Walioandaa mgomo UDSM kuadhibiwa

Walioandaa mgomo UDSM kuadhibiwa

huyo mwanafunzi mnyonge anayesubiri ka-boom kumhudumia yeye pamoja na extended family anawezaje kugoma? anapata wapi locus stand? pesa ya shule ni kwa matumizi ya kawaida mwanafunzi anapokuwa shuleni tu. matumizi mengine ni abuse tu. sasa mwanafunzi agome eti kwa sababu hajapewa pesa ya kutuma nyumbani kwa wazazi wake!
Uwezi elewa jamaa alichokisema kama wewe ulitoka familia bora ila wengine boom ilo inasaidia na wadogo zako waende secondary hapo hapo wapate ndoo moja ya unga, sikulaum kwani ni vigum kuelewa alichoandika kwani unaonekana hujapitia au hukuwa na maisha haya
 
Uongo huu tumeutumia sana ulipokuwa tunasoma, boom tulilitumia kwa ulabu, mademu, kununua simu kali, viwalo bomba, Tv rediao na vitu vingine vingi ambavyo havina uhusiano na masomo. Lakini kila tulipoaka sympathy ya wananchi tulitumia sababu hiyo ei wazazi masikini Tanzania wakati bar zote mikoani zinauza na TBL ndio mlipa kodi mkubwa, hao wau masikini wananunua magari, wanajenga nyumba kali, soko la bidhaa zote za china lakini linapokuja kulipia elimu eti wazazi masikini. Uongo huu ifike muda sasa usitumike tena. Hao wanaoimba hapo wanaonekana masikini hao?
Acha kukurupuka mkuu hujaona watu wanashindwa kwenda chuo kwa kukosa ada? Hujaona watu wanaahirisha masomo kwa kushindwa kulipa ada? Hujaona watu wanashindwa kufanya UE kwa kushindwa kulipa ada kisa hawana boom? Inapasa uelewe kama wewe familia yako ilikuwa inakupa fedha licha ya kwamba una boom wenzako hawapewi hata shilling moja wanapoenda chuo na mategemeo yao yote yapo kwenye boom.
 
huyo mwanafunzi mnyonge anayesubiri ka-boom kumhudumia yeye pamoja na extended family anawezaje kugoma? anapata wapi locus stand? pesa ya shule ni kwa matumizi ya kawaida mwanafunzi anapokuwa shuleni tu. matumizi mengine ni abuse tu. sasa mwanafunzi agome eti kwa sababu hajapewa pesa ya kutuma nyumbani kwa wazazi wake!
Hujamuelewa vizuri Wissman au pengine hujawahi kupata msoto wa boom chuoni.
 
Kumbe waligoma ndio wakapewa?
Sasa tatizo lipo wapi?
Mi nahisi watakao sapot uo upumbavu watakua hawajafika chuo kikuu na kuonja uchungu boom linapochelewa
Fateni huo ushauri mkikurupuka navyowajua hao wanafunzi mtafunga hicho chuo

Wakati wanagoma fedha tayari zilikuwa zimeshafika na utaratibu wa kuziingiza kwenye akaunti ulikuwa unakamilika...hao vijana walikurupuka, madai yao yalikuwa ni hewa...labda walikuwa wanawaiga wazee, kaka, dada zao kule wanakoita 'mje...'
 
Wanafunzi wa UDSM wanapaswa kupaaza sauti kupinga kitendo walichofanyiwa wenzao wa UDOM na pia Bunge kushindwa kuisimamia serikali katika hili. Kupewa kwao Boom ni kama Peremende tu za kuzima movement yoyote wakati Rais atakapotembelea

Ni wakati sasa UDSM kurudisha hadhi yake kwa kupinga kwa hoja kabisa mwenendo wa Serikali hii. Rais atataka kushangiliwa lakini muulizeni ni wapi aliona nchi ikiendeshwa hivi zaidi ya Korea ya Kaskazini. Kama anasema anataka kuleta mabadiliko muulizeni kwa nini asirejeshe katiba ya Warioba maana huko ndiko kulijenga upya Taifa?

Muulizeni kwa bajeti ya Bilioni 81 kwa mwaka ni viwanda gani vitajengwa na kutoa ajira kwenu? Ninyi pia mmeandaliwa incentives gani ili mkimaliza mjiajiri? Tena muulizeni maswali hayo kwa Kiingereza.Nawahakikishia hatakasirika kwa sababu mmemuuliza kwa Kiingereza

Mwisho,Msije mkajivua nguo kwa kumshangilia bila kumhoji labda mumshangilie kimkakati halafu mumkosoe. Maana akikubali kushangiliwa pia akubali kukosolewa
Daah maswali yote ni akili tupu....hapa kuna vikojozi watakuja kutokwa na povu
 
Hivi UDSM ni chuo cha boys tupu. Huoni bint hata mmoja kwny harakati. Na ndio hali halisi hata kwenye maisha, mwisho wa siki haki sawa wakati wenzetu wana nafasi za u baby.
 
Kumbe waligoma ndio wakapewa?
Sasa tatizo lipo wapi?
Mi nahisi watakao sapot uo upumbavu watakua hawajafika chuo kikuu na kuonja uchungu boom linapochelewa
Fateni huo ushauri mkikurupuka navyowajua hao wanafunzi mtafunga hicho chuo
JPM asipodhibitiwa hit Nchi itageuka kuwa KOREA KASAKAZINI
 
Menejimenti yaweza kupasisha mkusanyiko unao dai haki za kimsingi toka lini na wapi ilifanyika hiyo waache ushakunaku mtoa habari Mwenyewe haitajiki kuchunguzwa ukisoma tu utajuwa akili yake kuwa kila haki ya mtu inapodaiwa ina lengo la upinzani tuliza akili ndugu unapowasilisha jambo.
 
Nilitaka kushangaa, ule mgomo ni wa kisiasa kwa maana ulikuwa well organized na ilikuwa ni zaidi ya Wanafunzi tu waliokuwa na malalamiko, safi sana hawo waadhibiwe tena ikiwezekana wafukuzwe kabisa ili iwe fundisho kwamba Chuoni ni mahali pa kusomea na siyo kufanya Siasa, wafukuzwe wakajiunge na chadema, huko ndiyo wakafanye Siasa wanavyoweza kama wako tayari kuchezea future yao kwa ajili ya Wanasiasa ambao tayari wao wameshajijenga ...




Wakati Rais John Magufuli akitarajia kuwasili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo, wanafunzi walioandamana wakishinikiza malipo yao ya fedha za kujikimu juzi, huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu.

Wanafunzi hao huenda wakaadhibiwa kwa kosa la kukikuka sheria ndogo ya chuo kwa kuandaa mkusanyiko pasipo kibali cha menejimenti.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Florens Luoga alisema jana kuwa, mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinaendelea na uchunguzi kubaini nani aliyehusika katika tukio hilo.

“Taratibu na sheria ndogo za chuo haziruhusu mtu kuandaa mkusanyiko ambao haujaidhinishwa na menejimenti. Taratibu hizo lazima ziheshimiwe ili ziendelee kuwa imara. Hivyo tunasubiri ripoti ya waliohusika,” alisema Luoga.

Juzi, wakati wa maandamano ya wanafunzi hao walikuwa wakipaza sauti iliyotolewa na Rais Magufuli wakati wa kampeni za kuwania wadhifa huo akisema:

“Serikali yangu haitarajii kuona mwanafunzi akifukuzwa chuo kwa kosa la kugoma kisa mkopo, bali ikitokea mgomo, watawajibisha maofisa wa Bodi ya Mikopo kwa kuchelewesha fedha.”


Taarifa zilizopatikana jana zilieleza kuwa fedha za wanafunzi hao zimeshawekwa kwenye akaunti zao, juzi jioni.

Rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Erasmi Leon alisema licha ya wanafunzi hao kukiuka utaratibu, haoni sababu za kuwachukulia hatua kwani hawakusababisha madhara wala uharibifu wowote.

“Endapo kamati ya nidhamu itaamua kufanya hivyo ni vyema wakafanya suala hilo kimantiki na kibinadamu na endapo usimamizi wa sheria ukifuata zaidi unaweza ukasababisha kuibuka kwa mambo mengine tofauti,” alisema Leon.

Alisema wanaendelea kuwasihi wanafunzi kuhakikisha suala hilo halijitokezi tena kwani linaitia doa Serikali yake, uongozi wa chuo na Taifa kwa jumla.

Wanafunzi hao waligoma kuanzia Jumatatu usiku na mgomo wao kuisha juzi, baada ya kupewa fedha zao ambazo zilichelewa kwa madai ya uhakiki wanafunzi hewa unaondelea.

Ngoja tusubiri statement ya Rais leo. Tusikie Hilo kwake limekaaje.
 
Huyo Luoga na aseme je wanafunzi walikuwa wanadai kweli ama ilikuwa uzushi
Ni kwa nini pesa imetoka baada ya shinikizo? Je walikuwa wapi kuwapa on time? so waliachelewesha ili wagome then wawadhibu? - UPUUZI HUO mchafu sana
 
Miongoni mwa nchi zenye watu wanafki yetu inaongoza. Ulishawahi kwenda chuo wazazi hali zao ni za kawaida na unategemea boom kwanza kulipia ada ili uweze kufanyia usajili, then boom hilohilo ndio liendeshe maisha yako ya chuo, boom hilohilo utoe kidogo utume kwa wazazi ili maisha yao yasonge, then boom hilohilo usaidie wadogo zako, halafu hela hiyo unayoitegemea kwa hali na mali inacheleweshwa kwa sababu zisizo za msingi? Kama hujawahi kuwa katika hali hiyo huwezi jua kwanini wanafunzi wanagoma boom linapochelewa
...

....well NOTED Mkuu
 
Bila kugoma wangefanikiwa vipi kupata madai yao? Hao wanataka kuwaadhibu hao wanafunzi kwa kosa gani? Wanafunzi wanadai haki zao
 
Hakuna mtu anasusa kwa hiyari, labda kama huelewi maana ya kususa. Hapo kwenye RED ndio ukomo wa akili yako? Wanafunzi hawajiandai, WANAANDALIWA na ndio maana wako pale. Ubunifu unaanzia kwa waongozaji na kuhamishiwa kwa waongozwa. Unamjazia mwanafunzi changamoto ili ajifunze changamoto, sasa namna ya kukabiliana na hiyo changamoto ulioianzisha bila sababu za msingi ni maandamano, HAMTAKI.



Ni kweli si kila mtu anaweza kujiajiri, ndio maana inahitajika mifumo wezeshi kuongeza wigo wa watu wanaojiajiri, moja kati ya institutions za kuwaandaa watu kujiajiri ni vyuo. Kama bajeti ya serikali haijengi viwanda, misaada mmesema hatuihitaji, uwekezaji unaporomoshwa na siasa za ki-Ji Sung Park, sasa inamaanisha maneno meeeengi ya kufufua viwanda na kuanzisha vipya ni ngonjera?



Ashakhum si matusi, uliomalizia nao hapo ni upumbavu. Mkuu, unaniambia kwamba NI WAJIBU WA WANAFUNZI KUVUMILIA MAZINGIRA MAGUMU YANASABABISHWA NA WATU WENGINE PASIPO SABABU ZA MSINGI? MAISHA NDIYO YAKO HIVYO? KWAMBA MTU MMOJA KWENYE CHAIN HAWAJIBIKI IPASAVYO, ANALETA USUMBUFU HALAFU INAKUWA NI WAJIBU WA WANAFUNZI KUVUMILIA?

Serikari itaweka mazingira blah blah blah......na wengine mametusua...... . Well then, hao waliogoma ni wale ambao mazingira mazuri hayakuwapitia karibu, vipi hapo?

Nakujibu mwisho kabisa, maisha magumu mlaumu mzazi wako kwanza, pili serikali na tatu M/Mungu japokuwa umeanza na ashakum, wanafunzi wawe wapambanaji kunji hamkuanza nyie wenzenu walikuwa wanamaliza show wenyewe bila Bunge. By then watu walikuwa wanakanyaga Science kutokea mlimani mpaka posta nyie watoto wa siku hizi mnataka Bunge liwasemee ni kurudisha nyuma harakati zilizoasisiwa miaka mingi. Waziri akimbwela watu walikuwa wanafikisha ujumbe kwa Raisi bila madalali wala wanasiasa. Sasa hivi inakuwa ngumu kujua ipi issue ya wanafunzi na ipi ni siasa.

Wanafunzi wa chuo unataka kuandaliwa? Graduate ?!! dogo hauko serious hata kidogo, ki Ji Sung Park ni mtu wa kupigiwa mfano. By then hata kina Julius, Mandela, Patrice and etal wamagharibi ndio walikuwa wanawaona kama wewe unavyowaona kina Park leo.
 
Mbona vyuo kama Mzumbe hawagomi??? Au wao boom huwa alicheleweshwi?
Una uhakika Mzumbe hawagomi mkuu?Na Mzumbe lini wameanza kudahili wanafunzi wanaotegemea boom?Mfumo wa Mzumbe ulikuwa tofauti na vyuo vingine mkuu
 
Kwa sasa siasa za namna hii zinafaa mkutano wa hadhara, Manzese au Tandale kwa Mfuga-mbwa, siyo Nkrumah Hall. Kwa kuwa mwaka jana, kwa ubinafsi wenu, kwa kupenda pesa kwenu, kwa choyo chenu, na kwa upendeleo wa kikabila uliopiliza, mliamua kushindwa uchaguzi Mkuu, kuanzia mwaka huu mkome kuwafanya wanafunzi vyuoni kuwa kisingizio au nago ya aibu ya kushindwa kwenu uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
Shida yenu Lumumba ni kufikiri kwa kutumia TUMBO au utumiaji mbovu wa Viuongo vya mwili.
Kwanini huwa mnatoa mapovu kwenye hoja za msingi,unapokuwa mgonjwa alafu unabishana na Daktari utakufa maana hata akikochoma sindano huku unahangaika itakuvunjikia na dawa itashindwa kuingia mwilini vizuri.

Njooni na Points zenye Facts kama Ben alivyo nena ni UKWELI MTUPU,this is LIVE & Direct with NO chenga.
 
unabwabwaja tu hata huelewi maana, unaweza kuweka akiba ya hela ambayo hujaishika?! Kama dadako ananunua wanaume ni huyo huyo si wanawake wote, pole kwa kushindwa malezi ya mabinti zenu hapo home, tukana hao si wa nje ya familia yako. Naona umekuzwa na pesa za hongo ndio maana umekariri akili ya kuhongwa tu.
Hata majibu yako yatosha kuthibitisha nilicho kiandika. Elimu yako inatia shaka. Huwenda aliyefungua mlango alibeba na akili zako. Hapa kwenye kununua wanaume wewe ni muhusika kwa asilimia mia moja. Hii hasira kwa swala la jumla ni wazi wewe ndivyo ulivyo. Hata kama dada yangu ndiye uliyemuona hukuwa na sababu ya kung'aka.
Wewe ni miongoni mwa majuha kweli. Hivi nikimuacha mtoto wa nje ya familia yangu anaharibika na ninauwezo wa kumuasa nikae kimya? Wewe huko chuoni mzazi wako hayupo waungwana wanakuona unabadili masharobaro wasikuambie japo kukushauri. Wakikuambia ukweli unang'aka.Elimika vizuri utusaidie wewe ukielimika vizuri ukawa muuguzi au daktari mzuri mwenye maadili nikija kwako utanihudumia hutahudumia wa kwenu tu. Pia kama ukiwa kahaba au mwizi huenda ukaja kuniathiri mimi au ndugu na jamaa zangu. Kwa hali hii nilazima nikuase bila kujali wewe unatoka kwenye familia yangu.
Hayo machache yatakua yamekusaidia Acha ujinga elimika acha kuhonga wanaume.
 
Wanafunzi wa UDSM wanapaswa kupaaza sauti kupinga kitendo walichofanyiwa wenzao wa UDOM na pia Bunge kushindwa kuisimamia serikali katika hili. Kupewa kwao Boom ni kama Peremende tu za kuzima movement yoyote wakati Rais atakapotembelea

Ni wakati sasa UDSM kurudisha hadhi yake kwa kupinga kwa hoja kabisa mwenendo wa Serikali hii. Rais atataka kushangiliwa lakini muulizeni ni wapi aliona nchi ikiendeshwa hivi zaidi ya Korea ya Kaskazini. Kama anasema anataka kuleta mabadiliko muulizeni kwa nini asirejeshe katiba ya Warioba maana huko ndiko kulijenga upya Taifa?

Muulizeni kwa bajeti ya Bilioni 81 kwa mwaka ni viwanda gani vitajengwa na kutoa ajira kwenu? Ninyi pia mmeandaliwa incentives gani ili mkimaliza mjiajiri? Tena muulizeni maswali hayo kwa Kiingereza.Nawahakikishia hatakasirika kwa sababu mmemuuliza kwa Kiingereza

Mwisho,Msije mkajivua nguo kwa kumshangilia bila kumhoji labda mumshangilie kimkakati halafu mumkosoe. Maana akikubali kushangiliwa pia akubali kukosolewa
Rudi shule ukasome uulize hayo maswal..wasomi wazima hawawez tegema hoja mufilisi zako hzo.....toka mmsafishe lowasa sisi wazalendo tumewatema ukawa woteeee
 
UDSM enz zetu nilikuwa viongoz wa vyuo vyote vya umma hata binafsi,tatizo la udom,enz hizo udsm wangegoma mpaka wanafunz warejeshwe,kuna wanafunz walikuwa wakisimama hata kama huna hamu ya kugoma akisema mgomo usio na mwisho,umat unaripuka shangwe.Siyaon hayo kwa sasa.
 
Ulipomalizia ndio nimepapenda manake kukosolewa iwe na kwenu tatizo nyie ndio mkikosolewa mnarusha ngumi na mnapenda kukosoa tu. Wanafunzi wanatakiwa kuwa kama wanafunzi na kujiandaa kuwa wabunifu katika kukabiliana na changamoto za maisha sasa mkiendelea kuwatumia wengi na kuchagua wachache ndio mnawatunuku vyeo katika vyama vyenu ndio shida ilipo. Katiba ya Warioba mlisusa kwa hiyari yenu na maisha lazima yaendelee, mmevuruga mchakato wa katiba na kuibuka na UKAWA nyie ndio at least imewasaidia wenzenu mmewatumia na mmewaua kisiasa waasisi baada ya gia zenu za angani.

Tatizo lenu raisi mnamuogopa yeye hajawazuia msimpinge sema mnazunguka mara Tulia mara Sukari mara Lugumi, Bajeti ya serikali haijengi viwanda najua unajua sema mnavyotaka kujipendekeza kwa Mbowe hawaone mpo ndio shida. Kujiajiri sio kila mtu anaweza hata mzee Mengi ilimchukua miaka kuanza kujiajiri sasa ukimtwisha JPM wakati kazini hata mwaka hana itakuwa shobo tu.

Wanafunzi watimize wajibu wao hata kama wanakutana na mazingira magumu ndio maisha yako hivyo wachache ndio wako fortunate. Serikali itaweka mazingira rafiki na ukitaka kujua yapo utaona kuna wengine wametusua bila kusubiri na wako mbali.
Acheni kupenda kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa mbona msiwaoe mpk wamegoma kama mko makini hamtaki kunyooshewa vidole hamuwezi lakini wabishi mpk sasa hamuoni tu dont fool people for the name of uchama.Mangapi yanaenda ndivyo sivyo bado mnataka mpigiwe makofi.Watu kama nyie wenye uchama nnudhi sana wewe unaona haki watu wateseke kisa wewe umekaa mezani unakula ,kila kitu kwako kinaenda sawa acha ubinafsi kua na utu sema kweli na itakuweka huru pye nyie ndo mnaorudisha nyumma maendeleo.
 
Back
Top Bottom