Hii Dunia hatuishi na watu tu Wengine ni mapepo.Ndiyo maana tunaambiwa unapotaka kuoa mshirikishe Mungu .Wapo watu wameolewa na mapepo na mashetani BIla kujua Kwa sababu ya tamaa za ngono .Hawa mapepo Kwa macho ya kawaida wanaonekana ni watu ila Kwa macho ya rohoni sio watu ni mapepo yaliyovaa sura ya mwanadamu .
Kama wanaweza kumbadilisha mtu awe ngombe au mbuzi alafu anachinjwa watu wanakula nyama hiyo wakidhani wanakula nyama ya ngombe kumbe ni nyama ya mtu watashindwaje kujibadilisha kuonekana kama binadamu halisia.
Ndyo maana mnaambiwa msali na kumwomba Mungu kabla ya kuoa wengi wanadhani kuoa ni suala dogo dogo.
Na malengo ya huyo mwanamke shetani ni kukunyima penzi makusudi kabisa Ili mradi akusababishe uishi katika dhambi ya uzinzi .Ili utakapokufa unapokuwa katika hali hiyo Unakuwa Moja Kwa Moja wewe ni motoni alafu yeye anakuwa anakuwa amefanikisha mission yake ya kukupeleka motoni.
Mbaya zaidi unapokufa ndipo unapokuwa unagundua kumbe nilikuwa sijaoa mtu Bali shetani .Na huko motoni Kwa sababu huyo ni Pepo ana mamlaka zaidi Yako na anakutesa Tena huko huko motoni .Hii Dunia sio ya kawaida.