Walioongopea Kamati Watakiona - Dr. Mwakyembe

Hongereni sana. Bahati mbaya nimekuta imepita. Lakini inasikitish sana kuhusu Tanzania Daima, inawezekana kabisa kuna mkono wa mtu... sasa nataka kuamini hivyo. Suala la kuweka stories halihitaji utaalamu mkubwa, zaidi ya kumfundisha hata mtumishi wa Tanzania daima ama hata hao Raia Mwema, na humu JF kuna watu wako tayari hata kuwasaidia bureeeeeee kama wanakwama.

Lakini kwa kuongezea ni kwamba, Nasikia PMO wanasema, "sisi ndani ya serikali tuliahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwa kamati ya Richmond, ndio maana tukawaita watumishi wetu wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine kwa nia ya kuwaandaa kabla ya kuitwa katika kamati. Kwanza wataalamu tiliwataka wasisafiri kwenda popote, na pili tuliwambia waandae nyaraka zote muhimu ili zikitakiwa na akina Mwakyembe wasibabaike.. Huo ndio ushirikiano tuliahidi, sasa watu wengine wanataka kusema kwamba tuliwaita ili kuwafundisha kusema uongo na kughushi ama kuficha nyaraka za ushahidi ama kupotosha, huo ni uzushi mtupu..."

MUSIULIZE NANI KASEMA HAYO, TUSUBIRI TUSIKIE
 
Thanks Mwanakijiji, interview ilikuwa nzuri sana ingawa ilikuwa fupi lakini uligusa maeneo yote muhimu.
 
si mlisikia alikuwa yuko barabarani? Ila kuhusu mambo ambayo sikuyaingilia kwa undani ni kwa sababu uchunguzi unaendelea na mimi kugusia ni taarifa gani "zinagongana" yawezekana ingekuwa kumwaga mtama kwenye kuku wengi.. ila believe me, ninabahati ya kufahamu kidogo hicho kinachogongana, and its not joke! Nyie subirini tu msikie mtu anajiuzulu few days before the new House session au baraza kuvunjwa kuwaokoa nyuso zao.. na hawa wadogowadogo waliojifanya wajuaji mtaona watu wanaongozwa wakiwa na pingu!
 
Nami nilimsikia kwenye taarifa ya habari ya jana saa 2 ya ITV Dr. mwakyembe akieleza kwa kujiamini na kwa hamasa. moja kwa moja nika hisi kuwa kuna jambo huko vinginevyo asingekuwa na sababu za kusema vile. Ali rudia rudia sana juu ya wanafanya mzaha basi wasubiri na ushahidi wao wa kupika.
 
Lakini jamani mie nadhani kuna umuhimu wa kufahamu nani wanaohujumu magazeti kama TZ Daima na Raia Mwema kila yanapokuwa na habari nzito.I was surprised kwamba kwanini hadi muda huu TZ Daima haliko mtandaoni.Ni hujuma ndani ya magazeti hayo au.....?Wataalam wa IT mnisaidie hapo

Hii hujuma ni ya mafisadi. Nasema hivi kwa sababu hakuna Mtanzania yeyote aliye na wasiwasi na tuhumba mbali mbali zinazoandikwa katika magazeti yetu ya Tannzania Daima, Raia Mwema, THIS DAY, Mwananchi na mengineyo isipokuwa mafisadi, wala rushwa na viongozi wenye uroho wa utajiri wa haraka haraka. Hawa wanaona wigo wao wa kujidai unazidi kuwa finyu, hivyo wanajitahidi kila njia kuyafunika madhambi yao.

Wakae wakifahamu kwamba wanaweza tu kuchelewesha madhambi yao kuanikwa hadharani, lakini kamwe hawawezi kuyazuia maana Watanzania wameshaamka na wanahakikisha wanapambana na mafisadi kila kona ya nchi na mifano iko mingi mmoja wapo ni kuvuja kwa mkataba wa Buzwagi ambao ulitaka kufanywa siri.
 
Asante Mwanakijiji. Mahojiano mafupi, na yaloshiba taarifa muhimu. Kumbe mheshimiwa alikuwa barabarani na anaendesha mwenyewe gari. Anastahili kuwa na dereva, au siyo? Na kupokea simu wakti anaendesha gari ni hatari kwa usalama wake. Mkumbushe ajiangalie usalama wake pia, twamhitaji sana huyu mheshimiwa, ni mtu muhimu sana kwa nchi yetu.
 
mzee hapo umenipa wazo.. ngoja nikutumie maana podomatic hadi waibadili format nadhani ndio maana player inakimbia. Nitakutumia unedited..

...nawe mwanakiji unapenda cheap sana,hivyo vipodomatic sijui vipodozi ni usumbufu mtupu,hebu rahisisha mambo teknoloji inaruhusu sasa
 
Halisi and others, BIG UP. Naweza kusema tunuapoelekea mwisho wa mwaka Nyani amekomwa Giladi haswa, maslahi ya nchi yetu mbele, tuwe na moyo mchango wetu ingawa ni mdogo kwenye kubadilisha nchi, lakini una umuhimu wake....hujuma zipo hata humu zimekuwa zikionekana lakini they are doomed to failure. Taratibu taratibu mapapa yatatajwa na kuchukuliwa hatua.
Kuna haja ya wana JF kupongezwa, kwa moyo walioonesha kwa upendo wa taifa. Wasaliti watashindwa.
 
Mimi sioni hata haja kuwahoji mara ya pili wale watumishi wa serikali, maana hapo ni kuwapa chance ya ku-edit story zao. Akina Mwakyembe wangekaa na hizo taarifa za uongo walizopewa na watumishi, wakaendelea kusaka ukweli hali, ili pindi wanamalizia research yao, hawa watumishi wanabambwa vizuri tu! Tena hapo ndio angewadaka sawasawa. Sasa hivi wameshaona kuna utata kwa hiyo watafanya mbinu zote na unaweza kukuta kibao kinachange na kinapungua uzito kuliko tunavyofikiri. Dalili za mvua ni mawingu. JK akitoka USA nina uhakika ataondoa fisi wote na kubakiza kasuku.
Kuna ndugu hapo juu kamponda sana Mwanakijiji wetu anayetuletea habari hizi live eti anatumia technology cheap. Si vizuri kumpaka namna hiyo, mnaona kabisa anajitahidi kutuunganisha kimawasiliano katika kulitetea taifa letu. Tumpe moyo badala ya kumsakama kwa mambo ya kijinga.
Mwanakijiji nakupongeza sana.
 
Kamati ya Richmond 'yahamia' Marekani

*Yaenda kuhoji wamiliki, maofisa Ubalozi
*Ushahidi uliotolewa waingia mkanganyiko
*Ili kukamilisha kazi yaongezwa siku 15


WAJUMBE watatu wa Kamati Teule ya Bunge inayochunguza zabuni ya jenereta za umeme iliyopewa kampuni ya Richmond wamekwenda Marekani kufanya mahojiano na wamiliki wa kampuni hiyo na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania.

Akitoa taarifa jana kuhusu safari ya wajumbe wa kamati hiyo kwa waandishi wa habari katika ofisi za Bunge, Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dkt. Harrison Mwakyembe, alisema safari hiyo ina lengo la kupata taarifa zaidi kuhusu kampuni hiyo kutoka kwa wamiliki na maofisa hao.

Kwa mujibu wa Dkt. Mwakyembe, taarifa kutoka kwa wamiliki na maofisa hao, zinahitajika ili kuiridhisha Kamati kuhusu taarifa mbalimbali ambazo zilitolewa kwake nchini.

Hata hivyo, Kamati imeanza kuonesha wasiwasi kuhusu ukweli wa taarifa ambazo zimepatikana kutoka kwa watu mbalimbali waliohojiwa nchini.

Dkt. Mwakyembe aliyefuatana na makatibu wawili wa Kamati na Mwanasheria wa Bunge, katika kikao hicho, alisema Kamati iligundua taarifa za ushahidi zenye shaka, zikionesha kuwa mashahidi walifanya mzaha wakidhani ni mchezo wa kulindana.

"Kamati imegundua mgongano wa ushahidi usioridhisha na unaozidi kuleta shaka kuhusu dhamira ya baadhi ya mashahidi," alisema Dkt. Mwakyembe, huku akikataa kutaja majina, vyeo na idadi ya waliohojiwa.

Kutokana na shaka juu ya dhamira ya baadhi ya mashahidi, Kamati hiyo iliamua kuwaita tena kuhojiwa mara ya pili ili wathibitishe kauli zao za awali.

Akifafanua shaka iliyojitokeza kwenye taarifa za mashahidi hao, Dkt. Mwakyembe alibainisha, kwamba baadhi yao walitoa taarifa za mdomo zilizotofautiana na taarifa za maandishi.

Aidha, taarifa kutoka katika mahojiano yatakayofanyika Marekani, zinatarajiwa kuingizwa kwenye rasimu ya ripoti ya Kamati au kubadilisha baadhi ya masuala katika Kamati hiyo.

Vilevile, taarifa hizo kutoka Marekani zinatarajiwa kuongeza au kupunguza mgongano na idadi ya mashahidi watakaorudia kuhojiwa, kwa nia ya kuthibitisha kauli zao za awali.

"Watakaothibitika kuipa Kamati ushahhidi wa uongo wakiwa chini ya kiapo kwa sababu wanazozijua wao wenyewe, Kamati italazimika kuchukua hatua za kisheria dhidi yao," alisema Dkt. Mwakyembe.

Sheria itakayotumika dhidi ya watakaobainika kusema uongo ni Sheria ya Kinga, Haki na Madaraka ya Bunge.

Mashahidi waliohojiwa kwa mujibu wa Dkt. Mwakyembe ni maofisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini, wizara nyingine ambazo hazikutajwa, na baadhi ya maofisa kutoka kampuni zilizohusika ikiwamo ya Dowans na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kamati yaongezwa muda
Kutokana na safari hiyo na utata wa ushahidi uliotolewa, Kamati hiyo ilishindwa kuwasilisha ripoti yake ya uchunguzi kwa wakati kama ilivyoagizwa na Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, kukabidhi ripoti hiyo Desemba 15 mwaka huu.

Badala yake, baada ya kupeleka maombi ya kuongezwa muda Desemba 12 mwaka huu na kukubaliwa na Spika, Kamati hiyo iliyopewa muda wa nyongeza wa wiki mbili, itakabidhi ripoti hiyo Desemba 31 mwaka huu.

Wajumbe wa kamati hiyo inayoundwa na Wabunge watano waliokwenda kufanya mahojiano nje ya nchi kuanzia Desemba 10 mwaka huu, ni Bibi Stella Manyanya, Bw. Mohamed Mnyaa na Bw. Lukas Selelii. Wamefuatana na katibu wa Bunge Bw. Anselim Lyatonga Mrema.

Wajumbe hao ambao kwa mujibu wa Dkt. Mwakyembe, waliondoka jana Washington, D.C., kwenda Houston, Texas, na wanatarajiwa kurejea nchini Desemba 15 mwaka huu, siku ambayo walitarajiwa kukabidhi ripoti yao kabla ya kuongezewa muda.

Source: Majira
 
This is what our tax payers want to hear at least. Although I doubt if this panel has any teeth to unfold the truth to the public.
 
Richmond yachemka

SASA ni dhahiri kuwa, kazi ya Kamati ya Bunge ya Kuchunguza mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kati ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya Richmond Development Corporation (RDC) ni nzito na inayotiwa vidole ili kuharibu matokeo.
Katika kukabiliana na hali hiyo, kamati hiyo ya Bunge sasa imeamua kuchukua hatua kadhaa ili kuhakikisha ripoti litakayoitoa inakidhi matarajio ya wananchi na kulinda maslahi ya taifa.

Miongoni mwa hatua ambazo zimechukuliwa na kamati hiyo sasa ni kumuomba Spika wa Bunge, Samuel Sitta kuiongezea muda wa kazi uliokuwa ukimalizika leo, ombi ambalo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe limesharidhiwa na Spika.

Mbali ya hatua hiyo, kamati hiyo ambayo sasa itafanya kazi kwa wiki mbili zaidi hadi Desemba 31, imelazimika kuwaita tena kwa mahojiano ya chini ya kiapo, baadhi ya mashahidi ikiwa ni pamoja na kuwatuma wajumbe wake kadhaa nchini Marekani yaliko makao makuu ya Richmond ili kukusanya taarifa.

Uamuzi huo unakuja siku moja tu baada ya gazeti hili kuripoti kuhusu kuwapo kwa wasiwasi wa baadhi ya mashahidi kutoa ushahidi wa uongo mbele ya Kamati teule ya Bunge, baada ya kupata mafunzo mahususi ya awali (rehearsal), kutoka kwa maofisa wasiojulikana serikalini.

Hata hivyo, Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo ilitajwa katika gazeti hili kuwa maofisa wake kadhaa walihusika kuwaandaa mashahidi kwa lengo lililoonekana kuwa ni kuharibu ushahidi, ilikana kufanya hivyo.

Taarifa ya maandishi ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Vincent Mrisho iliyotolewa jana, pamoja na kukanusha habari ya jana ya gazeti hili, ilikiri kuhusika kwake katika kazi ya kile ilichokielezea kuwa ni kuratibu maofisa wote waliohusika na ambao wangehitajika kutoa ushahidi mbele ya kamati hiyo ya Bunge.

"Kama serikali ilivyoahidi kutoa ushirikiano wake, serikali, kwa kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Nishati na Madini, ilihusika katika kuratibu maofisa wote waliohusika katika mchakato mzima na kuhakikisha kuwa, wale wote wanaohusika na ambao watahitajika mbele ya kamati; kwanza hawasafiri nje ya nchi ili kuhakikisha uwepo wao iwapo watahitajika mbele ya kamati. Pili, kwa kuwa kazi hii ilifanyika miaka miwili iliyopita, wahakikishe kuwa nyaraka zote muhimu kuhusiana na suala hili zinapatikana ili ziweze kutumiwa na kamati endapo zitahitajika ," ilisema taarifa hiyo ya Mrisho.

Mrisho alisema serikali inaamini kuwa maelekezo yaliyotolewa kwa maofisa hao yalifanyika si kwa nia ya kuharibu, bali kuhakikisha kuwa nyaraka zote muhimu kuhusu suala hili zinapatikana ili ziweze kutumiwa na kamati endapo zitahitajika.

Wakati Ofisi ya Waziri Mkuu ikikanusha tuhuma hizo, taarifa ya maandishi ya kamati hiyo iliyosomwa mbele ya wanahabari na Mwenyekiti wake Dk. Mwakyembe jana ilikiri kuwapo kwa wasiwasi wa mashahidi kutoa taarifa za uongo.

Mwakyembe alisema hali ya shaka ambayo kamati imeipata kutoka kwa mashahidi hao ni moja ya mambo yaliyosababisha wafikie uamuzi wa kuomba muda wa ziada ili kuwahoji tena wale ambao wana wasiwasi nao.

Alisema wajumbe wa kamati yake wanahisi kuwepo kwa udanganyifu katika ushahidi waliokusanya, hali inayowalazimu kuwaita tena baadhi ya mashahidi na kuwahoji kwa lengo la kubaini ukweli.

"Kuhusu hili la mashahidi baada ya uchambuzi tumegundua kuwa, baadhi yao ushahidi wao wa mdomo ulitofautiana na ule wa maandishi.

"Hivyo basi, kwa kuwa Spika ameturuhusu kuongeza muda, kamati italazimika kuwaita tena baadhi ya mashahidi kuthibitisha kauli zao.

"Watakaothibitika kuipa kamati ushahidi wa uongo wakiwa chini ya kiapo kwa sababu wanazozijua wenyewe, kamati itawachukulia hatua za kisheria, chini ya Sheria ya Kinga, Haki na Maadili ya Bunge," alisema kwa ukali Dk. Mwakyembe.

Alisema kuwa sheria hiyo inatoa hadi adhabu ya kifungo na iwapo hilo litatokea, itakuwa ni funzo kwa maofisa wa serikali na mashirika ya umma waliotoa ushahidi wao kimzaha wakiamini watalindwa.

Pamoja na suala hilo, Dk. Mwakyembe alithibitisha jana kuwa, kamati hiyo imepeleka wajumbe wake wanne nchini Marekani katika miji ya Houston, Washington na Texas, ili kubaini ukweli kuhusu Kampuni ya Richmond.

Mwenyekiti huyo, aliwataja wajumbe hao kuwa ni Makamu wake, ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum, Injinia Stella Manyanya na Mbunge wa Nzega, Lucas Selelii wote kutoka CCM.

Wengine ni Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Mnyaa (CUF) na Katibu wa kamati hiyo, Anselem Mrema. Timu hiyo iliondoka nchini Desemba 10 na wakiwa Marekani watakusanya taarifa mbalimbali za kampuni hiyo ili kupata ukweli na kujiridhisha kuhusu RDC.

Alisema sababu nyingine ya kwenda Marekani ni kubaini ukweli kuhusu uwezo wa kiutendaji wa kampuni hiyo, kama walivyoagizwa kwenye hadidu za rejea walizopewa na Bunge.

"Wajumbe wa kamati na katibu wapo Marekani tangu Desemba 10. Huko watakutana na maofisa wa ubalozi wetu… wataenda jijini Houston, Washington na Texas, kote huko ni kutaka kujiridhisha kwa sababu tunapokea taarifa muhimu kutoka maeneo tofauti," alisema mwenyekiti huyo na kuongeza kuwa wajumbe hao watarejea nchini kesho.

Alisema taarifa za wajumbe hao kutoka Marekani zitaingizwa kwenye rasimu ya taarifa itakayowasilishwa kwa Spika wa Bunge.

Hali hiyo inakuja wakati taifa likionekana dhahiri kupata hasara kutokana na mradi huo wa Richmond uliogharimu sh bilioni 172.9 kuchukua muda mrefu kukamilika kwake.

Aidha, kuundwa kwa kamati hiyo ni matokeo ya kazi iliyofanywa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara, iliyowasilisha taarifa yake ya mwaka 2006/07 iliyotaka kuchunguzwa kwa mkataba wa Richmond.

Awali, mkataba huo ulichunguzwa na Takuru (sasa Takukuru) ambayo katika taarifa yake ya Mei mwaka huu, ilitangaza kubaini kuwapo kwa uzembe huku ikitamka bayana kushindwa kuthibitisha tuhuma zozote za rushwa.

Taarifa ya Takuru iliibua maneno ndani na nje ya Bunge, hali iliyosababisha suala hilo kubakia moja ya ajenda zilizoonekana kuipotezea imani serikali na baadhi ya viongozi wake waliohusishwa katika mkataba huo.

Mbali ya wabunge na Spika Sitta, kuahidi kuwa suala hilo lingefanyiwa kazi, Kamati ya Uwekezaji na Biashara iliendelea kulifuatilia jambo hilo kabla na baada ya taarifa ya Takuru.

Baada ya vuta nikuvute ya miezi kadhaa, Novemba 13 mwaka huu, kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo (CCM) iliwasilisha ripoti kuhusu utendaji kazi wa Tanesco, ikijumuisha suala la Richmond.

Pamoja na mambo mengine, kamati ya Shellukindo ilipendekeza kuundwa kwa kamati teule ya Bunge kuichunguza Richmond kutokana na kubaini kuwapo kwa maswali mengi magumu katika mkataba huo.

Takribani maswali yote yaliyobainishwa na Kamati ya Shellukindo, yalihusisha utata wa mazingira ya kufikiwa kwa mkataba huo tata kati ya Tanesco na Richmond.

Aidha, Kamati ya Shellukindo ilionyesha wazi wasiwasi wake kuhusu mchakato uliosababisha kutiwa saini kwa mkataba huo na mazingira yake yaliyohojiwa na Mamlaka ya Kudhibiti Manunuzi Serikalini (PPRA).

Suala jingine lililozua utata ni namna Richmond walivyouza mkataba huo wa kuzalisha umeme wa dharura kwa Kampuni ya Dowans, hatua ambayo hata hivyo ilizidisha mlolongo wa kushindwa kuzalisha umeme wa megawati 100.

Kutokana na kuchelewa huko, kamati hiyo ya Shellukindo ilitaka kuundwa kwa kamati ambayo ingechunguza iwapo Dowans waliokuwa wakipaswa kuilipa serikali dola 10,000 kila siku kwa kipindi walichoshindwa kuzalisha umeme walifanya kama mkataba unavyoelekeza.

Sakata hilo la Richmond lilikuja baada ya taifa kukumbwa na ukame mkali uliosababisha vyanzo vya umeme ambavyo ni maji kukauka kwa kipindi kirefu mwaka jana.

Kutokana na hali hiyo, serikali ilichukua hatua za haraka ili kuepusha nchi isikumbwe na janga la kukosa nishati ya umeme kwa kutafuta kampuni za kuzalisha umeme wa dharura.

Shirika la Umeme nchini (Tanesco) liliingia mikataba na wawekezaji binafsi wa nje kuleta mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kwa kutumia gesi asilia na dizeli.

Mbali na Richmond, kampuni nyingine iliyoitikia wito wa serikali kwa haraka ni Aggreko, ambayo ilianza uzalishaji wa umeme wa dharura bila kuchelewa, hivyo kusaidia mapema kuondoa kero na wasiwasi mkubwa uliozikumba sekta za viwanda, biashara na utoaji huduma nchini.
 
Suppose Kamati Teule ya Bunge ikigundua kwamba kulikuwa na harufu ya rushwa kwenye hili sakata la RDC, je, Dr. Hoseah atakuwa tayari kuachia ngazi?
 
Nimependa mahojiano sana MJ, big up. Dr Mwakyembe sound as one of the best professional in Tanzania history. Please someone need to tell me who is this guy.

MJ i want you to be more hard on this guy, your doing good job... But i want you to nell them down hard like Michael Savage and political zoo.
 
As Richmond probe gets hotter: PM's office back in the limelight

-Minister hastens to deny claims of undue influence on witness testimonies


THISDAY REPORTERS
Dar es Salaam

THE Prime Minister's Office is at the centre of new allegations suggesting that key government officials were either coached or intimidated prior to giving testimony before a parliamentary committee investigating the Richmond power generation scandal.

As the allegations of undue PMO influence surfaced, the chairman of the committee probing the highly-controversial 172.9bn/- deal declared yesterday that some witnesses already summoned appeared to have lied outright or otherwise sought to mislead the committee in their testimonies.

According to committee chairman Dr Harrison Mwakyembe, there were ''inconsistencies'' in the testimonies of some key witnesses, who will now have to be re-summoned before the committee to explain various discrepancies.

He also warned that any witness found to be making false statements could be charged with perjury for deliberately lying under oath before a parliamentary committee.

Responding to the allegations of witness coaching and intimidation, the Minister of State in the Prime Minister's Office (Parliamentary Affairs), Dr Batilda Burian, was quick to deny that the PMO has meddled in any way with the work of the parliamentary committee.

''The Prime Minister''s Office has never tried to influence the testimony of any government official who appeared before the parliamentary committee,'' Burian told THISDAY, adding: ''To the contrary, we have fully cooperated with the committee in its investigation.''

The minister further clarified that the PMO had in fact helped to ''prepare'' some of the government officials summoned by the committee by advising them not to travel out of the country during this period, as well as to make all relevant documents readily available.

''That was the first thing our office did. We gathered them (government officials) together and instructed every person who was involved (in the Richmond transaction) not to travel overseas, so that they remain available if called by the committee,'' Dr Burian said.

On the reported allegations that the PMO coached or intimidated some of the witnesses already called by the committee, the minister said: ''These reports are total fabrication...we will issue a formal public statement to clarify the matter.''

Addressing a media conference in the city yesterday, Dr Mwakyembe said the committee had discovered that some of the witnesses (whom he did not name) had given conflicting and inadequate testimonies when summoned.

''The committee is forced to summon some of these witnesses back to appear before us and corroborate their statements,''said the Kyela legislator on a ruling CCM party ticket, adding: ''We will not hesitate to take appropriate action - under the Parliamentary Immunities, Powers and Privileges Act - against those who are found to have deliberately lied under oath.''

Various sections of the local media have recently reported that some key government officials were not giving full cooperation to the parliamentary committee looking into the Richmond debacle.

In a related development, Dr Mwakyembe announced that the Speaker of the National Assembly, Samuel Sitta, has agreed to extend the timeline for the committee to conclude its work for another two weeks, to December 31 instead of December 15 (tomorrow) as earlier scheduled.

Three members of the committee are currently in the United States on a mission to determine the origins of Richmond Development Company LLC, which was registered in Houston, Texas. They are the committee vice-chairperson Ms Stella Manyanya (Special Seats - CCM), Lucas Selelii (Nzega - CCM) and Mohamed Mnyaa (Mkanyageni - CUF), who flew to the US on Monday this week accompanied by an official in the office of the parliament, Anselm Lyatonga Mrema.

As of yesterday, more than 30 officials have appeared before the committee in the course of its inquiry. It is also believed that the Prime Minister, Edward Lowassa, is amongst individuals in line to receive a summons to appear before the committee.

Lowassa was involved in overseeing government efforts to deal with the then-prevailing power shortage problems that led to the awarding of the contract for emergency power generation to the US-registered company last year. The PM is understood to have initially appointed a three-man government task force to work on the problem, including handling the tender process that eventually picked Richmond even after the company had been rejected as incompetent by the state-run Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO).
 
Back
Top Bottom