mgogoro:

Ikumbukwe, wakati wa uongozi wa Mh. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu kama vile Mamlaka ya Elimu (TEA), Tume ya vyuo vikuu (TCU), Mamlaka ya vyuo vya Ufundi (NACTE) na wadau mbali mbali a Elimu, waliadhimia na kuzindua program maalumu ya kusomesha waalimu wa masomo ya Sayansi katika shule za sekondari nchini ili kutatua changamoto za uhaba wa waalimu wa masomo ya sayansi.

Lakini ili kupata waalimu wenye sifa Serikali ikaweka sifa za Udahili kwamba itakuwa kwa wahitimu wa kidato cha nne tu waliopata daraja la 1,2 na 3 pia wawe na ufaulu wa alama A” au B” kutoka masomo ya sayansi. Na serikali ikawashawishi kwa ahadi ya kuwapa mkopo kwa 100%.

Tumeshangazwa kwamba, Sababu za kusimamishwa masomo wanafunzi hawa zimeendelea kubadilika badilika, sababu ya kwanza kabisa, ambayo ilisemwa na Prof. Joyce Ndelichako Bungeni ni Mgomo wa Wahadhiri uliotokana na kukosa posho za kuwafundisha Wanafunzi husika, Sababu ya pili ni wanafunzi kukosa sifa.

Mtandao huu umejiuliza, Kama suala kuu ni vigezo kwanini serikali isingeweka utaratibu maalumu wa kuwaondoa wanafunzi wasio na sifa na kuwawajibisha wale waliowadahili kinyume na standard zilizowekwa na serikali?

1. Tunapenda Kutumia fursA hii kukanusha taarifa zote za uongo zilizotolewa na watawala/Viongozi dhidi ya wanafunzi husika. Na kumekuwa na utamaduni wa Watawala kutumia Vyombo vya habari(Media coverage) kama silaha ya kupotosha taarifa kwa umma(Taarifa hii itasomwa na muwakilishi wa wahanga wa Wanafunzi (UDOM)

Ombi letu.
1. Tunaiomba serikali kupitia wizara yake ya Elimu ifanye hima kuwarudisha Wanafunzi husika ili kutoendelea kupoteza rasilimali muda wa wanafunzi husika

2. Kama hotuba ya Mh. Raisi hapo juzi katika chuo kikuu cha Dar es Salaam, akikiri kwamba kunawanafunzi wasio na vigezo walidahiliwa. Mtandao huu unaomba waliohusika kuwadahili wawajibishwe haraka iwezeanavyo lakini vile vile wanafunzi wafidiwe Rasilimali fedha na muda waliopoteza kwa wakati wote waliokuwa chuoni.

Hatma ya Wanafunzi (UDOM)
Kama itatokea, kunamwanafunzi au kundi Fulani la Wanafunzi, halitopewa haki zake, Mtandao huu utashirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu zikiwemo azaki zinazojihusisha na masuala ya utetezi kisheria kutafuta haki za Wanafunzi husika mahakamani

Chanzo cha Migogoro katika Sekta ya Elimu Nchini.

v Kutokuwa na Muafaka wa Kitaifa katika Mfumo wa Elimu.

Mtandao huu unaamini kwamba haya yote ni madhara ya kutokuwa na muafaka wa kitaifa/Msimamo wa itaifa katia Sekta ya Elimu nchini. Kwa mda mrefu, mfumo wetu wa Elimu, Sekta ya Elimu nchini imekuwa inaendeshwa na kiwango cha utashi wa Waziri wa Elimu aliyepo madarakani na sio kuongozwa na dira/Muafaka/Msimamo wa kitaifa katika sekta ya Elimu.

Tumeshuhudia, Mawaziri wa Elimu tofauti tofauti, katika awamu tofauti tofauti za uongozi tangu uhuru wa nchi hii (Mh.Jumanne Maghembe, Mh, Joseph Mongai, Mh. Shukuru Kawambwa na sasa Mh. Joyce Ndalichako), wakifanya maamuzi kutokana na kiwango cha utashi wao na mapenzi yao. Hii ni hatari katika taifa letu na imesababishwa na ukweli kwamba taifa limekosa dira/Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini.

Hitimisho.
Mtandao wa Wanafunzi Tanzania unaamini kwamba kilichotokea Chuo Kikuu cha DODOMA kitakuwa msingi wa Serikali kupitia Wizara ya Elimu kuanza harakati rasmi za kimapinduzi za kuunganisha wadau wote wa Elimu nchini ili kuwa na mjadala mpana wa kitaifa wa namna ya kufikia Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini.

Vile vile Mtandao huu umeshaandaa waraka maalumu kwa Waziri wa Elimu unaotoa muongozo wa namna taifa litakavyofanikisha kuwa na Muafaka wa kitaifa katika sekta ya Elimu nchini ambao tutauwasilisha wizarani mapema wiki ijayo.

Mwisho kabisa, tunaomba viongozi wote wa dini na wale wanaoamini, kuendelea kumwombea Mh. Raisi n a viongozi wengine ili waongoze taifa hili kwa hekima na busara na kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria za nchi hii.

Awa madogo wangepata mwanasheria mzuri na mahakama zingekua huru madogo wangelipwa pesa ya kutosha
 
Afsa uhusiano anasema kwa niaba ya Prof. Kikula! Mimi hata nashindwa kuelewa nini kinaendelea: Rais anasema, waziri anasema, chuo kinasema, wanafunzi wanasema! Nabaki kuwa kama Mr. Brown; Brown ashika tama.
Hayo ndio mambo yanayoendelea kila ofisi ya serikali,diwani anasema hiki,mwenyekiti wa halmashauri like,Mkuu wa Wilaya hiki,Mkuu wa mkoa lile,katibu tawala hiki,anakuja waziri anavuruga zaidi,naibu waziri naye anakuja na pombe zake,katibu Mkuu wa wizaraaa.....na wote wanaongelea jambo moja
...sasa hivi watendaji wa serikali wamekaa kitako...hawatendi kitu....wanasubiri wafanya vutugu wamalize vurugu zao ili Kazi zianze
 
Wasiwasi wangu ni kwamba inawezekana hili jambo halikujadiliwa hata kwenye Baraza la mawaziri...kama lingepita basi wasingepishana kauli,ndalichako na msemaji wa UDOM wana kauli moja,rais ana kauli nyingine, lingepita kwenye Baraza la mawaziri lazima wangeitisha ufaulu/matokea ya hao vijana,hii ingeuwa hoja kwamba hao vijana ni vilaza,hukohuko kwenye vikao vyao vya ndani, Pili lingefuata suala la milioni 800 wanazodai walimu,hili nalo si kubwa kwa serikali inayojigamba kuwa na makusanyo makubwa,wangebana huku na kule walipe waalim vijana wamalize shule,hizo hela walizobana kwenye semina na safari za nje wanapeleka wapi? Mbona Huduma za afya ziko vilevile?tunachoona ni ukosefu wa uongozi wa pamoja kati ya mawaziri na mwenyekiti wao rais..
Kuna mmoja anawavuruga
you seem to know little or nothing about how the state operates. The state is impersonal so are its decisions. Yet, corrupt mind people may distrust a non corrupt president but trust a mere spokesperson. shame! the era of graft train are gone, it is JPM train era. You are either with JPM and Tanzanians or with corrupt clique.
 
Mi nilijua tu baba jesca amekurupuka kama kawaida yake.Busara na hekima ni hamna kabisa...shame
 
Back
Top Bottom