Walioingiza mabomu Arusha wakamatwa!

Walioingiza mabomu Arusha wakamatwa!

Akili ndogo inajaribu kulazimisha kuishawishi na kuiongoza akili kubwa.

Polisi jipangeni mpige rigwaride upya, mpaka hapo hamjaweza kuteka hata moyo mmoja.

Kwetu Said Mwema na Jeshi lako zima la Polisi ndiyo watuhumiwa namba moja. Mmejaa damu zisizo na hatia mpaka maklioni.
 
>Mkiambiwa jeshi la polisi linaingiliwa na wanasiasa muamini bana!
 
Taarifa kutoka jijini Arusha zinasema kuwa jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu walioingiza mabomu yaliolipuliwa ktk kanisa catholic olasiti na kwenye mkutano wa chadema ambapo watu kadhaa wakifariki na wengine kujeruhiwa vibaya Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Arusha bwana Magesa Mulongo.

Mulongo amesema wako kwenye mahojiano ya mwisho na kila kitu kitakuwa hatharani muda si mrefu...


Breaking news (E.A.RADIO)

Mtuhumiwa mmoja yuko Marekani anaitwa Mwigulu Nchemba au alistuliwa akimbilie huko mwezi mzima hadi upepo upite???
 
Last edited by a moderator:
Kama wako kwenye mahojiano ya mwisho kulikuwa hakuna haja ya . kutumbia. Angesubiri wamalize mazungumzo yao then atuambie kitu kamili kuliko kuleta saisa kwenye upelelezi. Watu wengine bana...

Unaambiwa ili ujiandae kuwadhamini waumini wenzio na wanachama wako!!!!
 
Kwakua wameona vyama vya upinzani wameungana sasa kitakacho kuja ni kusema chadema ili umoja wao ukwame kwa jina la yesu washindwe
 
Kama wewe ni mwanaume halafu unazidanganya sehemu zako za siri kuwa kuwa umetembea na mwanamke fulani ni sawa na kujidanganya mwenyewe,Sidhani kama mwizi anaweza kumakamata mwizi mwenzake,wanajidanganya wenyewe,sisi walalahoi wa Tz tulishawang'amua zamani sana.
 
Unamaanisha nini hapo!?
Habari ni nzito lakini haina details zinazotarajiwa na watu wengi..., na tena habari yenyewe imevuta watu wengi bila kukidhi haja ya wenye kujua UNYAMA HUU UTAISHA LINI... Tunajiulize mabomu yalipigwa na CCM au polisi?.. Kwakuwa magaidi wasingeweza kupiga mkutano wa chama cha upinzani wakaacha kinachotawala.
 
Nadhani wanatakaa tu waturudishe kwenye ile sinema ya video ya CDM. Nayo hiyo ni karata bado kwa CCM.

Chako hicho kinatwa kiherehere, kwani ukisubiri ukajua atakuja nalo, ungevunjika guu, tuwaache polisi wafanye kazi yao, sisi tutakuwa na usemi tukishapata habaro kamili. au kuna unalolijua na unataka kutupotezea dira. ama umetumwa na wanaohusikana huo ujangili na uuaji wa ndugu zetu, ili utatie wasiwasi na mashaka na kuiharibu kesi.
 
Sisiem ikisaidiwa na chainise ndio waliolipua mkutano wa chadema.
Kutangaza kuwa wamekamata watuhumiwa sasa ni kutaka kufuta soo la balozi linalothibitisha kuwa walishirikiana.
 
Katika hili tunataka majibu na majina watuhumiwa wa kuingiza na kurusha mabomu. Siasa hatutaki.
Mulongo sipo polisi, hana uhalali wa kutangaza haya,zaidi hapa naona ni siasa tu na propaganda za kuimarisha chama cha zamani.
 
Sio kweli!Kuhusu Olasiti walikamatwa waarabu kitambo tu walikamatwa na ushahidi ulikamilika lakini serikali ya uarabuni ikaitunishia Tanzania. Na Tanzania ikawaachia waarabu wale. Wasidhani tumesahau. Hao wa sasa ni kubambikiana tu kesi. Sina imani na polisi Tanzania.Wewe je?
 
Mulongo ndo IGP au RPC, Wateule wengine bwana, in JANGA LA KIATAIFA!
 
Kama wako kwenye mahojiano ya mwisho kulikuwa hakuna haja ya . kutumbia. Angesubiri wamalize mazungumzo yao then atuambie kitu kamili kuliko kuleta saisa kwenye upelelezi. Watu wengine bana...

mkuu umeona mbwembwe za Mulongo?

huyu jamaa hakuwa na jambo la maana la kuongea, naanza kuamini uvumi wa kuwa Mulongo anapenda sana 'maigizo' na kuwatisha watu.
 
Back
Top Bottom