Walioongopea Kamati Watakiona - Dr. Mwakyembe

Ni kweli sasa wataonja utamu wa muwa kwa kuficha kwao kuweka wazi kila walichogundua. Kamati iligundua mengi na Mwakyembe aliwahi sema kama watuhumiwa wataendelea kulalamika atasema kila kitu. Kwa hiyo kuna mambo walificha kuwasitiri wengine.
 
Mapendekezo 18 ya Kamati ya Mwakyembe




  1. Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2004 (Public Procurement Act, 2004) ipitiwe upya ili kuiboresha kwa kuipa Mamlaka nguvu zaidi za udhibiti na uwezo wa kuchukua hatua pale sheria na kanuni zinapokiukwa, badala ya kutoa ushauri tu kama ilivyo sasa.
  2. Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma isiwajibike Wizara ya Fedha ambayo nayo ni taasisi ya ununuzi (procurement entity) badala yake iwe chombo huru kinachowajibika Ofisi ya Rais na taarifa zake kuwasilishwa bungeni.
  3. Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC na sasa Dowans Holdings S.A, kama ilivyo mikataba kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals inatoa unafuu usiostahili kwa makampuni hayo ya umeme na kuiumiza TANESCO na hatimaye watumiaji na walipa kodi kimapato, k.m mikataba hiyo kuwa na vipengele vya kuibana TANESCO kuyalipia makampuni hayo kodi zinazohusika na uendeshaji (operations), matengenezo/marekebisho ya mara kwa mara ya mitambo (maintenance) gharama za bima, ada za mawakili na washauri elekezi (consultants) gharama za mafuta na gesi ya kuendeshea mitambo, gharama za ukodishaji mitambo (capacity charges) ambazo TANESCO hulipa kila mwezi si chini ya wastani wa shilingi bilioni 2 kwa kila kampuni, izalishe au isizalishe umeme.
  4. Serikali ipitie upya mikataba yote kati ya Tanesco na wazalishaji wa umeme binafsi mapema iwezekanavyo kama ambavyo mikataba ya madini inavyopitiwa upya sasa kwani bila kufanya hivyo, mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea wananchi na kushindwa kufikia azma ya serikali ya maisha bora kwa kila Mtanzania.
  5. Kwa kuwa mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC ulikuwa wa uzalishaji umeme wa dharura kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali ngumu ya ukame uliokausha mabwawa yote ya kuzalishia umeme, serikali itathmini upya uhalali wa kuwepo na kuendelea kuwepo na mkataba huo kutokana na udanganyifu bayana uliofanywa na Richmond Development Company LLC kuhusu uwezo wake kifedha, kiufundi na uzoefu wake katika masuala ya uzalishaji umeme; usajili na uwepo wake kisheria kama kampuni halali yenye ukomo wa hisa nchini Marekani na Tanzania; uhusiano wake kisheria na kampuni kubwa ya kimataifa ya Pratt & Whitney.
  6. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye katika majadiliano yake na Kamati Teule alionyesha kutokuelewa kabisa kilichokuwa kinatendeka na wasaidizi wake, na mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Wakili wa Serikali, Donald Chidowu, ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yeyote, wawajibishwe na mamlaka ya juu ya nchi kwa kuchangia kuiingiza nchi katika mkataba wa aibu.
  7. Katika mikataba yote na makampuni ya nje, serikali ihakikishe kuwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inatumika kikamilifu katika kupata taarifa kamili za kampuni hizo, kama vile wanahisa, mitaji na anwani. Aidha, ofisi zetu za ubalozi zilizo sehemu mbalimbali duniani zihusishwe katika majadiliano na makampuni yanayotoka nje ya nchi kwa lengo la kupata taarifa zao za msingi na kuboresha nguvu ya hoja ya serikali.
  8. Wajumbe wote wa Kamati ya Serikali ya Mashauriano katika suala la Richmond ambao ni maafisa waandamizi wa serikali wawajibishwe mara moja kwa kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya taifa.
  9. Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi aliyeshabikia sana uhaulishaji huo, awajibishwe.
  10. Yafanyike mabadiliko ya haraka ya uongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru ambayo ilitoa ripoti mbovu ya kuisafisha Richmond.
  11. Wakati umefika sasa kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 (Public Leadership Code of Ethics Act) ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaoonekana wa kawaida sasa wa viongozi waandamizi wenye dhamana kisiasa kuendelea na biashara zao wakiwa madarakani, hivyo kuwaweka kwenye mtihani mkubwa wa mgongano wa kimaslahi katika maamuzi yao. Tufike mahali ambapo sheria iwalazimu kuchagua kati ya utumishi wa umma au biashara binafsi, viongozi waandamizi wenye dhamana kisiasa (mawaziri na kuendelea) kuendelea na biashara zao wakiwa madarakani hivyo kuwaweka kwenye mtihani mgumu wa mgongano wa kimaslahi.
  12. Serikali iondokane kabisa na utaratibu wa kutumia mawakala katika ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme nchini na kuhakikisha kuwa wizara husika ina taarifa za bei halisi ya mitambo kila wakati ili kujiepusha na mchezo wa kawaida wa mawakala kupandisha bei mara mbili au zaidi ya bei halisi.
  13. Utaratibu tuliourithi kutoka kwa wakoloni na kuuzoea wa kuiona mikataba ya kibiashara kuwa ni siri hata kwa walipa kodi wenyewe na kuwa uwanja wa pekee wa watendaji, umepitwa na wakati.
  14. Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, Ibrahim Msabaha na Katibu Mkuu, Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza taifa kwa makusudi kwenye mkataba na kampuni ya mfukoni ambao umesababisha hasara kubwa kwa nchi.
  15. Kamishna wa Nishati, Bashir Mrindoko achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na wizara toka mwaka 2004 kwenye mkataba wa bomba la mafuta.
  16. Utaratibu wa kuteua wakurugenzi na makamishna katika wizara kuwa wajumbe wa bodi za wakurugenzi za mashirika yaliyo chini ya wizara, unazua mgongano wa kimaslahi, kudhoofisha usimamizi na uwajibikaji, hivyo serikali iupige marufuku mara moja.
  17. Waziri Mkuu Edward Lowassa ambaye ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni apime uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge.
  18. Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu kwa mujibu wa Ibara ya 51, liangalie matokeo ya uchunguzi huu kama hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.


Sidhani kama mapendekezo yalifanyiwa kazi zaidi ya LOWASSA, KARAMAGI NA MSABAHA KUJIUZULU
 
nadhani selelii kasahaulika akitafutwa huyu jamaa n hivi walimtosa ubunge anaweza akafunguka mpaka tukashangaa. nakumbuka kuna siku ilikuwa bungeni au sijuini wapi mwakyembe alipandwa na hasira na akasema au tuseme mambo yote hadharani nahisi vitu flani muhimu walificha sasa vinaweza kuwarudia.
be

Huyu Seleli inaonekana anajua mengi tu
 
Ni kweli sasa wataonja utamu wa muwa kwa kuficha kwao kuweka wazi kila walichogundua. Kamati iligundua mengi na Mwakyembe aliwahi sema kama watuhumiwa wataendelea kulalamika atasema kila kitu. Kwa hiyo kuna mambo walificha kuwasitiri wengine.
Akhsante mkuu! hiki ndicho nilikuwa namaanisha, ile fichaficha!
 
Walichokosea akina Mwakyembe ni kutobainisha ya kuwa uteuzi wa Dr. Idrissa Rashidi ulifanywa na JK mwenyewe huku Dr. Rashid akiwa hajaiomba hata hiyo nafasi yenyewe................na pili Dr. Rashid hakuwa na sifa ambazo Bodi ya Tanesco ilizitangaza..........................na tatu Dr. Rashid alikuwa na umri wa miaka 62 wakati huo na hivyo asingepaswa kuwa mtumishi wa taasisi yoyote ile ya umma.......................................................

Haya mazingira ya kifisadi ndiyo JK kwa uroho wake wa utajiri wa fasta fasta alimtumia Dr. Rashid katika kuchora mchoro wa RICHMOND na baadaye DOWANS.........................

Haya mazingira yalitosha kwa kamati ya Mwakyembe kupendekeza JK achunguzwe na Bunge juu ya kuhusika na ajira ya Dr. Rashidi ambayo ndiyo ilizalisha RICHMOND na DOWANS......................na kama itabainika ndivyo ilivyokuwa basi Bunge lipige kura ya kukosa imani naye.............................................

Haya ndiyo makosa ya Kamati ya Mwakyembe na JK kwa kuelewa jinsi kamati hiyo ilivyomstahi shukrani yake ikawa ni kumhonga Mwakyembe na Unaibu Waziri...............
 
tatizo wanasiasa hawaaminiki walidai wao makamanda wa ufisadi huku wakiwa waoga na unafiki waliwezaje kuficha siri za mafisadi?
 
Back
Top Bottom