Kama hawajapotea na wataenda mbinguni kulikuwa na haja gani ya Yesu Kristo kuja kufa kwa ajili ya dhambi za binadamu na Muhammad kuja na Quran yake ?
Maisha si yangeweza kuendelea tu kama kawaida bila wao?!
Siku ya hukumu kutakuwa na makundi ya aina 5
1) Waislam
Watapiwa madhambi Yao na mema Yao katika mizani mema yakiwa mengi utaenda peponi na mabaya yakiwa mengi utaenda motoni
ila hautakaa motoni milele utatumikia adhabu Kwa muda wa madhambi yako Kisha utapelekwa peponi
2) Makafiri
Hawa hawatakuwa na mizani ya kupima mema na mabaya Kwa sababu walipinga uwepo wa Mungu Mmoja au walipinga kuwa hakuna Mungu kabisa hawa watakaa motoni Jahanam milele
3) Machizi
Hawa wataenda peponi haijalishi wametoka katika familia gani
4) Watoto
Walikufa wakiwa bado watoto Yani kabla hawajabalehe hawa wataingia peponi haijalishi wametoka katika familia gani
5) Wasiojua kitu ( wajinga)
Hawa wataingia peponi maana kutokumjua Mungu sio kosa lao
Na Mungu amesema hatomuadhibu mtu ambaye hakumpelekea mtume
Quran 17:15
- Anaye ongoka basi anaongoka kwa ajili ya nafsi yake. Na anaye potea basi anapotea kwa khasara yake mwenyewe. Wala habebi mbebaji mzigo wa mwengine. Wala Sisi hatuadhibu mpaka tumpeleke Mtume.
Je! Vipi kama Mungu angewaacha binadamu waishi tu bila ya kuwaletea ufunuo?
1) Binadamu wangeishi kama wanyama watoto wangefanya mapenzi na wazazi wao na wazazi wangefanya mapenzi na watoto zao
2) Kungekuwa hakuna amani
Kuna watu hapa Duniani wanaweza kumfanyia chochote binadamu mwenzake isipokuwa anamuogopa Mungu tu