Aug 31, 2022
54
99
Tume ya Utumishi wa Walimu Nchini (TSC), imekabidhiwa majina 78 ya walimu waliobainika kughushi nyaraka mbalimbali za wategemezi na matumizi mabaya ya kadi za bima za afya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano Serikalini cha TSC iliyotolewa jana Jumatano, Machi Mosi 2023, majina hayo yalikabidhiwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Walimu hao wanadaiwa kughushi nyaraka za vyeti vya kuzaliwa, vyeti vya ndoa kwa lengo la kutaka kuthibitisha uhusiano wao na wahusika hao ili waweze kusajiliwa na mfuko huo kwa ajili ya kupata huduma.

Makabidhiano hayo ya majina yamefanyika leo Machi Mosi katika Makao Makuu ya NHIF Jijini Dodoma wakati wa kikao kati ya menejimenti ya NHIF na TSC.

Katika kikao hicho ilitolewa ripoti inayoonesha namna walimu hao walivyohusika katika vitendo vya udanganyifu pamoja na hasara waliyoisababisha kwa mfuko.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga amesema mfuko umeshachukua hatua mbalimbali kwa watuhumiwa hao ambao walikiri kutenda makosa hayo.

Amezitaja hatua hizo ni pamoja na kuwafungulia kesi, kuwafungia matumizi ya kadi na kuwataka kurejesha fedha ambazo zilitumika kuhudumia wategemezi wasio halali.

“Tunachukua hatua nyingi kwa watuhumiwa wa udanganyifu na mpaka sasa kuna kesi zinaendelea katika Mikoa ya Geita, Dodoma na Dar es Salaam, kadi za matibabu za watuhumiwa hao zimefungiwa pamoja na kuwaandikia barua za onyo,” amesema.

Naye Katibu wa TSC, Paulina Nkwama amesema kuwa vitendo vilivyofanywa na walimu hao haviwezi kukubalika kwa kuwa ni ukiukwaji wa maadili ya utumishi wa umma hivyo kupitia mamlaka ya tume hiyo hatua zitachukuliwa.

Awali akiwasilisha taarifa ya uchunguzi wa udanganyifu uliofanywa na Watumishi wa Umma, Meneja wa Kitengo cha Kupambana na Udanganyifu cha NHIF, Dk Rose Ntundu amesema watumishi wa umma 99 waliobainika kufanya udanganyifu, 78 ni walimu wa shule za Serikali za msingi na sekondari.

MWANANCHI
 
Kwanini watajwe walimutu?

Hao NHIF wenyewe nimatapelitu wakati mwingine huduma hata kuziba jino bovu hawaitambui wanataka wateja wenye mapengo tu.
Yaani nikitengo cha hovyo wanakusanya hela huduma zina masharti kibao
 
Kama mtu anaishi na mwenza kuanzia miezi sita ndani ya nyumba sheria hiyo hiyo inawatambua kama ni mke na mume, lakini sheria hiyo hiyo haiwataki tena mpaka wawe na karatasi, na ni waTanzania , hakuna raia wa kigeni anayetumia hizo bima isipokua wao, yaani nchi hii
 
Wanajichanganya wenyewe. Hawajielewi
 
Kama mtu anaishi na mwenza kuanzia miezi sita ndani ya nyumba sheria hiyo hiyo inawatambua kama ni mke na mume, lakini sheria hiyo hiyo haiwataki tena mpaka wawe na karatasi, na ni waTanzania , hakuna raia wa kigeni anayetumia hizo bima isipokua wao, yaani nchi hii
Serikali ni kigeugeu, pumbavu kabisa
Yaani ukipata kiajira mshahara wa kwanza NHIF wamo hawakupi hata grace period ila fuatilia Bima Sasa
Ukipeleka cheti cha serikali wanataka cha dini Ukipeleka cha dini wanataka cha serikali, Ukipeleka vyote wanataka namba ya nida ya mkeo
Umbwa sana wale jamaa
 
Back
Top Bottom