Walioongopea Kamati Watakiona - Dr. Mwakyembe

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
636
Jafar, ukiona sinia linateremshwa wewe kaa mkao wa kula!

Mwanakijiji,

Usije ukashangaa kwenye sinia unaletewe mawe, sijui utayala huku ulishaanza kutoa mate ya tamaa? Tuna wasanii wengi TZ, kwahiyo lolote linawezekana, tusubiri sinia limetelemshwa chini na kweli ndani yake kuna ubwabwa, vinginevyo tunaweza kufungwa goli na hawa watu.
 

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
636
Asante Mwanakijiji. Mahojiano mafupi, na yaloshiba taarifa muhimu. Kumbe mheshimiwa alikuwa barabarani na anaendesha mwenyewe gari. Anastahili kuwa na dereva, au siyo? Na kupokea simu wakti anaendesha gari ni hatari kwa usalama wake. Mkumbushe ajiangalie usalama wake pia, twamhitaji sana huyu mheshimiwa, ni mtu muhimu sana kwa nchi yetu.

Kithuku,
Mimi nilicheka niliposikia hivyo maana najua Dr. Mwakyembed huwa haendeshi yeye gari lake, ana dereva muda wote, kwanini alisema hivyo? Mimi sijui, labda kwa mara ya kwanza jana alikuwa anaendesha mwenyewe tena Dar.
 

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
609
Naomba kuuliza swali,, Hivi PMO walitoa ushirikiano pia kwa kamati ya Madini? Waliwaandaa pia maofisa na wananchi kutoa ushahidi kwenye kamati ya madini ama ni hii tu ya Richmond? Je, KULIKONI?
 

Mtanzania

JF-Expert Member
May 4, 2006
4,812
636
Naomba kuuliza swali,, Hivi PMO walitoa ushirikiano pia kwa kamati ya Madini? Waliwaandaa pia maofisa na wananchi kutoa ushahidi kwenye kamati ya madini ama ni hii tu ya Richmond? Je, KULIKONI?

Mkuu Halisi,

Lowassa na genge lake wanatuona Watanzania wote wajinga, wanaona wanaweza kufanya madudu yoyote wanayotaka bila kuumbuliwa. Lakini hapa duniani kila jambo lina mwisho, swali kwasasa ni je huu ndio mwanzo wa mwisho wa Lowassa? Au ndio usanii ule ule wa kila siku?
 

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
335
Naomba kuuliza swali,, Hivi PMO walitoa ushirikiano pia kwa kamati ya Madini? Waliwaandaa pia maofisa na wananchi kutoa ushahidi kwenye kamati ya madini ama ni hii tu ya Richmond? Je, KULIKONI?

Watoto wangu watundu sana, ikitokea mmoja kafanya jambo, nitajua tu maana siku moja nilipofika nikasema, "Nani ame...." hara haraka yule mdogo akasema, "baba sio mimi", mkubwa akasema, "hapana ni....(mdogo) ndio amevunja kioo cha gari alikua akirusha mawe kupiga ndege alikua juu ya mti", mdogo akasema sijavunja ni jiwe lilidondoka bahati mbaya kutoka juu ya mti"... Hapa nasema kwamba, hii ni hadithi ya kitoto, ndio maana kila siku inakua kazi ya kusema, "si mimi" mara "bosi wetu hahusiki", "mara amezuia kamati ya bunge kuwasilisha" (kabla ya pumzi kujaa na kuundwa kamati)mara, "Mvua zimeanza kunyesha hivyo hakuna haja ya kujadili" Mara tena, "PCCB wametoa taarifa hakuna haja ya magazeti kujadili" alimradi ni mambo kwenda mbele, hapo hatuhitaji FBI waje kuchunguza matokeo hayoooooooooooooooooooooooooooooooooooooo.... Jamaa anahusika moja kwa moja, hata kama hakuna ushahidi wa maandishi... wa mazingira unahusika moja kwa moja.... Ningekua mimi Mwakyembe na nina nia ya kumsaidia mkuu huyu, ningesema, "Kwa kuwa PM ni mwanasiasa na ni kutoka chama tawala, na kwa kuwa serikali ni lazima isiwe na doa na kwa kuwa ushahidi uliopo ni wa mazingira zaidi tena ya kisiasa, ambao bosi huyu alifanya maamuzi ya kisiasa, na kwa kuwa uwajibikaji wa kisiasa unatokana na maamuzi ya kisiasa, KWA HIYO, wanasiasa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine akiwamo Lowassa, Dk. Msabaha na Rostam Aziz, wanapaswa kuwajibika kisiasa mara moja kwa Bunge kutoa AZIMIO la kuwataka kufanya hivyo ili KULINDA HADHI ZAO KISIASA."
 

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
335
Mkuu Halisi,

Lowassa na genge lake wanatuona Watanzania wote wajinga, wanaona wanaweza kufanya madudu yoyote wanayotaka bila kuumbuliwa. Lakini hapa duniani kila jambo lina mwisho, swali kwasasa ni je huu ndio mwanzo wa mwisho wa Lowassa? Au ndio usanii ule ule wa kila siku?

Mtanzania, usemayo hakika kabisa.... dunia ya sasa ina mambo mengi sana... mimi nadhani kama Lowassa akipona kipindi hichi, basi nitamtafta kumpa mkono kwa kauli, "mheshimiwa nadhani wewe unastahili kuwa Rais milele, maana pamoja na madudu yote haya bado unaendelea kutesa, basi una nguvu kuliko hata Rais na kuliko hata wananchi ambao wamekuchoka. kwa hiyo naona nianza kufanya kazi ya kukutetea kwa nguvu zote ili ufanikishe azma yako ya kutawala nchi hii." Najua nitaonekana MWENDAWAZIMU na wanaonijua lakini "Mkono ukishindwa kuukata UBUSU hata kama una kinyesi."
 

Pedro

Senior Member
Nov 17, 2006
114
3
Kamati ya Richmond 'yahamia' Marekani


Wajumbe wa kamati hiyo inayoundwa na Wabunge watano waliokwenda kufanya mahojiano nje ya nchi kuanzia Desemba 10 mwaka huu, ni Bibi Stella Manyanya, Bw. Mohamed Mnyaa na Bw. Lukas Selelii. Wamefuatana na katibu wa Bunge Bw. Anselim Lyatonga Mrema.

Wajumbe hao ambao kwa mujibu wa Dkt. Mwakyembe, waliondoka jana Washington, D.C., kwenda Houston, Texas, na wanatarajiwa kurejea nchini Desemba 15 mwaka huu, siku ambayo walitarajiwa kukabidhi ripoti yao kabla ya kuongezewa muda.

Source: Majira

Jamani samahani kutoka kwenye topic kidogo, ni curiosity tu ndio inanisumbua, huyo katibu wa Bunge ana undugu na Mzee wetu wa kiraracha?
 

Katibu Tarafa

JF-Expert Member
Feb 16, 2007
986
45
Hapa tumepigwa bao la kisigino,kumbukeni maneno haya"ninawajua wala rushwa nawapa muda wajirekebishe"alisema JK sasa mwakyembe anasema tutawaita ili wabadili kauli zao,baada ya hapo watapewa kinga ya kutokushitakiwa kwa kutoa ushirikiano na tume.mchezo umekwisha.
 

Nurujamii

JF-Expert Member
Jun 14, 2007
414
11
Hivi ripoti ya hii kamati atakabidhiwa spika au? je itawekwa hadharani kwa wabunge wote? Nina wasiwasi isije kuwa kama ile ya BoT. Sijui imekwama wapi masikini weee! Nchi hii!
 

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
335
Re:
Keil
View Post

Kamati ya Richmond 'yahamia' Marekani


Wajumbe wa kamati hiyo inayoundwa na Wabunge watano waliokwenda kufanya mahojiano nje ya nchi kuanzia Desemba 10 mwaka huu, ni Bibi Stella Manyanya, Bw. Mohamed Mnyaa na Bw. Lukas Selelii. Wamefuatana na katibu wa Bunge Bw. Anselim Lyatonga Mrema.

Wajumbe hao ambao kwa mujibu wa Dkt. Mwakyembe, waliondoka jana Washington, D.C., kwenda Houston, Texas, na wanatarajiwa kurejea nchini Desemba 15 mwaka huu, siku ambayo walitarajiwa kukabidhi ripoti yao kabla ya kuongezewa muda.

Source: Majira


Jamani samahani kutoka kwenye topic kidogo, ni curiosity tu ndio inanisumbua, huyo katibu wa Bunge ana undugu na Mzee wetu wa kiraracha?
Reply With Quote

Ni kweli, Anselm Mrema na Augustine Mrema ni ndugu
 

JAYJAY

JF-Expert Member
Oct 31, 2008
5,990
5,074
kutokana na kauli za viongozi mbalimbali nalazimika kusema hivi kuwa kamati haikufanya kazi yake sawasawa.kwamba kuna taarifa ambazo naamini haikuziweka wazi ambayo ingeonesha nani hasa ni mmiliki wa ukweli Richmond na wahusika wote kutajwa na sio baadhi kuachwa kitu ambacho kinajenga chuki kwa wale waliotajwa.mashaka yangu ni kuwa walifanya hayo kwa kulinda maslahi ya chama au/na serikali.mhalifu siku zote huona haki imetendeka kama alioshirikiana nao, nao wanashughulikiwa jambo ambalo naamin kwenye suala hili halikufanyika, ndio maana leo hii sitashangaa kukiwa na jitihada za baadhi ya wahusika kujisafisha kwa sababu wanaamini hukumu haikuwa ya haki.kwao ni ama wahusika wote watajwe ili wasijione wameonewa au wote wasafishwe warudi kwenye mchakato na ndoto zao pia.
kwa nini pia nasema hivi, kumekuwepo na kauli kupinga malipo ya dowans kutoka kwa mheshimiwa Sitta ambaye anasema kuna mtu anamiliki makampuni mengi(karibia 17) lakini kwenye documents za umiliki jina nale halipo.hii inamaanisha kuwa mtu huyo huyo ndio ama mmiliki wa Richmond au Dowans kwa pamoja, kwa sababu kauli hii imetajwa kuhusiana na suala hilo.je, yeye alipata wapi taarifa hizi, ni wazi wahusika wa kamati walimpatia taarifa hizi hasa ukizingatia ukweli kwamba yeye ndie aliyekuwa spika wa bunge wakati huo kwa hiyo anachokisema ni ukweli,(sidhani kuwa wahusika wa kamati watakuwa walimdanganya) ingawa officially kamati hiyo haikumtaja mtu huyo na hapo ndipo udhaifu au makosa ambayo naamini yanatugharimu sasa yalikoanzia. makosa ya kamati kuficha mambo ili kumlinda/kuwalinda mtu/watu fulani ndio yamezaa yote haya.
 

Click_and_go

JF-Expert Member
Nov 21, 2010
451
5
....speak from the roots, not the branches!!!!,,,,,JE, MAPENDEKEZO YA ILE KAMATI YA DR. MWAKYEMBE YALIFANYIWA KAZI??????
 

mwakabana

Member
Dec 15, 2010
31
7
ile issue bora wangeendesha tu akina dr. slaa coz wat i see by that time mwakyembe was very commited ila sasa baadaye aliangalia maslahi ya chama zaidi and kwa upande wa kamati unaona walivyokuja kunywea so it goes as we see now hata mwakyembe wa 2008 sio huyu wa sasa ingekuwa sio waziri i think hiki kipindi angeuza sana magazeti ila this time is under conditions hata kama anaongea not that much.
 

Baiskeli

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
336
61
kama kuna mwanajf anayejua wajumbe wote waliounda hiyo kamati awabandike humu ili tuweze kuwatathmini maana namsikia mwakiyembe tu, nivizuri tuone na hao wengine michango yao, wako kimya mno!
 

mtu chake

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
27,816
57,612
1.lucas seleli...

2.habib mnyaa

3.injinia stela manyanya

4.........

5.........
 

Kamakabuzi

JF-Expert Member
Dec 3, 2007
2,687
1,166
....speak from the roots, not the branches!!!!,,,,,JE, MAPENDEKEZO YA ILE KAMATI YA DR. MWAKYEMBE YALIFANYIWA KAZI??????
Mapendekezo 18 ya Kamati ya Mwakyembe 1. Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2004 (Public Procurement Act, 2004) ipitiwe upya ili kuiboresha kwa kuipa Mamlaka nguvu zaidi za udhibiti na uwezo wa kuchukua hatua pale sheria na kanuni zinapokiukwa, badala ya kutoa ushauri tu kama ilivyo sasa.
 2. Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma isiwajibike Wizara ya Fedha ambayo nayo ni taasisi ya ununuzi (procurement entity) badala yake iwe chombo huru kinachowajibika Ofisi ya Rais na taarifa zake kuwasilishwa bungeni.
 3. Mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC na sasa Dowans Holdings S.A, kama ilivyo mikataba kati ya TANESCO na IPTL, SONGAS, AGGREKO na Alstom Power Rentals inatoa unafuu usiostahili kwa makampuni hayo ya umeme na kuiumiza TANESCO na hatimaye watumiaji na walipa kodi kimapato, k.m mikataba hiyo kuwa na vipengele vya kuibana TANESCO kuyalipia makampuni hayo kodi zinazohusika na uendeshaji (operations), matengenezo/marekebisho ya mara kwa mara ya mitambo (maintenance) gharama za bima, ada za mawakili na washauri elekezi (consultants) gharama za mafuta na gesi ya kuendeshea mitambo, gharama za ukodishaji mitambo (capacity charges) ambazo TANESCO hulipa kila mwezi si chini ya wastani wa shilingi bilioni 2 kwa kila kampuni, izalishe au isizalishe umeme.
 4. Serikali ipitie upya mikataba yote kati ya Tanesco na wazalishaji wa umeme binafsi mapema iwezekanavyo kama ambavyo mikataba ya madini inavyopitiwa upya sasa kwani bila kufanya hivyo, mzigo mkubwa wa gharama za umeme utawaelemea wananchi na kushindwa kufikia azma ya serikali ya maisha bora kwa kila Mtanzania.
 5. Kwa kuwa mkataba kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC ulikuwa wa uzalishaji umeme wa dharura kipindi ambacho nchi ilikuwa katika hali ngumu ya ukame uliokausha mabwawa yote ya kuzalishia umeme, serikali itathmini upya uhalali wa kuwepo na kuendelea kuwepo na mkataba huo kutokana na udanganyifu bayana uliofanywa na Richmond Development Company LLC kuhusu uwezo wake kifedha, kiufundi na uzoefu wake katika masuala ya uzalishaji umeme; usajili na uwepo wake kisheria kama kampuni halali yenye ukomo wa hisa nchini Marekani na Tanzania; uhusiano wake kisheria na kampuni kubwa ya kimataifa ya Pratt & Whitney.
 6. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye katika majadiliano yake na Kamati Teule alionyesha kutokuelewa kabisa kilichokuwa kinatendeka na wasaidizi wake, na mwakilishi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Wakili wa Serikali, Donald Chidowu, ambaye ushiriki wake katika GNT haukuwa na tija yeyote, wawajibishwe na mamlaka ya juu ya nchi kwa kuchangia kuiingiza nchi katika mkataba wa aibu.
 7. Katika mikataba yote na makampuni ya nje, serikali ihakikishe kuwa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inatumika kikamilifu katika kupata taarifa kamili za kampuni hizo, kama vile wanahisa, mitaji na anwani. Aidha, ofisi zetu za ubalozi zilizo sehemu mbalimbali duniani zihusishwe katika majadiliano na makampuni yanayotoka nje ya nchi kwa lengo la kupata taarifa zao za msingi na kuboresha nguvu ya hoja ya serikali.
 8. Wajumbe wote wa Kamati ya Serikali ya Mashauriano katika suala la Richmond ambao ni maafisa waandamizi wa serikali wawajibishwe mara moja kwa kushindwa kutumia elimu na ujuzi wao kulinda maslahi ya taifa.
 9. Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi aliyeshabikia sana uhaulishaji huo, awajibishwe.
 10. Yafanyike mabadiliko ya haraka ya uongozi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru ambayo ilitoa ripoti mbovu ya kuisafisha Richmond.
 11. Wakati umefika sasa kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma ya mwaka 1995 (Public Leadership Code of Ethics Act) ifanyiwe marekebisho makubwa ili kudhibiti utaratibu unaoonekana wa kawaida sasa wa viongozi waandamizi wenye dhamana kisiasa kuendelea na biashara zao wakiwa madarakani, hivyo kuwaweka kwenye mtihani mkubwa wa mgongano wa kimaslahi katika maamuzi yao. Tufike mahali ambapo sheria iwalazimu kuchagua kati ya utumishi wa umma au biashara binafsi, viongozi waandamizi wenye dhamana kisiasa (mawaziri na kuendelea) kuendelea na biashara zao wakiwa madarakani hivyo kuwaweka kwenye mtihani mgumu wa mgongano wa kimaslahi.
 12. Serikali iondokane kabisa na utaratibu wa kutumia mawakala katika ununuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme nchini na kuhakikisha kuwa wizara husika ina taarifa za bei halisi ya mitambo kila wakati ili kujiepusha na mchezo wa kawaida wa mawakala kupandisha bei mara mbili au zaidi ya bei halisi.
 13. Utaratibu tuliourithi kutoka kwa wakoloni na kuuzoea wa kuiona mikataba ya kibiashara kuwa ni siri hata kwa walipa kodi wenyewe na kuwa uwanja wa pekee wa watendaji, umepitwa na wakati.
 14. Waziri wa Nishati na Madini wa wakati huo, Ibrahim Msabaha na Katibu Mkuu, Arthur Mwakapugi wachukuliwe hatua kali za kinidhamu kwa kuliingiza taifa kwa makusudi kwenye mkataba na kampuni ya mfukoni ambao umesababisha hasara kubwa kwa nchi.
 15. Kamishna wa Nishati, Bashir Mrindoko achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kushindwa kumshauri Katibu Mkuu mpya wa wizara kuhusu udhaifu wa Richmond Development Company LLC ambao ulijulikana dhahiri na wizara toka mwaka 2004 kwenye mkataba wa bomba la mafuta.
 16. Utaratibu wa kuteua wakurugenzi na makamishna katika wizara kuwa wajumbe wa bodi za wakurugenzi za mashirika yaliyo chini ya wizara, unazua mgongano wa kimaslahi, kudhoofisha usimamizi na uwajibikaji, hivyo serikali iupige marufuku mara moja.
 17. Waziri Mkuu Edward Lowassa ambaye ndiye mwenye madaraka ya juu ya udhibiti, usimamiaji, utekelezaji wa siku hadi siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano na ndiye kiongozi wa shughuli za serikali bungeni apime uzito wa matokeo ya uchunguzi huu na wajibu wake kikatiba ndani na nje ya Bunge.
 18. Bunge ambalo linathibitisha uteuzi wa Waziri Mkuu kwa mujibu wa Ibara ya 51, liangalie matokeo ya uchunguzi huu kama hayajaathiri hadhi na uzito wake ndani ya Bunge.
 

Chimunguru

JF-Expert Member
May 3, 2009
10,678
4,319
nadhani selelii kasahaulika akitafutwa huyu jamaa n hivi walimtosa ubunge anaweza akafunguka mpaka tukashangaa. nakumbuka kuna siku ilikuwa bungeni au sijuini wapi mwakyembe alipandwa na hasira na akasema au tuseme mambo yote hadharani nahisi vitu flani muhimu walificha sasa vinaweza kuwarudia.
be
 

ifolako

Member
Nov 8, 2010
98
0
ile issue bora wangeendesha tu akina dr. slaa coz wat i see by that time mwakyembe was very commited ila sasa baadaye aliangalia maslahi ya chama zaidi and kwa upande wa kamati unaona walivyokuja kunywea so it goes as we see now hata mwakyembe wa 2008 sio huyu wa sasa ingekuwa sio waziri i think hiki kipindi angeuza sana magazeti ila this time is under conditions hata kama anaongea not that much.

Mwakabana=Mwakyembe dugu moja
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom