Walioishi kabla ya Yesu na Muhammad wamepotea ?

Walioishi kabla ya Yesu na Muhammad wamepotea ?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
63,283
Reaction score
106,740
Kama hawajapotea na wataenda mbinguni kulikuwa na haja gani ya Yesu Kristo kuja kufa kwa ajili ya dhambi za binadamu na Muhammad kuja na Quran yake ?

Maisha si yangeweza kuendelea tu kama kawaida bila wao?!
 
Hapana mkuu!

Kwa upande wa ukristo!
YESU alikuwa anawakilishwa na dhabihu za wanyama, ambapo mtu akitenda dhambi alitakiwa kutoa kafara ya mnyama!

kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti, kwa hiyo mnyama ndiye alichukua hatia ya dhambi na kufa!!

Baada ya YESU kuja ndiye alilipa deni la dhambi, kwa hiyo kila mwanadamu anaye mwamini, atasamehewe kupitia kumwamini YESU!
 
Kabla ya wao kulikua na manabii kwa upande wa uislam Muhammad ndo wa mwisho hakutakuja Mtume mwengine ila kwa upande mwengine wapo hao akina mwamposa na manabii wengine.
 
Hao dhambi zao zimesamehewa pale msalabani.
Kwa nini hakuja afe msalabani siku ya mwisho wa dunia kabisa ili watu walioishi duniani wasamehewe kwa pamoja bila kuhitajika kumuamini? Maana wale walioishi kabla yake wao wataingia mbinguni kwa mtelezo/kitonga sana kuliko walioishi baada yake waliolazimika kumuamini.
 
Hapana mkuu!

Kwa upande wa ukristo!
YESU alikuwa anawakilishwa na dhabihu za wanyama, ambapo mtu akitenda dhambi alitakiwa kutoa kafara ya mnyama!

kwa sababu mshahara wa dhambi ni mauti, kwa hiyo mnyama ndiye alichukua hatia ya dhambi na kufa!!

Baada ya YESU kuja ndiye alilipa deni la dhambi, kwa hiyo kila mwanadamu anaye mwamini, atasamehewe kupitia kumwamini YESU!
Kwa nini hakuja afe siku za mwisho wa dunia kabisa ili alipe deni la dhambi la watu wote duniani na waokolewe bila kuhitajika kumuamini kama hao wengine ?
 
Amen Man Of God
Yesu Yu Karibu Kurudi Kulinyakua Kanisa
Kila Jicho Litamwona.....
 
Kabla ya wao kulikua na manabii kwa upande wa uislam Muhammad ndo wa mwisho hakutakuja Mtume mwengine ila kwa upande mwengine wapo hao akina mwamposa na manabii wengine.
Manabii waliokuwepo kabla habari zao ziliishia mashariki ya kati tu tena sehemu ndogo sana. Hakukuwa na TV, radio, simu na magazeti ya kufikia watu wote mpaka huku Sub-Sahara Africa, China, India, Ulaya, Marekani Kusini na Kaskazini.
 
Kama hawajapotea na wataenda mbinguni kulikuwa na haja gani ya Yesu Kristo kuja kufa kwa ajili ya dhambi za binadamu na Muhammad kuja na Quran yake ?

Maisha si yangeweza kuendelea tu kama kawaida bila wao?!

Miujiza inatendeka kuthibitisha jambo fulani. Na hii ni kwa pande zote hata kwa upande wa pili.

Kuna mtiririko wa matukio/visa vingi. Ujio wa Yesu na mtume ni miongoni. Kila tukio na zama zake.

Kwa mfano watu wa mwanzo kabisa walihishi kwa agizo la Mungu kwa Adam na Eva. Kadri nyakati zilizosogea uasi ukataradadi. Ikaja sheria ya Mussa. Sheria ya Mussa ilitilia mkazo kulingana na mambo ambayo wanadamu waliibua na hayakumpendeza Mungu ila ilikuwa kali.

Kuna matukio mengine pia kama sodoma na Gomorrah, gharika la Nuh. Ujio wa Yesu na Mtume Muhammad ulilenga kukomboa kizazi cha wakati huo na sio kilichokwishapita. Kukifanya kizazi cha wakati huo na baadaye kuenenda kwenye misingi inayotakiwa tofauti na watangulizi.
 
Kwa nini hakuja siku za mwisho wa dunia kabisa ili alipe deni la dhambi la watu wote duniani na waokolewe bila kuhitajika kumuamini ?
Asante!!! baada ya dhambi kuingia shetani aliwafanya wanadamu waende against na MUNGU.

Hivyo MUNGU akatafuta njia ya kumrudisha mwanadamu katika uhusiano na yeye.

Kwa hiyo ni jukumu la mwanadamu kufanya uamuzi binafsi kumchagua MUNGU na sio lazima kwa neema ya YESU.

Kama angefanya hivyo maana yake angewalazimisha wote wampende kwa lazima na sio kwa hiari.
 
Manabi waliokuwepo kabla habari zao ziliishia mashariki ya kati tu tena sehemu ndogo sana. Hakukuwa na TV, radio, simu na magazeti ya kufikia watu wote mpaka huku Sub-Sahara Africa, China, India, Ulaya, Marekani Kusini na Kaskazini.
Acha zako kule ndipo ustaarabu umeanzia , wazungu hawana historia ni watoto wa juzi ..Ukiinza hata uingereza ni ya juzi hapa tena baada ya kuanzishwa kwa Aglican , kule USA walikuwa jamii kama red indian .

Katika uislamu , unatumbua kipind cha ujahili(watu kabla ya kustaarabik) , uislamu unaenda mbali kwa kuonyesha watu walifikiwa na ujumbe kwa wale ambao hakuwafikiwa basi hawana kosa . Dini ni ustaarbu ndiyo maana kulikuwa na muendelezo wa manabii kuja kuwajuza watu ...America , Europe za juzi tu kihistoria kama mwafrika, wengi wamepata nguvu kipind cha utumwa na mapinduzi ya viwanda .​
 
Amen Man Of God
Yesu Yu Karibu Kurudi Kulinyakua Kanisa
Kila Jicho Litamwona.....
Itakuwa vigumu kila hicho kumuona kwa sababu katika kila wakati nusu ya dunia ni mchana na nusu ya dunia ni usiku watu wamelala.
 
Acha zako kule ndipo ustaarabu umeanzia , wazungu hawana historia ni watoto wa juzi ..Ukiinza hata uingereza ni ya juzi hapa tena baada ya kuanzishwa kwa Aglican , kule USA walikuwa jamii kama red indian .

Katika uislamu , unatumbua kipind cha ujahili(watu kabla ya kustaarabik) , uislamu unaenda mbali kwa kuonyesha watu walifikiwa na ujumbe kwa wale ambao hakuwafikiwa basi hawana kosa . Dini ni ustaarbu ndiyo maana kulikuwa na muendelezo wa manabii kuja kuwajuza watu ...America , Europe za juzi tu kihistoria kama mwafrika, wengi wamepata nguvu kipind cha utumwa na mapinduzi ya viwanda .​
Utumwa ulioenezwa na dini za Mashariki ya kati sio ustaarabu,
Vita vilivyotokana na dini za Mashariki ya kati sio ustaarabu.
Ubaguzi uliotokana na dini za Mashariki ya kati sio ustaarabu.
 
Manabii waliokuwepo kabla habari zao ziliishia mashariki ya kati tu tena sehemu ndogo sana. Hakukuwa na TV, radio, simu na magazeti ya kufikia watu wote mpaka huku Sub-Sahara Africa, China, India, Ulaya, Marekani Kusini na Kaskazini.
Kuna manabii walishushwa kw ajili ya kulingania sehem ndogo tu na sio kwa ulimwengu wote sio ni Mtume Muhammad pekee ndo alitumwa kulingania kwa ajili ya ulimwengu mzima.
 
Kuna manabii walishushwa kw ajili ya kulingania sehem ndogo tu na sio kwa ulimwengu wote sio ni Mtume Muhammad pekee ndo alitumwa kulingania kwa ajili ya ulimwengu mzima.
Nipe jina la nabii mmoja aliyetumwa kulingania sehemu yoyote ya Africa Mashariki kabla ya Muhammad na Yesu kuja duniani.
 
Mwenyezi mungu ni muadilifu. Kwenye Quran ameahidi hatomuadhibu mtu ambaye kaishi hadi kufa hajawahi kusikia habari za mitume .Qur-an 17:15 9"Wala Sisi hatukuwa wenye kuadhibu mpaka tuwapelekee Mtume." Hapo kundi la msamaha wanaingia vichaa, watoto na watu waloishi bila kusikia habari za Muumba.
 
Itakuwa vigumu kila hicho kumuona kwa sababu katika kila wakati nusu ya dunia ni mchana na nusu ya dunia ni usiku watu wamelala.
Kwa logic ya elimu ya kidunia, upo sahihi. Lakini kwa Mungu hakuna kinachoshindikana. Wanafunzi wa Yesu siku moja walimshangaa wakasema "huyu ni nani hata pepo zinamtii?", ilikuwa wakati wa dhoruba baharini huku Yesu amelala.

Pia, siku ya kufa msalabani, Biblia inanukuu kuwa JUA LILIACHA KUTOA NURU YAKE, KUKAWA GIZA KUU JUU YA NCHI wakati ilikuwa mchana.

Yoshua anarekodiwa kuombea jua lisimame na mwezi usimame (yaani masaa yasimame (au Dunia isijizungushe)).

Mfalme Hezekiah aliambiwa aombee ishara. Achague Kati ya jua kurudishwa nyuma masaa kumi, au kusogezwa mbele masaa kumi, aliomba lirudishwe nyuma masaa kumi.

Najua swali linaweza kuwa KUNA UTHIBITISHO GANI kuwa hayo yote yalitojea?

Hapo nakuachia msomaji na mleta mada. Mimi nilikuwa najaribu kumwonyesha ile kauli ya Mungu anayosema MAWAZO YANGU SI MAWAZO YENU, NA NJIA ZANGU SI NJIA ZENU.
 
Utumwa ulioenezwa na dini za Mashariki ya kati sio ustaarabu,
Vita vilivyotokana na dini za Mashariki ya kati sio ustaarabu.
Ubaguzi uliotokana na dini za Mashariki ya kati sio ustaarabu.
Dini ipi imeeneza utumwa ? Hakuna dini ambayo imeenzea utumwa bali jamii ilikuwa katika enzi za utumwa , mitume ilikuwa dhalili . Nitajie mtume mmoja aliyekuwa ana miliki watumwa ?

Hakuna vita ya dini hata siku , vita ipo katika watu kujilinda , dini hailindwi kwa mujibu wa kiislamu ila watu kama wanasimamia haki wanaweza kupigana dhidi ya dhulma mpaka hao madhulmat waijue haki ..Dini hailindwi hata siku moja wlaa haipiganiwi .

Ubaguzi ni stori za miaka na miaka , ubaguzi ni kinyume cha dini .
 
Back
Top Bottom