Waliochaguliwa SUA 2017/18 tukutane hapa

Waliochaguliwa SUA 2017/18 tukutane hapa

Hao 9 watakosaje Ajira ,

Mtie Moyo mwenzako , sisi tuliomaliza miaka ya 1990 , hiyo program ilikuwa inalipa sana

Mkuu, Mimi nimeongea ukweli. Ni bora uongee ukweli ili mhusika katika jambo fulani ajue jinsi ya kuweza kukabiliana na changamoto ambazo tayari amekwisha zijua mapema. Hakuna haja ya kuanza kumtia moyo kwenye uongo haisaidii hata kidgo.

Sasa nikimwambia uongo eti kisa nimtie moyo itamsaidia nini, au eti nimpambe sana Kwa uongo itamsaidia nini.

Zama zinabadilika mkuu tambua hilo. Hata sheria miaka ya 2000 ililipa sana ilikua na soko sana.

Ni hayo tu.
 
Shukrani kiongozi Kwa ukaribisho naweza kupata details za hiyo faculty Mkuu?
Sio faculty ni kozi... Faculty ni kitu kingine... Anyways...

Watabe wote wameondolewa na magu wamepewa vitengo serikalin wengine walistaafu enzi zetu kwa sasa wapo vijana vijana tu.

Kipindi cha kwanza mtaanza na remote sensing by then alikua anafundisha prof kimaro ila kwa sasa nadhan atakua amepewa jamaa mwingine ni Dr Proches !!

Semester ya kwanza mtakutana na engineering drawings... Na static mechanics hizi ndio kozi zinazokimbiza semester ya kwanza!!

Ofcoz kuna maths ila ni ile pure ya form6, hii maths kupata A ni nje nje kama ulisoma pure!!! Mtakutana na computer applications which is simple ila pia mtakua na elective ya DS100 haka kakozi ni kakijinga sana japo nlisomaga ila najuta mpaka leo...

Kama ukiweza chagua elective ya remote sensing tu hiyo ds100 piga chini maana unaweza lamba C au ukadakwa kabisa!!

All in all penda kusoma kwa discussion hasa kwenye kozi kama mechanics na drawings... acha kukomaa mwenyewe kama upo form6 maana huku hamna mashindano na hamna kuwa TO!!

Hongera sana na kila heri...
 
Mlengera was smart. Nilitaman kabla haja staafu Anisimie SP yangu bahati mbaya akastaafu!!

Ni mwalim ambaye kila prof alikua anamkubali... Tarimo mzee wa mjungu ila yule jamaa alikua anamvulia kofia!!

Kozi yake ya maji machafu nilipata A swafi kabisa!!

Alikua anatembea na baiskeli... Ukimuona unaweza zan ni mfanyakazi wa bustan kumbe ni prof wa kiwango cha lami daaaah!!

Sizan kama pale dept ya engineering atakaa atokee mwalimu kama yeye!!
Alinitisha sana huyu Mzee ChupuChupu angenitia doa la Probation kabisa,Test zote nilipiga Below.Lakini UE ilikuja kuniokoa kwani nasikia alisisha mara 3 anakuta maksi zinazidi 100%.Weka mbali na Vilaza huyu Dr.Mathayo Mulengera.
 
Nimemaliza hiyo course ktk department of agricultural engineering and land planning chini ya prof. Mpanduji. Ila daaah mdogo wangu sikufichi kabisa Mimi nimemaliza 2016 ila tumeisoma namba kitaa mpka sasa, na hata walomaliza mwaka 2015 walikua 9 tu. Ila bado wapo mtaani wanasota sana, kipindi namaliza walikuja vijana wa st Joseph baada ya chuo chao kufungwa. Kuna wengine wamejoin na hawa walomaliza mwaka huu wanafika hata 100. Na wengine walijoin na hawa wanamaliza mwakani wale ndo wako ka 200 aiseee fikiria jam hiyo.
Mimi nimeamua kupiga zangu ujasiriamali , chamsingi wewe ukienda hiyo usitegemee ajira sana uwe na plan B tunza pesa zako sana uje ujikte kwenye ujasiamali kama sisi kaka zako, nakwambia ukweli ili ujioange AGE haina dili kabisa Kwa sasa, sasa hiv nimesikia mkuu wa department ni baanda salim
Hakuna shida Toka 2014/2015 mpaka sasa ajira zimekuwa adimu hii ni kutokana na kusitishwa kwa Suala la Ajira,Lakini Ajira zitakuwepo cha msingi usikate tamaa mapema.
 
Alinitisha sana huyu Mzee ChupuChupu angenitia doa la Probation kabisa,Test zote nilipiga Below.Lakini UE ilikuja kuniokoa kwani nasikia alisisha mara 3 anakuta maksi zinazidi 100%.Weka mbali na Vilaza huyu Dr.Mathayo Mulengera.
Hahaaha wewe ulimkuta akiwa dr nini?? Nilichompendea jamaa alikua smart asee... Yaani humwambii chochote kwenye maji... Civil na soil!! Nakumbuka test yake ya kwanza nililamba below ya pili nikapiga B UE nikamaliza na A!!

Kozi kapewa kijana mmoja anaitwa festo... Kwa kifupi imepoteza mvuto kabisa baada ya mlengera kustaafu!!
 
Sio faculty ni kozi... Faculty ni kitu kingine... Anyways...

Watabe wote wameondolewa na magu wamepewa vitengo serikalin wengine walistaafu enzi zetu kwa sasa wapo vijana vijana tu.

Kipindi cha kwanza mtaanza na remote sensing by then alikua anafundisha prof kimaro ila kwa sasa nadhan atakua amepewa jamaa mwingine ni Dr Proches !!

Semester ya kwanza mtakutana na engineering drawings... Na static mechanics hizi ndio kozi zinazokimbiza semester ya kwanza!!

Ofcoz kuna maths ila ni ile pure ya form6, hii maths kupata A ni nje nje kama ulisoma pure!!! Mtakutana na computer applications which is simple ila pia mtakua na elective ya DS100 haka kakozi ni kakijinga sana japo nlisomaga ila najuta mpaka leo...

Kama ukiweza chagua elective ya remote sensing tu hiyo ds100 piga chini maana unaweza lamba C au ukadakwa kabisa!!

All in all penda kusoma kwa discussion hasa kwenye kozi kama mechanics na drawings... acha kukomaa mwenyewe kama upo form6 maana huku hamna mashindano na hamna kuwa TO!!

Hongera sana na kila heri...
. Shukrani Mkuu
 
Wakuu mliopo sua..vp kuhusu hostel hapo zinapatikana za chuo au tujiandae kupanga tu
 
Tupen maujanja ya kutoboa sua pale kwa coz zote!!! Wakuu
Sua ni chuo kizur kinakubarka almost the same na udsm tu , hivyoo graduate wanakua na uwezo wa Ku compete na graduate wa vyuo vkubwa kama mzumbe, na mliman (udsm)
Hivyoo Hakka tuliopo sua mi naona weng wetu hatujut japo kina complications zake ikiwepo misuli mirefuu, hivyoo karibu sana ndugu maisha ya sua hayatakiw kujisahau utajikuta unashuka GPA yako or kukosa chuo, but vngine kawaida kama , michezo, maswala ya iman n.k
Karibun sana
 
Tupen maujanja ya kutoboa sua pale kwa coz zote!!! Wakuu
Mdogo wangu hakuna ushauri kama kuwa na "NIDHAMU YA SHULE" nakusisitiza tena na tena usifanye chochote ila kuwa na "NIDHAMU YA SHULE" mdogo narejea tena fanya chochote utakacho wewe katika maisha yako ya shule ila tu usijeacha na kusahau "NIDHAMU YA SHULE"

Nawaombe taufiq kwa MUNGU MWENYEZI akutilieni baraka katika masomo yenu
 
Back
Top Bottom