Baada ya miaka 10: Tujikumbushe mashujaa wa kamati ya Richmond

Baada ya miaka 10: Tujikumbushe mashujaa wa kamati ya Richmond

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Kamati ya Richmond iliundwa na Spika wa bunge la kasi na viwango rip Sitta kuchunguza ufisadi katika mkataba wa Serikali na kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Mashujaa hao ni pamoja na mzee William Shellukindo( Bumbuli
) Dr Harison Mwakyembe( Kyela) mh Herbet Mtangi (Muheza)mh Lucas Selelii (Nzega)mh Stella Manyanya ( viti maalumu)na mh Habib Mnyaa( Mkanyageni).

Ingependeza zaidi kama mashujaa hawa wangepatiwa Nishani ya uzalendo uliotukuka kwa taifa letu ili iwe mfano kwa wabunge wengine na hasa wale waliorithi majimbo yao akiwemo Dr Hamis Kigwangalla, Hussein Bashe, Rajab Adadi na January Makamba. Ni hayo machache ahsante!
 
Tungekuwa China, kuna baadhi ya mashujaa hawa wangenyongwa!.

  1. Taarifa ya Kamati, ililiaminisha Bunge letu tukufu kuwa Richmond ni kampuni hewa!.
  2. Hivyo wakashauri tuuvunje mkataba na hatufanywa chochote.
  3. Serikali ikauvunja mkataba na watu tukashangilia.
  4. Zitto na kamati ya PAC wakashauri au tuitaifishe mitambo au tuinunue.
  5. Wabunge wakagoma kuwa Tanzania hatununi mitambo chakavu.
  6. Maji yakapungua Mtera, kukatokea mgao.
  7. Serikali ikaamua kuiwasha mitambo ya IPTL ambayo ni chakavu mara 10 ya Richmond.
  8. Gharama ya kuwasha IPTL ni mara 20 ya Richmond!.
  9. Huku mitambo ya IPTL ikichafua mazingira mara 100 ya Richmond!
  10. Yote haya yalifanyika ili kujionyesha serikali yetu ni kidume!, kuliko kuwasha Richmond, bora tule hasara na ndia hapa Escrow ilipotengenezwa.
  11. Tukapelekwa mahakamani ICSD, Dowans wakashinda kesi, tukatozwa tozo ya Dowans.
  12. Wanasheria wale wale walioongoza kamati, wakashauri tusilipe na kujiapiza "over my dead body hatulipi!"
  13. Ukweli ni kuwa, japo ni kweli Richmond ilikuwa ni kampuni hewa, lakini mitambo ya Richmond sio mitambo hewa, ni mitambo kweli na Umeme unaofuliwa na mitambo hiyo sio Umeme hewa ni Umeme kweli, hivyo tozo ya Dowans sio kulipia kampuni hewa ya Richmond, bali ni Malipo ya capacity charges halali za mitambo ile na Malipo halali ya Umeme uliolipiwa!.
  14. Tozo hiyo ikasajiliwa Mahakama Kuu ya Tanzania kwa utekelezaji na uhalali wa tozo hiyo kuthibitishwa!.
  15. Serikali yetu ikalipa kwa siri every cent!, Watanzania hatukuambiwa ila Umeme ulipandishwa bei na kila Mtanzania bara alilipia!, Zanzibar waligomea ongezeko hilo!.
  16. Kampuni ya Dowans ikanunuliwa na Simbion, mitambo ile ile, mkataba ule ule, na capacity charges ile ile! na serikali yetu ikaendelea kulipa!. Tulikataa nini, tukalipia nini!?.
  17. Alipokuja Obama, watu wale wale walioshauri tuvunje mkataba, ndio waliokuwa waki dance na Obama kushangilia Simbion!.
  18. Wamelitia hasara taifa, kuvunja mkataba, tumelipishwa tozo, kisha tumerudia matapishi ya mkataba ule ule kwa jina la Simbion!.
  19. Hasara yote hii imefidiwa na Watanzania kupitia ongezeko la bili ya Umeme!.
  20. Ingekuwa ni China, amini usiamini, kuna watu wangenyongwa!.
Paskali
 
Kama ushauri wako utapokelewa kwenye hilo kundi asiwemo mwakiyembe mpaka pale atakopoiweka wazi ripoti yote ya kile walichokibaini katika uchunguzi wao
 
Mashuja wanaosema kwa vinywa vyao kwamba walichosema ni ukweli nusu wangesema yote serekali ingeanguka,wewe unajua kitu kinachoitwa ukweli nusu ni nini?
 
Richmond inazalisha umeme ingawa yawezakuwa kwa jina jingine kama Celtel na airtel.Wakizima mitambo utatukana huko ulipo. Mgao

Mwakyembe alisema eti hawana uwezo hata wa kufunga balbu.

Reasoning capacity ya wengi wetu ni ndogo. Mwanasiasa mwenye mshipa,pumzi,panchi,tone kibabe kwenye kuongea ndio tunahisi ndio mkweli.

Tunawalipa kwa namna mbili.

1) kutuuzia umeme. Wasipozalisha kwenye mwezi husika hatuwalipi

2)Kutuuzia mitambo polepole ili mkataba ukiisha mitambo iwe yetu. Inaitwa capacity charge. Hii hata umeme usipozalishwa tunalipa. Wanasiasa ili kuwapampu wananchi hawanyooshi maelezo hapa.

Pesa yetu inaliwa umeme wanatupatia.

Of course inawezekana jamaa walipata mkataba kimagumashi (jambo ambalo ni typical kwa Afrika) ila kazi wanaiweza.

Kwenye tender nyingi bongo ikichungwa watu wanavyopata tender ni ujanja ujanja. But wengi wao wanaweza
 
Richmond hsijawahi kuzalisha umeme labda useme Dowans!
 
Kamati ya Richmond iliundwa na Spika wa bunge la kasi na viwango rip Sitta kuchunguza ufisadi katika mkataba wa Serikali na kampuni ya kufua umeme ya Richmond.

Mashujaa hao ni pamoja na mzee William Shellukindo( Bumbuli
) Dr Harison Mwakyembe( Kyela) mh Herbet Mtangi (Muheza)mh Lucas Selelii (Nzega)mh Stella Manyanya ( viti maalumu)na mh Habib Mnyaa( Mkanyageni).

Ingependeza zaidi kama mashujaa hawa wangepatiwa Nishani ya uzalendo uliotukuka kwa taifa letu ili iwe mfano kwa wabunge wengine na hasa wale waliorithi majimbo yao akiwemo Dr Hamis Kigwangalla, Hussein Bashe, Rajab Adadi na January Makamba. Ni hayo machache ahsante!
Jiulize pia wako wapi katika list uliyotaja wangapi bado wako hai Kisiasa
 
Mkuu, hiyo ndiyo list ya wale wasaliti walioficha ripoti ili serikali ya majizi isianguke?! Kweli raia wengi wa nchi hii mimba zao zilipatikana kwa madawa ya kishirikina.... maana siyo kwa unafiki na kujitoa ufahamu kwa kiwango hiki!
 
Back
Top Bottom