Walioandaa mgomo UDSM kuadhibiwa

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Nilitaka kushangaa, ule mgomo ni wa kisiasa kwa maana ulikuwa well organized na ilikuwa ni zaidi ya Wanafunzi tu waliokuwa na malalamiko, safi sana hawo waadhibiwe tena ikiwezekana wafukuzwe kabisa ili iwe fundisho kwamba Chuoni ni mahali pa kusomea na siyo kufanya Siasa, wafukuzwe wakajiunge na chadema, huko ndiyo wakafanye Siasa wanavyoweza kama wako tayari kuchezea future yao kwa ajili ya Wanasiasa ambao tayari wao wameshajijenga ...

Wakati Rais John Magufuli akitarajia kuwasili Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) leo, wanafunzi walioandamana wakishinikiza malipo yao ya fedha za kujikimu juzi, huenda wakakumbwa na hatua za kinidhamu.

Wanafunzi hao huenda wakaadhibiwa kwa kosa la kukikuka sheria ndogo ya chuo kwa kuandaa mkusanyiko pasipo kibali cha menejimenti.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (Taaluma), Florens Luoga alisema jana kuwa, mamlaka za nidhamu chuoni hapo zinaendelea na uchunguzi kubaini nani aliyehusika katika tukio hilo.

“Taratibu na sheria ndogo za chuo haziruhusu mtu kuandaa mkusanyiko ambao haujaidhinishwa na menejimenti. Taratibu hizo lazima ziheshimiwe ili ziendelee kuwa imara. Hivyo tunasubiri ripoti ya waliohusika,” alisema Luoga.

Juzi, wakati wa maandamano ya wanafunzi hao walikuwa wakipaza sauti iliyotolewa na Rais Magufuli wakati wa kampeni za kuwania wadhifa huo akisema:

“Serikali yangu haitarajii kuona mwanafunzi akifukuzwa chuo kwa kosa la kugoma kisa mkopo, bali ikitokea mgomo, watawajibisha maofisa wa Bodi ya Mikopo kwa kuchelewesha fedha.”

Taarifa zilizopatikana jana zilieleza kuwa fedha za wanafunzi hao zimeshawekwa kwenye akaunti zao, juzi jioni.

Rais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo, Erasmi Leon alisema licha ya wanafunzi hao kukiuka utaratibu, haoni sababu za kuwachukulia hatua kwani hawakusababisha madhara wala uharibifu wowote.

“Endapo kamati ya nidhamu itaamua kufanya hivyo ni vyema wakafanya suala hilo kimantiki na kibinadamu na endapo usimamizi wa sheria ukifuata zaidi unaweza ukasababisha kuibuka kwa mambo mengine tofauti,” alisema Leon.

Alisema wanaendelea kuwasihi wanafunzi kuhakikisha suala hilo halijitokezi tena kwani linaitia doa Serikali yake, uongozi wa chuo na Taifa kwa jumla.

Wanafunzi hao waligoma kuanzia Jumatatu usiku na mgomo wao kuisha juzi, baada ya kupewa fedha zao ambazo zilichelewa kwa madai ya uhakiki wanafunzi hewa unaondelea.
 
Miongoni mwa nchi zenye watu wanafki yetu inaongoza. Ulishawahi kwenda chuo wazazi hali zao ni za kawaida na unategemea boom kwanza kulipia ada ili uweze kufanyia usajili, then boom hilohilo ndio liendeshe maisha yako ya chuo, boom hilohilo utoe kidogo utume kwa wazazi ili maisha yao yasonge, then boom hilohilo usaidie wadogo zako, halafu hela hiyo unayoitegemea kwa hali na mali inacheleweshwa kwa sababu zisizo za msingi? Kama hujawahi kuwa katika hali hiyo huwezi jua kwanini wanafunzi wanagoma boom linapochelewa
 
Wanafunzi wa UDSM wanapaswa kupaaza sauti kupinga kitendo walichofanyiwa wenzao wa UDOM na pia Bunge kushindwa kuisimamia serikali katika hili. Kupewa kwao Boom ni kama Peremende tu za kuzima movement yoyote wakati Rais atakapotembelea

Ni wakati sasa UDSM kurudisha hadhi yake kwa kupinga kwa hoja kabisa mwenendo wa Serikali hii. Rais atataka kushangiliwa lakini muulizeni ni wapi aliona nchi ikiendeshwa hivi zaidi ya Korea ya Kaskazini. Kama anasema anataka kuleta mabadiliko muulizeni kwa nini asirejeshe katiba ya Warioba maana huko ndiko kulijenga upya Taifa?

Muulizeni kwa bajeti ya Bilioni 81 kwa mwaka ni viwanda gani vitajengwa na kutoa ajira kwenu? Ninyi pia mmeandaliwa incentives gani ili mkimaliza mjiajiri? Tena muulizeni maswali hayo kwa Kiingereza.Nawahakikishia hatakasirika kwa sababu mmemuuliza kwa Kiingereza

Mwisho,Msije mkajivua nguo kwa kumshangilia bila kumhoji labda mumshangilie kimkakati halafu mumkosoe. Maana akikubali kushangiliwa pia akubali kukosolewa
 
Kumbe waligoma ndio wakapewa?
Sasa tatizo lipo wapi?
Mi nahisi watakao sapot uo upumbavu watakua hawajafika chuo kikuu na kuonja uchungu boom linapochelewa
Fateni huo ushauri mkikurupuka navyowajua hao wanafunzi mtafunga hicho chuo
 
Wanafunzi wa UDSM wanapaswa kupaaza sauti kupinga kitendo walichofanyiwa wenzao wa UDOM na pia Bunge kushindwa kuisimamia serikali katika hili.

Kupewa kwao Boom ni kama Peremende tu za kuzima movement yoyote wakati Rais atakapotembelea

Ni wakati sasa UDSM kurudisha hadhi yake kwa kupinga kwa hoja kabisa mwenendo wa Serikali hii

Rais atataka kushangiliwa lakini muulizeni ni wapi aliona nchi ikiendeshwa hivi zaidi ya Korea ya Kaskazini.

Kama anasema anataka kuleta mabadiliko muulizeni kwa nini asirejeshe katiba ya Warioba maana huko ndiko kulijenga upya Taifa?

Muulizeni kwa bajeti ya Bilioni 81 kwa mwaka ni viwanda gani vitajengwa na kutoa ajira kwenu?

Ninyi pia mmeandaliwa incentives gani ili mkimaliza mjiajiri?

Tena muulizeni maswali hayo kwa Kiingereza.Nawahakikishia hatakasirika kwa sababu mmemuuliza kwa Kiingereza

Mwisho,Msije mkajivua nguo kwa kumshangilia bila kumhoji labda mumshangilie kimkakati halafu mumkosoe. Maana akikubali kushangiliwa pia akubali kukosolewa

Ulipomalizia ndio nimepapenda manake kukosolewa iwe na kwenu tatizo nyie ndio mkikosolewa mnarusha ngumi na mnapenda kukosoa tu. Wanafunzi wanatakiwa kuwa kama wanafunzi na kujiandaa kuwa wabunifu katika kukabiliana na changamoto za maisha sasa mkiendelea kuwatumia wengi na kuchagua wachache ndio mnawatunuku vyeo katika vyama vyenu ndio shida ilipo. Katiba ya Warioba mlisusa kwa hiyari yenu na maisha lazima yaendelee, mmevuruga mchakato wa katiba na kuibuka na UKAWA nyie ndio at least imewasaidia wenzenu mmewatumia na mmewaua kisiasa waasisi baada ya gia zenu za angani.

Tatizo lenu raisi mnamuogopa yeye hajawazuia msimpinge sema mnazunguka mara Tulia mara Sukari mara Lugumi, Bajeti ya serikali haijengi viwanda najua unajua sema mnavyotaka kujipendekeza kwa Mbowe hawaone mpo ndio shida. Kujiajiri sio kila mtu anaweza hata mzee Mengi ilimchukua miaka kuanza kujiajiri sasa ukimtwisha JPM wakati kazini hata mwaka hana itakuwa shobo tu.

Wanafunzi watimize wajibu wao hata kama wanakutana na mazingira magumu ndio maisha yako hivyo wachache ndio wako fortunate. Serikali itaweka mazingira rafiki na ukitaka kujua yapo utaona kuna wengine wametusua bila kusubiri na wako mbali.
 
Kwa sasa siasa za namna hii zinafaa mkutano wa hadhara, Manzese au Tandale kwa Mfuga-mbwa, siyo Nkrumah Hall. Kwa kuwa mwaka jana, kwa ubinafsi wenu, kwa kupenda pesa kwenu, kwa choyo chenu, na kwa upendeleo wa kikabila uliopiliza, mliamua kushindwa uchaguzi Mkuu, kuanzia mwaka huu mkome kuwafanya wanafunzi vyuoni kuwa kisingizio au nago ya aibu ya kushindwa kwenu uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.
 
Miongoni mwa nchi zenye watu wanafki yetu inaongoza. Ulishawahi kwenda chuo wazazi hali zao ni za kawaida na unategemea boom kwanza kulipia ada ili uweze kufanyia usajili, then boom hilohilo ndio liendeshe maisha yako ya chuo, boom hilohilo utoe kidogo utume kwa wazazi ili maisha yao yasonge, then boom hilohilo usaidie wadogo zako, halafu hela hiyo unayoitegemea kwa hali na mali inacheleweshwa kwa sababu zisizo za msingi? Kama hujawahi kuwa katika hali hiyo huwezi jua kwanini wanafunzi wanagoma boom linapochelewa
huyo mwanafunzi mnyonge anayesubiri ka-boom kumhudumia yeye pamoja na extended family anawezaje kugoma? anapata wapi locus stand? pesa ya shule ni kwa matumizi ya kawaida mwanafunzi anapokuwa shuleni tu. matumizi mengine ni abuse tu. sasa mwanafunzi agome eti kwa sababu hajapewa pesa ya kutuma nyumbani kwa wazazi wake!
 
Mbona vyuo kama Mzumbe hawagomi??? Au wao boom huwa alicheleweshwi?

Tatizo la wanafunzi wa UDSM wajiona wao ndio wanafunzi pekee wa chuo kikuu na hakuna wanafunzi vyuo vingine,hata ukisikikiza kauli zao wakati wa mgomo utagundua hilo,nilidhani kupitia mgomo huo watapaaza sauti zao kuhusu wanafunzi wa udom,lakin wamekua wabinafsi na hili linatokana na wao kutumiwa na wanasiasa kuanzisha mgomo huo na sio kudai maslahi ya wanafunzi wa vyuo vikuu vyote.
 
wewe bogus kweli kweli. huyo mwanafunzi mnyonge anayesubiri ka-boom kumhudumia yeye pamoja na extended family anawezaje kugoma? anapata wapi locus stand? pesa ya shule ni kwa matumizi ya kawaida mwanafunzi anapokuwa shuleni tu. matumizi mengine ni abuse tu. sasa mwanafunzi agome eti kwa sababu hajapewa pesa ya kutuma nyumbani kwa wazazi wake!
Kama unafikiri watanzaniq wote wanamaisha kama yako pole sana. Umeenda chuo kweli wewe? Uliza ni wanafunzi wangapi wanshindwa kufanya usajili ili waweze kuingia darasani boom linapochelewa?
 
Wanawaadhibu kukwepa aibu tu, walijinasibu mkopo fasta kwa wote, mambo yamekuwa kinyume kama awamu iliyopita tu, sasa kwa kuwa watoto wamemuumbua malaika hadharani wanafanywa kuku wa kafara, haita saidia kuwaumiza bali tekelezni waibu wenu mapema kama hela ilikuwepo kwa nini itoke baada ya mgomo? Malaika angeanza na bodi ya mikopo sio watoto wa maskini hawa.
 
Mbona vyuo kama Mzumbe hawagomi??? Au wao boom huwa alicheleweshwi?
Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Kuzilwa alivyokuwa pale alidhibiti sana, yaani ikionekana tu dalili za kugoma alikuwa anatoa tahadhari, hata sasa Prof. Itika anaendeleza nyendo hizo hizo. Huwa kuna manung'uniko lakini wanabanwa na kudhibitiwa. mfano pale huruhusiwi kufanya siasa wala kuvaa nguo ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la chuo
 
hili siyo jambo jipya kama una uelewa mpana kuhusu mambo ya chuo. hata akina Samweli sita, Zitto, Mnyika waliwahi kuadhibiwa tena zaidi ya hivyo unavyopenda wewe, lakini haikuzuia nyota zao kung'ara, so we endelea kupiga makofi tu
 
Wafukuzwe tu, tena ingependeza rais awachape hata fimbo na kuwafukuza. Mi nilishasema tangu mwanzo kuwa serikali ya Dr Magufuli ilishajitanabaisha toka mwanzo kuwa wanafunzi lazima watapata mikopo hakuna wa kukosa sasa wao kilichowafanya wagome ni nini????? Wapumbafu sana hawa vijana. Mbona wafanyakazi wa halmashauri safari hii mishahara ilichelewa kwa siku kazaa mbona hawakugoma?? Ina maana hao vijana wanadharau serikali, wanamdharau rais. Yaani wafukuzwe wale wote waliochochea mgomo liwe fundishooooo.
 
Ulipomalizia ndio nimepapenda manake kukosolewa iwe na kwenu tatizo nyie ndio mkikosolewa mnarusha ngumi na mnapenda kukosoa tu. Wanafunzi wanatakiwa kuwa kama wanafunzi na kujiandaa kuwa wabunifu katika kukabiliana na changamoto za maisha sasa mkiendelea kuwatumia wengi na kuchagua wachache ndio mnawatunuku vyeo katika vyama vyenu ndio shida ilipo. Katiba ya Warioba mlisusa kwa hiyari yenu na maisha lazima yaendelee, mmevuruga mchakato wa katiba na kuibuka na UKAWA nyie ndio at least imewasaidia wenzenu mmewatumia na mmewaua kisiasa waasisi baada ya gia zenu za angani.

Hakuna mtu anasusa kwa hiyari, labda kama huelewi maana ya kususa. Hapo kwenye RED ndio ukomo wa akili yako? Wanafunzi hawajiandai, WANAANDALIWA na ndio maana wako pale. Ubunifu unaanzia kwa waongozaji na kuhamishiwa kwa waongozwa. Unamjazia mwanafunzi changamoto ili ajifunze changamoto, sasa namna ya kukabiliana na hiyo changamoto ulioianzisha bila sababu za msingi ni maandamano, HAMTAKI.

Tatizo lenu raisi mnamuogopa yeye hajawazuia msimpinge sema mnazunguka mara Tulia mara Sukari mara Lugumi, Bajeti ya serikali haijengi viwanda najua unajua sema mnavyotaka kujipendekeza kwa Mbowe hawaone mpo ndio shida. Kujiajiri sio kila mtu anaweza hata mzee Mengi ilimchukua miaka kuanza kujiajiri sasa ukimtwisha JPM wakati kazini hata mwaka hana itakuwa shobo tu.

Ni kweli si kila mtu anaweza kujiajiri, ndio maana inahitajika mifumo wezeshi kuongeza wigo wa watu wanaojiajiri, moja kati ya institutions za kuwaandaa watu kujiajiri ni vyuo. Kama bajeti ya serikali haijengi viwanda, misaada mmesema hatuihitaji, uwekezaji unaporomoshwa na siasa za ki-Ji Sung Park, sasa inamaanisha maneno meeeengi ya kufufua viwanda na kuanzisha vipya ni ngonjera?

Wanafunzi watimize wajibu wao hata kama wanakutana na mazingira magumu ndio maisha yako hivyo wachache ndio wako fortunate. Serikali itaweka mazingira rafiki na ukitaka kujua yapo utaona kuna wengine wametusua bila kusubiri na wako mbali.

Ashakhum si matusi, uliomalizia nao hapo ni upumbavu. Mkuu, unaniambia kwamba NI WAJIBU WA WANAFUNZI KUVUMILIA MAZINGIRA MAGUMU YANASABABISHWA NA WATU WENGINE PASIPO SABABU ZA MSINGI? MAISHA NDIYO YAKO HIVYO? KWAMBA MTU MMOJA KWENYE CHAIN HAWAJIBIKI IPASAVYO, ANALETA USUMBUFU HALAFU INAKUWA NI WAJIBU WA WANAFUNZI KUVUMILIA?

Serikari itaweka mazingira blah blah blah......na wengine mametusua...... . Well then, hao waliogoma ni wale ambao mazingira mazuri hayakuwapitia karibu, vipi hapo?
 
Back
Top Bottom